Thursday, May 16, 2019

TRA Tarime wapokea maombi 152 ya msamaha wa kodi ya majengo


Na Timothy Itembe-Mara

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Wilaya Tarime mkoani Mara kwa kuzingatia sheria ya Mamlaka ya mapato Tanzania namba 9 sura ya 399 sheria ya kodi ya majengo namba 2 sura ya 289 na sheria ya fedha ya serikali za mitaa namba 9 sura ya 290 wamepokea maombia 152 ya msamaha wa kodi kwa wazee na walemavuili kuyafanyia kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake meneja TRA Wilaya Tarime mkoani hapa, Frank Lwesya alisema kuwa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)ina jukumu la kusimamia na kukusanya kodi ya majengo kwa hali hiyo wamepokea maombi 152 kutoka kwa wazee ili kuyafanyia kazi kwa mwaka wa fedha 2019.

"Majengo yaliyosamehewa na serikali kulipa kodi ya majengo kwa mujibu wa sheria ni pamoja na Nyumba moja ambayo inapaswa kulipiwa kodi ya majengo ambayo inamilikiwa na kuishi na Mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka sitini (60) au Nyumba anayoishi mlemavu ambaye hana kipato chochote ambapo TRA Tarime tumepokea maombi 152 kati yao maombi 2 yamefanyiwa kazi na wamiliki wamesamehewa kodi ya majengo huku maombi  mengine yanafanyiwa kazi"alisema Lwesya 

Kwa upande wake Afisa Kodi TRA Wilaya Tarime,Taiboye Mwita alisema kuwa maombi hayo ni ya kila mwaka kwa kuzingatia sheria ya mamlaka ya mapato Tanzania TRA inayowataka wamiliki kutuma maombi kwa kila mwaka ili kufanyiwa tadhimini na maafisa wa TRA kuhakiki umiliki kwa kila muombaji.

Mwita aliongeza kuwa Mamlaka hiyo inafanya hivyo ili kuepuka mgongano na wamiliki wa Nyumba kubadilika kila mwaka ambapo katika tadhimini wanawatumia wenyeviti wa mitaa,Vitongoji na wale wa serikali za vijiji pamoja ma watendaji wao ili kupata  uhakika zaidi na endapo mmiliki hana nyumba ya pili na nyumba ya biashara  anapaswa kusamehewa kodi kama serikali ilivyoelekeza.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...