Wakati zoezi la uchukuaji wa fomu na kurejesha kwa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) likifikia tamati, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar kinawapongeza kwa dhati wanawake wote waliojitokeza kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa wagombea wa kiti cha Urais Zanzibar kupitia Chama hicho.
Katika mchakato wa kutafuta nafasi ya mgombea Urais Zanzibar ulioanza Juni 15, mwaka huu, jumla ya wanachama 32 wamejitokeza kwenye kinyanganyiro hicho ambapo wanachama watano (5) sawa na asilimia 15 walikuwa ni wanawake.
Wanawake hao ni pamoja na Mwantum Mussa, Hassna Attai, Fatma Kombo, Mgeni Hassan na Maudline Castico.
Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kujitokeza wanawake kugombea katika nafasi hiyo ya juu ya nchi kutokana na mifumo dume ambayo inamtenga mwanamke katika kuwania nafasi za maamuzi sambamba na mwenziwe mwanamme.
Hadi miaka ya 1940 ilionesha kuwa mwanamke alikatazwa kuhudhuria hata skuli, nyenzo muhimu katika kukwaa ngazi za kisiasa na kijamii kwa madai kuwa anaweza kupoteza ujanajike wake.
Hali hii ilirejesha nyuma sana maendeleo ya wanawake na nchi kwa jumla kwa vile wanawake ni zaidi ya asilimia 50 ya wakaazi wa Zanzibar kwa mujibu wa Sensa ya 2012 na makisio ya idadi ya watu yaliyofuata.
Tafiti duniani kote ikiwemo na Zanzibar zinaonesha kuwa wanawake ni watendaji wazuri, waaminifu, waadilifu na wanaofanya maamuzi kwa njia ya ushirikishi na hivyo wakiwa kwenye uongozi huharakisha sana maendeleo ya nchi.
Ni Mh. Amina Salim Ali tu ndiye aliyewahi kuomba ridhaa ya wananchi kupitia chama hicho kikuu nchini mwaka 2000 ambapo hakuweza hata hivyo kuchaguliwa na hivyo Zanzibar kukosa kabisa mgombea mwanamke pamoja na Rais mwanamke kwa maisha yote.
TAMWA ZNZ inapenda kukipongeza CCM kwa kuwawezesha wanawake hao kutoka chama hicho kuweza kugombea hadi katika hatua hiyo ya uongozi.
Tunaamimi sasa wakati umefika kwa jamii wakiwemo wanasiasa kulichukulia suala hili kwa uzito unaostahiki na hivyo kuwapa nafasi wanawake kuonesha uwezo wao wa kuongoza katika nyanja mbali mbali.
Tunatamani pia CCM itachagua mmoja kati ya wanawake hao ili kuweza kupeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.
TAMWA Zanzibar inaamini kwamba ujasiri huo ulioonyeshwa na wanawake hao waliojitokeza utasaidia kuongeza hamasa zaidi kwa wanawake vijana kuendelea kujiamini na kuona kuwa wanayo nafasi sawa ya kushiriki katika ngazi zote za maamuzi kwa mstakabali wa taifa lao.
TAMWA Zanzibar inawaomba wanawake wa vyama vyengine vyote kujitokeza katika kugombea nafasi mbali mbali ili kuongeza mabadiliko haya ya wanawake katika ngazi za maamuzi itakayopelekea pia kutatuka kwa matatizo mbali mbali yanayowaaathiri kiuchumi na kijamii.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...