Monday, March 30, 2020

Huu Ndio Ukweli Sahihi Kuhusu Elimu Uliyonayo

eLIMU
Ni utaratibu wangu ambao niliuona unafaa sana katika Maisha yangu, kwani umeweza kuyabadili sana maisha Yangu kwa kiwango cha hali ya juu sana,  sitaki kujisifia wala kujipaka mafuta kwa mgongo wa chupa maana nitakuwa najidanganya mwenyewe, ila huo ndo ukweli wenyewe, najua bado una zungusha akili yako huku na huko bila kujua ni nini ambacho nitakuwa nazungumzia je ni utaratibu upi? wala Usipate tabu ni utaratibu wa kujifunza vitu vipya Kila wakati.

Inawezekana ukawa unashangaa nawezaje kufanya hivyo? Wala usipate tabu leo nitakueleza ukweli kwani mara baada ya kugundua ya kwamba hatma ya Mafanikio yangu, ipo kwenye mandishi  hivyo nikashuru kimoyomoyo yule ambaye alinifundisha kusoma, kuhesabu na kuandika kwa kunijengea msingi imara ambao ndio nguzo kubwa ya Maisha ya kila mmoja wetu  katika dunia yenye kila aina ya kila kitu, hivyo kazi ni kwako ni aina gani ya vitu ambavyo unavihiitaji katika dunia hii.

Na Kuna wakati huwa inafika pahala naona ni vyema ni bora usinipe chakula kwanza, ila unipe vitu vya kusoma kwanza ambayo vitasaidia kwa namna moja ama nyingine. Sitaki pia kukwambia na wewe usome peke yake vitu ambavyo vitakusaidia katika maisha yako, la hasha kusoma peke yake haitoshi ila jambo la msingi ni kuweza kusoma yale ambayo uliyasoma kuyaweka katika matendo.

Suala hili na kugeuza kile ambacho umekisoma na kukiweka katika matendo ni suala gumu sana, kuwepo kwa hali hii ndiko ambako kunasababisha  kuwe na wimbi kubwa la watu ambao ni wazuri sana katika kulalamika tu kuliko kufikiri ni namna gani ya kubadili ambacho unakijua kuweka kwenye matendo.

Labda inawezekana ya kwamba bado unalalamika ya kwamba hakuweza kupata elimu kwa kiwango ambacho ulihitaji, lakini nikutie moyo kwa kukwambia ya kwamba elimu ambayo unayo inatosha kabisa, kuweza kubadili historia mpya ya maisha yako leo endapo , utaamua kuutafuta undani wako ni upi? Nimesema hivyo kwa sababu elimu yeyote ambayo uliyonayo huwa ina faida zaidi ya kumi lakini leo naomba kueleze faida kubwa tatu tu hii ni kutokana na muda ambao ninao siku ya leo.

Faida ya elimu yeyote uliyona Ni vyema itakusaidia kufanya yafuatayo;

1. Kujua
Elimu yeyote ile ambayo unataka kuipata, au umekwisha kuipata ni lazima ikusaidie kufahamu mambo mbalimbali, baada ya kujua ukweli wa mambo hayo ni Lazima ufikirie ni jinsi gani unaweza kuugeuza ujuzi huo kuwa bidhaa. Yamkini ukawa bado unalalamika kwamba suala la ajira ni suala gumu kwako lakini jiulize ya kwamba  ujuzi ulio nao unawezaje kuwa bidhaa? baada ya kupata majibu ndipo utapojua ni kitu gani ambacho namaanisha.

2.kutenda
Hili ni suala la msingi sana, ambalo ni vyema kulifahamu siku ya leo. Watu wengi wanafahamu mambo mengi sana, lakini ukakasi huwa unakuja katika kutenda. Lakini kabla sijaweka nukta siku ya leo nikwambie ya kwamba maisha ni leo, wala sio jana wala kesho. Nimesema Maisha ni leo kwa sababu Maisha yako yatabadilika kama unataamua kutenda leo, na mara kadhaa nikwambie ya kwamba tuyakumbuke yale maneno mazuri ambayo yanasema ngoja ngoja yaumiza matumbo, na chelewa chelewa utakuta mtoto sio wako hivyo nikusihi amua sana kuanza kutenda jambo lako ili uweze kutimiza ndoto zako.

3. Kushirikiana pamoja.
Hii ni faida nyingine ambayo itakufanya wewe kuweza kuwa bora zaidi kila mara. kuweza kuwashirikisha mawazo yako watu wengine ili kuweza kupata majibu ya maswali yako na hatimaye kutimiza Ndoto kubwa uliyonayo. Usipende kufanya vitu peke yako. Ubinafsi ndio umaskini wako, hivyo kila wakati ni vyema ukajua namna katika kuwaongezea thamani  watu wengine. Maana kama hautajua kuwaongezea watu wengine thamani na wao hawataweza kukuongezea thamani pia.

Kufanya kazi kwa ushirikiano ni njia bora sana katika kufanikisha malengo yako. Maana ushirikiano na Mafanikio na utengano ni udhaifu. Lakini kabla sijamaliza labda nikumbushe ya kwamba ni lazima uweze kushirikiana na watu sahihi kwa kila jambo lako.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...