Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka wafugaji nchini kuhakikisha kuwa wanachukua tahadhari juu ya virusi vya homa ya Mafamu Covid -19 ambavyo vinasababisha Ugonjwa wa Corona.
Akizungumza na wafugaji mara baada ya kutembelea minada ya mifugo katika soko la kimataifa la mifugo lilipo wilayani longido pamoja na mnada wa Miserani,uliopo wilayani monduli mkoani Arusha,Ulega alisema kuwa tahadhari ni muhimu kuchukuliwa na kuhakikisha kuwa wafugaji na wafanyabishara wanawana mikono.
Aidha alisema kuwa pindi biashara ya mifugo inapofanyika ili kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima ni vyema wafugaji wakarejea majumbani ili kujikinga na gonjwa hilo.
Katika hatua nyingine naibu waziri Ulega alitembelea kituo cha wizara ya mifugo na uvuvi kilichopo katika boda ya namanga na kuzungumza na maafisa hao,ambapo alisema kuwa serikali imeruhusu biashara kufanuyika kama kawaida hivyo waisaidie serikali katika eneo hilo.Alisema ni lazima biashara na shughuli za kiuchumi ziendelee ili serikali ipate mapato, huku familia zipate mahitaji yao muhimu.
"Hatuwezi kufunga minada hii sababu maisha ya watanzania walio wengi huishi kwa kutafuta mlo a kila siku, hivyo kuzuia minada hii ni sawa na kuataka wafe kwa njaa, sasa hili serikali tumelitafakari ka kina na tumeona haifai kuifunga minada hii,"alisema.
"Ninachosisitiza hapa kwenye minada hii wawepo tu wale wanaouza mifugo na wanaonunua, lakini mkishauziana tu ondokeni mara moja mnadani na sitaki muweke mikusanyiko,"alisema.
Aidha alipongeza minada hiyo kutokana na tahadhari zilizochukiwa ambapo ili kuthubiti mikusanyiko makundi ya wafugaji na wafanyabishara imepungua kwa kiasi kikubwa tangu kulipozuka Ugonjwa huo huku kila anayeingia ananawa mikono kwa maji safi yanayotiririka.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frack Mwaisumbe,alishukuru serikali kuruhusu wananchi wake kuendelea na minada ya mifugo, sababu ni sehemu ya maisha yao,huku akieleza wazi kuwa hapo awali minada huo wa longido ulifunngwa kutokana na kuzua taaruki kubwa kwa wananchi mara baada mgonjwa wa kwanza wa Corona kutangazwa.