Tuesday, March 31, 2020

Kikwete "Nimepoteza Rafiki wa Muda Mrefu"



Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ameonesha kuguswa na msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman, aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia leo na kusema kuwa amepoteza rafiki yake wa muda mrefu.

Dkt Kikwete ameyabainisha hayo leo Machi 31, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, na kutoa pole kwa Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wanachama wote na kwamba wamepoteza kada wa kuaminiwa na kutumainiwa.

"Ni kweli tulikuwa pande mbili tofauti, lakini kama wanadamu tulikuwa marafiki tangu wakati tukiwa wote bungeni na hata baada ya mimi kuacha Ubunge, daima nitamkumbuka kwa moyo wake wa upendo, ukarimu, ucheshi na huruma, tuko pamoja katika majonzi na kuomboleza, tunakuombea wewe binafsi, wanachama wote wa CUF na familia ya marehemu moyo wa subira na ustahamilivu. Innalilahi Wainna Ilaihi Rajiun" ameandika Dkt Kikwete.


Source

Naibu waziri awataka wafugaji Kuzuia Mikusanyiko Minadani


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka wafugaji nchini kuhakikisha kuwa wanachukua tahadhari juu ya virusi vya homa ya Mafamu Covid -19 ambavyo vinasababisha Ugonjwa wa Corona.

Akizungumza na wafugaji mara baada ya kutembelea minada ya mifugo katika soko la kimataifa la mifugo lilipo wilayani longido pamoja na mnada wa Miserani,uliopo wilayani monduli mkoani Arusha,Ulega alisema kuwa tahadhari ni muhimu kuchukuliwa na kuhakikisha kuwa wafugaji na wafanyabishara wanawana mikono.

Aidha alisema kuwa pindi biashara ya mifugo inapofanyika ili kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima ni vyema wafugaji wakarejea majumbani ili kujikinga na gonjwa hilo.

Katika hatua nyingine naibu waziri Ulega alitembelea kituo cha wizara ya mifugo na uvuvi kilichopo katika boda ya namanga na kuzungumza na maafisa hao,ambapo alisema kuwa serikali imeruhusu biashara kufanuyika kama kawaida hivyo waisaidie serikali katika eneo hilo.Alisema ni lazima biashara na shughuli za kiuchumi ziendelee ili serikali ipate mapato, huku familia zipate mahitaji yao muhimu.

"Hatuwezi kufunga minada hii sababu maisha ya watanzania walio wengi huishi kwa kutafuta mlo a kila siku, hivyo kuzuia minada hii ni sawa na kuataka wafe kwa njaa, sasa hili serikali tumelitafakari ka kina na tumeona haifai kuifunga minada hii,"alisema.

"Ninachosisitiza hapa kwenye minada hii wawepo tu wale wanaouza mifugo na wanaonunua, lakini mkishauziana tu ondokeni mara moja mnadani na sitaki muweke mikusanyiko,"alisema.

Aidha alipongeza minada hiyo kutokana na tahadhari zilizochukiwa ambapo ili kuthubiti mikusanyiko makundi ya wafugaji na wafanyabishara imepungua kwa kiasi kikubwa tangu kulipozuka Ugonjwa huo huku kila anayeingia ananawa mikono kwa maji safi yanayotiririka.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frack Mwaisumbe,alishukuru serikali kuruhusu wananchi wake kuendelea na minada ya mifugo, sababu ni sehemu ya maisha yao,huku akieleza wazi kuwa hapo awali minada huo wa longido ulifunngwa kutokana na kuzua taaruki kubwa kwa wananchi mara baada mgonjwa wa kwanza wa Corona kutangazwa.

AFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI AKIENDESHA PIKIPIKI KUTOKA SHAMBANI


Mkazi wa kata ya Kabungu mkoani Katavi, Paulo Chundu (27) amefariki dunia kwa ya kupigwa na radi wakati akitoka shambani.

Tukio hilo lilitokea machi 29 mwaka huu majira ya saa 12: 45 jioni katika mbuga za Kalilankulukulu kata ya Kabungu wilayani Tanganyika mkoani Katavi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoni Katavi Benjamin Kuzaga amesema kijana huyo alikutwa na umauti akiwa katika mbuga hiyo akiendesha pikipiki kutokea katika Kijiji cha Ikaka akielekea nyumbani kwake.

Kamanda alisema majira ya saa 12:45 alipatiwa taarifa za kijana huyo kufariki kwa kupigwa radi akiwa anatokea shambani kuelekea nyumbani

Baba mdogo wa kijana huyo, John Laurent alisema alimuagiza shambani kumpeleka mtu wa kufanya kazi za shambani ikiwemo kutoa majani, hivyo wakati anarudi akafariki kwa kupigwa na radi.

Alisema tukio hilo limemuumiza na kwamba mtoto huyo aliachiwa na kaka yake baada ya kufariki na kupewa jukumu la kumlea.


Waziri Mpina asimamisha malipo ya mkandarasi wa mahabara ya TAFIRI


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesimamisha malipo yote kwa Mkandarasi wa
Kampuni ya Petra Construction co. Limited inayojenga maabara ya kisasa ya Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaam hadi uhakiki wa gharama halisi za mradi huo utakapokamilika baada ya kubaini kuwepo matumizi mabaya ya fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 2.6

Hivyo
Waziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha
wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya
Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo.
Akizungumza
mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)  jijini Dar es Salaam, Waziri
Mpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogo
ikilinganishwa na mkataba ulioridhiwa  wa
sh. bilioni 2.6 na kwamba taarifa ya uhakiki ya mradi huo itawasilishwa
wizarani ikiwa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya wizi huo wa fedha
za umma.
Waziri
Mpina alisema thamani halisi ya mradi huo hailingani na fedha zilizotolewa na
Serikali huku akitolea mfano baadhi ya miradi ya ujenzi wa majengo mbalimbali
ikiwemo vituo vya afya na hospitali za wilaya zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.
Hata
hivyo wakati wa mjadala ukiendelea wa kuhoji matumizi ya fedha hizo kwenye
mradi huo, mmoja wa wakandarasi wanaojenga majengo hayo alimweleza Waziri Mpina
kuwa hadi mradi utakapomika kutabaki 'chenji' kiasi cha shilingi milioni 500
jambo lililotilia mashaka na kuibua maswali mengi juu ya gharama halisi za
mradi huo.
Kufuatia mkanganyiko huo wa maelezo ya
mkandarasi na hali halisi iliyoonekana kwenye mradi huo ndipo Waziri Mpina
akalazimika kutangaza uamuzi huo wa kuundwa tume hiyo ili iweze kufanya tathmini
ya gharama ya mradi iliyofanywa na Mshauri mwelezi wa mradi, namna zabuni ya
kumpata mkandarasi ilivyotangazwa na namna mshauri mwelekezi alivyopatikana na
hali ya ujenzi unavyoendelea kwa sasa ili kujua dosari ilisababishwa na nani.

Hivyo Waziri Mpina akabainisha kuwa baada ya kazi hiyo ya uhakiki kukamilika ndani ya siku saba ukweli utajulikana na hatua zote zilizopitiwa katika mradi huo ili kubaini kama Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 ilikiukwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha za umma.

 "Sikubaliani na hizi gharama za mradi majengo
na miundombinu ni midogo ikilinganishwa na mkataba wa bilioni 2.6, BOQ
ilihakikiwa na wahandisi wa wizara, washauri waelekezi walijiridhisha kwamba
iko sawa na ujenzi ukaenda hadi bilioni 2.6 mtu yeyote akija anakataa" alihoji
Waziri Mpina
Hivyo
Waziri Mpina ameagiza ujenzi wa mradi huo uendelee bila kusimama na ukamilike ifikapo
Aprili 20 mwaka huu kama mkataba unavyoeleeza na baada ya jengo litazinduliwa
ikiwa ni sehemu ya kuleta mageuzi makubwa ya sekta ya uvuvi kupitia eneo hilo
muhimu la utafiti.
"Nitaleta
timu ya ukaguzi itakayofanya uhakiki wa thamani ya fedha katika ujenzi wa jengo
hili, kuanzia kwenye kutangaza tenda yenyewe, thamani ya mradi, kumpata
mkandarasi mwenyewe, cost estimates zilizofanywa na wizara na baadae watafanya
uhakiki wa kinachoendelea kujengwa hapa na kujua thamani halisi inayotakiwa na
kwanini mradi huu upitishwe hadi kusainiwa"alihoji Waziri Mpina.
Meneja
wa Mradi wa Swiofish, Flora Luhanga alisema mradi huo wa ujenzi wa Jengo la
Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ulianza Juni 10, 2019 kwa gharama ya
shilingi bilioni 2, 609,491,754 unajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Petra
Construction Limited na kusimamiwa na Kampuni ya YP Architect.
Luhanga
alisema mradi huo unajumuisha  pia ujenzi
wa uzio, ofisi ya walinzi, kuchimba kisima cha maji, ujenzi wa tenki la maji ya
mvua na kujenga mnara wa maji.
Mkandarasi
wa Mradi huo, Nicholaus Mlayi alisema hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia
asilimia 70 na tayari ameshalipwa shilingi milioni 963 na unatarajia kukamilika
mwezi Aprili.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Uvuvi, Magese Bulayi alimhakikishia Waziri Mpina kuwa maagizo yote
aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu hasa katika kuangalia thamani ya fedha
'value for money' katika mradi huo na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa
wote watakaobainika kuhusika katika mchakato huo.
Source

Afariki kwa kupigwa na radi akiendesha pikipiki Toka Shambani

Mkazi wa kata ya Kabungu mkoani Katavi, Paulo Chundu (27) amefariki dunia kwa ya kupigwa na radi wakati akitoka shambani.

Tukio hilo lilitokea machi 29 mwaka huu majira ya saa 12: 45 jioni katika mbuga za kalilankulukulu kata ya kabungu wilayani Tanganyika mkoani katavi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoni katavi Benjamin Kuzaga amesema kijana huyo alikutwa na umauti akiwa katika mbuga hiyo akiendesha pikipiki kutokea katika Kijiji cha ikaka akielekea nyumbani kwake.

Kamanda alisema majira ya saa 12:45 alipatiwa taarifa za kijana huyo kufariki kwa kupigwa radi akiwa anatokea shambani kuelekea nyumbani

Baba mdogo wa kijana huyo, John Laurent alisema alimuagiza shambani kumpeka mtu wa kufanya kazi za shambani ikiwemo kutoa majani, hivyo wakati anarudi akafariki kwa kupigwa na radi.

Alisema tukio hilo limemuumiza na kwamba mtoto huyo aliachiwa na kaka yake baada ya kufariki na kupewa jukumu la kumlea.


Hatuwezi Tuka 'Copy' na Kupest Kwa Wazungu - Spika Ndugai


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kama nchi haiwezi kuchukua tahadhari kama zilivyochukuliwa na Mataifa mengine duniani ya kupambana na Virusi vya Corona kwa kuwa watu wengi nchini maisha yao ni ya kubangaiza siku kwa siku.

Hayo ameyabainisha leo Machi 31, 2020, Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Mkutano wa 19.

"Hatuwezi kuchukua measure za wazungu na kuzi copy na ku- paste hapa kwetu kama zilivyo, tutaua watu wetu, lazima tuangalie maisha yetu ya Kitanzania na kujaribu kuchukua hatua kufuatana na mazingira yetu" amesema Spika Ndugai.

Aidha wakichangia hoja zao bungeni wabunge wa CHADEMA Halima Mdee na Peter Msigwa, wameishauri Serikali kuja na taarifa zote zinazohusu mwenendo wa ugonjwa wa Virusi vya Corona hapa nchini na kuangalia ni kwa namna gani kwa pamoja wataweza kukabiliana na athari ikiwemo uchumi pindi ugonjwa huo utakaposambaa zaidi.

Ndugu wathibitisha corona ilivyoondoa uhai wa Iddy Mbita

Ibrahim Mbita amesema mdogo wake, Iddy amefariki kwa ugonjwa wa corona leo Jumanne Machi 31, 2020 katika kituo cha matibabu ya wanaougua ugonjwa huo kilichopo Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam.

"Familia ya Marehemu Alhaj Brigedia Generali Hashim Mbita kwa huzuni kubwa inasikitika kuarifu msiba wa mdogo wetu mpendwa IDDI HASHIM MBITA uliotokea usiku wa kuamkia leo hospitalini Mloganzila.
Kutokana na tatizo lililopelekea kifo chake, CORONA, serikali itamzika mpendwa wetu leo mchana. Wawakilishi wachache sana wa familia wataruhusiwa kuhudhuria mazishi. Hakutakuwa na msiba wala matanga ya pamoja kuepuka kueneza maambukizi. Kila mtu aomboleze kwake.
Dua nyingi tumuombee Iddi Allah amuweke pema peponi. Amina."

Leo taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu imethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa alikuwa akipatiwa matibabu katika kituo hicho.

"Marehemu ni Mtanzania mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine."



Source

Halima Mdee Ashauri Wabunge Wote Wapimwe Virusi Vya Corona

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Mbunge wa jimbo la Kawe jijini  Dar Es  Salaam Mhe.Halima  Mdee ameishauri  Serikali kufanya mchakato wa kupima Corona wabunge wote na watakaobainika wawekwe karantini.

Mhe.Mdee amesema hayo leo Machi 31,2020 bungeni jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa inatakiwa kila mbunge apimwe homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona[COVID -19]na akibainika  na maambukizi ya  virusi hivyo atengwe eneo maalum[karantini] na wale watakaobainika kutokuwa na maambukizi waendelee na mkutano ili kujadili bajeti kuu ya serikali ikiwa ni mkutano wa Mwisho kuelekea uchaguzi mkuu.

"Leo wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi wote,kwa nini tusipime wote atakayebainika ana virusi apelekwe karantini na akiwa salama abaki hapa kujadili mambo ya msingi kwa mstakabali wa taifa letu  maana ni mkutano wa mwisho"amesema.

Naye,Mbunge wa   Iringa Mjini  Mch.Peter  Msigwa ameiomba serikali kuja na mpango wa pamoja katika kujadili katika mapambano ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona[COVID-19].

Spika wa bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema katika mkutano wa bunge  la bajeti  ni vyema majadiliano ya pande zote mbili yakazingatiwa huku akitoa wito kwa wabunge kusikilizana na kuelekeza zaidi kwenye bajeti kwani ni mkutano wa Mwisho ambapo bunge litavunjwa kuelekea uchaguzi mkuu  2020.

"Kikao ni chetu kisiwe cha upande mmoja au watu wachache hata kidogo kwa hiyo natoa wito kusikilizana kwa pande zote mbili na ni vyema zaidi mbunge ukajielekeza kwenye bajeti kuliko ukasimama na yako tu ni muhimu sana kuzingatia muda"amesma.

Katika hatua nyingine Mhe.Ndugai ametoa maelekezo kwa serikali kuandaa majibu haraka iwezekanavyo juu ya Hoja Za Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali[CAG] zilizowasilishwa hivi karibuni kwa  Mhe.Rais .


Viongozi wa Dini Rukwa waazimia kupunguza muda wa ibada kujihadhari na Corona

Viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Rukwa wamekubaliana kuwa kila dhehebu kulingana na imani zao kuona namna ya kupunguza muda wa kufanya ibada katika misikiti na makanisa mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19).

Wamekubaliana hayo wakati wa kikao kifupi kilichoitishwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura katika kikao hicho kilicholenga kuwaelimisha viongozi hao juu ya Chanzo, usambaaji na namna ya kujikinga na ugonjwa huo ambao unaendelea kuisumbua dunia huku jukumu la kutoa elimu likifanywa na Mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Wakati akielezea namna ya kutekeleza azma hiyo Shekhe wa mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali alisema kuwa atazungumza na mashekhe wa wilaya na Maimamu wa miskiti ya mkoa huo kupunguza muda wa ibada ili kukwepa kuwaweka watu wengi katika eneo moja kwa muda mrefu lakini pia kuwafanya waumini hao wasikose ibada hizo.

"Niungane na Askofu wa Monravian, tupunguze nyakati za ibada zetu, na kubwa iwe ni kuongoza dua na maombi kwaajili ya nchi yetu, sisi tumelipunguza hili baada ya kutokea hili, ibada ya nusu saa tumekwenda dakika kumi na tano, dakika kumi inakuwa ni mahubiri na dakika tano ni kuiombea nchi ili Mungu atuepushe na jambo hili," alisema

Naye Mwakilishi wa Kanisa la Anglikan Mkoani Rukwa Mchungaji Mathias Gwakila alisema kuwa atajitahidi kufikisha ujumbe na elimu aliyoipata kutokana na namna alivyojifunza na kuwasisitiza waumini hao kuendelea kufanya maombi ili kuepukana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa ugonjwa huo ni pepo na hivyo hatunabudi kulikemea na kisha kushauri juu ya kufupisha ibada.

"Hicho ni kitu muhimu mno, ibada ziwe fupi zisiwe ndefu, kwahiyo kwa ushauri wangu kupitia madhehebu mengine yote, viongozi wote wa madhehebu wajitahidi kufupiza, kwa mfano kanisa la Anglican ibada zetu ni masaa mawili, sasa tufupishe, ibada ichukue saa moja katika vipengele vyovyote vile ambavyo wewe utaviona upunguze kipi na kipi ilimradi ibada iwe fupi watu watoke mapema," Alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Ziwa Tanganyika Mchungaji Haruni Kikiwa alisema kuwa kupitia kikao hicho wamepata elimu ya kutosha ya namna ya kuwaelekeza wananchi ambao ni waumini wao juu ya namna ya kupambana na janga la kirusi cha Corona na kusisitiza kuwa atayafikisha kwa askofu ili kusambazwa kwa makanisa.

"Tunachukua hatua za kunawa kabla ya ibada na baada ya ibada, lakini pia hatua za kupunguza muda wa ibada ili kupunguza muda wa waumini kukaa pamoja katika msongamano lakini pia hatua za kupunguza misongamano kwa makanisa makubwa kwa maana wanaweza wakafanyia hata nje ili kupunguza msongamano watu wakae mbalimbali, haya yote nitayafikisha," alisema.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu wakati akieleza namna ya kujikinga na ugonjwa huo alitoa msisitizo kwa viongozi hao kutumia maji tiririka pamoja na sabuni ya maji wakati wa kunawa huku akieleza madhara ya kutumia sabuni ya unga na ya kipande kuwa na tabia ya kushikwa na kila mtumiaji.

"Sabuni ya unga ambayo imechanganywa na maji ikawekwa kwenye chombo maalum kama chupa, kwahiyo mtu anaweza kuitumia hii, tunaepuka kuweka sabuni ya unga kama ilivyo kwamba mtu mmoja achukue na mwingine aje achukue na mwingine achukue, tunaepuka kuweka sabuni ya kipande kwasababu lazima mtu aje aishike akishajipaka arudishe mwengine aje aishike, kwahiyo tunasema ni sabuni ya maji na kama ni sabuni ya unga basi ichanganywe na maji," Alisisitiza.

Wakati akifunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura aliwaomba viongozi hao kuzingatia makubaliano ya kikao hicho na kuongeza kuwa anaamini viongozi wa dini wasingependa waumini wao wateketee na kisha kusisitiza juu ya kupunguza muda wa ibada pamoja na mikusanyiko hasa kwa madhehebu ambayo yana waumini wengi.

"Kuna makanisa ambayo ni madogo sana au misikiti midogo watu wanajua lakini kama mikiti naona wameshajipanga wao wanasali muda mfupi lakini kuna makanisa mengine tunatumia masaa mengi, mkishaingia saa 4 mpaka saa 9 kwahiyo huo ni muda mrefu sana mnaweza mkajichanganya sana, hivyo ninaona kwamba hii kumbunguza mud ani muhimu zaidi, vile vipindi vyetu tuvipunguze zaidi tutoe elimu hasa ya kuwa na imani," Alisistiza
Aidha, alibainisha kuwa kama serikali hawataweza kuwapangia muda wa kufanya inbada hizo huku akiweka msisitizo kuwa imani zinatofautiana na kufafanua kuwa waumini hao wanaweza hata kulala ndani ya makanisa yao kwa kuomba lakini msisitizo ni kuwa wachache ili kuepusha msongamano.


Elimu juu ya Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona itolewe katika Maeneo ya Vijijini.

SALVATORY NTANDU
Wakazi wa mkoa wa Shinyanga wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wananchi wanaokaidi maagizo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee na Watoto juu ya kujikinga na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya  Corona kwa kutonawa mikono kwa maji yaliyowekewa dawa za kuzuia maabukizi ya ugonjwa huo.

Hayo yalibainishwa Machi 28 na  Kisena Mihambo Mkazi wa Igwamanoni katika Halmashauri ya Ushetu mkoani humo baada ya kutembelewa na shirika lisilo la kiserikali la (REDCROSS) lililokuwa linatoa elimu kwa njia ya vipeperurishi na mabango kuhusina na kuchukua tahadhari juu ugonjwa unaosababishwa na virusi vya  Corona.

Alisema baadhi yao wamekuwa wakikaidi kutii maagizo ya serikali kwa kutonawa mikono hali ambayo inaweza kusababisha wakapatwa na maambukizi ya ugonjwa huo pindi utakapojitokesha na kuiomba serikali kupitia maafisa afya wa ngazi ya kata kuwachukulia hatua kali ili waweze kutii maagizo hayo.

"Katika Maeneo yote ya kutolea huduma za kijamii Serikali imeweka ndoo zenye Maji yaliyokwisha wekewa dawa za kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Corona lakini baadhi yetu tumekuwa wagumu kunawa mikono na badala yake tunaendelea kushikana mikono pindi tunaposalimiana",alisema Mihambo.

Zubeda Ramadhani ni Mkazi wa Ntobo katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama alisema endapo wananchi wakihimizwa kwa kupewa elimu sahihi juu ya ugonjwa wa Corona na serikali hususani maeneo ya vijijini itawezakuzuia mlipuko wa virusi vya homa ya Mapafu (Corona).

"Tunaiomba serikali iwashirikishe viongozi wetu wa ngazi za mitaa,vijiji na kata ili kusaidia kuwafikia wakazi wengi hususani wakulima ambao kwa sasa wanaendelea na shughuli za uvunaji wa mazao mashambani ili kuwakinga na maambukizi ya Ugonjwa huo"alisema Ramadhani.

Kwa upande wake Mratibu wa RED CROSS Mkoa wa Shinyanga Samwel Katamba alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la kuwahudumia  watoto Duniani (UNCEF) limewapa jukumu la kusambaza vipeperushi na Mabango nchi nzima kuhusiana na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Corona.

"Tumeweza kuzifikia Halmashauri Sita  za mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Mabango sambamba na kugawa vipeperushi vya ujumbe kuhusiana na ugonjwa huu wa Corona ikiwa ni pamoja na kutumia magari ya Matangazo lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu hii"alisema Katamba.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Ushetu Dk Nichodemas Senguo alisema mpaka sasa wameweza kutembelea kata 20 kwa kuwapatia elimu sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa Corona huku mwitikio wa wananchi ukiwa ni mkubwa.

"Niwatake wananchi wa Ushetu waendelee kuzingatia maelekezo ya Wizara ya afya ya kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kutumia vitakasa mikono (Sanitaizer) sambamba na kuepuka kupeana mikono,pamoja na kujizuia kukaa kwenye mikusanyiko isiyokuwa na ulazima"alisema Dk Senguo.

Mwisho


Taulo Alilotumia Kobe Bryant Katika Mchezo Wake wa Mwisho Lauzwa Kwa Mamilioni

Taulo alilotumia Kobe Bryant katika mchezo wake wa mwisho kuichezea Los Angeles Lakers limeuzwa kwa Sh 76,367,804 katika mnada likinunuliwa na mmoja ya mashabiki wa timu hiyo.

Kobe Bryant alifunga pointi 60 katika mchezo huo ambao Lakers ilishinda 101-96 dhidi ya Utah Jazz

Kama unatabia hii sahau kuhusu kufanikiwa

Watu wanaotaka kufanikiwa huchukulia kushindwa kama hatua ya kuelekea kwenye mafanikio, lakini watu wasioweza kufanikiwa wanapojaribu mara moja au mbili kuvuka kikwazo fulani cha kimaisha na kushindwa hukata tamaa na kutotaka kujaribu tena kusonga mbele.

Wanye tabia ya kushindwa kimaisha hawako tayari kudumu na jambo moja linaloonekana kushindikana kwao kwa muda mrefu. Akiona mwanamke ambaye ni mkorofi kidogo, haraka hukimbilia kumwacha na kutafuta mwingine, mara nyingi si watu wavumilivu.

Akijaribu biashara ya vitumbua kwa wiki moja na akaona havinunuliwi, anaaza kupika maadazi, wiki moja baadaye yuko kwenye mihogo, basi ilimradi ni kuhangaika kusikokuwa na tija katika maisha.



Ukitaka kuwa mmoja kati ya watu wasiweza kufanikiwa kimaisha, basi jaribu kuishi maisha ya kukata tamaa mapema unapofanya mambo.

Mke wa Boss Ananitega...

Kibarua changu kipo hatarini kuota mbawa, anayeniponza ni mke wa boss.
Boss wangu ni mtu mzima kidogo umri umeenda lakini mke wake ni kabinti kadogo alafu bado kabichi kabisa ni kabinti ambako saizi yake ni kijana mchapakazi kama mimi.

Nimeingia kwenye mtihani mzito mimi ni Dereva mara nyingi huwa namchukua na kumpeleka anapotaka tukiwa wawili tu mimi na yeye nguo anazovaa ni full mtego naona hadi pichu ya jana nyeupe, ya leo nyekundu namuheshimu kama boss story anazoniambia ndio zilezile ivi unamke? Mara unamtoto, mara nihamie kwake, tukiwa tunakula mara anikanyage makusudi ilimradi tu visa.

Sasa wikendi ndo ilikuwa balaa badala atoke na mumewe anatoka na mimi aliniambia nimpeleke akaogelee kufika huko ananiambia vua nguo tuoge. Jamaniii! Ni zaidi ya visa kibarua nakipenda lakini ndo hivyo kinaota mbawa. Nikimduu boss akijua si ataniua, achilia mbali kazi ishtoshe mzee mwenyewe pisto kiunoni.

Monday, March 30, 2020

CORONA YABADILI RATIBA YA BUNGE LITAKALOANZA KESHO TANZANIA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Vikao vya Bunge  la bajeti  kuu  vinatarajia kuanza kesho huku utaratibu mpya  ukiwekwa juu ya tahadhari ya Corona ambapo wataruhusiwa kuingia wabunge 150 pekee ukumbini tofauti na  ilivyokuwa hapo awali.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Machi ,30,2020 jijini Dodoma  Spika Wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema kutokana na tahadhari ya Ugonjwa unaotokana na virusi vya corona[COVID-19] idadi ya wabunge watakaokuwa wakiingia ukumbini ni  wasiopungua 150  kati ya wabunge 393 .

Amesema kwa kawaida vikao vya  Bunge huhudhuriwa na zaidi ya watu 700 ukumbini ikijumuisha na watumishi wengine bungeni hivyo kutokana na tahadhari ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona wabunge wengine watakuwa wanafuatilia kupitia Mitandao na watagawanyika katika kumbi mbalimbali zilizopo bungeni.

Aidha,Mhe.Ndugai amesema masaa ya vikao vya bunge yamepunguzwa  ambapo vikao vyote vya bunge vitakuwa vinafanywa kwa masaa yasiyozidi manne kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi jioni isipokuwa siku ya kesho.

Kuhusu Maswali na Majibu bungeni Mhe.Ndugai amesema wabunge watakuwa wanapata fursa ya kuuliza maswali kupitia Mtandao  wa Bunge hivyo hakutakuwa na Maswali ya ana kwa ana pia Maswali ya papo kwa  hapo kwa Waziri mkuu hayatakuwepo.

Katika kupiga kura za Ndiyo au Hapana kuhusu kupitisha bajeti Mhe.Ndugai amesema kura hizo zitapigiwa kupitia mtandaoni ambapo pia amebainisha kuwa Waziri mwenye dhamana husuka atalazimika kujibu swali akiwa anatumia kipaza sauti [mic] cha kwenye kiti alichokalia na hatolazimika kuchangia kipaza sauti kimoja kwa Mawaziri wengi kama ilivyokuwa awali.

Ikumbukwe kuwa katika bunge hili la Bajeti kuu  Jumla ya Maswali 525   yatakuwepo ambapo mkutano huo unaanza Machi 31 ,2020 hadi Juni 30,2020    Bunge  litakapovunjwa kwa ajili ya Uchaguzi mkuu 2020.


Ijue historia ya mwigizaji maarafu nchini india Shahrukh Khan

Novemba 2, 1965 alizaliwa mwigizaji nyota na prodyuza raia wa India maarufu Shahrukh Khan.

Amekuwa akitumia kifupisho cha maneno SRK. Alizaliwa New Delhi nchini India lakini kwa sasa anakaa Mumbai, Maharashtra. Miaka mitano ya kwanza aliishi Mangalore ambapo babu yake alikuwa mhandisi wa meli miaka ile ya 1960. Mwigizaji huyu wa Bollywood amekuwa akichukuliwa na vyombo vya habari kama Mfalme wa Bolywood au Badshah of Bollywood. Shahrukh ameonekana katika filamu zaidi ya 80 huku akipokea tuzo mbalimbali za filamu zikiwamo 14 za Filmfare.

Serikali ya India ilimtunuku tuzo ya Padma Shri ikiwa ni tuzo ya nne yenye hadhi nchini humo. Serikali ya Ufaransa nayo ilimtunuku tuzo ya Ordre des Arts et des Lettres ikiwa ni tuzo ya pili ya heshima nchini humo. Pia serikali ya Ufaransa imewahi kumtunuku tuzo ya tano kwa heshima nchini humo ya Legion of Honour. Khan amekuwa kioo barani Asia na Wahindi wanaoishi nje ya India.

Ufuatiliaji mkubwa wa mashabiki na wapenzi wa filamu zake umempa mapato makubwa, hivyo amekuwa akichukuliwa kuwa ni miongoni mwa nyota wa filamu mwenye mafanikio zaidi duniani. Shahrukh Khan alianza kuonekana katika filamu mwishoni mwa miaka 1980. Mnamo mwaka 1992 alitoa filamu yake ya kwanza ya Deewana.

Pia katika filamu ya Darr (1993), Baazigar (1993) na Anjaam (1994). Baada ya hapo alianza kuonekana zaidi katika kipengele cha mapenzi kwa wafuatiliaji wake nchini Tanzania alipewa jina la 'Mzee wa Malavidavi.' Filamu zake kama Dilwale Dulhania Le Jayenge (1995), Dil To Pagal Hai (1997), Kuch Kuch Hota Hai (1998), Mohabbatein (2000) na Kabhi Khushi Kabhie Gham... (2001); zilimpa umaarufu mkubwa.



Ameigiza filamu nyingi na amekuwa msaada mkubwa kwa wasanii wengi wakiwamo Deepika Padukone na Shilpa Shetty. Mnamo mwaka 2008 Jarida la Newsweek lilimtaja kama mtu wa tano mwenye nguvu duniani. Mnamo mwaka 2011 alitunukiwa tuzo na Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa kuunga mkono elimu kwa watoto ambapo alitunukiwa tuzo ya Pyramide con Marni. Amekuwa na ushawishi mkubwa katika kukuza utamaduni wa Kihindi.

Aika, Nahreel Karantini Siku 14

MEMBA wawili wa Kruu ya Navy Kenzo, Aika Marealle na Emmanuel Mkono 'Nahreel' wamejiweka karantini kwa siku 14 sasa kujikinga na maambuziki ya Virusi vya Corona vinavyosababisha Ugonjwa wa COVID-19.

Aika ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, walivyosikia tu virusi hivyo vimeingia Bongo, waliamua kujiweka karantini kwa kujifungia ndani kwao na watoto wao wawili wa kiume, Gold na Jamaica.

"Tunaogopa sana ukizingatia tuna watoto wadogo, tumeamua kujifungia na hatutoki hadi tusikie janga hili (Virusi vya Corona) limepita," alisema Aika ambaye kuna tetesi kuwa ana ujauzito mwingine wa mtoto wao wa tatu.

Corona: Bodaboda Aliyeuawa Alimpeleka Mjamzito Hospitali

Familia moja nchini Kenya yataka haki itendeke baada ya kifo cha Khamisi Juma Bega (49), bodaboda ambaye alipigwa na polisi hadi kufa.

Inadaiwa Khamisi alipigwa na maafisa wa polisi wakishinikiza kufuatwa kwa sheria ya kubaki ndanii kwa kipindi hiki chenye tishio la #Covid19.

Ijumaa, siku ya kwanza ya zuio la kutoka nje, Khamisi alipigiwa simu na mteja wake mjamzito, aliyetarajia kujifungua hivi karibuni. Mjamzito huyo alimuomba Khamisi ampeleke hospitali, ambako alikutwa na mkasa huo.

Ilikuwa ni majira ya saa moja na nusu usiku alipokuwa akirudi kutoka hospitali, alikutana na maaskri waliokuwa kwenye doria. Inasemekana alipigwa na hakuweza kupatiwa matibabu kwa usiku huo na alipaswa kutulia hata kesho yake, Khamisi alifariki kutokana na majeraha hayo.

Polisi wamekataa madai hayo, kamanda wa Polisi Francis Mguli amesema watachunguza tukio hilo. Wakazi wameomba IGP awaatahadharisha polisi kwenye kutumia nguvu katika kutekeleza agizo.

Huu Ndio Ukweli Sahihi Kuhusu Elimu Uliyonayo

eLIMU
Ni utaratibu wangu ambao niliuona unafaa sana katika Maisha yangu, kwani umeweza kuyabadili sana maisha Yangu kwa kiwango cha hali ya juu sana,  sitaki kujisifia wala kujipaka mafuta kwa mgongo wa chupa maana nitakuwa najidanganya mwenyewe, ila huo ndo ukweli wenyewe, najua bado una zungusha akili yako huku na huko bila kujua ni nini ambacho nitakuwa nazungumzia je ni utaratibu upi? wala Usipate tabu ni utaratibu wa kujifunza vitu vipya Kila wakati.

Inawezekana ukawa unashangaa nawezaje kufanya hivyo? Wala usipate tabu leo nitakueleza ukweli kwani mara baada ya kugundua ya kwamba hatma ya Mafanikio yangu, ipo kwenye mandishi  hivyo nikashuru kimoyomoyo yule ambaye alinifundisha kusoma, kuhesabu na kuandika kwa kunijengea msingi imara ambao ndio nguzo kubwa ya Maisha ya kila mmoja wetu  katika dunia yenye kila aina ya kila kitu, hivyo kazi ni kwako ni aina gani ya vitu ambavyo unavihiitaji katika dunia hii.

Na Kuna wakati huwa inafika pahala naona ni vyema ni bora usinipe chakula kwanza, ila unipe vitu vya kusoma kwanza ambayo vitasaidia kwa namna moja ama nyingine. Sitaki pia kukwambia na wewe usome peke yake vitu ambavyo vitakusaidia katika maisha yako, la hasha kusoma peke yake haitoshi ila jambo la msingi ni kuweza kusoma yale ambayo uliyasoma kuyaweka katika matendo.

Suala hili na kugeuza kile ambacho umekisoma na kukiweka katika matendo ni suala gumu sana, kuwepo kwa hali hii ndiko ambako kunasababisha  kuwe na wimbi kubwa la watu ambao ni wazuri sana katika kulalamika tu kuliko kufikiri ni namna gani ya kubadili ambacho unakijua kuweka kwenye matendo.

Labda inawezekana ya kwamba bado unalalamika ya kwamba hakuweza kupata elimu kwa kiwango ambacho ulihitaji, lakini nikutie moyo kwa kukwambia ya kwamba elimu ambayo unayo inatosha kabisa, kuweza kubadili historia mpya ya maisha yako leo endapo , utaamua kuutafuta undani wako ni upi? Nimesema hivyo kwa sababu elimu yeyote ambayo uliyonayo huwa ina faida zaidi ya kumi lakini leo naomba kueleze faida kubwa tatu tu hii ni kutokana na muda ambao ninao siku ya leo.

Faida ya elimu yeyote uliyona Ni vyema itakusaidia kufanya yafuatayo;

1. Kujua
Elimu yeyote ile ambayo unataka kuipata, au umekwisha kuipata ni lazima ikusaidie kufahamu mambo mbalimbali, baada ya kujua ukweli wa mambo hayo ni Lazima ufikirie ni jinsi gani unaweza kuugeuza ujuzi huo kuwa bidhaa. Yamkini ukawa bado unalalamika kwamba suala la ajira ni suala gumu kwako lakini jiulize ya kwamba  ujuzi ulio nao unawezaje kuwa bidhaa? baada ya kupata majibu ndipo utapojua ni kitu gani ambacho namaanisha.

2.kutenda
Hili ni suala la msingi sana, ambalo ni vyema kulifahamu siku ya leo. Watu wengi wanafahamu mambo mengi sana, lakini ukakasi huwa unakuja katika kutenda. Lakini kabla sijaweka nukta siku ya leo nikwambie ya kwamba maisha ni leo, wala sio jana wala kesho. Nimesema Maisha ni leo kwa sababu Maisha yako yatabadilika kama unataamua kutenda leo, na mara kadhaa nikwambie ya kwamba tuyakumbuke yale maneno mazuri ambayo yanasema ngoja ngoja yaumiza matumbo, na chelewa chelewa utakuta mtoto sio wako hivyo nikusihi amua sana kuanza kutenda jambo lako ili uweze kutimiza ndoto zako.

3. Kushirikiana pamoja.
Hii ni faida nyingine ambayo itakufanya wewe kuweza kuwa bora zaidi kila mara. kuweza kuwashirikisha mawazo yako watu wengine ili kuweza kupata majibu ya maswali yako na hatimaye kutimiza Ndoto kubwa uliyonayo. Usipende kufanya vitu peke yako. Ubinafsi ndio umaskini wako, hivyo kila wakati ni vyema ukajua namna katika kuwaongezea thamani  watu wengine. Maana kama hautajua kuwaongezea watu wengine thamani na wao hawataweza kukuongezea thamani pia.

Kufanya kazi kwa ushirikiano ni njia bora sana katika kufanikisha malengo yako. Maana ushirikiano na Mafanikio na utengano ni udhaifu. Lakini kabla sijamaliza labda nikumbushe ya kwamba ni lazima uweze kushirikiana na watu sahihi kwa kila jambo lako.

VIDEO: Wagonjwa wa Corona waongezeka Tanzania, wafikia 19


Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema wagonjwa wa corona nchini Tanzania wamefikia 19, baada ya watano kuongezeka leo Jumatatu Machi 30, 2020.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Jiko la mkaa lasababisha vifo vya wanafamilia wanne


Watu wanne wamefariki dunia katika Kitongoji cha Ngilimba B, Halmashauri ya Ushetu, Shinyanga baada ya kuvuta hewa yenye sumu iliyotokana na mkaa waliouwasha kwenye jiko na kisha kuliweka ndani ya nyumba yao ili kujikinga na baridi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amesema watu hao ni wanafamilia ambapo waligundulika wamefariki baada ya kuvuta hewa hiyo wakiwa wamelala.

Kamanda Magiligimba amewataja waliofariki kuwa ni Masanja Emmanuel (35) ambaye ni baba wa familia hiyo, Mngole Masanja (25) mkewe, Holo Masanja,(05) na Matama Masanja (03) wote wakazi wa Ngilimba. "Tukio hili limesababishwa na mvua iliyonyesha Machi 27 iliyoambatana na baridi kali ndipo marehemu hao waliamua kulala na jiko la mkaa ndani ya nyumba yao na kusababisha mgandamizo wa hewa kuwa mdogo uliosababisha wavute hewa yenye sumu ya carbon monoxide,"amesema Magiligimba.

Miili ya marehemu hao imekabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.

Mama Mwenye Nyumba Anataka Kuniozesha Mwanae Kinguvu Nguvu


Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Mimi ni mpangaji nimepanga nyumba moja hapa mjini na nina kama miezi sita kwenye hii nyumba niliyopanga ambayo mpangaji ni mimi mwenyewe mama mwenye nyumba ni mjane yaani single mother na ana watoto watatu wote wa kike.

Kinachonisukuma kuomba ushauri hapa ni nyenendo za huyu mama na binti yake mmoja yule wa pili, yaani huyu mama anaforce mwanae nimuoe yaani niishi nae gheto kwangu niwe nalala naye na kuamka naye.

Kila chakula kikiiva naletewa nguo nafuliwa na hadi maji bafuni napelekewa na wanafanya yote haya si kwamba mimi nataka hapana ni kwa lazima, yaani chakula unaletewa ki nguvu nguvu kama ni wali unakuwa hadi ushamwagiliziwa maharage na mchuzi sasa kwa mazingira haya ni vigumu sana kukataa.

Jana binti kaja usiku kuniletea msosi na hakurudi tena ndani kwao akabaki hadi asubuhi, mimi leo nimeondoka kwenda kazini nimemuacha gheto nimerudi nimekuta kapika chakula chetu wawili tofauti na chao kile cha kwa mama yake.

Sasa kwa staili hii ya kuja gheto Jana usiku na leo nimemkuta kapika si tiari nishakabiziwa mzigo hivi.

Ushauri wenu nifanyaje? Nihame hii nyumba au nifanye nin?


LONDON BABY

Zitto Ataka Bunge, Mahakama Kusitishwa Kujikinga Dhidi Ya Corona


Waitara na Zitto Kabwe Moto Unawaka Bungeni, Pilipili imetiwa ...Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametaka vikao vya bunge la bajeti kuhairishwa kwa muda mpaka mwenzi Mei ili kuzuia ueneaji wa virusi vya Corona vinavyosabaisha ugonjwa wa Covid9

Zitto ametoa ujumbe huo kwenye barua yake alimuandiia rias wa jamhuri ya muungano ww Tanznaia ikiwa ni sehu myanushauri kwa serikali juu ya ugonjwa huo uliua zadia ya watu 19,000 dunia kote

"Nimeuomba Mheshimiwa rais kwa heshima kubwa kabisa haua zichukuliwa kusimaisha vikao vyote vya serikali mahakama na kadhalika bunge linaweza kukutana mwezi Mei tukiondokana na janga hili tukajadili bajeti ya serikali kwa mwezi mmoja tukamaliza naomba kusisitisha jambo hili tusitoe picha mbaya kwa watoto tuliowarusha nyumbani,lakini wanatuona wazazi wao tukiendela na mikusanyiko  nimeomba mheshimiwa rais yeye kama mkuu wa nchi akionekana hajali picha inayotoka kwa nchi ni kwamba ugomjwa huu ni poa tu" amesema Zitto 

Aidha Zitto amesema kuwa anafahamu kuwa wananchi wengi wa Tanzania ni lazima waaamke asubih ili wanendele kupata chakula cha kila siku lakini ameshauri wakati kama huu shuguli hizi za kawaida zisimamishwe kwa muda ili kuzia ugonjwa huu kuenea zaidi

RC Mghwira afanya ziara ya kutembelea makanisa

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira amefanya ziara ya kutembelea baadhi ya makanisa mjini Moshi kufuatilia endapo tahadhari zilizotolewa na Serikali zinatekelezwa.

Dkt Mghwira ametembelea Makanisa ya Kristo Mfalme(RC), Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT)usharika wa Moshi mjini ,kanisa la Pentekosti (TAG) Moshi na Kanisa la Anglikana.

Jifunze namna ya kutenda wema kwa wengine


Kisa cha baba ambae alikuwa akitembelea mashambani na mwanawe. Katika kutembea kwao wakakuta kiatu kimoja chakavu ambacho anaonekana mwenyewe ni masikini sana.

Mwana  akamwambia Baba yake, unaonaje kama tutamfanyia mzaha huyu mwenye kiatu, tukifiche hiki kiatu kisha sisi wenyewe tujifiche halafu tuangalie mwenyewe akirudi atafanyaje ili tumcheke?

Yule  Baba akamjibu "Hatutakiwi kujifurahisha kwa kuwaudhi wengine" lakini wewe kijana wangu ni tajiri unaweza kufanya kitu kikakufurahisha wewe mwenyewe na kikamfurahisha huyu bwana mwenye kiatu pia."

Kijana akamuuliza baba yake kivipi!?
Baba akamwambia;Badala ya kukificha kile kiatu, unaweza kukiacha palepale na ukaingiza pesa ndani yake.Kisha tujifiche ili uone athari yake.

Mwana  akafurahishwa na rai ya  Baba yake na akafanya kama alivyoelekezwa, kisha  wakajificha nyuma ya miti.

Sio muda mrefu akarudi yule masikini ili achukue kiatu chake. Tahamaki anakuta pesa ndani ya kiatu kile na pesa kama ile katika kiatu kingine.

Akaziingiza pesa mfukoni na akapiga magoti kusujudu hali yakuwa ni mwenye kulia, kisha akamwambia Mungu kwa sauti ya juu : "Ninakushukuru Ewe Mungu wangu, Ewe ambae umejua kwamba mke wangu ni mgonjwa na wanangu wana njaa hawana mkate, ukaniokoa mimi na watoto wangu."

Kijana wa tajiri aliathirika sana kwa kuona huruma zaidi na macho yake nayo yakajaa machozi ya furaha kuona amemsaidia mtu mwenye uhitaji.

Hapo ndipo yule  Baba akamwambia nwanawe  "huoni kwamba sasa una furaha zaidi kuliko vile ulivyotaka kufanya mwanzo"?
Mwana  akajibu nimejifunza  Na  sitoisahau muda nitakao kuwa hai.

Hivi sasa nimejifunza kitu kwamba ukitoa utakuwa na furaha zaidi kuliko ukizuia au ukichukua.
Baba akasema kama hivyo ndivyo basi unatakiwa ujue kwamba,  kutoa ni SADAKA na kuna namna nyingi.

Kumsamehe mtu pamoja na uwezo wa kumuadhibu unao ni  SADAKA .
Kumuombea dua ndugu yako bila yeye mwenyewe kujua ni  SADAKA.
Kumpa ndugu yako udhuru na ukamuondolea dhana mbaya ni  SADAKA .
Kumchungia heshima ndugu yako  wakati hayupo ni  SADAKA .


kushare ujumbe huu na ndugu zako pia ni  SADAKA .

Source

JIKO LA MKAA LAUA BABA,MAMA NA WATOTO WAKIJIKINGA NA BARIDI YA MVUA KAHAMA



Nyumba ambayo marehemu walikuwa wamelala

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuvuta ya hewa yenye sumu ya Carbon monoxide iliyotokana na mkaa waliowasha kwenye jiko la mkaa kisha kulala ndani ya nyumba yao wakijikinga na baridi iliyotokana na mvua kubwa katika kitongoji cha Ngilimba 'B' kijiji cha Ngilimba kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 28,2020 ambapo ndugu hao wa familia moja waligundulika kuwa wamefariki dunia wakiwa nyumbani kwao wamelala baada ya kuvuta hewa yenye sumu ya Carbon Monoxide. 

"Chanzo cha tukio hilo ni kwamba siku hiyo mvua kubwa ilinyesha kijijini hapo na kupelekea uwepo wa baridi nyumbani kwa marehemu hao na ndipo wakati wakijiandaa kulala waliacha jiko la mkaa likiwa limewashwa ndani ya nyumba na kufunga mlango na dirisha hali iliyopelekea mgandamizo wa hewa kuwa mdogo ndani ya nyumba yao na kuvuta hewa hiyo iliyokuwa na sumu ya carbon monoxide",amesema Kamanda Magiligimba. 

"Waliofariki dunia ni Masanja Emmanuel (35) ambaye ni baba wa familia hiyo  na mkewe Mngole Masanja (25), Holo Masanja,(05) na Matama Masanja (03) wote wakazi wa Ngilimba wote wa familia moja",ameeleza Kamanda Magiligimba 

Amesema miili ya marehemu imekabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.

Mfanyabiasha Afariki Dunia Kwa Mshtuko Wa Kuunguliwa Maduka Samunge Jijini Arusha




Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mtu mmoja amefariki dunia Mara baada ya moto mkubwa kuzuka na kuunguza soko la Samunge jijini Arusha baada ya kufika na kushuhudia maduka yake yote yakiwa yameketea na moto.

Akiongea na waandishi wa habari Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo 

Aidha wakati zoezi la kuzima moto likiendelea mtu  mmoja aliyefahamika kwa majina ya James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda vilivyoungua ndani ya Soko hilo, alifika eneo hilo na kukuta vibanda vyake vimeungua.

Kaimu kamanda Koka  alieleza kuwa majira ya saa 23:30hrs, katika soko la Samunge, lililopo Mtaa wa NMC, kata ya Kati, Tarafa ya Themi, katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana uliwaka na kuteketeza vibanda vya Soko hilo ambavyo idadi na thamani yake bado haijajulikana. 

Ameeleza kuwa vibanda hivyo vilikuwa vinamilikiwa na wafanyabiashara wa Soko hilo ambavyo vilijengwa kwa Mabati, Mbao na Mabanzi. Mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Wananchi walifanikiwa kuzima moto huo ambao haukuleta madhara kwa binadamu. 

Mtu huyo alipata mshtuko na kuanguka chini na kuzimia ambapo alichukuliwa na kupelekwa katika Hospital ya Mkoa ya Mount Meru na alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu. 

Hata hivyo Uchunguzi unaendelea ili kubaini thamani halisi ya mali zilizoungua pamoja na chanzo cha moto huo. 

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa Daktari. 

Natoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona majanga kama haya ya moto kwa Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kudhibiti matukio kwa haraka kabla ya kuleta madhara makubwa. 

 Alitoa wito kwa wananchi na kuwaomba  pamoja na wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya Ulinzi na Usalama vikifanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo halisi cha tukio hilo

Sunday, March 29, 2020

Zitto amuandikia barua JPM kuhusu Corona




Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu janga la virusi vya Corona linalosambaa duniani hivi sasa. 

Akisoma na kufafanua ujumbe huo katika mkutano na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Zitto amesema kuwa yeye na chama chake wameamua kumuandikia barua Rais Magufuli kwakuwa janga hilo ni kubwa, hivyo kuna haja ya kushirikiana kwa pamoja na Serikali. 

"Nimemuandikia barua rasmi mhe. Rais Magufuli kuhusiana na mapendekezo yangu na ya chama changu cha ACT wazalendo juu ya namna bora ya kudhibiti na kukabiliana na virusi vya Corona hapa nchini", amesema Zitto. 

"Rais na Serikali yake wametangaza hatua za kupunguza kasi ya virusi hivi zikiwemo wananchi kujizuia na mikusanyiko isiyo ya lazima, kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni pamoja na kuundwa kwa kamati 3 za baraza la mawaziri kuratibu mpango mzima. Hatua hizi ni za kupongezwa", ameongeza. 

Kuhusu mapendekezo aliyoyatoa, Zitto amesisitiza umoja kwa Watanzania wote bila kujali itikadi ya chama, dini wala makabila, huku akimuomba Rais Magufuli kuanzisha kampeni ya kupima virusi vya Corona nchi nzima. 

"Kama kuna jambo ninalolisisitiza kwa ukubwa wake basi ni kupima kupima kupima, lakini jambo lingine ni kuwepo kwa uwazi wa maambukizi mapya, wagonjwa mahututi na vifo vinavyotokana na ugonjwa huu. Nimemnasihi Mhe. Rais kwamba tusiongope kuwa wawazi kuhusu jambo hili kwa sababu uwazi una faida kubwa kuliko kuficha", amesema Zitto.

Ngoma Mpyaa : MWANASELEWA Ft NTEMI 'Ng'wana Kang'wa' - MILEMO

Nakualika kutazama video mpya kutoka kwa Mwana Selewa amemshirikisha Ntemi 'Ng'wana Kang'wa' kutoka Kahama Mkoani Shinyanga inaitwa Milimo...Tazama Video hapa chini

Nimeridhishwa na maandalizi ya kituo - Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea eneo lililotengwa kwa ajili kuwahudumia watu watakaobainika kuwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) na amesema ameridhishwa na maandalizi.

Aliyasema hayo jana (Jumamosi, Machi 28, 2020) wakati akizungumza na wananchi wilayani Kibaha, Pwani baada ya kukagua hospitali ya wilaya ya Kibaha ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu watakaogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Alisema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabilia na COVID-19, ambapo kwa sasa watu wote wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege, vituo vya mabasi na bandari lazima wapimwe na wakigundulika wanamaambukizi wanawekwa kwenye maeneo maalumu kwa muda wa siku 14.

"Tunazingatia sana wale wanaotoka kwenye nchi ambazo zimeathirika sana wakiingia hapa Tanzania tunawazuia kwanza, tunawapima na tunafuatilia historia yake anatoka wapi na tunaangalia katika siku 14 amepita kwenye nchi zipi."

Waziri Mkuu alisema wawaweka kwenye maeneo maalumu ili kuweza kuwapima kila siku na kujirishika kama hawana maambukizi kwani mtu anaweza kupimwa leo akaonekana yuko vizuri lakini ana maambukizi ambayo bado hayaonekani kwenye vipimo. Kama katika kipindi cha siku 14 mtu atabainika hana maambukizi anaruhusiwa kwenda kujiunga na familia.


Pia, alisisitiza wananchi waendelee kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuzuia mikusanyiko na kwa wale wanaosafiri kwenye usafiri wa umma wasibanane kila mtu akae kwenye kiti.

Waziri Mkuu alisema wananchi wanapokwenda kufuata huduma kwenye masoko wahakikishe wanapeana nafasi baina ya mtu mmoja na mwingine na kabla hawajaingia katika maduka wanawe mikono kwa sabuni na maji tiririka ili kujikinga na maambukizi ya corona.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kuwachukulia hatua watu wote wanaopotosha kuhusu taarifa za ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). "Aliyetangaza kuwa shule zinafunguliwa tumeshamkamata na atachukuliwa hatua."

Hivyo aliwataka wananchi wajihadhari na taarifa zinazotolewa na watu ambao si wasemaji rasmi. Alisema taarifa kuhusu virusi vya corona itatolewa na Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Msemaji wa Serikali.

VIDEO: Mfanyabiashara afariki kwa presha baada ya kushuhudia mali zake zikiteketea kwa moto soko la Samunge


Jeshi la Polisi jijini Arusha limetoa taarifa ya athari zilizojitokeza baada ya kutokea ajali ya moto katika Soko la Samunge jijini hapo.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Korea Kaskazini yafyatua baharini Makombora Mawili

Korea Kaskazini imefyatua leo kile kilichoonekana kuwa ni makombora mawili ya masafa mafupi katika pwani yake ya mashariki, ikiwa ni jaribio la nne la aina hiyo katika mwezi huu wakati ulimwengu ukipambana na janga la virusi vya corona. 

Taarifa ya pamoja ya Wakuu wa Jeshi la Korea Kusini imesema makombora mawili yalifyatuliwa kuelekea mashariki kutokea mji wa bandari wa Wonsan na kuanguka katika Bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Mashariki. 

Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema makombora hayo hayakuvuka mipaka yake ya baharini au kufika katika kanda ya kipekee ya kiuchumi ya nchi hiyo. 

Korea Kaskazini wiki moja iliyopita ilifyatua makombora mawili ya masafa mafupi. 

Siku moja baadaye, chombo cha habari cha nchi hiyo yenye silaha za nyuklia kikatangaza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alimtumia barua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ikielezea kwa kina mpango wa kukuza mahusiano. 

Credit: DW


VIDEO: Hadi huruma, mfanyabiashara azimia baada ya kushuhudia mali zikiteketea kwa moto soko la Arusha


Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo la Samunge jijini Arusha limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Machi 29 ambapo mmoja ya wafanya biashara amezimia baada ya kushuhudia mali zake zikiteketea kwa moto.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Saturday, March 28, 2020

Aurlus Mabele hatimaye azikwa

MWILI wa nyota wa zamani wa kundi la Loketo, Aurlus Mabele hatimaye umehifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele, baada ya kufariki dunia wiki iliyopita nchini Ufaransa.

Mabele aliyekuwa na umri wa miaka 66, alikumbwa na mauti Machi 20 kutokana na kukumbwa na virusi vya covid-19 zinavyosababisha ugonjwa wa corona na alizikwa jana Ijumaa nchini Ufaransa.

Kwenye mazishi hayo yalishirikishwa wanandugu wachache wakiwamo wanafamilia pekee kutokana na sakata la ugonjwa wa corona ambao umekuwa tishio kwa sasa dunia.

Mabele aliyezaliwa Congo Brazzaville, anakumbukwa kwa umahiri wake wa kutunga na kuimba akipitia makundi mbalimbali, lakini umaarufu zaidi akiwa na Loketo Group lililotamba na nyimbo mbalimbali zilizomtangaza yeye na memba wenzake akiwamo Dibla Dibala na wengine.

Kifo chake kilitangazwa na mwanae wa kike ambaye naye ni mwanamuziki, Liza Monet, ikiwa ni miaka kadhaa tangu alipokuwa akiugua kansa ya koo iliyomfanya awe nje ya fani kwa muda mrefu.

Source

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Atakiwa Kujiuzulu



Inaelezwa mnamo Januari 23, 2020, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus alikataa kutangaza mlipuko wa virusi vya #COVID19 kama janga la dharura ya kiafya duniani

Idadi ya walioambukizwa na vifo imeongezeka kwa kiwango kikubwa sana na kupelekea Tedros Ghebreyesus kuonekana hafai kuendelea na jukumu lake kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo

Wananchi wanahamasishana kusaini 'petition' ya kuushinikiza Umoja wa Mataifa kumuondoa Mkurugenzi huyo kwenye wadhifa wake kwa kushindwa kudhibiti #COVID19 mapema


WANAKIJIJI 6 WANUSURIKA KUFA KWA KUSHAMBULIWA NA FISI WALIYEMZINGIRA WAMUUE SHINYANGA

Picha haihusiani na habari hapa chini
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watu sita wamenusurika kufa kwa kushambuliwa na fisi baada ya kumzingira wakitaka kumuua katika kijiji cha katika kijiji cha Mwangh'alanga, kata na tarafa ya Samuye, wilaya na mkoa wa Shinyanga. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Ijumaa Machi 27,2020 majira ya saa nne. 

"Chanzo cha tukio hilo ni watu hao kuvamiwa na fisi huyo baada ya kumzingira wakitaka kumuua. Hata hivyo wananchi walifanikiwa kumuua fisi huyo",amesema Kamanda Magiligimba. 

Amewataja waliojeruhiwa kujeruhiwa na fisi kwa kung'atwa maeneo mbalimbali ya miili yao katika tukio hilo kuwa ni Zengo Jitonja , Nkuba Deteba , Juma Salaganda, Limbu Mihambo , Dutu Mdese na John Matana wote wakazi wa kijiji cha Mwangh'alanga Samuye 

Amesema majeruhi watano kati yao wamepata majeraha madogo madogo na hivyo wamepatiwa matibabu hospitalini na kuruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri. 

"Majeruhi mmoja Zengo Jitonja (56), amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa Shinyanga baada ya kujeruhiwa na fisi huyo mikononi na mdomoni na hali yake siyo mbaya sana",ameongeza Kamanda Magiligimba.

WAGONJWA WA CORONA WAONGEZEKA UGANDA NA KENYA, WAWILI WAPONA

Kenya imethibitisha visa saba zaidi vya maambukizi ya ugonjwa wa coronavirus, huku Uganda ikiandikisha visa vingine vitano vya ugonjwa huo hatari.

Akizungumza katika kikao na wanahabari siku ya Jumamosi, waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amesema kwamba idadi hiyo inaongeza visa vya maambukizi nchini Kenya kufikia 38, huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki naye mwingine akipona maambukizi hayo.

Waziri Kagwe amesema kwamba kufikia sasa mji mkuu wa Nairobi unaongoza kwa maambukizi ya visa 28.

Amesema kwamba kati ya visa hivyo saba kuna Wakenya wanne raia wawili wa DR Congo na raia mmoja wa China.


Ameongezea kwamba idadi hiyo ni miongoni mwa watu 81 ambao walifanyiwa vipimo katika maabara tofauti nchini katika kipindi cha saa 24.
Amesema wanne kati ya visa hivyo ni watu wenye historia ya kusafiri katika mataifa yenye idadi kubwa ya maambukizi huku mmoja akiripotiwa kusafiri hadi Mombasa nao wengine wawili wakiambukizwa na visa vya awali.

Vilevile waziri huyo alikuwa na habari njema pale aliposema kwamba wagonjwa wawili waliokuwa wakiugua virusi hivyo wamepona.

''Mgonjwa wetu wa kwanza na watatu wamepona virusi hivyo , watafanyiwa vipimo vingine katika kipindi cha saa 48 , tuna matumaini kwamba vipimo hivyo vya pili vitabaini kwamba wamepona kabisa ili kuruhusiwa kutoka katika vituo vyetu vya tiba'', alisema.

Amesema kwamba visa vyote saba vinatoka katika kaunti ya Nairobi ikiwa ndio inayoongoza , ikifuatiwa na kilifi visa 6, Mombasa visa 2 huku kajiado na Kwale zikiwa na kisa kimoja kila moja.

Aidha waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kujitenga akisema mwanae na mpwa wake wametengwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.


''Mimi mwenyewe nina mwanangu ambaye amewekwa karantini . Pia nina mpwa wangu ambaye amewekwa karantini . Tunachosisitiza ni kwamba wakati mtu anapowekwa katika karantini anajilinda yeye na maisha ya wengine'', alisema Kagwe bila kutoa maelezo zaidi.

Wakati huohuo Idadi ya watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda imeongezeka na kufikia 23 kutoka 18 baada ya watu wengine watano kukutwa na maambukizi siku ya Ijumaa.

Kati ya sampuli 227 zilizofanyiwa vipimo siku ya Ijumaa watu 222 hawakupatikana na virusi vya corona huku watu watano wakipatikana na ugonjwa huo, alisema Dkt. Jane Ruth Aceng katika chapisho lake la mtandao wa twitter.

''Waganda tafadhalini fuateni maelezo na mikakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivi. Tunaweza kuzuia maambukizi ya virusi hivi pamoja'', alisema afisa huyo.
Hata hivyo Aceng hakutoa maelezo ya watu walioambukizwa.

Rais Museveni alisema kwamba kutokana na visa hivyo vipya huenda kukawa na umhimu wa kuchukua hatua kali zaidi ili kuzuia maambukizi kulingana na ujumbe wa twitter uliotumwa na katibu wake wa maswala ya habari bwana Don Wanyama .

Maafisa wa afya wanasema kwamba watu wote 14 waliothibitishwa hapo awali kuwa na virusi hivyo wanaendleea vyema katika hospitali ya Entebbe Grade B , Hospitali ya Mulago na hospitali kuu ya Adjumani.

CHANZO:BBC SWAHILI

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...