Tuesday, May 28, 2019

TAKUKURU yamkabidhi Nyalandu Polisi kwa mahojiano

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Singida imewakabidhi kwa jeshi la polisi mkoani humo wanachama watatu wa CHADEMA akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini na waziri wa awamu ya nne Bwana Lazaro Nyalandu kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Singida Bwana Joshuwa Msuya ambapo ameeleza kuwa imewalazimu kuwakabidhi kwa jeshi la polisi wananchama hao kwa madai ya kuwa walikuwa wakifanya mikutano bila kibali ya nyumba kwa nyumba katika kijiji cha Itaja halmashauri ya Singida.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Sweetbert Njewike amesema kuwa wananchama hao watatu waliwekwa katika kituo cha polisi cha kati kwa ajili ya hifadhi, lakini TAKUKURU wao wenyewe bado wanaendelea na uchunguzi.

Katika hatua nyingine Bwana Msuya amewataka wananchi hasa wana siasa kuacha kujihusisha na uvunjaji wa sheria kwa kufanya mikutano bila vibali na kujihusisha na rushwa kwani taasisi ya kupambabana na rushwa itawakamata.

Mei 27, 2019, TAKUKURU mkoa wa Singida ilithibitisha kuwakamata na kuwahoji wanachama watatu wa  chama cha CHADEMA, kwa tuhuma za rushwa akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini na waziri katika serekali ya awamu ya nne Bwana Lazaro Nyalandu.

Nyalandu na wenzake walishikiliwa na TAKUKURU wakati Wakiwa kwenye kikao

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...