
Picha haihusiani na habari hapa chini
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watu sita wamenusurika kufa kwa kushambuliwa na fisi baada ya kumzingira wakitaka kumuua katika kijiji cha katika kijiji cha Mwangh'alanga, kata na tarafa ya Samuye, wilaya  na mkoa wa Shinyanga. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea  Ijumaa Machi 27,2020 majira ya saa nne. 
"Chanzo cha tukio hilo ni watu hao kuvamiwa na fisi huyo baada ya kumzingira wakitaka kumuua. Hata hivyo wananchi walifanikiwa kumuua fisi huyo",amesema Kamanda Magiligimba. 
Amewataja waliojeruhiwa kujeruhiwa na fisi kwa kung'atwa maeneo mbalimbali ya miili yao katika tukio hilo kuwa ni Zengo Jitonja , Nkuba  Deteba , Juma Salaganda, Limbu  Mihambo , Dutu Mdese na John Matana wote wakazi wa kijiji cha Mwangh'alanga Samuye 
Amesema majeruhi watano kati yao wamepata majeraha madogo madogo na hivyo  wamepatiwa matibabu hospitalini  na kuruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri. 
"Majeruhi mmoja  Zengo Jitonja (56), amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa Shinyanga baada ya kujeruhiwa na fisi huyo mikononi na mdomoni na hali yake siyo mbaya sana",ameongeza Kamanda Magiligimba.