Wednesday, July 8, 2020

NUNUA TV BRAND YA HISENSE KWA BEI YA PUNGUZO WARRANTY MIAKA MITATU

Msimu Huu Wa Saba Saba Wahii Offa zetu Za Tv Bora Zenye Warranty Miaka 3 Tunakupatia Free Delivery/ Free Wall Bracket / Free HDMI CABLE/ Free Kufungiwa Ukutani Piga / WhatsApp 0658666996 Tunapatikana Makumbusho Kwa Mkazi Wa Dar Tunakuletea Mpaka Ulipo Ukipokea Mzigo Ndio Unalipia Kwa Mkoani

Kuna taratibu Tatu
1.kama unandugu Dar unaweza ukamuagiza Dukani
2.kama Unaagent wa Bus / Lorry si tunampelea mzigo wako mpaka alipo anakikisha alafu analipia
3.unatuma hela sisi tunaenda kukutumia mzigo wako

LED TVS
inch 32 = 390,000 ( Model : 32N50HTS )
Inch 40 = 570,000 ( Model : 40B5200PT )
Inch 43 = 700,000 ( Model : 43B5200PT)
Inch 49 = 900,000 ( Model : 49B5200PT)

SMART TV
Inch 32 = 500,000 ( Model : 32B6000HW)
Inch 43 = 800,000 ( Model : 43B6000PW)
Inch 49 = 950,000 ( Model : 49B6000PW)

SMART UHD / 4K
Inch 43 = 890,000 ( Model : 43B7100UW)
Inch 50 = 1,150,000 ( Model :50B7100UW)
Inch 50 = 1,200,000 Android ( 50B72000UW)
Inch 55 = 1,250,000 ( Model :55B7100UW)
Inch 55 = 1,650,000 ( Model :558000UW)
Inch 55 = 2,550,000 ( Model : 55Q8600)
Inch 65 = 2,100,000 ( Model :65B7100UW)
Inch 65 = 2,500,000 (Model : 65B8000UW )
Inch 65 = 3,400,000 ( Model : 65Q8600 )
Inch 75 = 4,750,000 ( Model : A6500 UHD )





MKE AZIKA MWILI WA MME WAKE MARA MBILI


Makaburi
Mwanamke mmoja Afrika Kusini amelazimika kufanya mazishi ya mume wake mara mbili aliyekufa kwa ugonjwa wa Covid-19 baada ya kubainika kwamba mwili wake ulitambuliwa makosa.

"Walikataa kuniruhusu nione mwili wa mpendwa wangu katika chumba cha kuhifadhia maiti kwasababu ya kanuni za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19. Sasa nimemzika mtu mwingine."

Hayo ndio yalikuwa maneno ya kusikitisha ya mke wake baada ya kubainika kwamba mwili wa mume wake, 79, umechanganyika na wa mwingine.

Micheal Vukile Noda, kutoka Uitenhage, mashariki mwa Cape alianza kuonesha dalili za ugonjwa wa Covid-19 na hali yake ilipoanza kuzorota mke wake akatafuta matibabu Juni 16. Mara ya mwisho familia yake kumuona ni pale alipobebwa na gari la kubebea wagonjwa akipelekwa hospitali.

Kulingana na mke wa Vukile, Nomsa Noda, 69, alikuwa na mafua kwa muda wa wiki mbili.

"Alienda kumuona daktari lakini hakumaliza matibabu kwasababu alilazwa kabla ya kumaliza dawa," anasema.

Hali yake ilibadilika na akapelekwa kitengo cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi, anasema.

Hospitali iliarifu familia kwamba amepata maambukizi ya mapafu.

Baadae alihamishwa hadi wadi ya wagonjwa wa kawaida na kuwa huko kwa wiki moja.

"Kwasababu hatukuruhusiwa kumtembelea, mara nyingi tulizungumza kwa simu. Lakini kadiri tulivyokuwa tunaendelea kuzungumza, alionekana kuwa dhaifu na mchovu sana hata kuongea ilikuwa shida. Ikafika kipindi ikawa hawezi hata kujibu simu zake unapompigia," amesema Nomsa.

Nomsa aliendelea kuwasiliana na wauguzi kuhusu hali ya mgonjwa wake lakini kila wakati walikuwa wanamuarifu kwamba mume wake yuko salama.

Nyimbo Mpya: Rosa Ree - Kayor Aleng' {Official Lyrics Video}


Nyimbo Mpya: Rosa Ree - Kayor Aleng' {Official Lyrics Video}

Bonyeza HAPA Kudownload

Bonyeza Play Kutazama:

Tuesday, July 7, 2020

Huyu Ndiye Sallam Mendez Aliyekataa Mkono wa Harmo!


KWENYE ulimwengu wa soka, kuna mtu hatari aitwaye Jorge Mendez. Ni mzaliwa wa pale jijini Lisbon, Ureno. Huyu ni wakala wa wanasoka wakubwa duniani kama Jose Mourinho, Felipe Scolari, Carlos, Anderson, Fabio Coentrao, Pepe, Angel Di Maria, Cristiano Ronaldo, Radamel Falcao, Ricardo Carvalho, Nani, Ricardo Quaresma, Burak Yilmaz, Joao Moutinho, James Rodriguez, David de Gea, Victor Valdes, Pedro na wengine wengi.

Huyu Jorge Mendez anatajwa kuwa mtu anayejua figisufigisu na fitina mno kwenye madili ya uhamisho wa wachezaji wakubwa kutoka timu moja kubwa kwenda nyingine duniani.

Jorge Mendez anatajwa kama mtu hatari zaidi kwenye eneo hilo na amekuwa tajiri mkubwa kutokana na madili hayo.

Tabia hiyo ya Jorge Mendez, imemfanya mtu aitwaye Sallam Sharrif 'SK' hapa Bongo, naye kupachikwa jina la Mendez kutokana na kuwa na tabia kama hizo.

Huyu Sallam ni mmoja wa mameneja wa mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'. Ukubwa wa Diamond au Mondi kwenye muziki wa Afrika unafahamika. Mameneja wengine wa Mondi ni Hamis Taletale 'Babu Tale' na Said Fela 'Mkubwa na Wanawe'. Tofauti na wengine, huyu Sallam anaongoza kwa kuchukiwa mitandaoni.

NI NANI HASA HUYU SALLAM?

Kutoka lile tukio la kudaiwa kusababisha mwanamuziki Ali Saleh Kiba 'King Kiba' kuzimiwa maiki jukwaani pale Mombasa nchini Kenya; Oktoba 8, 2016 mbele ya mwanamuziki mkubwa duniani, Chris Brown hadi kukataa mkono wa mwanamuziki Rajab Abdul 'Harmonize' pale Morogoro wiki iliyopita, kila mtu anajiuliza huyu jamaa ni nani hasa?

OVER ZE WEEKEND imechimba na hapa inakuletea safari nzima ya Sallam kwenye Bongo Fleva, figisufigisu anazohusishwa nazo na tabia zake zinazodaiwa zitaupeleka muziki huu kaburini;

Sallam anatajwa kuwa mmoja wa watu muhimu mno kwenye menejimenti ya Mondi. Sifa yake kubwa ni mtu mzuri wa kutengeneza connections nyingi zilizompaisha Mondi kimataifa.

Mashabiki wengi wa Mondi na wadau wa Bongo Fleva hawamfahamu kiundani. Lakini huyu jamaa ni mzaliwa wa jijini Dar na siyo Morogoro kama baadhi ya watu wanavyodhani.

SALLAM NA MOROGORO

Kule Morogoro, Sallam alikwenda kusoma tu, kabla ya kujiingiza kwenye Bongo Fleva enzi hizo wakati muziki huu unaibuka.

Kama ulikuwa hujui, Sallam alianza kujiingiza kwenye muziki akiwa Shule ya Sekondari ya Forest pale Morogoro akiwa anarap.

Alikuwa na kundi lake la kurap lililoitwa Watukutu akiwa na Swedi na Puzzo. Wakati huo, Sallam alifahamika kwa jina la kisanii la OG. Watukutu lilileta ushindani kati ya wasanii wa Dar na Morogoro. Wale wa Dar walikuwa ni akina Sugu, Hard Blastaz na Dilpomatz.

UANDAAJI WA SHOO

Baadaye, kundi hilo lilisambaratika ambapo Sallam aliamua kujikita kwenye uandaaji wa shoo. Baada ya kuandaa shoo za ndani na kupata uzoefu, alianza uwakala wa kuleta wasanii wa nje ya nchi kuja kufanya shoo na kolabo na wasanii wa Bongo.

Hapa ndipo alipofanikiwa kuwaleta wasanii kama Prezzo na Huddah (Kenya) na J Martins (Nigeria). Baada ya shoo, J Martins akafanya kolabo na AY na MwanaFA kwenye ile Ngoma ya Bila Kukunja Goti na Ommy Dimpoz kwenye Ngoma ya Tupogo.

KOLABO YA MONDI NA DAVIDO

Baadaye alimshusha Bongo msanii Davido kutoka Nigeria, ndipo akafanikisha ile kolabo ya Mondi na jamaa huyo ya Number One Remix na kuanzia hapo akaanza na Mondi.

FIGISUFIGISU

Unaikumbuka ile Shoo ya Tigo iliyofanyika Viwanja vya Leaders jijini Dar, miaka mitano iliyopita? Shoo ile iliwajumuisha Mondi na Kiba jukwaani na haijatokea tena hadi leo. Shoo ile iliweka rekodi nyingi kuanzia vurugu nje ya uwanja na hata ndani kutokana na kuwepo kwa makundi mawili makubwa. Team Kiba ilikuwa na kazi moja tu; kumzomea Mondi. Team Mondi na yenyewe ilikwenda mbali zaidi kwa kuzomea na kumrushia Kiba chupa za maji?

Baada ya shoo hii, ndipo Sallam alipoanza kuonesha figisufigisu dhidi ya mahasimu wa Mondi. Baada ya shoo ile ambayo Kiba alikimbiza, kesho yake, Sallam aliweka kijiji pale Twitter akimtukana Kiba kuwa ni mchawi na muoga. Alikwenda mbali zaidi na kutoa madai kuwa Kiba na timu yake waliruka ukuta kuingia Viwanja vya Leaders.

Pia alidai Kiba hakumsalimia msanii yeyote. Hapo ndipo utashikwa na mshangao kwamba mambo ya Kiba kuruka ukuta na kutomsalimia msanii yeyote kama ni kweli au si kweli, yeye Sallam ilimhusu nini? Mbona wasanii wengine au mameneja wao hawakuzungumza, kwa nini yeye imuume kiasi kile na kukimbilia Twitter kumchafua Kiba?

SHOW YA CHRISS BROWN

Tukio lingine ni ile shoo ya Chriss Brown pale Mombasa ambapo Sallam alinaswa nyuma ya jukwaa na kudaiwa kufanya figisufigisu kumharibia Kiba kwa kuwa msanii wake Mondi hakupata chansi hiyo ya kufanya shoo mbele ya Chriss Brown.

Kiba alitakiwa afanye shoo ya live. Timu yake ilipaswa kufunga vifaa vya shoo ya live ambapo zoezi hilo lingechukua nusu saa halafu ndipo Kiba apande kufanya shoo. Hapa tatizo halikuwa kwa Kiba, bali kwa waandaaji wa shoo na fundi mitambo ambao walichelewa kufunga mitambo yao, hivyo Kiba alipopanda akaimba nyimbo mbili kisha akazimiwa maiki.

Baada ya kushuka jukwaani, Kiba alisema; "Nilimuona bosi wa Diamond, Sallam akiwa back stage (nyuma ya jukwaa) wakati ninashuka stejini. Kwa maana hiyo, Sallam alikuwa back stage wakati mimi ninapafomu, lakini ninajiuliza mwenyewe, Sallam alifuata nini back stage wakati mimi ninapafomu na ikiwa inafahamika mimi na wao hatuna maelewano mazuri? Unadhani watu watachukuliaje yeye kukaa back stage wakati mimi ninapafomu? Yeye ni nani mpaka akae back stage kwangu? Kama angetaka kuangalia shoo, si angekaa VIP aangalie shoo? Kwa nini aje back stage?"

Baadaye kuliibuka madai kwamba, Sallam alikula mchongo na meneja wa msanii Wizkid wa Nigeria aitwaye Mr Sande ambaye pia ni meneja wa Mondi kwa Afrika Magharibi, wakashirikiana kumhujumu Kiba.

TUKIO LA COKE STUDIO

Kuna kipindi Kiba alikwenda Coke Studio pale Nairobi ambapo aliungana na mwanamuziki wa Marekani, Neyo ambaye alikuwa yupo tayari kufanya naye kolabo.

Kuna madai kwamba, usiku wa tukio hilo, baada ya Sallam kuinyaka ishu hiyo, hakulala, alifunga safari usiku huohuo kwenda Nairobi. Alipofika kule alidaiwa kumtia maneno Neyo na kuvuruga kabisa mipango yote ya Kiba na Neyo. Unajua nini kilifuata? Neyo alifanya kolabo ya Ngoma ya Marry You akiwa na Mondi. Huyo ndiye Sallam Mendez!

KUKATAA MKONO WA HARMO

Tupo msibani Morogoro kumpumzisha kwenye nyumba ya milele mke wa Babu Tale, Shamsa Kombo 'Shammy' aliyefariki dunia wiki iliyopita.

Inafahamika kwamba mwishoni mwa mwaka jana, mwanamuziki Rajab Abdul 'Harmo' alijitoa kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Mondi. Kumbe kuondoka kwa Harmo kulimuacha Sallam na kinyongo au gubu, jambo ambalo ni baya mno hasa likifanywa na mtoto wa kiume!

Harmo anafika msibani na kusalimiana na watu wa kila aina, lakini anapofika kwa Sallam, jamaa anakataa kumpa mkono. Harmo anabaki amegandisha mkono akiwa amemnyooshea Sallam anayejifanya yupo bize na simu kisha kutaka kuupiga mkono huo ili Harmo aondoke mbele yake. Watu wanapatwa na mshangao!

Watu wanamshangaa Sallam kuonesha bifu msibani. Harmo anajisikia vibaya, lakini anaamua kuchukulia poa kwa sababu mbona mameneja wengine wa Wasafi walisalimiana vizuri tu? Kwa nini Sallam anaonesha tabia za kitoto msibani? Kwa nini Sallam anaonesha tabia za Kiswahili msibani? Kwa nini Sallam anaonesha chuki msibani? Jibu ni moja tu;

Huyu ndiye Sallam Mendez anayepaswa kujitafakari, yeye anajiona shujaa wa kuifikisha Bongo Fleva kimataifa, lakini si ajabu anaichimbia kaburi kwa tabia zake!

Monday, July 6, 2020

Corona Yamtesa PETER wa P-Square



MWANAMUZIKI mkubwa barani Afrika aliyekuwa akiunda Kundi la P Square kutoka Nigeria, Peter Okoye 'Mr P' anateseka baada ya kukutwa na Virusi vya Corona vinavyosababisha Ugonjwa wa COVID -19.


Kwa mujibu wa Mr P, yeye, mkewe pamoja na binti yao walipatikana na Corona wiki tatu zilizopita. Mr P anasema, yeye na familia yake wanapitia wakati mgumu mno ila anamshukuru Mwenyezi Mungu wapo hai.


Mbali na yeye, mkewe na mtoto wao, pia wafanyakazi wake wawili wa nyumbani nao walikutwa na virusi hivyo mapema mwezi uliopita.


"Kwa muda wa wiki tatu zilizopita, nimepitia wakati mgumu na wengi hamkujua kwa nini nilikuwa kimya, nilisema iwe siri kwangu, nimekuwa na Virusi vya COVID -19, mke wangu pia alipatikana na virusi hivyo," amesema Mr P.


Ameongeza kuwa, mkewe Lola na mwanawe walipatikana na virusi hivyo na kwa sasa wamewekwa karantini.

"Nilikuwa mgonjwa sana na nikawekwa karantini, nisingeweza kumuona binti yangu mgonjwa, nilijisikia vibaya sana, najutia sana kuwaletea familia yangu ugonjwa huu hatari," anasema Mr P akikiri kwamba, yeye ndiye alileta virusi hivyo nyumbani kutoka kwenye mizunguko yake duniani.

Mr P na pacha wake Paul walikuwa wakiunda Kundi la P-Square ambalo lilivunjika miaka kadhaa iliyopita kutokana na kutoelewana kwenye mgawanyo wa mapato.


Thursday, July 2, 2020

Waandamanaji Afrika Kusini wapinga chanjo ya corona, wasema wao si nguruwe wa Guinea



Wananchi wa Afrika Kusini wanaopinga kutolewa chanjo ya corona jana waliandamana katika mji wa Johannesburg wakieleza kusikitishwa kwao na majaribio ya kwanza ya chanjo hiyo kufanywa kwa binadamu barani Afrika kwa ajili ya chanjo ya corona. 

Jumatano iliyopita, wataalamu wa Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha nchini Afrika Kusini kwa ushirikiano na kile cha Oxford waliandaa chanjo ya kwanza ya majaribio kuwahi kufanywa nchini Afrika Kusini ambayo itawahusisha watu waliojitolea 2000. 

Taarifa zinasema kuwa, kujumuishwa nchi ya Afrika Kusini katika majaribio ya chanjo hiyo ya corona kumesudiwa ili kuhakikisha kuwa, bara la Afrika linapata chanjo hiyo kwa gharama nafuu na lisiachwe nyuma katika uwanja huo. 

Waandamanaji walikusanyika mbele ya Chuo Kikuu cha Witwatersrand katika mji wa Johannesburg wakipiga nara za "hatutaki Waafrika kutumiwa kama nguruwe wa Guinea." Waandamanaji hao wamehoji kwamba inakuwa vipi watu wafanyiwe majaribio ya chanjo hiyo ya corona bila ya kujua hatari na madhara yake? Wamesema majaribio hayo yaliyopangwa kufanywa nchini Afrika Kusini kwanza yanapasa kufanyiwa kwa watoto wa wabunge na wa mawaziri na si kwa watu maskini wa nchi hiyo. 

Afrika Kusini ina idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya corona barani Afrika ambapo hadi sasa nchi hiyo imethibitisha kesi zaidi ya 150,000 na vifo zaidi ya 2,600. 


Source

Mike Pompeo asisitiza kuwa Marekani imesimama wima dhidi ya Urusi

Serikali ya Rais Donald Trump inasisitiza kwamba imekuwa na msimamo mkali kwa Urusi kuhusiana na suala la Afghanistan ila imeuweka wazi mlango wake kwa kumualika Rais Vladimir Putin kwa mkutano wa kilele.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema "si jambo jipya" kwamba Urusi imekuwa ikienda kinyume na maslahi ya Marekani huko Afghanistan.

Haya yanajiri wakati ambapo uongozi wa Trump umekasirishwa na ripoti zilizochapishwa kwenye magazeti kwamba idara ya ujasusi ya Marekani inaamini kuwa Urusi iliwalipa wanamgambo wa Taliban kwa ajili ya kuwauwa wanajeshi wa Marekani.

Rais Trump kupitia kwa katibu wa ikulu ya White House, Kayleigh McEnany amekanusha kwamba hakufahamishwa kuhusiana na suala hilo.

Mwaandishi wa habari wa Muungwana Blog Zanzibar anyakua Tunzo 3 za utetezi wa watoto


Mwandishi wa Habari wa Muungwana Blog visiwani Zanzibar,Thabit Hamidu Madai amepata  Tunzo Tatu ya Umahiri wa Uwandishi wa habari Mitandaoni  kwa habari zinazohusu udhalilishaji na ukatili wa watoto visiwani Zanzibar.



Tunzo hizo zimetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia haki za watoto Duniani (UNICEF) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) na kukabidhiwa na Wazira wa Kazi,Uwezeshaji Wanawake,Wazee na Watoto Zanzibar, Moudline Cyrus Castico.



Hafla ya kukabidhi Tunzo ilifanyika katika Ukumbi wa Jumuiya walemavu Zanzibar uliopo weilesi Kikwajuni na kushirkisha Waandishi wa Habari, Wahariri wa vyombo vya Habari na wadau mbalimbali wa Habari kutoka ndani na nje ya Nchi.



Jumla ya Tunzo 9 zimetolewa ambazo ni Tunzo za Waandishi wa habari bora wa habari za watoto katika vipindi vya Redioni, Makala za magazeti, vipindi vya televisheni na Habari na makala za mitandaoni ambapo Thabit Madai alichukua nafasi kwanza,Nafasi ya Pili na Nafasi ya kwanza katika kundi la Mwandishi wa Habari za mitandao.



Akizungumza Mara baada ya kukabidhi Tunzo hizo, Wazira wa Kazi,Uwezeshaji Wanawake,Wazee na Watato Zanzibar,Moudline Cyrus Castico aliwataka waandishi wa Hbari kuongeza kasi katika kuandika habari zinazohusu changamoto za watoto visiwani humo ili Serikali na wadau mbalimbali kuweza kuzitatua.



"Waandishi wa Habari bado muna kazi kubwa sana ya kuandika hizi changamoto zinazowakabiliwa watoto visiwani Zanzibar ili zitatuliwe na watoto wetu waishi kwa amani, hivyo nawaomba zidisheni kasii hii kwa mashirikiano na Serikali" alisema Waziri Castico.

Wednesday, July 1, 2020

TAMWA yawapongeza wagombea wanawake

Wakati zoezi la uchukuaji wa fomu na kurejesha kwa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) likifikia tamati, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar kinawapongeza kwa dhati wanawake wote waliojitokeza kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa wagombea wa kiti cha Urais Zanzibar kupitia Chama hicho.

Katika mchakato wa kutafuta nafasi ya mgombea Urais Zanzibar ulioanza Juni 15, mwaka huu, jumla ya wanachama 32 wamejitokeza kwenye kinyanganyiro hicho ambapo wanachama watano (5) sawa na asilimia 15 walikuwa ni wanawake.

Wanawake hao ni pamoja na Mwantum Mussa, Hassna Attai, Fatma Kombo, Mgeni Hassan na Maudline Castico.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kujitokeza wanawake kugombea katika nafasi hiyo ya juu ya nchi kutokana na mifumo dume ambayo inamtenga mwanamke katika kuwania nafasi za maamuzi sambamba na mwenziwe mwanamme.

Hadi miaka ya 1940 ilionesha kuwa mwanamke alikatazwa kuhudhuria hata skuli, nyenzo muhimu katika kukwaa ngazi za kisiasa na kijamii kwa madai kuwa anaweza kupoteza ujanajike wake.

Hali hii ilirejesha nyuma sana maendeleo ya wanawake na nchi kwa jumla kwa vile wanawake ni zaidi ya asilimia 50 ya wakaazi wa Zanzibar kwa mujibu wa Sensa ya 2012 na makisio ya idadi ya watu yaliyofuata.

Tafiti duniani kote ikiwemo na Zanzibar zinaonesha kuwa wanawake ni watendaji wazuri, waaminifu, waadilifu na wanaofanya maamuzi kwa njia ya ushirikishi na hivyo wakiwa kwenye uongozi huharakisha sana maendeleo ya nchi.

Ni Mh. Amina Salim Ali tu ndiye aliyewahi kuomba ridhaa ya wananchi kupitia chama hicho kikuu nchini mwaka 2000 ambapo hakuweza hata hivyo kuchaguliwa na hivyo Zanzibar kukosa kabisa mgombea mwanamke pamoja na Rais mwanamke kwa maisha yote.

TAMWA ZNZ inapenda kukipongeza CCM kwa kuwawezesha wanawake hao kutoka chama hicho kuweza kugombea hadi katika hatua hiyo ya uongozi.

Tunaamimi sasa wakati umefika kwa jamii wakiwemo wanasiasa kulichukulia suala hili kwa uzito unaostahiki na hivyo kuwapa nafasi wanawake kuonesha uwezo wao wa kuongoza katika nyanja mbali mbali.

Tunatamani pia CCM itachagua mmoja kati ya wanawake hao ili kuweza kupeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

TAMWA Zanzibar inaamini kwamba ujasiri huo ulioonyeshwa na wanawake hao waliojitokeza utasaidia kuongeza hamasa zaidi kwa   wanawake vijana kuendelea kujiamini na kuona kuwa wanayo nafasi sawa ya kushiriki katika ngazi zote za maamuzi kwa mstakabali wa taifa lao.

TAMWA Zanzibar inawaomba wanawake wa vyama vyengine vyote kujitokeza katika kugombea nafasi mbali mbali ili kuongeza mabadiliko haya ya wanawake katika ngazi za maamuzi itakayopelekea pia kutatuka kwa matatizo mbali mbali yanayowaaathiri kiuchumi na kijamii.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...