Friday, May 31, 2019

MJAMZITO AJIPASUA TUMBO KUTOA MTOTO TUMBONI RUKWA

Mwanamke mmoja anadaiwa kujipasua tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto, wilayani Nkasi mkoani Rukwa Kusini Magharibi mwa Tanzania.


Tukio hilo limevuta hisia za wengi na wengine wakiwa katika taharuki wengi wakifika katika kituo cha afya kushuhudia ukweli wa tukio hilo linalodaiwa kutekelezwa na bi Joyce Kalinda.

Wakati taarifa za awali zikisema kuwa mwanamke huyo alijipasua umbo, Mganga mkuu wa wiaya ya Nkasi Dokta Hashi Mvogogo alizungumza na gazeti la Habari Leo alisema bado uchunguzi unafanyika ili kujua ukweli wa kilichotokea kwa mama huyo.

Uchunguzi unafanyika kubaini kama alijifanyia upasuaj mwenyewe kutoa mtoto au kuna mtu mwingine alifanya hivyo.

Daktari huyo amesema saa tisa alfajiri ya kuamkia siku ya Alhamisi, mwanamke huyo alifika katika kituo cha afya cha Kirando na kuanza kupiga kelele, akimtaka muuguzi aliyekuwa zamu ampe huduma za kumsaidia kujifungua.

Alisema kutokana na kuwepo kwa wagonjwa wengine kituoni hapo, muuguzi alimshauri mama huyo mja mzito kusubiri kidogo kisha alikwenda kumhudumia mgonjaw mwingine, lakini aliporejea mahali apokuwepo hakumkuta.

Kwa mujibu wa Dokta Mvogogo,ilipotimu alfajiri saa 11 mja mzito huyo alirudishwa hospitalini hapo akiwa amepasuka sehemu ya tumbo, huku watu waliomfikisha hospitalini hapo wakiwa wamembeba mtoto mchanga.

Watu hao walisema mwanamke huyo alikuwa amejipasua tumbo na kumtoa mtoto tumboni.

''Tumbo lilionekana limepasuliwa na kitu chenye ncha kali.Alipofika aliwekewa dripu tatu za damu ili kuokoa maisha yakekwani alikua amepoteza damu nyingi, lakini pia mtoto alipewa matibabu kutokana na kutolewa tumboni bila kufuata utaalamu unaotakiwa na sasa wote wanaendelea vizuri na matibabu,'' Dokta Mvogogo aliiambia Habari Leo.

Dokta Mvogogo amesema tukio hilo limeripotiwa polisi ili uchunguzi wa kina ufanyike kubaini ni nini kilichotokea kwa mama huyo.

''Uchunguzi unaofanywa pia unahusisha mtaalamu wa magonjwa wa akili ambaye tunataka achunguze ili kubaini kama mama huyo ambaye huo ni uzao wake wa nane ana ugonjwa wa akili au la,'' alieleza Daktari huyo.

Chanzo - BBC

Hoteli Yajipanga Kumuomba Radhi Meek Mill

Hoteli Yajipanga Kumuomba Radhi Meek Mill
Baada ya siku chache rapper Meek Mill kuilalamikia hoteli ya Cosmopolitan kwa ubaguzi wa rangi, leo May 31,2019 imeripotiwa kuwa hoteli hiyo imepanga kuomba radhi hadharani kwa kitendo hicho ambacho kilitokea Jumapili ya May 26.

Meek Mill alitoa malalamiko kuwa alizuiliwa kuingia kwenye hoteli hiyo iliyopo mjini Las Vegas ambapo walinzi wa eneo hilo walisema kuwa hakufata utaratibu uliowekwa kwenye hoteli hiyo na endapo ataingia lazima wamkamate. Ilielezwa kuwa rapper huyo alikwenda kwa nia ya kuhudhuria tamasha la Dj Mustard.

Iliripotiwa kuwa Mwanasheria wa rapper huyo, Joe Tacopina aliandika barua ikiwataka wamiliki wa hotel hiyo kuomba radhi kwa kitendo hicho ikiwa ilielezwa kuwa ni tabia ya hoteli hiyo kuwazuzia mastaa weusi kuingia mahali hapo.

UN wapokea mashtaka 37 ya udhalilishaji wa kingono dhidi ya wafanyakazi wake


Umoja wa Mataifa (UN) umepokea mashtaka 37 ya udhalilishaji wa kingono dhidi ya wafanyakazi wake katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

 Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema katika madai hayo, kuna wahanga 49 wakiwemo wanawake 28, wasichana 11, mvulana mmoja, na wanaume saba.

Msemaji huyo ameeleza kuwa juhudi zao za kupambana na vitendo hivyo zinaendelea kupiga hatua siku kwa siku ili kuhakikisha wanafanikiwa kabisa kutokomeza vitendo hivyo viovu.


Rekodi mbovu na mkosi wa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, kushindwa katika mchezo wa fainali, fahamu fainali alizoshindwa

Rekodi ya Jurgen Klopp ya kufikisha timu yake katika fainali hi ya kupigiwa mfano- lakini kiwango cha ufanisi wake ni cha kuvunja moyo. Kocha wa Liverpool anaelekea katika fainali ya ligi ya mabingwa ya siku ya Jumamosi dhidi ya Tottenham akiwa na mkosi kushindwa katika fainali sita mfululizi. Mbili kati ya mkosi huo ni kushindwa …

The post Rekodi mbovu na mkosi wa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, kushindwa katika mchezo wa fainali, fahamu fainali alizoshindwa appeared first on Bongo5.com.


Source

Japan na Urusi Zashutumiana

Japan na Urusi Zashutumiana
Mawaziri wa mambo ya nje wa Japan na Urusi waliokutana kwa mazungumzo katika mji mkuu wa Japan, Tokyo, wameshutumiana kwa serikali zao kujipanua kijeshi katika visiwa vya Kurils.

Japan imesema kujipanua kijeshi kwa Urusi katika visiwa hivyo vinavyozozaniwa ni hatua isiyokubalika, huku Urusi ikisema mpango wa Japan wa kuweka mfumo wa kujilinda na makombora uliotengenezwa Marekani kwa jina la Aegis Ashore ni tishio kubwa kwa nchi yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Takeshi Iwaya, alimjibu mwenzake wa Urusi Sergei Shoigu kuwa mfumo huo ni wa kujilinda tu, na kamwe haototumiwa kuidhuru Urusi au nchi nyingine yoyote.

Visiwa hivyo vinavyozozaniwa vilikamatwa na Umoja wa Kisovieti kutoka Japan baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

VIDEO: TFF yaokoa milioni 689/ Wasaini makataba wa jezi mpya timu za Taifa


Shirikisho la soka nchini TFF kupitia kwa Rais wake Wallace Karia, Ijumaa hii wamesaini mkataba na kampuni mpya ya kutengeneza vifaa vya wachezaji wa timu za taifa za Tanzania. Kampuni ambayo imepata tenda hiyo ni Uhlsport kupitia Romario Sports 2010 ambayo inasimamia kazi za kampuni hiyo.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Yadaiwa taifa la Ufilipino limerudisha shehena za takataka nchini Canada,sababu zaelezwa (+Video)

Ufilipino imerejesha tani za takataka nchini Canada, baada ya mvutano wa kidiplomasia wa majuma kadhaa ambapo Rais wa nchi hiyo Rodrigo Duterte kutishia ” kusafirisha takataka kwa njia ya maji kuelekea Canada”. Ufilipino imesema takataka hizo ziliwekwa nembo kimakosa kuwa zilikua za plastiki tayari kwa kutengenezwa upya (recycling) zilipofikishwa Manila mwaka 2014. Canada imekubali kulipa …

The post Yadaiwa taifa la Ufilipino limerudisha shehena za takataka nchini Canada,sababu zaelezwa (+Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Golikipa wa Simba SC, Manula kupewa Tsh. Milioni 10 na RC Makonda


Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam, Paul Makonda ameahidi kutoa zawadi ya Tsh. milioni 10 kwa Golipika wa Simba SC, Aishi Manula na Tsh. Milioni 1 kwa wachezaji wengine ambao hapo jana walishinda kwenye MO Simba Awards 2019.

MHUBIRI ATUKANA MAASKOFU WASIOMHESHIMU...WAUMINI WANAOMVIZIA MKEWE

Mhubiri mwenye utata James Ng'ang'a wa Kanisa la Neno Evangelism Center nchini Kenya ametishia kuchukua hatua mikononi mwake na kuyafunga matawi mengine ya kanisa lake kwa kile alichokitaja kama kukosewa heshima. 


Wakati wa ibada, Ng'ang'a amewaonya waumini, maaskofu dhidi ya kummezea mate mkewe.

Ng'ang'a aliyekuwa mwingi wa hasira aliyataja majina ya baadhi ya waumini wa kanisa hilo la Neno Evangelism Center.

 "Mengi yamekuwa yakisemwa. Iwapo mtashindwa kumheshimu mke wangu nitawafukuza katika kanisa hili. Wakati huu sasa nitawaonesha uwezo wangu,You will know my true colour" Ng'ang'a alitishia. 

Haijabainika wazi kile mtumishi huyo alimaanisha kwa kutamka kukosewa heshima lakini aliwakemea baadhi ya waumini kwa madai ya kumvizia mkewe.

Hakukomea hapo tu bali alizidi kuwaonya baadhi yao kwamba iwapo hawatabadili mienendo atawachukulia hatua. 

"Vile vile, mwanamke yeyote ambaye atamkosea heshima mke wangu nitamfurusha humu kanisani. Utaondoka katika kanisa langu na kuanzisha lako,"aliongeza.

 Matamshi yake yaliwashtua waumini kanisani humo, ambao hawakuwa na la kufanya ila kuketi kitako na kumsikiza kwa makini huku wakisalia kumkodolea tu macho.

 Machi, 2019 alijipata pabaya baada ya kushtakiwa kwa kumtishia mwanahabari Linus Kaikai wa Citizen TV, baada ya Linus kupendekeza wachungaji wote ni sharti wawe na shahada ndipo wahudumu kama mapasta.

 Mhubiri huyo ambaye amezongwa na utata si haba alifunga ndoa na mkewe Mercy Murugi kwenye sherehe ya kifahari ilyoandaliwa Windsor Golf Club na kuhudhuriwa na wanasiasa mashuhuri. 

MSIKILIZE HAPA

VAZI LA WAZIRI MKUU LAZUA GUMZO...ATINGA NA SUTI YA SKETI NA SANDOZI IKULU

Mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi amepata fursa ya kumtembelea rais wa Kenya Uhuru kenyatta

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha kupigwa na butwaa na vazi alilovaa Waziri mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi.

Waziri mkuu Bainimarama ambaye ni mwanamume alikuwa amevalia suti ya sketi na viatu vya wazi (sandozi) wakati alipopata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa makazi nafuu katika eneo la Ngara jijini Nairobi.

Vazi alilovalia ni maarufu nchini kwa wanaume wa Fiji likifahamika kama na jina Suti ya Sulu.

Lakini Sulu ya wanawake hufahamika kama Sulu-i-ra.Suti ya Sulu inachukuliwa kama vazi la kitaifa la Fiji na huangaliwa kama utambulisho wa jamii ya Wafiji . Vazi hili ambalo huwa wakati mwingine sketi yake inakatwa katwa upande wa chinihuvaliwa na wanaume na wanawake wa Fiji.

Urefu wa vazi hili unategemea na mtu apendavyo kuanzia chini ya magoti au urefu wa kufika kwenye kisigino.

Zamani ulikuwa unavaliwa mkanda tumboni. Hata hivyo wanaume wa kisasa wanaweza kukutumia pini.



Sulu zilivaliwa na watu wa Fiji Tangu enzi za ukoloni katika katika karne ya kumi na tisa. Mwanzo zililetwa na wamishonari waliokuwa wakitoka Tonga na katika kipindi hiki sketi hizi zilikuwa zikivaliwa na Wafiji kuonyesha kuwa wamejiunga na ukristo.

Sulu za wanawake zinazovaliwa kila siku hufahamika kama sulu-i-ra, na Sulu ndefu wanazovaa rasmi au wakati wa matukio ya sherehe hufahamika kama sulu jaba.

Sulu za wanaume wanazovaa rasmi huitwa -sulu vakataga.

Vazi la sulu pia huvaliwa kama sare rasmi ya polisi na jeji nchini Fiji

Sulu zilizoshonwa na mifuko huvaliwa kawaida kama vazi la ofisi na rasmi pamoja na shati na viatu vya wazi (sandozi) na upande wa juu huvaa koti na tai.

Katika hali fulani, mtu anapoingia na Sulu kanisani huonekana kama mtu mwenye heshima nchini Fiji.

Sulu zilizoshonwa pia huvaliwa kama sare za polisi na jeshi.

Vazi rasmi la sulu huwana na urefu wa hadi chini ya magoti na hukatwa kwa mathalani umbo la pembe tatu.

Huku uvaaji wa Sulu mara nyingi huwa ni wa lazima kwa Wafiji wakati fulani, baadhi ya jamii wakati mwingine hukatazwa kuzivaa.

Thursday, May 30, 2019

Tatizo la Maumivu ya Chini ya Kitovu kwa Wanaume na Wanawake

Tatizo hili huwakumba watu wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadae hupelekea watu wengi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula. 


Maumivu Chini Ya Kitovu Hutokea Kama Ifuatavyo: 

Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa marefu. 


Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi. 


Maumivu chini ya Kitovu Yanaashiria Matatizo Gani Kwa Wanawake? 

Mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya uzazi na wakati huo huo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu. 


Kutokukomaa kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba(ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi. Mwanamke ambaye anamaumivu chini ya kitovu na wakati huo huo ana matatizo ya hedhi mfano hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum kunauwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi. 


Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huo huo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kunauwezekano akawa na PID hasa hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla haijafikisha miezi mitano. 


Afya mbovu ya kibofu cha mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI). Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara. 


Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria nini? 

Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia tatizo la tezi dume liitwalo Prostatitis yaani kuvimba kwa tezi dume. Maumivu haya hujikita kwenye shina la uume na huashiria tatizo hili hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa unaelekea miaka 50 au zaidi. 


Dalili nyingine ambatano ni kutoa haja ndogo ambayo ina kasi ndogo sana tofauti na kawaida, ikiambatana na maumivu ya kiuno na mgongo, kuvimba kwa korodani, haja ndogo inayoambatana na usaha na damu, maumivu ya uume wakati wa kufika kileleni, na damu katika maji ya uzazi (semen) 

Kwa wanaume, maumivu haya ya chini ya kitovu huashiria pia tatizo ambalo kitaalamu hujulikana kwa jina la Hernia ambapo waswahili tunaita ngiri. 


Mwanaume anaposikia maumivu haya ya chini ya kitovu ikiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na nyingine kukua zaidi au zote mbili kukua au kupotea, ni dalili ya ugonjwa huu ambao huharibu ubora wa uzalishwaji wa mbegu za kiume ambazo zaweza kuzalishwa chache au ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vywa mwanamke na hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba. 


Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake huashiria tatizo la maambukizi katika mfumo wa haja ndogo yaani (Urinary Track Infection/UTI) ambapo dalili zake ni kama zile za mwanamke hapo juu. 


Vipimo na tiba vyahitajika mapema bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata wa chakula 


Bangi yamuibua Afande Sele, aishauri Serikali kuliangalia zao la bangi kwa jicho la tatu, (+Video)

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop hapa Tanzania, Afande Sele amefunguka mengi sana na kuiomba Serikali ya tanzania kuruhusu matumizi ya bangi. Akiongoa na Bongo5 Afande Sele amesema hayo ingawa kulishawahi kuibuka mijadala bungeni kuhusu zao hilo. Afande Sele amesema hay:- By Ally Juma.  

The post Bangi yamuibua Afande Sele, aishauri Serikali kuliangalia zao la bangi kwa jicho la tatu, (+Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Naibu Waziri Nditiye Awataka Watanzania Kusoma Kwanza Maelekezo Ya Tiketi Kabla Ya Kukata Tiketi Ili Kuondoa Migogoro.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye amewataka watanzania  Kuwa na desturi ya kusoma kwanza maelekezo yaliyopo kwenye tiketi  ya kusafiria  pindi wanapotaka kusafiri ili kuondoa migongano na migogoro baina yao na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri. 

Mhe.Nditiye ameyasema hayo Mei 30,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa ShauriMoyo  Mhe.Mattar Ali Salum  aliyehoji juu ya  baadhi ya kampuni za usafiri hususan Usafiri wa Majini kwa njia ya Boti  kuuza tiketi kwa abiria  kwa ajili ya Safari  lakini abiria anapochelewa safari tiketi hiyo  huwa haitumiki  na hivyo kusababisha hasara na usumbufu kwa abiria . 

Katika Majibu yake Mhe.Nditiye amesema tiketi ni moja ya mkataba kati ya abiria na mmiliki wa chombo cha usafiri hivyo abiria  anatakiwa kusoma kwanza maelekezo yaliyo kwenye tiketi na kama hatoridhika na maelekezo hayo ana ruksa ya kusitisha kukata tiketi ili kuondoa usumbufu.

Hata hivyo,Mhe.Nditiye amesema ufuatiliaji wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano  kupitia TASAC Umebaini kuhusu changamoto hizo na serikali inalifanyia uchunguzi.


Tuzo za Mo Awards Kutolewa Leo Dar

TUZO za Mo Awards zilizoasisiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji zinatolewa leo Alhamisi ukiwa ni msimu wake wa pili. Tukio hilo la aina yake litafanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency na zitatolewa tuzo 12 kwa kikosi hicho cha Mabingwa wa Ligi Kuu Bara.



Hii itakuwa ni mara ya pili kwa tuzo hizo kutolewa baada ya mara ya kwanza mwaka jana.

Msimu huu tuzo hizo zitakuwa na mabadiliko tofauti na msimu uliopita baada ya vipengele kadhaa kuongezwa.


Tuzo hizo zitakuwa katika vipengele 12 ambavyo ni mchezaji bora wa mwaka, golikipa bora wa mwaka, goli bora la mwaka, beki bora wa mwaka, kiungo bora wa mwaka na mshambuliaji bora wa mwaka mchezaji mwenye umri mdogo, mchezaji bora wa kike na nyingine.



Hata hivyo tuzo hizo zilikuwa zinapigiwa kura katika kurasa tofauti za mitandao ya kijamii ya klabu ya Simba. Wachezaji ambao walipata tuzo hizo msimu uliopita ni pamoja na Aisha Manula, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi kwa Simba Queens alikuwa Zainabu Rashid. Kwa upande wake, Mohammed Dewji amesema kuwa tuzo za mwaka huu zitakuwa na hadhi kubwa zaidi tofauti ya zile za mwaka uliopita kutokana na maandalizi ambayo yamefanyika.

Wednesday, May 29, 2019

Rais wa FIFA aipongeza Klabu ya Simba




Source

RAIS MAGUFULI ATAKA JUMUIYA ZA KIMATAIFA KUONDOA VIKWAZO DHIDI YA ZIMBABWE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kwa hatua madhubuti za kufanya mageuzi ya kiuchumi katika nchi hiyo na ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe.


Rais Magufuli amesema hayo wakati akitoa hotuba katika Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Mnangagwa kwa heshima yake na kufanyika Ikulu Jijini Harare.

Rais Magufuli amesema katika kipindi kifupi cha tangu Rais Mnangagwa aingie madarakani hali ya uchumi imeanza kuimarika ambapo kwa sasa uchumi wa Zimbabwe unakua kwa wastani wa asilimia 3.5, mwaka ujao unatarajiwa kukua kwa wastani wa asilimia 4.2 na mwaka unaofuata kuongeza hadi wastani wa asilimi 4.4.

Kufuatia hali hiyo ameisihi Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo mbalimbali vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe kwa kuwa vikwazo hivyo vinawaumiza wananchi wa Zimbabwe wakiwemo watoto na wanawake.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli kwa mara nyingine amewapa pole Rais na wananchi wote wa Zimbabwe kwa kupoteza watu takribani 400 waliofariki dunia katika mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Idai kilichoikumba Zimbabwe Machi 2019. Amesema Watanzania wanaungana na ndugu zao Wazimbabwe katika majonzi ya kuondokewa na jamaa zao na wanawaombea kwa Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi, Amina.

Kuhusu uhusiano wa Tanzania na Zimbabwe ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Mzee Robert Mugabe, Rais Magufuli amesema Tanzania inatambua na inathamini uhusiano huu wa kihistoria na kidugu na amebainisha kuwa jukumu lililopo sasa ni kuelekeza nguvu nyingi zaidi katika uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi utakaoziwezesha Tanzania na Zimbabwe kuongeza biashara na uwekezaji.

Rais Magufuli amebainisha kuwa katika mazungumzo yake ya faragha na Rais Mnangagwa leo mchana wamekubaliana kusimamia ipasavyo makubaliano yaliyopo katika Kamati ya Pamoja ya Kudumu (Joint Permanent Commission – JPC) kwa manufaa ya nchi zote mbili.

"Rais Mnangagwa ujio wangu hapa Zimbabwe ni kuthibitisha kuwa urafiki wetu bado upo imara na sisi Tanzania tumejipanga kuuimarisha zaidi, tunataka tufanye biashara zaidi na nyinyi ndugu zetu wa Zimbabwe ili tukuze uchumi wa nchi zetu na kuongeza kipato cha wananchi wetu" amesisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande wake, Rais Mnangagwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kukubali mwaliko wake, na amemthibitishia kuwa yeye na wananchi wa Zimbabwe wanatambua kuwa Watanzania ni ndugu zao waliojitolea kwa dhati katika ukombozi wao wakiongozwa na dhamira ya dhati ya Hayati Mwl. Nyerere.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwa kiongozi wa kwanza katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutoa msaada wa chakula, dawa na vifaa vya kujihifadhi wakati Zimbabwe alipokumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Idai mwezi Machi 2019.

Rais Mnangagwa amesema msaada huo uliwagusa Wazimbabwe wengi na kuwakumbusha umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya majanga na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesisitiza kuwa daima Zimbabwe itabaki kuwa rafiki na ndugu wa kweli wa Tanzania na hivyo amemhakikishia Rais Magufuli kuwa nchi hiyo ipo tayari kukuza zaidi ushirikiano wa kiuchumi kwa kuongeza biashara na uwekezaji pamoja na kushirikiana katika usafiri wa anga.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kumpa mbinu mbalimbali za kiuongozi ikiwemo kuondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo mkubwa kwa Serikali na ameahidi kudumisha ushirikiano kati ya chama chake ZANU-PF na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Watu 16 Washtakiwa kwa Kumchoma Moto Msichana Akiwa Hai

Watu 16 wameshitakiwa nchini Bangladesh kuhusiana na mauaji ya kushtusha ya msichana ambaye alichomwa moto hadi kufa baada ya kuripoti unyanyasaji wa kingono

Nusrat Jahan Rafi, aliyekuwa na umri wa miaka 19, alimwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto juu ya paa la shule ya kiislamu tarehe 6 Aprili, siku kadhaa baada ya kuripoti unyanyasaji wa kingono

Mwalimu mkuu wa shule yake Siraj Ud Doula, ambaye alidaiwa kumfanyia unyanyasaji huo ni miongoni mwa washitakiwa.

Polisi wanasema aliagiza mauaji yake alipokuwa gerezani wakati alipokataa kuondoa mashtaka dhidi yake.

Walielezea maandalizi ya mauji yake kuwa yalikuwa sawa na "mpango wa jeshi".

Nusrat, ambae alikuwa na umri w amiaka 19, alikuwa anatoka katika mji mdoto wa Feni, uliopo maili 100 kutoka mji mkuu Dhaka. Alikuwa anasoma katika shule ya Kiislamu ya madrassa, tarehe na 7 Machi alisema kuwa Mkuu wa shule alimuita ofisini kwake na kumtomasa. Kabla mambo hayafika mbali alikimbia nje ya ofisi.

Wasichana wengi na wanawake wenye umri mdogo nchini Bangladesh huamua kunyamaza kimya wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono au kubakwa kwa kuhofia kudhalilisha na jamii au familia zao . Kilichomfanywa tofauti na Nusrat Jahan ni kwamba hakuzungumzia suala hilo kwa sauti tu bali - alikwenda pia kwa polisi kwa msaada wa familia yake katika siku ambayo unyanyasaji huo ulidaiwa kufanyika.

Katika kituo cha polisi mjini humo alieleza mashtaka. Alitakiwa kupewa mazingira salama ili aweze kuthathmini yaliyomtokea. Badala yake alichukuliwa video na afisa wa polisi husika kupitia simu yake huku akielezea yaliyompata.

Wanawake wanaofanya kazi wakati wa Ramadhan
Mwili wa Savimbi wazozaniwa
'Roho Mtakatifu' amuepusha dereva na faini
Katika video hiyo Nusrat anaonekana wazi akiwa na mkanganyiko huku akijaribu kuficha uso wake kwa mikono. Polisi anasikika akisema malalamiko hayo "sio jambo kubwa " na kumueleza nusrat aondoe mikono usoni . Baadaye video hiyo ilivifikia vyombo vya habari nchini humo.

Nusrat Jahan Rafi alikuwa anatoka katika mji mdogo, na alizaliwa katika familia yenye ya kihafidhina, na akasomea katika shule ya dini. Kwa msichana kama yeye, kuripoti unyanyasaji wa kingono ni jambo linalokuja na madhara . mara nyingi waathiriwa hukabiliwa na hukumu kutoka kwa jamii zao, udhalilishwaji wa moja kwa moja na kupijtia mtandao , na wakati mwingine hupigwa. Nusrat alikabiliwa na yote haya.

Tarehe 27 Machi, baada ya kwenda polisi, walimkamata mwalimu wake mkuu. Baada ya hapo mambo yakaanza kuwa mabaya kwa Nusrat. Kundi la watu walikusanyika kwenye mitaawakidai aachiliwe. Waandamanaji walikuwa wamekusanywa na wanafunzi wawili wa kiume na wanasiasa wa eneo hilo wanaripotiwa kuwa walihudhuria maandamano hayo . Watu walianza kumlaumu Nusrat. familia yake inasema ilianza kuhofia usalama wake.

Licha ya hayo , tarehe 6 Aprili, siku 11 baada ya unyanyasaji huo unaodaiwa, Nusrat alikwenda shuleni kwake kufanya mitihani yake ya mwisho.

"Nilijaribu kumchukua dada yangu shuleni na kujaribu kuingia shuleni, lakini nikazuwiwana sikuruhusiwa kuingia ," alisema kaka yake Nusrat, Mahmudul Hasan Noman.

"Nisingezuwiwa, jambo kama hili lisingemtokea dada yangu ," alisema.

Kwa mujibu wa taarifa ya mashtaka iliyotolewa na Nusrat, mwanafunzi mwenzake wa kike alimpeleka kwenye paa la shule, alisema mmoja wa marafiki zakealikuwa amechapowa . Wakati Nusrat alipofika juu ya paa watu wanne au watano, waliokuwa wamevalia burqa, walimzingira na kumshinikiza aachane na kesi dhidi ya mwalimu mkuu. Alipokataa ndipo walipomwagia mafuta ya taa na kumchoma kwa moto.

Mkuu wa Idara ya upelelezi ya polisi Banaj Kumar Majumder alisema kuwa wauaji wanaotafutwa "walitaka kufanya mauaji hayo yaonekane kama Nusrat alijiua mwenyewe ". mpango wao uliharibika wakati Nusrat alipookolewa baada baada ya kutoroka eneo la tukio. Aliweza kutoa taarifa kabla ya kufa.


Umati mkubwa wa watu ulikusanyika katika mji alikozaliwa Nusrat wa Fenkuhudhuria mazishi yake
" Mmoja wa wauaji wake alishindilia kichwa chake chinikwa kutumia mikono yake, kwa hiyo mafuta ya taa hayakumwagika palena ndio maana kichwa chake hakikuungua ," Bwana Majumder aliiambia BBC mjini Bengali.

Lakini wakati Nusrat alipopelekwa katika hospitali iliyopo karibu majeraha mwili wake ulikuwa na 80% ya majeraha ya mwili wake . Hawakuweza kutibu vidonda , na kuamua kutuma katika hosptali ya chuo cha tiba cha Dhaka.

Alipokuwa katika ambilansi, kwa kuhofia kuwa hatapona, alirekodi taarifa katika simu ya mkononi ya kaka yake.

Tuesday, May 28, 2019

AFRICAN LYON,KAGERA SUGAR ZASHUKA DARAJA,MATOKEO YOTE HAYA HAPA


Source

TAKUKURU yamkabidhi Nyalandu Polisi kwa mahojiano

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Singida imewakabidhi kwa jeshi la polisi mkoani humo wanachama watatu wa CHADEMA akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini na waziri wa awamu ya nne Bwana Lazaro Nyalandu kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Singida Bwana Joshuwa Msuya ambapo ameeleza kuwa imewalazimu kuwakabidhi kwa jeshi la polisi wananchama hao kwa madai ya kuwa walikuwa wakifanya mikutano bila kibali ya nyumba kwa nyumba katika kijiji cha Itaja halmashauri ya Singida.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Sweetbert Njewike amesema kuwa wananchama hao watatu waliwekwa katika kituo cha polisi cha kati kwa ajili ya hifadhi, lakini TAKUKURU wao wenyewe bado wanaendelea na uchunguzi.

Katika hatua nyingine Bwana Msuya amewataka wananchi hasa wana siasa kuacha kujihusisha na uvunjaji wa sheria kwa kufanya mikutano bila vibali na kujihusisha na rushwa kwani taasisi ya kupambabana na rushwa itawakamata.

Mei 27, 2019, TAKUKURU mkoa wa Singida ilithibitisha kuwakamata na kuwahoji wanachama watatu wa  chama cha CHADEMA, kwa tuhuma za rushwa akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini na waziri katika serekali ya awamu ya nne Bwana Lazaro Nyalandu.

Nyalandu na wenzake walishikiliwa na TAKUKURU wakati Wakiwa kwenye kikao

Wednesday, May 22, 2019

SIMBA SC YATWAA TENA UBINGWA WA LIGI KUU YA BARA


Simba SC wamefanikiwa kutetea taji lao ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Singida United jioni ya leo Uwanja wa Namfua.

Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems imefikisha pointi 91 baada ya ushindi wa leo katika mchezo wa 36 ikijihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu, kwani hakuna timu inayoweza tena kuwafikia. 

Hilo linkuwa taji la pili mfululizo la ubingwa wa Ligi Kuu kwa Simba SC na la 19 jumla kihistoria baada ya awali kulibeba katika miaka ya 1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007, 2010, 2012 na 2018.

Watani wao, Yanga SC ndio mabingwa mara nyingi zaidi wa Ligi Kuu, mara 26 wakiwa wamebeba taji hilo miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011, 2013, 2015, 2016 na 2017.

Timu nyingine zilizowahi kubeba taji hilo ni Cosmopolitan 1967, Mseto SC ya Morogoro 1975, Pan African 1982, Tukuyu Stars ya Mbeya 1986, Coastal Union ya Tanga 1988, Mtibwa Sugar mara mbili 1999 na 2000 na Azam FC 2014.

Katika mchezo wa leo, mabao ya SImba SC yalifungwa washambuliaji wake tegemeo, Meddie Kagere kutoka Rwanda kipindi cha kwanza na mzawa, John Raphael Bocco kipindi cha pili.

Kagere alifunga bao lake dakika ya tisa tu akitumia makosa ya beki Kennedy Wilson Juma kuzubaa na mpira kufuatia krosi ya beki wa kushoto wa Simba SC, Mohammed Hussein 'Tshabalala' ambaye pia ni Nahodha Msaidizi wa klabu. 

Nahodha John Bocco akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 60 akimalizia krosi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi aliyenzishwia mpira wa kurushwa na Tshabalala. 

Hata hivyo, bao hilo kidogo lilikuwa la utata, kwani kwani refa Shomary Lawi kutoka Kigoma aliwaruhusu Simba kuanza mpira wakati kipa wa Singida United, Said Saleh Lubawa akiwa nje anaugulia maumivu baada ya kuumia wakati akiokoa.

Wachezaji wa Singida United walibishana na refa kwa dakika mbili kabla ya mchezo kuendelea, huku kipa Lubawa akibebwa mabegani kutolewa nje nafasi yake ikichukuliwa na David Kissu.

Kikosi cha Singida United kilikuwa; Said Lubawa/David Kissu dk66, Frank Mkumbo, Gilbert Mwale, Salum Kipaga, Kennedy Wilson, Rajab Zahir, Boniface Maganga/Mathew Michael dk78, Issa Makamba, Jonathan Daka, Habib Kyombo na Geoffrey Mwashiuya/Assad Juma dk58.

Simba SC; Deogratius Munishi 'Dida', Nicholas Gyan, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei, Muzamil Yassin, Haruna Niyonzima/Hassan Dilunga dk79, John Bocco, Meddie Kagere/Clatous Chama dk85 na Emmanuel Okwi/Jonas Mkude dk75.

Tuesday, May 21, 2019

Mambo ambayo mjasiriamali na mfanyabiashara wanatofautiana


Watu wengi wapo kwenye biashara hata hivyo hujiita wajasiriamali. Hii ni kwa sababu kumekua na mchanganyiko mkubwa kuhusu nani haswa ni mjasiriamali na nani mfanyabiashara.

Makala hii itakufanya usichanganye maneno hayo mawili, na ufahamu kama wewe ni mfanyabiashara au mjasiriamali na mwisho ni matumaini yetu Makala hii itakufanya uwe na hamu ya kuwa mjasiriamali badala ya kuwa mfanyabiashara.

1. Utofauti wa lengo kuu kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara
Mjasiriamali ingawa anaweza kunufaika yeye kama yeye kutoka na anachofanya, lengo lake la msingi huwa sio yeye kama yeye afanikiwe, bali lengo lake ni kuona suluhu Fulani ya tatizo ambalo anataka kulitatua. Hivyo basi mjasiriamali hujikita Zaidi katika jamii, kuangalia nini anaweza kufanya cha kuleta ahueni.

Mjasiriamali huhamasika zaidi na vile ambavyo anaweza kutatua changamoto fulani. Kwa upande wa mfanyabiashara lengo kuu ni kupata faida, hakuna mtazamo wa kina kuhusu changamoto gani au kwa namna gani jamii husika itapata haueni.  Ingawa anachofanya mfanyabiashara kinaweza kuleta ahueni na kutibu changamoto Fulani, lakini hilo sio wazo lake kuu au sio ambacho haswa kimemuingiza katika biashara. Yeye mfanyabiashara kinachompa hamasa kweli ni "kupiga hela" fasta.

2. Utofauti katika ubunifu kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara
Mjasiriamali hujihusisha zaidi na kubuni bidhaa au huduma mpya au namna mpya ya kuwasilisha bidhaa na huduma zilizopo, au kufikia kwa namna ya kipekee soko jipya kwa bidhaa ambazo tayari zipo. Unaona katika kila jambo mjasiriamali hujihusisha na UPYA Fulani.

Kwa upande wa mfanyabiashara hujishughulisha na vitu ambavyo tayari vimekwisha buniwa bila kuongeza kitu cha ziada. Hii ni kwa sababu lengo la mfanyabiashara ni kufanya chochote kile kitakachomuingizia faida. Mfano kwakua kaona mwingine anauza nguo na zinatoka, basi yeye ataenda kununua nguo za aina ile auze tena kwa soko lile lile ambalo mwenzake anauza.

3. Mahusiano na watu wa karibu katika shughuli
Mjasiriamali kwakua ana lengo la kutengeneza kitu fulani na mtazamo wake upo katika jamii, mara nyingi hujikita katika kutafuta timu bora ya kufanya nayo kazi kwakua mjasiriamali ana mtazamo mpana wa kuona kitu alichonacho kinafikia mbali na anajua bila watu wazuri wakaribu yake hatoweza.

Wakati huo mfanyabiashara kwakua hujikita zaidi katika kutafuta faida, na yeye mara nyingi manufaa yake binafsi ndio jambo la msingi zaidi, huwa hatilii maanani sana mambo ya mahusiano na kukua kwa pamoja na wale anaofanya nao shughuli yake.

Mjasiriamali huboresha na kuzingatia hata mahusiano yake na mteja, na kwamba mteja na mfanyakazi ni sehemu muhimu ya biashara wakati kwa mfanyabiashara mteja ni mtu tuu wa pembeni wa nje ya biashara yake, na wafanyakazi kama tuu watoa huduma wa kumnufaisha yeye mfanyabiashara afikie malengo.

4. Hatari ya kupata hasara ilivyo kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara
Kwakua mara nyingi mjasiriamali ni mwanzishaji wa bidhaa au huduma mpya au namna mpya ya kufikisha bidhaa au huduma iliyopo katika soko jipya au ambalo tayari lipo, mara nyingi mjasiriamali huwa hatari kubwa sana ya kupata hasara ukizingatia huo upya wa kufanya jambo.

Kwa upande wake mfanyabiashara ingawaje nae anaweza kupata hasara katika shughuli yake , hatari yake ya kupata hasira haiwezi linganishwa na mjasiriamali kwakua yeye mfanyabiashara anahusika na bidhaa au huduma ambayo tayari imekwishafahamika utaratibu wake wa jinsi ya kutengeneza na kuuza.

Saturday, May 18, 2019

Producer S2kizzy afunguka “Eti kupewa gari na Rayvanny ni kiki ? awataja wasanii hawa wakubwa anaotamani sana kufanya nao kazi (+Video)

Mtayarishaji wa muziki hapa nchini Tanzania S2kizzy amefunguka na kueleza juu ya yeye kupewa gari na msanii kutoka WCB Rayvanny kuonekana kuwa ni kiki, kupitia mahojiano aliyofanya na Bongo5 S2kizzy ameeleza za sababu za kupewa gari lakini pia kupewa Tsh mil mbili na Diamond Platnumz. na kuongelea mambo mengine mengi. msikilize S2kizzy:- By Ally Juma. …

The post Producer S2kizzy afunguka “Eti kupewa gari na Rayvanny ni kiki ? awataja wasanii hawa wakubwa anaotamani sana kufanya nao kazi (+Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Thursday, May 16, 2019

Paul Pogba atembelea Mecca na kuandika ujumbe huu ‘Kamwe usisahau vitu muhimu katika maisha’

Nyota wa Manchester United, Paul Pogba amewasili mji mtakatifu kwa imani ya dini ya Kiislam wa Mecca (Maka) katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ameonekana akiwa karibu kabisa na al-Ka bah ambayo ipo kwenye nchi ya Saudi Arabia mara baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu. …

The post Paul Pogba atembelea Mecca na kuandika ujumbe huu ‘Kamwe usisahau vitu muhimu katika maisha’ appeared first on Bongo5.com.


Source

Watu 80 Wakamatwa Kwa Kula Mchana Wakati wa Ramadhan


Polisi wanaosimamia sheria ya kiislam (Sharia) katika jimbo la Kano nchini Nigeria wamewashikilia watu 80 kwa tuhuma za kula mchana hadharani, wakati wa mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Polisi hao ambao wanafahamika kama Hisbah wameeleza kuwa watu hao walishikiliwa katika maeneo mbalimbali kwenye jiji la Kano ndani ya kipindi cha siku chache zilizopita.

Jimbo la Kano ni moja kati ya majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria ambayo yanafuata sheria ya kidini (Sharia) tangu mwaka 2000, lakini wanazingatia pia sheria za nchi.

Msemaji wa Polisi wa Hisbah katika jimbo hilo, Adamu Yahaya ameiambia BBC kuwa watu hao waliokamatwa ni waumini wa dini ya Kiislam na kwamba maafisa wa jeshi hilo hawawakamati watu ambao sio waumini wa dini hiyo kwakuwa sheria za kiislam haziwahusu.

Alisema kuwa baadhi ya watu waliokamatwa waliwaambia maafisa wa polisi kuwa walikuwa wanakula kwa sababu wao binafsi hawakuuona mwezi ukiandama, na wengine walitoa sababu za ugonjwa ambazo zilionekana kuwa hazina mashiko.

Hata hivyo, Yahaya alisema kuwa watu hao wote 80 waliachiwa huru kwa sababu walibainika kuwa walifanya kosa hilo kwa mara ya kwanza.

Hisbah wameeleza kuwa wataendelea na msako wao katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na watawakamata waislamu wote ambao hawafuati masharti ya kufunga katika kipindi hiki bila kuwa na sababu za msingi.

CHADEMA WAZUNGUMZIA SINTOFAHAMU INAYOENDELEA BUNGE LA AFRIKA (PAP) , SPIKA NDUGAI NA MASELE


Makamu wa rais wa Kwanza wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akiendelea na shughuli za bunge la Afrika leo Mei 16,2019,Midrand,Johannesburg nchini Afrika Kusini, juu ni Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akiendesha kikao cha bunge .

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kumekuwa na taarifa zinazosambaa katika njia mbalimbali za upashanaji habari mitandaoni na baadae kwenye vyombo vya habari tangu asubuhi ya leo kuhusu kile kinachoonekana kuwa ni sintofahamu kubwa inayoendelea katika Bunge la Afrika (PAP) ambako taarifa zimedai kuwa Rais wa PAP, Roger Nkodo Dang anatakiwa kujadiliwa na Bunge hilo kutokana na tuhuma nzito zinazomkabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, unyanyasaji wa kingono, upendeleo na unyanyasaji kwa wafanyakazi wa Ofisi za Makao Makuu ya Bunge hilo, nchini Afrika Kusini.

Taarifa hizo za maneno zilizokuwa zikisambaa zilipewa nguvu na video fupi iliyorekodiwa ikimuonesha Makamu wa Rais wa PAP, Stepehen Maselle (ambaye ni mmoja wa wawakilishi wanne katika PAP) akizungumza wakati akiongoza mojawapo ya vikao vya Bunge hilo vinavyoendelea nchini Afrika Kusini kwa sasa, ambapo amesikika (tafsiri yetu ya Kiswahili) akimlalamikia Rais wa PAP kuwa amemwandikia barua Spika wa Bunge la Tanzania ili amrejeshe Stephen Masele nchini (recalling) ili ikiwa ni namna ya Rais huyo kupambana kuzuia agenda au taarifa ya Kamati Maalum iliyoundwa kuchunguza tuhuma zake isisomwe, kujadiliwa au kufanyiwa kazi na Bunge hilo. Katika video hiyo Mbunge huyo amesikika akisema anayo ruhusa kutoka kwa Waziri Mkuu (Serikalini) hivyo hataondoka nchini Afrika Kusini kama ambavyo Rais huyo wa PAP anataka iwe, katikati ya mapambano yake ya kujisafisha na tuhuma hizo nzito zinazomkabili.

Kabla Watanzania hawajaelewa hasa kinachoendelea, kutokana na mkanganyiko huo ambao umeanza kushika kasi kwenye vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, Spika wa Bunge Ndugu Job Ndugai ametoa taarifa ya Bunge akithibitisha maneno yaliyokuwa yakisambaa mitandaoni kuwa Bunge limemuagiza Stephen Maselle arejee nyumbani haraka kuja kujibu tuhuma za ukosefu wa maadili zinazomkabili mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge pamoja na Kamati ya Maadili ya Chama chake.

Katikati ya mkanganyiko huu, CHADEMA inapenda kuweka msimamo wake wazi kuwa jina la nchi yetu Tanzania lisitumike vibaya wala kuwekewa taswira hasi na kuendelea kuharibu sura yetu kidiplomasia na katika mahusiano ya kimataifa.

Tunasema hivyo tukiwa na taarifa za uhakika kuwa PAP ililazimika kuunda Kamati Maalum kuchunguza tuhuma hizo nzito zinazomkabili Rais wake, Roger Nkodo Dang, za unyanyasi wa kingono kwa watumishi wa kike walioko Makao Makuu ya PAP (imedaiwa takriban wanawake 10 wamejitokeza mbele ya kamati kuthibitisha walivyonyanyaswa kingono bila ridhaa yao), matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo dani ya bunge hilo na unyanyasaji kwa watumishi wa ofisi hiyo hali iliyosababisha kuwepo kwa mgomo wa watumishi kwa takriban wiki nzima.

Taarifa tulizozipata kutoka ndani ya Bunge hilo zimedai kuwa Rais Roger Nkodo Dang anatumia njia mbalimbali kupambana kujisafisha na tuhuma hizo kwa sababu mbali ya kupoteza nafasi yake hiyo kwenye Bunge la PAP, iwapo zikithibitika kuwa ni kweli, pia zitamuondolea kinga za kidiplomasia alizonazo, huku ikijulikana wazi kuwa tuhuma hizo zinazomkabili ni mojawapo ya makosa makubwa ya kijinai yanayochukuliwa kwa uzito mkubwa nchini Afrika Kusini.

Katika mazingira hayo, kitendo cha Bunge kumrejesha nyumbani kwa haraka Makamu wa Rais wa PAP, Stephen Masele ambaye kiutaratibu ndiye aliyetakiwa kuongoza vikao vya Bunge hilo vinapojadili taarifa ya Kamati Maalum kuhusu tuhuma za Rais na kusimamia utekelezaji wa maazimio, inaibua shaka kubwa na kujenga taswira hasi kwa nchi yetu kuwa inatumika au inataka kutumika kumuokoa Rais Roger Nkodo Dang dhidi ya tuhuma hizo au haitaki kuonekana kuwa imesimamia na kuongoza taratibu zinazotakiwa katika suala linalomsibu na pengine kitakachofuatia.

Hivyo basi ili kuiweka nchi yetu katika mahusiano mazuri ya kimataifa na kuendeleza sifa yetu iliyojengwa kwa miaka mingi huko nyuma kuwa Tanzania inasimamia misingi na taratibu na kuondoa kadhia itakayoijengea nchi yetu picha mbaya, si ndani ya nchi pekee mbali kimataifa pia, tunalitaka Bunge (lililomrejesha nyumbani Stephen Masele) na Serikali ya Tanzania ambayo imedaiwa kumwagiza Stephen Masele aendelee kubaki huko hadi amalize majukumu yake, kutoa kauli ya msimamo wetu Tanzania kuhusu tuhuma zinazomkabili Rais wa PAP. Je ni kweli tunaunga mkono unyanyasaji wa kingono? Je tunaunga mkono matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo rushwa? Je tunaunga mkono unyanyasaji? Je tunaunga mkono upendeleo katika taasisi hiyo ya kimataifa?

Ni msimamo huo pekee utaweza kuiokoa Tanzania katika jambo hilo ambalo limeanza kuchukua mkondo mbaya kuwa nchi yetu inatumika kulinda tuhuma za uhalifu wa kijinai.
Aidha, kwa sababu Spika wa Bunge ameshalizungumzia na kulitolea taarifa suala hilo hatua iliyomaliza utata wa iwapo taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zilikuwa za kweli, tunalitaka Bunge kuweka wazi tuhuma zinazomkabili Mbunge Stephen Masele zilizosababisha arejeshwe nchini na uwakilishi wake (wa nchi) katika taasisi hiyo ya kimataifa kusitishwa.

Halikadhalika, CHADEMA inaitaka mihimili ya Serikali na Bunge kutoka hadharani na kutoa kauli kuueleza umma juu ya madai kuwa kuna hali ya mgongano wa kauli, misimamo na maamuzi baina ya mihimili hiyo miwili juu ya suala hilo, kiasi ambacho kimeanza kuleta athari katika uwakilishi wa nchi yetu kwenye PAP. Kauli ya mihimili hiyo itawasaidia wawakilishi watatu wa Tanzania waliosalia kwenye PAP kujua misingi ya hoja zao na masuala wanayotakiwa kusimamia katika mtanziko huu uliopo.

Imetolewa leo Alhamis, Mei 16, 2019 na;


TRA Tarime wapokea maombi 152 ya msamaha wa kodi ya majengo


Na Timothy Itembe-Mara

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Wilaya Tarime mkoani Mara kwa kuzingatia sheria ya Mamlaka ya mapato Tanzania namba 9 sura ya 399 sheria ya kodi ya majengo namba 2 sura ya 289 na sheria ya fedha ya serikali za mitaa namba 9 sura ya 290 wamepokea maombia 152 ya msamaha wa kodi kwa wazee na walemavuili kuyafanyia kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake meneja TRA Wilaya Tarime mkoani hapa, Frank Lwesya alisema kuwa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)ina jukumu la kusimamia na kukusanya kodi ya majengo kwa hali hiyo wamepokea maombi 152 kutoka kwa wazee ili kuyafanyia kazi kwa mwaka wa fedha 2019.

"Majengo yaliyosamehewa na serikali kulipa kodi ya majengo kwa mujibu wa sheria ni pamoja na Nyumba moja ambayo inapaswa kulipiwa kodi ya majengo ambayo inamilikiwa na kuishi na Mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka sitini (60) au Nyumba anayoishi mlemavu ambaye hana kipato chochote ambapo TRA Tarime tumepokea maombi 152 kati yao maombi 2 yamefanyiwa kazi na wamiliki wamesamehewa kodi ya majengo huku maombi  mengine yanafanyiwa kazi"alisema Lwesya 

Kwa upande wake Afisa Kodi TRA Wilaya Tarime,Taiboye Mwita alisema kuwa maombi hayo ni ya kila mwaka kwa kuzingatia sheria ya mamlaka ya mapato Tanzania TRA inayowataka wamiliki kutuma maombi kwa kila mwaka ili kufanyiwa tadhimini na maafisa wa TRA kuhakiki umiliki kwa kila muombaji.

Mwita aliongeza kuwa Mamlaka hiyo inafanya hivyo ili kuepuka mgongano na wamiliki wa Nyumba kubadilika kila mwaka ambapo katika tadhimini wanawatumia wenyeviti wa mitaa,Vitongoji na wale wa serikali za vijiji pamoja ma watendaji wao ili kupata  uhakika zaidi na endapo mmiliki hana nyumba ya pili na nyumba ya biashara  anapaswa kusamehewa kodi kama serikali ilivyoelekeza.


Wednesday, May 15, 2019

Hii Hapa Ratiba ya leo Ligi Kuu Soka Tanzania Bara

Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) inatarajiwa kutimua vumbi tena leo ambapo timu nne zitashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu. Chini ni ratiba ya michezo ya leo iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF

Source

Namna ya kuishi na ndugu wa mume


Ndoa nyingine zinaingia kwenye migogoro kutokana na kuingiliwa na ndugu wa mme pamoja na gubu za wanawake wa siku hizi, pamoja kwamba hawa wanawake wa siku hizi hawana uvumilivu na ni wakorofi haswa, lakini wakati mwingine ndugu wanaweza kuwa tatizo kwenye mahusiano yako wewe mwenza wako.

Wanaume wengi tumekuwa tukilichukulia hili suala kijuu juu lakini inawaumiza wenza wetu, jambo la kufanya kama mwanaume ijue tabia ya mkeo, na ndugu zako, kuna wanawake wanaficha makucha lakini hakikisha unaigundua, ili linapotokea tatizo iwe ni rahisi kufanya uchunguzi wako na kugundua nani mkorofi na ni nani ana matatizo.

Ishi mbali na ndugu zako kama mama unaweza kumjengea nyumba mbali na unapoishi ukawa unatuma mahitaji yote huko,utashangaa urafiki utakaokuwepo kati ya mkeo na mamako, hata akitaka kuja kukusalimia asikae muda mrefu sana mpaka kujenga mazoea.

Wakanye ndugu wengine wasiingie ndoa yako, kama kuna anachombeza vimaneno mpe onyo kali ambalo linamfanya aongoze, kitendo cha kuruhusu kuwasikiliza ndugu hupelekea kuletewa maneno ambayo huleta misukosuko kwenye ndoa.

Vilevile hata kama mke analeta maneno naye aonywe.Usiruhusu dada zako kuzoea kwako kama wameolewa wakae kwao watulie na familia zao hizi habari za kuja kuishi kwako mara kwa mara zinaweza sababisha migogoro kati yao na mke.

Kwa upande wa wanawake,mchukulie mama mkwe kama mzazi wako chochote atakachokutamkia kichukulie kawaida, lakini kabla ya kuolewa tambua kuna karaha kama hizo za ndugu wa mme na jua jinsi ya kukabiliana nazo.

Dogo Janja Atoboa Siri Yake na Nandy

MSANII wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende 'Dogo Janja' amefichua siri yake na msanii mwenzake, Faustina Charles 'Nandy' kwa kusema kuwa akiwa naye popote pale familia yake huwa na amani.



Dogo Janja aliyazungumza hayo leo katika mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 GLOBAL RADIO ambapo alisema kuwa, alijuana na Nandy kabla hata hajaanza muziki.


"Nandy ni mshikaji wangu tangu zamani sana. Nakumbuka tangu hajaanza muziki wala kushiriki yale mashindano ya kuimba ambayo yalimtoa (Tekno Own Stage) yaliowahi kufanyika nchini Kenya na Nigeria.



"Ujue damu zetu zinaendana sana na ni mtu ambaye hata familia zetu zinafahamiana. Leo Nandy atakuja kwetu na mimi hivyohivyo kwao kwa hiyo hata nikiwa naye popote familia yake inakuwa na amani kabisa," alisema Dogo Janja.


Mbali na hilo, Dogo Janja pia alimuongelea msanii wa Bongo Fleva, William Lyimo 'Billnass' ambaye alidaiwa kutoka na Nandy kipindi cha nyuma kuwa akimuonea wivu atashangaa sana.


"Billnas hata akihisi kitu chochote kibaya kwangu mimi na Nandy atakuwa ni mtu wa ajabu sana. Ngoja nikwambie kitu, nikiwa na Nandy hakuna chochote kibaya kinaweza kutokea kati yetu," aliongeza Dogo Janja

Thursday, May 9, 2019

Picha : MWILI WA DR MENGI WAZIKWA NYUMBANI KWAO MACHAME - MOSHI


Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited, Dkt. Reginald Mengi umezikwa katika makaburi ya familia yao yaliyopo nyumbani kwa wazazi wake, Nkuu, Machame, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, leo Alhamisi, Mei 9, 2019.

Mazishi ya Dkt. Mengi ambayo yameanza na ibada katika Kanisa la KKKT, Usharika wa Moshi Mjini, yamehudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika Job Ndugai, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge, viongozi wa dini, siasa na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.

Mengi ameacha simanzi kubwa kwa Watanzania wengi kutokana na ukarimu wake katika kuwasaidia watu mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu, vijana, wazee na maskini ili kujikwamua katika wimbi la umaskini.

Akihubiri wakati wa ibada ya kuaga mwili huo, Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Fredrick Shoo amemtaka Spika Job Ndugai, Bunge na wote wenye mamlaka wakatende haki kwa watu wote.

"Nashukuru Mheshimiwa Ndugai uko hapa. Kazi ya Bunge ni kutetea maslahi ya wananchi. Teteeni maslahi ya wananchi mnaowawakilisha, kama kweli tunasema tumejifunza kutoka kwa Dk Mengi," amesema Dkt. Shoo.

Mengi alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita, Mei 2, 2019, nchini Dubai katika Falme za Kiarabu na mwili wake uliwasili nchini Jumatatu, Mei 6 kabla kuagwa Karimjee na kusafirishwa kwenda Machame ambako umezikwa leo.

Ameacha mjane, Jacqueline Ntuyabilwe, watoto wanne ambapo watatu ni wa kiume na mmoja wa kike.


Iran yatishia kurejea katika matumizi ya nyuklia

Baraza la Usalama la Taifa la Iran limeamua kusitisha mara moja baadhi ya ahadi zake ilizozitoa chini ya mkataba wake wa nyuklia na nyengine katika siku 60 zijazo, iwapo hakutakuwa na hatua zozote kushughulikia mkwamo wa kiuchumi unaolikabili taifa hilo.

Katika barua yake kwa mataifa yaliyoendelea kusalia kwenye makubaliano hayo ambayo Marekani ilijitoa, Iran imelalamikia kusitasita kwa makampuni ya mataifa hayo kufanya biashara nayo.

Viongozi wa China, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Urusi wamepokea barua hiyo, lakini walengwa zaidi ni viongozi wa mataifa ya Ulaya walioshindwa kutimiza ahadi zao ambazo zingesaidia kufufua uchumi wa Iran.

Wataalamu wameliambia shirika la habari la AFP kwamba mkataba huo wa nyuklia unazitaka nchi zilizoweka saini kuimarisha uchumi wa Iran, lakini makampuni ya nchi za Ulaya bado yanaogopa kufanya biashara na Iran kwa hofu ya kuwekewa vikwazo na Marekani.

VIDEO: Mamia wafurika mwili wa Mengi ulivyoingizwa kanisani


Viongozi mbali mbali pamoja na wananchi wamejumuika kwa pamoja   kumuaga mpendwa wa watu Dk. Reginald Mengi kwa sala ya mwisho katika kanisa la KKKT Moshi Mjini.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USIKOSE KU-SUBSCRIBE

Wednesday, May 8, 2019

Askofu Gwajima mbele ya mkewe aeleza chanzo cha video ya ngono inayosambaa mitandaoni, adai hatobadili msimamo wake uchaguzi 2020 (+Video)

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu video ya ngono inayoonesha mtu mwenye sura inayofanana na yeye kusambaa mitandaoni.

The post Askofu Gwajima mbele ya mkewe aeleza chanzo cha video ya ngono inayosambaa mitandaoni, adai hatobadili msimamo wake uchaguzi 2020 (+Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka, ni mtu aliye jaliwa kubuli Shufaa pia anatoa Duah  za Ruhia. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho,  UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu  Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!? Muone Akutatulie,
 
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa..Unataka nyota ing'ae Au huna hamu na Mkeo/ Mumeo.
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa.
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu.Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN

Mawasiliano: Sheikh Omary 0673531992 WhatsApp/Call
Tembelea Page ya @Mtabibu_Omar  @Mtabibu_Omar
Usome Makala Tofauti Tofauti Kama.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...