Klabu ya soka ya Yanga, huenda itawakosa nyota wake wawili kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara (TPL), Jumapili dhidi ya watani wao wa jadi Simba.
Kwa mujibu wa meneja wa kikosi hicho ambacho kimepiga kambi mkoani Morogoro, Nadir Haroub Cannavaro, wachezaji Juma Mahadhi na Juma Abdul hali zao bado si nzuri.
''Kambi inaendelea vizuri hapa Morogoro na wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo isipokuwa beki wetu Juma Abdul na mshambuliaji Juma Mahadhi ambao bado ni majeruhi na hawapo tayari kwa mchezo wa Jumapili'', amesema Cannavaro.
Cannavaro ameeleza kukosekana kwa wachezaji hao hakutaathiri chochote kwani wachezaji waliopo wanauwezo wa kuipa timu matokeo kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Singida United ambapo walikosekana Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa na Heritier Makambo, lakini timu ilipata ushindi.
Mchezo huo wa jumapili utakuwa wa tano kwa Yanga SC msimu huu, ambapo tayari wamecheza mechi 4 na kushinda zote. Wana alama 12 katika nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...