📌 Asema Wizara ya Nishati inalo la kujivunia kutokana na uwepo wanawake katika nafasi za uongozi.
***
Mbuja ameyasema hayo alipokuwa akieleza safari ya mwanamke katika kudai haki, usawa na uwezeshaji kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo nchini kitaifa yatafanyika mkoani Arusha.
"Wanawake wengi walipambana kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia, usawa wa utendaji kazi na ushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi na tangu kufanyika kwa Mkutano wa Beijing mwaka 1995 mambo yote ya usawa kwa sasa yanaonekana kwa vitendo",amesema Mbuja.
Ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa kinara katika kuhakikisha haki kwa mwanamke inapatikana.
Ameongeza kuwa, Wizara ya Nishati inajivunia kwa uwepo wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Source