Monday, March 30, 2020

Ijue historia ya mwigizaji maarafu nchini india Shahrukh Khan

Novemba 2, 1965 alizaliwa mwigizaji nyota na prodyuza raia wa India maarufu Shahrukh Khan.

Amekuwa akitumia kifupisho cha maneno SRK. Alizaliwa New Delhi nchini India lakini kwa sasa anakaa Mumbai, Maharashtra. Miaka mitano ya kwanza aliishi Mangalore ambapo babu yake alikuwa mhandisi wa meli miaka ile ya 1960. Mwigizaji huyu wa Bollywood amekuwa akichukuliwa na vyombo vya habari kama Mfalme wa Bolywood au Badshah of Bollywood. Shahrukh ameonekana katika filamu zaidi ya 80 huku akipokea tuzo mbalimbali za filamu zikiwamo 14 za Filmfare.

Serikali ya India ilimtunuku tuzo ya Padma Shri ikiwa ni tuzo ya nne yenye hadhi nchini humo. Serikali ya Ufaransa nayo ilimtunuku tuzo ya Ordre des Arts et des Lettres ikiwa ni tuzo ya pili ya heshima nchini humo. Pia serikali ya Ufaransa imewahi kumtunuku tuzo ya tano kwa heshima nchini humo ya Legion of Honour. Khan amekuwa kioo barani Asia na Wahindi wanaoishi nje ya India.

Ufuatiliaji mkubwa wa mashabiki na wapenzi wa filamu zake umempa mapato makubwa, hivyo amekuwa akichukuliwa kuwa ni miongoni mwa nyota wa filamu mwenye mafanikio zaidi duniani. Shahrukh Khan alianza kuonekana katika filamu mwishoni mwa miaka 1980. Mnamo mwaka 1992 alitoa filamu yake ya kwanza ya Deewana.

Pia katika filamu ya Darr (1993), Baazigar (1993) na Anjaam (1994). Baada ya hapo alianza kuonekana zaidi katika kipengele cha mapenzi kwa wafuatiliaji wake nchini Tanzania alipewa jina la 'Mzee wa Malavidavi.' Filamu zake kama Dilwale Dulhania Le Jayenge (1995), Dil To Pagal Hai (1997), Kuch Kuch Hota Hai (1998), Mohabbatein (2000) na Kabhi Khushi Kabhie Gham... (2001); zilimpa umaarufu mkubwa.



Ameigiza filamu nyingi na amekuwa msaada mkubwa kwa wasanii wengi wakiwamo Deepika Padukone na Shilpa Shetty. Mnamo mwaka 2008 Jarida la Newsweek lilimtaja kama mtu wa tano mwenye nguvu duniani. Mnamo mwaka 2011 alitunukiwa tuzo na Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa kuunga mkono elimu kwa watoto ambapo alitunukiwa tuzo ya Pyramide con Marni. Amekuwa na ushawishi mkubwa katika kukuza utamaduni wa Kihindi.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...