Sunday, September 30, 2018

Waziri Mwakyembe Awataka Wasanii wa Filamu kuthamini kazi Zao


Na Anitha Jonas – WHUSM – MWANZA
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wasanii wa filamu nchini kutambua thamani ya kazi zao za filamu.


Mheshimiwa Mwakyembe  ametoa agizo hilo leo jijini Mwanza alipokuwa akizindua filamu ya BROTHER  iliyotengenezwa na wasanii wa filamu wa mkoa huo kwa kushirikiana na msanii mkongwe wa filamu Bi.Johary Changula.


"Kwanza niwapongeze kwa kazi nzuri mliyofanya nimeanza kuona mabadiliko katika tansia hii sasa, kuna mabadiliko makubwa katika upande wa sauti, mwanga na hata namna ya uigizaji ongezeni bidii mkiendelea hivi mtapata mafanikio makubwa na pia msipende kuuza kazi zenu nje kwa bei chini tofauti kazi za nchi jirani,"alisema Dkt.Mwakyembe.


Akiendelea kuzungumza na Waziri Mwakyembe aliupongeza uongozi wa ukumbi wa Sinema wa Misterious wa jijini Mwanza kwa kutenga siku mbili ambazo ni Ijumaa na Jumamosi kwa ajili ya kuonyesha filamu za Kiswahili kutoka ndani ya nchi hii ni hatua kubwa ya uthubutu ningependa kuona na kumbi zote nchini zinaiga mfano huo.


Aidha,Nae Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alifafanua kuhusu  changamoto ya upatikanaji wa stempu za TRA kwa kazi za filamu kwa kusema kuwa tayari serikali imeshaanza  kulishughulikia suala hilo kwa kuaandaa nakala laini ya stempu hizo zitakazo sambazwa katika ofisi za TRA mikoani ili kuondoa kero hiyo.


"Kufuatia maombi yenu ya kuitaka ofisi yangu ije tena kwa ajili ya kutoa elimu ya uandaaji wa kazi za filamu basi tutajipanga na tutahitaji kuona wadau wengi wakifika ili tuweze kuhakikisha wadau wa filamu wanaanda  kazi bora mara baada ya kupata elimu ya uaandaji wa miswada ya filamu,"alisema Bibi.Fissoo.


Pamoja na hayo Katibu Mtendaji huyo aliendelea kusisitiza kuwa ukaguzi wa kazi za filamu kwa mikoani upo kisheria chini ya bodi ya filamu katika Halmashauri ambapo inaongozwa na Afisa Utamaduni hivyo siyo lazima kazi ya filamu ipekwe katika ofisi za Bodi ya Filamu Dar es Salaam kwa ukaguzi.


Halikadhalika nae Mwenyekiti wa Chama cha Waandaji wa Filamu Mkoa wa Mwanza Bw.Abdallah Mohamed  alimweleza Waziri Mwakyembe kuwa umoja huo unatarajia kujenga jego la uandaaji wa kazi za filamu kwa kushirikiana na wawekezaji.

HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA YANGA LEO

Leo 30.9.2018 ni siku ya pambano la watani wa jadi kati ya SImba na Yanga mechi ya ligi kuu soka ya Tanzania Bara TPL.
Kuelekea mchezo huo tayari makocha wa timu hizo wameonekana kuwa na vikosi wanavyoviandaa kwaajili ya mechi ya Leo.
Kocha Patrick Aussems kwa siku za Karibuni akiwa na Kikosi cha Simba amekuwa akitumia Kikosi hiki kikionekana ndicho anachokiandaa kwaajili ya Pambano dhidi ya Yanga.
Golini Aishi Manula akisaidiwa na mabeki wa kulia na Kushoto Shomari Kapombe na Mohammed Hussein Zimbwe.
Mabeki wa Kati Erasto Nyoni na Pascal wawa ambao toka ligi kuu imeanza wamekuwa wakicheza kama beki pacha.
Eneo la kiungo Jonas Mkude, Cletous Chama huku James Kotei akicheza kama namba 7 ambaye anasidia zaidi eneo la katikati ya uwanja huku winga ya Kushoto Shiza Kichuya akionekana kupewa nafasi katika kikosi cha Simba.
Washambuliaji : Emmanuel Okwi na Meddie Kagere ndiyo washambuliaji ambao wamekuwa wakionekana kuanza kwenye kikosi kinachoandaliwa kumuua Yanga leo 30.9.2018.Kukipata Kikosi kwa wakati cha Simba hakikisha Umelike Ukurasa wetu wa Facebook BONYEZA HAPA

Vodacom, govt ICT body in $11m deal

Vodacom Tanzania and the National Information Communication Technology Broadband Backbone (NICTBB) have signed a partnership contract, which brings the total value of pacts inked between the two parties to $45.8 million (about Sh103.5 billion) to date.
Source

Friday, September 28, 2018

Dkt. Mwakyembe: Viongozi wa Kimila Nchini Himizeni Uzalendo na Utaifa

PIXX4
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wazee wa Kimila wa Kimasai Bw. Amani Lukumay (Kulia) baada ya kuwasili katika Chuo cha Ufundi  cha Arusha (Arusha Technical College) kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Kimila wa Wazee hao leo Jijini Arusha.
PIXX5
 Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiongozana na Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai kuelekea mahali ambapo mkutano wa kimila unafanyika.
PIXX%2B1
Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai  Bw. Isack Lekisongo (kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati)  njia ambayo ilikuwa ikitumiwa na Ukoo wa Mollel kuingia  katika eneo  ambalo  hutumika kufanya mila mbalimbali za kabila hilo, eneo hilo limo ndani ya nyumba za Waalimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).
PIXX%2B2
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(Katikati) akijadiliana jambo na Viongozi na Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai , alipohudhuria mkutano wa kimila wa viongozi hao leo Jijini Arusha.
PIXX%2B3
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(Aliyekaa) akipewa fimbo na Mwenyekiti Mstaafu wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai Bw. Langidare Manapi (kulia) ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika kabila hilo, kabla ya kuanza kwa mkutano wa viongozi hao Leo Jijini Arusha.
PIXX%2B6
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(katikati) akisema jambo wakati wa Mkutano wa Kimila wa Viongozi na Wazee wa Kimasai leo Jijini Arusha, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddy Kimata ambaye alimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kulia ni Mwenyekiti wa Wazee wa Kimasai Bw. Isack Lekisongo.
PIXX%2B7

PIXX%2B8
 Viongozi na Wazee Mbalimbali wa kabila la Kimasai wakimsikiliza Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika Picha) alipokuwa akizungumza nao wakati wa mkutano wa kimila wa Wazee hao leo Jijini Arusha. (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha).

Na Lorietha Laurence- WHUSM, Arusha.

Wazira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa rai kwa Viongozi na Wazee wa Kimila nchini , kuhakikisha wanatumia nafasi walizonazo kuhimiza  uzalendo na utaifa kwa kuikumbusha jamii dhawabu ya kudumisha Utamaduni.

Hayo amesema leo Jijini Arusha katika Mkutano na Viongozi na Wazee wa Kimila wa Kabila la Wamasai,ambao hukutana mara kwa mara kujadili  mila na desturi za kabila hilo .

 Aidha Dkt. Mwakyembe amesisitiza kuwa viongozi wa kimila wana nafasi kubwa ya kujenga na kudumisha mila na desturi kwa kurithisha tamaduni hizo kwa kizazi kilichopo ili kutokupoteza tamaduni hizo muhimu.

"Kumbukeni kuwa mnanafasi kubwa ya kulea jamii yetu kwa misingi ya mila na desturi  nzuri ,kwa kuwa jamii inawasikiliza, inawaelewa na kuwaheshimu " amesema Dkt. Mwakyembe.

Anazidi kufafanua kuwa kwa kutumia mila na desturi nzuri itasaidia kurejesha vijana ambao kwa asilimia kubwa wameadhiriwa na maendeleo ya Teknolojia na Utandawazi,hivyo kuupuza utamaduni wa mtanzania .

Vilevile Dkt. Mwakyembe amewaahidi viongozi hao kufanyia kazi changamoto wanayokumbana nayo   kuhusu eneo la kukutania lililopo ndani ya Chuo Cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).

Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddy Kimata ameahidi kushirikiana na Mhe. Dkt. Mwakyembe katika kuhakikisha  changamoto hiyo inapata ufumbuzi ili kudumisha urithi wa Utamaduni.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Kimasai Bw. Isack Lekisongo kwa niaba ya Wazee wenzake ameahidi kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kuhakikisha mila na desturi zinadumishwa na kuheshimiwa .

Video: Sheikh aliyefungisha ndoa ya Sister Fey na Hollystar ‘kijana amebadili dini baada ya wazazi wake kukubali’

Shehk Yahaya Hussein kutoka Msikiti wa Zaidu Tabata amefunguka kuzungumzia jinsi alivyomfungisha ndoa Sister Jay na @holystar_holystar ambaye amebadili dini.

The post Video: Sheikh aliyefungisha ndoa ya Sister Fey na Hollystar ‘kijana amebadili dini baada ya wazazi wake kukubali’ appeared first on Bongo5.com.


Source

Nyota Hawa wa Yanga Kuikosa Mechi yao Dhidi ya Simba

Nyota Hawa wa Yanga Kuikosa Mechi yao Dhidi ya Simba
Klabu ya soka ya Yanga, huenda itawakosa nyota wake wawili kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara (TPL), Jumapili dhidi ya watani wao wa jadi Simba.

Kwa mujibu wa meneja wa kikosi hicho ambacho kimepiga kambi mkoani Morogoro, Nadir Haroub Cannavaro, wachezaji Juma Mahadhi na Juma Abdul hali zao bado si nzuri.

''Kambi inaendelea vizuri hapa Morogoro na wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo isipokuwa beki wetu Juma Abdul na mshambuliaji Juma Mahadhi ambao bado ni majeruhi na hawapo tayari kwa mchezo wa Jumapili'', amesema Cannavaro.

Cannavaro ameeleza kukosekana kwa wachezaji hao hakutaathiri chochote kwani wachezaji waliopo wanauwezo wa kuipa timu matokeo kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Singida United ambapo walikosekana Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa na Heritier Makambo, lakini timu ilipata ushindi.

Mchezo huo wa jumapili utakuwa wa tano kwa Yanga SC msimu huu, ambapo tayari wamecheza mechi 4 na kushinda zote. Wana alama 12 katika nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi.

Gigy Money Ampigia Magoti Mh Rais.

Msanii wa bongo fleva na ‘video vixen’ nchini, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameiomba serikali ya Magufuli kuwapa msaada watanzania hususani wasanii, katika kulinda kazi zao sanaa ili kusudi waweze kutuliza akili zao sehemu moja nasio kutanga tanga na maisha. Gigy Money ameeleza hayo alipokuwa anapiga stori na www.eatv.tv na kusema kwamba wasanii wapo tayari kubadilisha maisha yao ya mtandaoni na kufuata vile sheria za nchi zitakavyo, ila na wao wawaangalie namna ya kuwawezesha. “Naiomba serikali ituangalie na sisi wasanii katika kazi zetu maana tunabanwa sana ndio maana utakuta wasichana wanaamua kujifyatua akili zao ili mradi apate pesa kwa njia yoyote, aweze kukizi mahitaji yake…..Tupo tayari kubadilika ila na wao tunaomba watusaidie baadhi ya vitu. Ninaamini sio mimi pekee yangu bali ni Tanzania nzima wanahitaji msaada, sema sisi tupo kwenye uoga sana, yaani watanzania wote ni waoga sana tena hususani wasanii pale inapokuja suala la kufungiwa kazi zao”, amesema Gigy Money. Gigy Money ametoa kauli hiyo baada ya kupewa onyo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii na endapo hatofanya hivyo basi watamchukulia sheria stahiki dhidi yake.

The post Gigy Money Ampigia Magoti Mh Rais. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

Thursday, September 27, 2018

Hizi ndizo Dalili za awali za kuharibika kwa Mimba


Leo tumeamua kuzungumzia jambo hili ambalo huwakumba watu wengi sana katika familia zao, wengi wamekuwa wakitokewa na jambo hili katika mimba zao za kwanza na mimba zao zinazoendelea katika familia zao na kushindwa kupata watoto.

Kuna wengine wanapata watoto au mtoto mmoja na baadaye wanashindwa kupata mtoto kwa sababu ya mimba zao kuwa zinaharibika mara kwa mara.

Kwa kawaida kitabibu inaaminika kwamba asilimia 50 ya mimba zote huwa zinaharibika, najua watu wengi wanaweza wakashangaa lakini ni kweli tafiti za kitabibu zinasema hivyo isipokuwa watu wengi huwa hawaelewi au wanawake wengi huwa hawaelewi kama mimba zao zimeharibika kwani hutoka au huaribika kabla wao hawajagundua kama walikuwa wajawazito.

Isipokuwa wale ambao hujua kwamba walikuwa na ujauzito na umetoka hao wanaweza kuwa asilimia 10 hadi 20, na hizo asilimia zinazobaki kama 35 ni kwa wale ambao hawajui kama mimba zao zimeharibika au walikuwa wajawazito.

Kwa maana hiyo basi wewe ambaye unatafuta ujauzito kwa muda mrefu sasa na umekuwa haupati lakini unakuwa unaandamwa na matatizo ya hedhi kwa mara kadhaa halafu hedhi inakaa sawa basi kuna uwezekano mkubwa kwamba mimba zako zimekuwa zikiharibika pasipo wewe kujua.

Dalili za kuharibika kwa mimba
Ni vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika hadi wiki ya 20 (miezi 5) kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasahasa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) lakini huweza fika hadi wiki ya 20.

Na dalili hizo ni kama;

Damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba.
pale mwanamke anapopata ujauzito basi ni vema kabisa kujua kwamba hatakiwi kabisa kupata hedhi au kutokwa na damu katika via vyake vya uzazi, kwa maana hiyo basi wewe mwanamke ambaye umepata ujauzito na bado unaona damu inatoka kidogokidogo basi ni vema kuwahi mapema kituo cha afya kabla tatizo halijawa kubwa kwani kutoka kwa mimba (miscarriage) huwa hakutokei ghafla tu huanza taratibu na dalili yake kubwa ni hii kutokwa na damu ilihali wewe ni mjamzito.

kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito
Wakati mwingine  mwanamke anaweza akakumbwa na kutokwa na damu nyepesi na kabla hajatahamaki, damu ile nzito inaanza kutoka tena, na hii ni dalili mbaya sana ya kwamba ujauzito wako uko kwenye hatari zaidi na kuna uwezekano ujauzito ulionao ukatoka, kwa maana hiyo basi mwanamke anapopatwa na dalili ile ya kwanza ni vema zaidi kufuata ushauri wa daktari ili kuulinda ujauzito wako.

Uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo.
kwa wewe mwanamke ambaye mimba bado ni changa na unapatwa na maumivu makali sana ya mgongo au kiuno au vyote kwa pamoja basi ni vema kuwahi kituo cha afya ili kuangalia ni jinsi gani unaweza kuzuia ujauzito wako usitoke au usikumbwe na tatizo hili la kutokwa na ujauzito (miscarriage).

Kama unapatwa na dalili kama hizi kutokwa na damu nyepesi au nzito ilihali wewe ni mjamzito basi ni vema kuwahi kituo cha afya au wasiliana nasi ili kukusaidia. Kwa ushauri vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.

Nilikuwa tayari kuwa mke wa pili kwa Diamond kama angemuoa Zari – Hamisa

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka kwa kudai kwamba yeye kwa Diamond alikuwa tayari kuwa mke wa pili kama muimbaji huyo angemuoa Zari The Boss Lady. Wawili hao kwa sasa ameachana na wamekuwa wakitupiana maneno mtandaoni baada Diamond kuanza kuzungumzia madai ya kwamba familia yake inarogwa na mrembo huo. Akiwa nchini Kenya Mobetto amefunguka kwa kudai kwamba …

The post Nilikuwa tayari kuwa mke wa pili kwa Diamond kama angemuoa Zari – Hamisa appeared first on Bongo5.com.


Source

Hayo Mazoezi ya Simba Balaa Tupu

Hayo Mazoezi ya Simba Balaa Tupu
Baada ya Simba kubaki jijini Dar na kuweka kambi katika Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach, jana Jumatano kikosi hicho kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko.

Katika mazoezi hayo, uongozi wa Simba uliwawekea ulinzi mkali nyota wake hao kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika mazoezi hayo ya jana, licha ya mashabiki kuwepo hapo uwanjani lakini kulikuwa na makomandoo kadhaa ambao walikuwa wanazungu kazunguka wakati mazoezi yakiendelea.

Hata hivyo, katika mazoezi hayo, wachezaji wa Simba walionekana kufanyishwa mazoezi ya nguvu na makocha wa kikosi hicho.

Katika zoezi hilo, wachezaji walionekana wakipambana licha ya baadhi yao kulalamika kutokana na aina ya mazoezi ambayo walikuwa wanayafanya kuonekana ni ya nguvu.

Katika mazoezi hayo, Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin ndiyo wachezaji ambao hawakufanya mazoezi na wenzao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ni majeruhi.

Katika mazoezi hayo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Masoud Djuma alionekana uwanjani akiendelea na majukumu yake kama kawaida licha ya kwamba hapo awali hakusafiri na timu ilipokwenda kucheza mikoani ikiripotiwa kutokuwa na maelewano mazuri na wenzake wa benchi la ufundi.

African journalists set for USD3000 media award on infertility

Dar es Salaam. Journalists in Tanzania and the rest of Africa can now win up to USD 3000 following an announcement by Merck Foundation, a German philanthropic organization that it has opened applications for the 'Merck More Than a Mother' Media recognition Awards 2018.
Source

HATIMAYE KIVUKO CHA MV NYERERE CHANYANYULIWA... HIKI HAPA KIANGALIE


Kivuko cha Mv. Nyerere kikiwa kimegeuzwa na kusimama wima leo mchana. Picha na Jovither Kaijage 

Hatimaye kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Alhamisi Septemba 20, 2018 kimenyanyuliwa leo mchana Alhamisi Septemba 27, 2018.

Kivuko hicho kimenyanyuliwa baada ya jitihada za siku tano tangu Jumapili Septemba 23, 2018 zilizofanywa na wataalam wa uokoaji kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).


Na Peter Saramba, Mwananchi 

    UVCCM YAMTUNUKU HATI MAALUMU YA PONGEZI MBUNGE AZZA HILAL HAMAD


    Umoja wa Vijana wa Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Vijijini kimemtunuku hati maalum ya pongezi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad kwa uongozi bora na wa mfano uliotukuka,kuunganisha na kuimarisha mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi,usimamizi wa vitendo katika utekelezaji wa wa Ilani ya CCM pamoja na ufadhili wa hali na mali kwa chama na jumuiya zake. Pichani ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Cha Mapinduzi Ndugu Kheri Denis James akikabidhi hiyo kwa Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (kushoto) wakati wa ziara yake katika wilaya ya Shinyanga Septemba 26,2018.

    Video: Wema Sepetu amtaja Van Vicker, Diamond na Idris usiku wa Birthday Gala

    Mwanadada Wema Sepetu amefunguka kuhusu maandalizi ya Birthday Gala yake pamoja na Movie premier ya filamu yake mpya ambao umeambatana na ugeni mzito wa msanii mkubwa wa filamu kutoka nchini Ghana, Van Vicker.

    The post Video: Wema Sepetu amtaja Van Vicker, Diamond na Idris usiku wa Birthday Gala appeared first on Bongo5.com.


    Source

    Wednesday, September 26, 2018

    Over Sh13.6 trillion needed for Africa digital identification drive

    The World Bank Group has said that an estimated Sh13.6 trillion ($6 billion) is needed to meet Africa's digital identification and civil registration needs.
    Source

    Dr. Reginald Mengi Aguswa Na Mkakati Wa Rc Makonda Kusaidia Walemavu, Amuahidi Bilion 5


    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika mkakati wake wa kuwapa tumaini jipya watu wenye ulemavu leo ameahidiwa Kiasi cha Shilingi Billion 5 na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi kwaajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachowaajiri watu wenye ulemavu ambao wana ujuzi wa aina mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi.

    Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kueleza mpango wa kuwasiliana na wizara ya ardhi ombi la kupatiwa eneo la kujenga kiwanda cha kuajiri watu wenye ulemavu jambo lililomgusa Dr. Mengi na kuahidi kutoa shilingi billion 5 kuunga mkono mpango huo.

    Hayo yote yamejiri leo wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya kusaidia walemavu ya Dr. Reginald Mengi persons with disabilities Foundation iliyozinduliwa na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambae pia amemsifu RC Makonda kwa agizo alilotoa kwa wenye viwanda kuwapa ajira walemavu kwa mujibu wa sheria na pia kampeni ya miguu bandia inayoendelea kuwasaidia walemavu.

    Aidha RC Makonda pia ameeleza Mkakati wa kukutana na wamiliki wa shule binafsi kwaajili ya kuwaomba kusomesha watoto wawili wenye ulemavu bure kwa kila shule kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari ili kuwawezesha walemavu kupata elimu bora.

    Kwa upande wake Naibu waziri Wizara ya Ajira, Wazee, watoto na watu wenye ulemavu Mhe. Anton Mavunde, Mbunge wa viti maalumu Mhe. Amina Molel na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu wamemshukuru RC Makonda kwa namna anavyopambana kuwakwamua watu wenye ulemavu.

    Fiesta Mwaka Huu..Amsha Amsha Yapungua...List Yajaa Wasanii Wachanga

    Hawa ndo wasanii watakao zindua rasmi msimu was Fiesta 2018 jumamosi hii uwanja was jamuhuri kwa kiingilio Cha 7000
    Belle9
    Fid Q
    Nandy
    Jolie 
    Malkia Karen
    Whozu
    Mr blue
    Jaymolody
    Janjaro
    Z anto
    Luludiva
    Amber Lulu
    Chege
    Bryan Simba

    List ya mwaka huu imejaa Wasanii wengi Wachanga tofauti na mwaka Jana ilipozinduliwa Arusha list ilikuwa yakushiba hasa....

    WAWILI WAUAWA KISHA KUNYOFOLEWA VIUNGO VYAO


    Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo.
    Wakazi wawili wa Kijiji cha Lubanga mkoani Geita wameuwawa kwa kukatwa mapanga na kunyofolewa viungo mbalimbali vya mwili, tukio linalodaiwa kufanywa na watu wasiojulikana na kutoweka na viungo hivyo.

    Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki na waliouawa ni mtu na shangazi yake suala ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.

    Kamanda Mponjoli amewataja waliouawa kuwa ni Kija Lushanga (70) na Pendo Bukelebe (48) ambapo amesema kuwa imani potofu za kishirikina imekuwa jambo la kawaida kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa na ni changamoto kwa Jeshi la Polisi katika majukumu yake kwani matukio mengi yanafanywa na wanafamilia.

    "Kufuatia mauaji hayo jeshi la polisi tumekamata watu wanne kwa mahojiano na uchunguzi bado unaendelea na hatuwezi wataja kutokana na sababu za kiusalama, lakini Kanda ya Ziwa hakuna uelewa wa wananchi kutoamini kuwa imani za kishirikina ni matatizo na wao kujichukulia sheria mkononi", amesema Mponjoli

    Ameongeza kuwa, "Jamii inayozunguka eneo hili inahusisha mauaji haya na imani za kishirikina lakini sisi kama Jeshi la Polisi kwa sasa tunachukulia kuwa ni mauaji isipokuwa tutakapokamilisha uchunguzi ndio tutajua nini kiini cha mauaji na watu kuondoka na viungo hivyo".

    Mkoa wa Geita ni miongoni mwa mikoa yenye matukio ya mauaji ya wanawake kukatwa mapanga kutokana na kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo Mei 17, 2018 Sophia Sitta mkazi wa kijiji cha Mwabasabhi wilayani Chato aliuawa na mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.

    April 05, 2018 wanawake wanne wilayani Nyang'hwale waliuawa kwa kunyongwa kisha miili yao kutupwa porini. Juni 06 ,2018 polisi walimuua kwa kumpiga risasi Panda Kinasa (36) ambaye alikua akiteka watu kudai fedha kisha kuwaua.

    Takwimu za polisi za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa watu 32 walipoteza maisha mkoani Geita kwa kipindi cha miezi mitatu Oktoba Disemba 2015 kutokana na mauji ya kutumia mapanga yanayodaiwa kusababishwa na imani za kishirikina.

    Chanzo- EATV

    Irene Ana Mwili Mkubwa ila Umri Mdogo, Wanaendana na Janjarao :-khadija Kopa

    Mwanamuziki mkongwe wa Taarab nchini Khadija Omar Koppa, amewakingia kifua wanandoa wawili kutoka tasnia ya sanaa ya bongo, Irene Uwoya na Dogo Janja, na kusema kwamba wawili hao wanastahili kuwa pamoja. Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Khadija Kopa amesema kitendo cha watu kumuona Dogo Janja ni mdogo kwa Irene Uwoya si kweli, kwani hata Irene Uwoya ni mdogo isipokuwa ana mwili mkubwa. "Mbona nyie Irene na Dogo Janja mnawaonea sana!? Hivi yule Irene nyie mnamuona mkubwa sana kwa sababu ya ule mwili!? Wala si mkubwa yule mtoto mdogo yule wa juzi, yule Dogo Janja kimwili chake kidogo dogo, ndio kampita lakini sio wa hivyo, lakini vilevile yule si mdogo, mdogo kwa mama yake ndio mwenye kujua kadi yake ya clinic iko wapi, na alokuwa anampeleka kupiga sindano, kwa Irene sio mdogo yule, yule mtu mzima kashaacha shule na mambo yake yapo kama kawaida", amesema Khadija Kopa. Khadija Kopa ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha Dogo Janja kumuoa Irene Uwoya sio ajabu kwani hata Mtume Mohamad kwenye imani ya dini ya Kiislam, alioa mwanamke aliyemzidi umri.

    The post Irene Ana Mwili Mkubwa ila Umri Mdogo, Wanaendana na Janjarao :-khadija Kopa appeared first on Ghafla!Tanzania.


    Source

    VIDEO: INASIKITISHA: Idadi ya Waliofariki MV Nyerere Yaongezeka Tena, Mkuu wa Majeshi Asema haya


    Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, amesema kuwa shughuli ya kuinasua MV Nyerere Bado inaendelea na kudai kuwa Vifaa vingi Tayari Vimeletwa eneo la tukio na wazamiaji wakiwa badi wapo chini ya kivuko wakitafuta namna ya kuweka mapulizo (AIR BAGS) Ili kukiinua kivuko.

    TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.........USISAHAU KUSUBSCRIBE..........

    Tuesday, September 25, 2018

    Profesa Ibrahim Lipumba Ataja Sababu za Kung'atuka CUF


    Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) anayetambulika na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema yuko tayari kuachia madaraka ya chama hicho endapo atapatikana mtu mwenye sifa.


    Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) anayetambulika na ofisi ya Msajili, Prof. Ibrahim Lipumba.

    Amesema hayo leo Septemba 25, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa CUF inafuata demokrasia hivyo ikiwa kuna mwanachama hai mwenye sifa ajitokeze kuwania uenyekiti kwani muda ukifika wa uchaguzi hakuna sababu ya kung'ang'ania madaraka.

    "Nitampisha atakayekuja kuwania nafasi ya uenyekiti ili mradi tu awe na sifa za uenyekiti na akubalike kwenye chama, sitokuwa na pingamizi lolote", amesema Lipumba.

    Amesema mpaka sasa hakuna mtu aliyejitokeza kuwania uenyekiti wa chama hicho ambaye atapitishwa pia kuwa mgombea urais 2020.

    Lipumba akizungumzia suala la Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kutajwa kuitwa CHADEMA haitakidhuru chama hicho kwa sababu CUF bado inakubalika Zanzibar na kusisitiza kuwa chimbuko la CUF ni Zanzibar, hivyo CHADEMA hawawezi kuiua CUF Zanzibar.

    Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Chama cha Wananchi (CUF) kipo kwenye mgogoro mkubwa wa kiutawala uliosababishwa na hatua ya Profesa Ibrahimu Lipumba kujiuzulu na baadaye kutengua uamuzi huo.

    Profesa Lipumba alitangaza kujiuzulu uenyekiti, Agosti 5, 2015 lakini baada ya mwaka mmoja akatengua uamuzi huo na kutangaza kurejea katika wadhifa huo jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

    Huu ndio mwisho wa Ronaldo na Messi katika ulimwengu wa soka ?

    Katika historia ya soka duniani hajawahi kutokea mchezaji aliyewahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora duniani Ballon d or zaidi ya mara tano kama walivyo wachezaji wawili walioandikwa kwenye historia ya soka dunia ambao ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Wachezaji hawa wakizitumikia timu tofauti wamefanikiwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora duniani Ballon d’ or kwa …

    The post Huu ndio mwisho wa Ronaldo na Messi katika ulimwengu wa soka ? appeared first on Bongo5.com.


    Source

    Audio: Catrima – Stata

    Msanii wa muziki kutoka Mkubwa na Wanae, Catrima ameachia audio ya wimbo wake mpya uitwao, Stata. Wimbo huo umeandaliwa na producer Mupher Touch.

    The post Audio: Catrima – Stata appeared first on Bongo5.com.


    Source

    'Tigermania' roars into France as Ryder Cup showdown looms

    "Tigermania" is back after crowds mobbed Tiger Woods like a rock star to see him snap a five-year win drought, and it's about to hit France in a major way at the 42nd Ryder Cup.
    Source

    Yafahamu magonjwa yanayowapata Ng'ombe


    1. Ugonjwa wa mapele ya ngozi.
    Mapele ngozi ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyojulikana kama Capripoxvirus. Virusi hivi huweza kukaa kwenye ngozi iliyokauka hadi siku 18.

    Ugonjwa huu huwapata ng'ombe wa umri wowote, aidha virusi hivi hufa kwa muda mfupi katika kemikali mbalimbali kama ether 20% chloroform, farmalin 1% na phenol 2%

    Jinsi ugonjwa huu unavyoambaukizwa.
    Virusi vya mapele ngozi hupatikana kwenye mapele, mate na majimaji mengine ya mnyama mgonjwa. Ugonjwa huu unaambukizwa kwa kuumwa na mbu jamii ya Andes Culex baada ya kumuuma mnyama mwenye virusi.

    Dalili za ugonjwa huu.
    Homa kali ambayo inaambatana na kutokea kwa mapele katika ngozi. Mapele haya yanaweza kuwa na ukubwa wa sentimeta 1 hadi 7 na huonekana katika sehemu ya kichwa, shingo, kiwele na miguuni.

    Mapele haya hukauka, kunyofoka na kuacha vidonda ambavyo huweza kushambuliwa na bakteria.
    Mapele haya yanaweza pia kutokea katika mdomo. Dalili nyingine ni homa kali ya nyuzi joto sentigredi 40-41.5, mnyama hukosa hamu ya kula, kutoa machozi, kutokwa na makamasi mazito, kuvimba matezi, kupunguza uzalishaji maziwa na kutupa mimba. Baadae mapele hutokea mwili mzima.

    Jinsi ya kuzia ugonjwa huuu.
    Mapele ngozi unazuilika kwa kuchanja ng'ombe na kurudia chanjo mara moja kila mwaka ili kuongeza nguvu ya kinga.

    Zingatia kanuni zifuatazo:
    1.Ogesha mifugo kwa kutumia dawa ambazo zinaua wadudu ikiwa ni pamoja na mbu wanaoeneza magonjwa ya mifugo.

    2.Hamasisha wafugaji wengine kuchanja dhidi ya mapele ngozi na magonjwa mengine ya mifugo kama vile homa ya mapafu, ugonjwa wa miguu na midomo na ndigana kali.

    3.Toa taarifa kwa mganga wa mifugo aliyekaribu nawe unapoona dalili za ugonjwa huu ili hatua zinazopaswa zichukuliwe.

    3. Tenga wanyama wagonjwa na kuwapatia matibabu ya vidonda.

    4. Nunua ng'ombe kutoka eneo ambalo halina ugonjwa.
    Kwa leo hebu tukomee hapa na tuweze kuhudumia mifugo yetu kwa ueasaha.

    Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, kwa siku ya leo tukutane tena siku nyingne.

    Monday, September 24, 2018

    Haiwezekani Nataka Kupima DNA Nimestuka!! Wanangu Hawajafanana na Mimi


    Mwenzenu jamani nahisi nmechakachuliwa,nina mke wangu tumezaa watoto wawili mmoja yuko na miaka mitano na wa pili miwili,kati yetu mimi na mke wangu nahisi kuna kitu kinaendelea na nimefanya uchunguzi wa kina na kuishia kwa majibu ambayo hayaniingii aklini na pili vilevile hawa watoto wanafanana exactly na watu ninao wahisi
    Nkijaribu kurudisha hisia nyuma naona matukio yanafanana na mke wangu pia alikuwa amejipatia ujauzito kwenye mazingira ya kutatanisha,Huyu wa kwanza anafanana sana na boyfriend wake wa zamani ambaye mimi namjua!kipindi yuko mjamzito nilishawahi kumfuma na meseji kibao za mahapa na njemba hilo!
    Huyu wa pili anafanana sana na Babu mmoja hapa mtaani kwetu anashona viatu
    Huyu mara nyingi nmeshawahi kumkuta home anajisingizie kuja kuchukua viatu,mbaya zaidi hata huyu mtoto huyu mwwanamke anajitahidi sana kumjengea mazoea nae
    Sasa naombeni ushauri jamani mm nifanye nini?

    Davido aijia juu Tume ya Uchaguzi Nigeria, ataka Wananchi wakatae matokeo ya uchaguzi ‘miaka mitatu hakuna maendeleo’

    Msanii wa muziki nchini Nigeria, Davido amewaomba wafuasi wa chama cha kisiasa nchini humo cha  Peoples Democratic Party (PDP) wapingane na kauli ya Tume ya Uchaguzi nchini humo. Davido amesema matokeo ya uchaguzi wa Gavana katika jimbo la Osun nchini humo, yanaonesha mjomba wake Ademola Adeleke kupitia chama cha PDP, ameshinda kwa kishindo kwenye uchaguzi huo lakini …

    The post Davido aijia juu Tume ya Uchaguzi Nigeria, ataka Wananchi wakatae matokeo ya uchaguzi ‘miaka mitatu hakuna maendeleo’ appeared first on Bongo5.com.


    Source

    Friday, September 21, 2018

    Hatimaye Lil Wayne Kupewa Tuzo ya Heshima ‘I am Hip Hop’

    Kwa mujibu wa mtandao wa Hip Hop Dx umeripoti kuwa Rapper Lil Wayne atapokea tuzo ya heshima ya 'I am Hip Hop' atakayopewa kwenye tuzo za BET Hip Hop zitakazofanyika October 6,2018 Marekani.

    Lil Wayne atapokea tuzo hiyo ya heshima kutokana na kuwahi kuuza zaidi ya nyimbo 100 ikiwa pia amewahi kuwa msanii wa kiume wa kwanza kuzipita rekodi za Elvis Presley katika chart ya Billboard Hot 100 na jina lake kutokea mara 138 katika chart hizo.

    Mashabiki wanasubiri kwa hamu ujio wa Album mpya ya Lil Wayne "Tha Carter V " ambayo inatajwa kuwa sokoni September 21,2018, Album hiyo imekuwa ikishikiliwa kwa miaka mingi kutokana na mivutano ya kisheria iliyokuwepo kati yake na kundi la Cash Money.

    Tanzania receives 59 US Peace Corps volunteers

    A total of 59 United States Peace Corps Volunteers will be stationed in 35 districts across Tanzania for two years of service in the education sector.
    Source

    Thursday, September 20, 2018

    Updates : IDADI YA WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO KUZAMA ZIWA VICTORIA YAFIKIA 44..WAMEOKOLEWA 37


    Mpaka usiku huu jumla ya watu 44 wanaripotiwa kufariki dunia na wengine 37 kuokolewa baada ya Kivuko cha MV Nyerere mkoani Mwanza kinachofanya safari kati Bugorora katika Kisiwa cha Ukerewe na Kisiwa cha Ukara katika Ziwa Victoria kuzama leo Alhamis Septemba 20,2018 mchana katika ziwa Victoria.

    Kwa Mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella zoezi Zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere limesitishwa kutokana na giza, na litaendelea kesho alfajiri.ambapo hadi sasa waliyookolewa wakiwa hai ni 37, waliokufa 44.




    #UPDATES:Zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere limesitishwa kutokana na giza, na litaendelea kesho alfajiri.ambapo hadi sasa waliyookolewa wakiwa hai ni 37, waliokufa 44.
    Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.


    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara.

    Kamanda Shana amesema kuwa kivuko hicho kimezama leo mchana baada ya kupinduka. "Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka," amesema.

    Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho Kivuko hicho cha Mv Nyerere kina uwezo wa kubeba abiria 100, tani 25 za mizigo na magari madogo matatu.

    Mbowe atakiwa kuacha upotoshaji, NEC yatoa ushahidi wake


    TUME ya Taifa ya Uchaguzi NEC imejibu tuhuma zilizotolewa dhidi yao na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuhusu kufukuzwa kwa mawakala wa chama hicho kwenye vituo vya uchaguzi mdogo wa jimbo la Monduli uliofanyika Septemba 16 mwaka huu akisema ni uongo na kwamba tume haitotishwa na tuhuma hizo.

    Akijibu tuhumu hizo Mkurugenzi wa NEC, Dk Athuman Kihamia amesema siyo kweli kwamba walifukuzwa bali kilichotokea ni kwamba wapo mawakala walioenda kwenye vituo ambavyo siyo vyao huku wengine wakiwa hawajafika asubuhi ya uchaguzi hivyo Chadema wakateua mawakala wengine ambao walikuwa hawatambuliki.

    " Nilikuwepo Monduli mimi na waliniomba niwasaidie kwa sababu mawakala wao walikamatwa na Polisi nilipowaambia twendeni nikawaone hawakuja wao walikuwa wanaongea kwa simu tu.

    " Natoa ushahidi kituo cha Siditi I cha pili, wakala aliyeapa ni George Ole Ngalimo lakini aliyefika kituoni ni Bosco Lawrence, hii habari ndugu zangu haikubaliki na huu siyo mchezo wa kuigiza wakala asiyeapa hawezi kuwa wakala rasmi. Lakini kituo cha Zaburi moja na kituo cha Isimangoni Chadema hawakusimamisha kabisa hivyo wasingeweza kuruhusiwa na msimamizi," amesema Dk Kihamia.



    Simba Kufungwa na Mbao Leo...Haji Manara Kawaomba Watanzania Msamaha


    From @hajismanara - Bodi ya Wakurugenzi,Sekretarieti,Benchi la Ufundi na wachezaji wa klabu ya Simba,wanawaomba radhi Wanachama na Washabiki wetu kwa matokeo ya leo. Tumeumia sote na tunawaomba mjue hii ni mechi ya nne tu..tutafanya maamuzi sahihi bila pressure kwa maslahi MAKUBWA ya Timu na klabu..nawaomba mtulie ktk kipindi hiki

    Dogo Janja na Uwoya Wabambwa Chumbani Baada Ya Tetesi Za Kuachana (Video)

    Staa wa Muziki wa Bongo fleva Dogo Janja na Mke wake Movie Star Irene Uwoya wamebambwa na kamera za Clouds Fm wakiwa wamekaa chumbani wakifanya yao.

    Baada ya Tetesi kusambaa sana Kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanandoa hao wamepeana kibuti hatimaye wameonekana hadharani kwa mara ya kwanza Kupitia Clouds Tv.

    Katika moja ya matangazo ya Fiesta Inayorushwa na Clouds Media , kamera ziliwanasa wawili hao pamoja wakiwa pamoja Kwenye moja ya vyumba hotelini.

    Baada ya mtangazaji huyo kuingia, Dogo Janja amedai hakuwa na taarifa kama kuna mtu yoyote anakuja hivyo ameshtukizwa huku akidai yeye na mke wake huyo walikuwa wanafanya mazungumzo.

    VIDEO:

    VIDEO: Madiwani Kinondoni walivalia njuga sakata la mgambo wa Makonda


    Sakata la operesheni ya usafi wa mazingira lililoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  ambalo limeshirikisha askari 400 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kuhakikisha jiji linakuwa safi limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwenye baraza la madiwani Manispaa ya Kinondoni wakitaka kujua uhalali na sheria zinazosimamia operesheni hiyo.

    TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE 

    MBARONI KWA KUMTIA MIMBA BINTI YAKE....ADAI 'SHETANI ALIMPITIA'


    Polisi katika Mkoa wa Mjini Magharibi wanamshikilia Muhammed Juma Muhammed kwa tuhuma za kumtia mimba binti yake wa kambo mwenye umri wa chini ya miaka 18.

    Hata hivyo, kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Thobias Sedeyoka alisema jana kuwa kwa sasa yupo likizo, lakini amesikia uwepo wa taarifa za binti aliyetiwa mimba na baba yake.

    Taarifa za kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo zilijulikana baada ya polisi kupatiwa taarifa na sheha wa Shehia ya Kijichi, Simba Ally Makame ambaye alipewa taarifa hizo na vijana wanaoshiriki ulinzi shirikishi. Binti huyo kwa sasa ameshajifungua.

    Baada ya kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi katika Kituo cha Polisi Bububu, baba huyo alikiri kufanya kitendo hicho huku akidai kuwa "shetani alimpitia".
    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...