Tuesday, September 25, 2018
Yafahamu magonjwa yanayowapata Ng'ombe
1. Ugonjwa wa mapele ya ngozi.
Mapele ngozi ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyojulikana kama Capripoxvirus. Virusi hivi huweza kukaa kwenye ngozi iliyokauka hadi siku 18.
Ugonjwa huu huwapata ng'ombe wa umri wowote, aidha virusi hivi hufa kwa muda mfupi katika kemikali mbalimbali kama ether 20% chloroform, farmalin 1% na phenol 2%
Jinsi ugonjwa huu unavyoambaukizwa.
Virusi vya mapele ngozi hupatikana kwenye mapele, mate na majimaji mengine ya mnyama mgonjwa. Ugonjwa huu unaambukizwa kwa kuumwa na mbu jamii ya Andes Culex baada ya kumuuma mnyama mwenye virusi.
Dalili za ugonjwa huu.
Homa kali ambayo inaambatana na kutokea kwa mapele katika ngozi. Mapele haya yanaweza kuwa na ukubwa wa sentimeta 1 hadi 7 na huonekana katika sehemu ya kichwa, shingo, kiwele na miguuni.
Mapele haya hukauka, kunyofoka na kuacha vidonda ambavyo huweza kushambuliwa na bakteria.
Mapele haya yanaweza pia kutokea katika mdomo. Dalili nyingine ni homa kali ya nyuzi joto sentigredi 40-41.5, mnyama hukosa hamu ya kula, kutoa machozi, kutokwa na makamasi mazito, kuvimba matezi, kupunguza uzalishaji maziwa na kutupa mimba. Baadae mapele hutokea mwili mzima.
Jinsi ya kuzia ugonjwa huuu.
Mapele ngozi unazuilika kwa kuchanja ng'ombe na kurudia chanjo mara moja kila mwaka ili kuongeza nguvu ya kinga.
Zingatia kanuni zifuatazo:
1.Ogesha mifugo kwa kutumia dawa ambazo zinaua wadudu ikiwa ni pamoja na mbu wanaoeneza magonjwa ya mifugo.
2.Hamasisha wafugaji wengine kuchanja dhidi ya mapele ngozi na magonjwa mengine ya mifugo kama vile homa ya mapafu, ugonjwa wa miguu na midomo na ndigana kali.
3.Toa taarifa kwa mganga wa mifugo aliyekaribu nawe unapoona dalili za ugonjwa huu ili hatua zinazopaswa zichukuliwe.
3. Tenga wanyama wagonjwa na kuwapatia matibabu ya vidonda.
4. Nunua ng'ombe kutoka eneo ambalo halina ugonjwa.
Kwa leo hebu tukomee hapa na tuweze kuhudumia mifugo yetu kwa ueasaha.
Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, kwa siku ya leo tukutane tena siku nyingne.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...