Thursday, September 20, 2018

Mbowe atakiwa kuacha upotoshaji, NEC yatoa ushahidi wake


TUME ya Taifa ya Uchaguzi NEC imejibu tuhuma zilizotolewa dhidi yao na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuhusu kufukuzwa kwa mawakala wa chama hicho kwenye vituo vya uchaguzi mdogo wa jimbo la Monduli uliofanyika Septemba 16 mwaka huu akisema ni uongo na kwamba tume haitotishwa na tuhuma hizo.

Akijibu tuhumu hizo Mkurugenzi wa NEC, Dk Athuman Kihamia amesema siyo kweli kwamba walifukuzwa bali kilichotokea ni kwamba wapo mawakala walioenda kwenye vituo ambavyo siyo vyao huku wengine wakiwa hawajafika asubuhi ya uchaguzi hivyo Chadema wakateua mawakala wengine ambao walikuwa hawatambuliki.

" Nilikuwepo Monduli mimi na waliniomba niwasaidie kwa sababu mawakala wao walikamatwa na Polisi nilipowaambia twendeni nikawaone hawakuja wao walikuwa wanaongea kwa simu tu.

" Natoa ushahidi kituo cha Siditi I cha pili, wakala aliyeapa ni George Ole Ngalimo lakini aliyefika kituoni ni Bosco Lawrence, hii habari ndugu zangu haikubaliki na huu siyo mchezo wa kuigiza wakala asiyeapa hawezi kuwa wakala rasmi. Lakini kituo cha Zaburi moja na kituo cha Isimangoni Chadema hawakusimamisha kabisa hivyo wasingeweza kuruhusiwa na msimamizi," amesema Dk Kihamia.



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...