Tuesday, September 4, 2018

VIDEO: Counry Boy awajibu Afande Sele na Nikki Mbishi baada ya kuambiwa hajui muziki

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Country Boy amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na maneno waliyoyatoa wasanii wenzake ambao ni Afande Sele pamoja na Nikki Mbishi kuwa Country hajui muziki pia sio MC wa kweli. <img src=”http://bongo5.com/wp-content/uploads/2018/09/mbishiiiiiiii-300×200.jpg” alt=”” width=”300″ height=”200″ class=”alignnone size-medium wp-image-238081″ /> Msanii huyo ameonge yote baada ya kupiga stori na Bongo Five kuhusiana …

The post VIDEO: Counry Boy awajibu Afande Sele na Nikki Mbishi baada ya kuambiwa hajui muziki appeared first on Bongo5.com.


Source

The Rock Ampa Shavu Nono Rapper Maarufu wa Kutoka Kenya, Stella Mwangi

The Rock ampa shavu nono rapper maarufu wa kike kutoka Kenya, Stella Mwangi
Muigizaji anayeingiza mkwanja mrefu kwa sasa duniani, The Rock ametoa shavu nono kwa rapper wa kike kutoka Kenya, Stella Mwangi a.k.a STL kwa kutumia ngoma yake ya No Games kama soundtrack ya episode mpya ya Ballers HBO.

The Rock amethibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika "Oh Lord look what I got though
No Dwayne but I Rock though! Shout to bad ass rapper @stellamwangi for the dope lyrics – clearly I'm biased".

Episode hiyo tayari imeanza kuoneshwa kupitia Cable ya HBO na bado haijajulikana ni kiasi gani amelipwa kwenye mkataba wake

Video: Ukinuna, ukiumia ukweli ni wasanii wanaofanya vizuri TZ wanatoka WCB! – Babu Tale

Mmoja kati ya Wakurugenzi wa WCB, Babu Tale amefunguka kwa kudai kwamba kwa sasa wasanii ambao wanafanya vizuri nchini Tanzania wanatoka katika label yake ya WCB. Akizungumza na Bongo5 mapema leo, Babu Tale alisema suala la mikataba ya wasanii wao lipo vizuri na hawana mpango wa kuipitia kama baadhi ya wadau wanavyoshauri baada ya kutokea …

The post Video: Ukinuna, ukiumia ukweli ni wasanii wanaofanya vizuri TZ wanatoka WCB! – Babu Tale appeared first on Bongo5.com.


Source

Monday, September 3, 2018

Dalili za awali za mtu mwenye ujauzito


Zipo dalili mbalimbali ambazo huwapata wanawake wakati wa ujauzito, Kila mwanamke hupata dalili tofauti na si wanawake wote  wataona dalili hizi ambazo nitazitabainisha hapa.

Dalili za awali za mtu mwenye mimba ni;

1. Kuhisi kuumwa
Baadhi ya wanawake hujihisi kuwa wanaumwa. Wengi huhisi kichefuchefu na kutapika hasa nyakati za asubuhi.

2. Kuhisi uchovu
wanawake wengi hujihisi uchovu na mwili kulegea. Hii hufanya wanawake wapende kulala. Mabadiliko ya homoni yanayotokea wakati huu ndio kiini ya matatizo haya.

3. Kuumwa maziwa-baadhi ya wanawake hujaa na kuumwa maziwa.

4. Kujisikia kichefuchefu.
Mara nyingi mwanamke anapokuwa amepata ujauzito hujisikia kichefufu, hii ni kutokana na mabadiliko na ukuaji wa kijusi.

5. Kupenda na kutopenda baadhi ya vyakula.

6. Kuwa na hasira zisikuwa na chanzo cha kuelewaka.

Serikali yapanga kuigomea Kenya kutumia Mto Mara


Serikali ya Tanzania imesema itapinga mipango ya serikali ya Kenya kujenga mabwawa ya kuzalisha umeme na kilimo cha umwagiliaji kwenye Mto Mara.

Kwa mujibu wa waziri wa mazingira wa Tanzania, January Makamba iwapo mipango hiyo ya Kenya itatekelezwa, itapunguza mtiririko wa maji na kutishia ustawi wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mto Mara unaanzia nchini Kenya kwenye milima ya Mau na kutiririka mpaka Tanzania ambako unatengeneza sehemu ya mpaka wa nchi hizo mbili. Mto Mara pia unatenganisha Hifadhi za Taifa za Masai Mara ya Kenya na Serengeti ya Tanzania.

Ni katika Mto Mara pia ambapo Nyumbu huvuka kwa wingi kutoka upande wa Tanzania kwenda Kenya na kuvutia maelfu ya watalii kwenye mbuga za Serengeti na Masai Mara kushuhudia tukio hilo ambalo linatajwa kama moja ya kivutio cha asili cha dunia.

"…Mto Mara, unaoanzia Kenya, ni mhimili wa Hifadhi ya Serengeti. Kulikuwa na taarifa za mipango ya Kenya kujenga mabwawa. Tulituma timu ya wataalam kufuatilia. Tuna Protocol ya Mto Mara, pia Lake Victoria Basin. Nitaenda Kenya na wenzangu kuongea na ndugu zetu," ameandika Makamba kwenye mtandao wake wa Twitter.

Ujumbe huo wa Twitter pia umeambatana na video ambayo inamwonesha Makamba akizuru kando ya Mto Mara ambapo amesema, "... Hii rasilimali (Mto Mara) ni ya kwetu sote, na sisi kama nchi hatuwezi kuruhusu jambo ambalo linaweza kuhujumu uchumi. Serengeti ni moja ya mali kubwa sana ya nchi yetu, na uti wa mgongo ni huu mto na ukiuvuruga huu mto kama nchi hatuwezi kukubali."

"Hairuhusiwi wewe mto unatoka nchi moja kwenda nyengine basi wewe (wa nchi ya) kule juu kufanya chochote maji yasifike huku chini. Kuna mikataba ya kimataifa tuliyosaini na tutasimama katika hiyo," amesema Makamba.

Sakata la Mto Mara linakuja siku chache baada ya vyombo vya habari nchini Kenya kuripoti kuwa mamlaka za hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania zimefanya hujuma kwa kuchoma moto eneo la hifadhi ili kuzuia nyumbu kuvuka kuelekea nchini Kenya. Serikali ya Tanzania ilikanusha tuhuma hizo.

Diamond Ataja Kilichomsibu Mpaka Kusuka Rasta

Staa wa muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka kuhusu staili yake ya kichwani inayoendelea kutengeneza headlines. Siku ya leo Diamond amezua gumzo baada ya kuanika staili yake baada ya kutupia picha iliyomuonyesha akiwa amesuka Rasta katika staili ya kipekee. Mara moja Diamond alianza kutrend huku watu wengi wakimponda na kudai amesuka Rasta kama mwanamke huku mashabiki wengine wakimpongeza kwa ubunifu. Kwenye mahojiano na Bongo 5, Diamond aliulizwa maswali ya Nini hasa kilichomsukuma mpaka kufikia uamuzi wa kusuka nywele kwa staili na akafunguka kuwa ameamua kubadilisha staili ya nywele zake: Nimeamua kubadilisha muonekano lakini baadae nitabadilisha Tena". Hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kutengeneza nywele na kuzua gumzo mara kwa mara amekuwa akija staili mpya ambayo inazua gumzo na kutrend sana.

The post Diamond Ataja Kilichomsibu Mpaka Kusuka Rasta appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

VIDEO: Azam wafunguka kuhusu Donald Ngoma, Kutinyu na Wadada


Klabu ya soka ya Azam FC, kupitia kwa msemaji wake, Jaffar Idd Maganga, wameelezea kuhusu hali ya mchezaji wao Donald Ngoma ambaye anaendelea matibabu. Pia amezungumzia kuhusu wachezaji wao wengine Tafadzwa Kutinyu na Nicholas Wadada.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Source

Uchumi suppliers fret about pay

Uchumi and Nakumatt Supermarket suppliers are worried that they may lose their money after the Kenyan government reportedly informed them to take legal action in the Sh14 billion claim.
Source

Picha : MKUTANO MKUU WA MUUNGANO WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA - UTPC WAFANYIKA JIJINI ARUSHA ... 'WAANDISHI SIYO MAADUI'


Mgeni rasmi,Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting akifungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC) unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha Septemba 3,2018 hadi Septemba 4,2018 - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog 

******

Rais  wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo ameiomba serikali kuwaangalia waandishi wa habari kwa jicho la tofauti ili kuwalinda kwa kuwa tasnia hiyo sio adui bali ni wadau muhimu wa maendeleo ya nchi. 


Amesema hayo katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania unaofanyika JiJini Arusha,ambapo amesema ndani ya miaka miwili waandishi 57 wamepata matatizo ya kupigwa,kuumizwa na kunyang'anywa vifaa vya kazi na baadhi kupotea jambo ambalo linaleta woga katika utendaji kazi.

Nsokolo amesema hawawezi kutupia lawama kwa serikali kwa sababu hawajafanya uchunguzi wa kutosha,bali wanaomba kulindwa ili waweze kuchangia maendeleo kupitia kalamu zao.

''Napenda ifahamike pote kuwa waandishi wa habari sio maadui bali ni wadau muhimu wa maendeleo hivyo vema kushirikiana na sio kuonana maadui,"alisema.

Aidha amemshauri Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuangalia aina ya viongozi anaowateua kutokana na hivi karibuni kujitokeza hadharani baadhi ya kiongozi mmoja kutoa kauli tata kwa mwandishi wa habari aliyepigwa uwanja wa mpira Dar es Salaam.

"Ni wazi tukio hilo la kulaaniwa na halipaswi kufumbiwa macho tunaomba wahusika wachukuliwe hatua maana tunafahamu kabla ya kuingia uwanjani kuna kukaguliwa hivyo huwezi kuingia mtu na silaha,"alisema Nsokolo.

Pia alisema katika mkutano huo iliohudhuriwa na wajumbe 81 toka Klabu 28 Tanzania Bara na Visiwani watatoa Tuzo ya tatu ya Daudi Mwangosi kama ishara ya kuonyesha waandishi hawako salama.

"Lakini tunaomba wafadhili wetu SIDA waangalie jinsi ya kusaidia Klabu ya Dodoma na tutapeleka andiko maalum ili wajengewe ofisi zenye hadhi kulingana na hali ilivyo sasa na kuwapatia mafunzo wanahabari ili wafahamu jinsi ya kuandika habari za viongozi mbalimbali wanaotembelea Dodoma,"alisema

Naye Mkuu wa Idara ya ushirikiano wa Balozi wa Sweden Tanzania (SIDA) Ulf Kallsting aliwakumbusha wanahabari kuhakikisha wanaandika habari za utafiti ili kuepuka kuleta shida katika nchi.

"Lakini ili Klabu zenu ziendelee kuwa na vyanzo vingi vya mapato vema mkaongeza idadi ya wanachama,"alisema

Alipongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Klabu za wanahabari na UTPC na kusema jambo la kuigwa kwani linajenga Demokrasia ya kweli.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro aliwaasa wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao licha ya kukabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ajira.

Alisema Wilaya yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi ambayo sehemu kubwa inasabishwa na ukosefu wa uelewa wa sheria ya umiliki ardhi na baadhi ya wanasiasa kuitumia kujipatia kura.

"Mimi sitakubali kabisa kuachia wanasiasa wajinufaishe na migogoro hii lazima nibadilishe badala ya ardhi kuwalaana bali iwe baraka hasa Halmashauri ya Meru, na hili nimeanza kuzungumza na viongozi wadini tusaidiane kulimaliza,"alisema.

Habari imeandaliwa na Vero Ignatus- Malunde1 blog Arusha. 


Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC) ,Abubakar Karsan akitafsiri kwa lugha ya Kiswahili hotuba ya Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting.
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC),Deogratius Nsokolo akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC).
Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha wakati wa wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC).
Jerry Muro akizungumza wakati wa mkutano huo.
Kushoto ni Makamu wa Rais UTPC,Jane Mihanji,Rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo na Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akishikana mkono na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC),Deogratius Nsokolo.
Wajumbe wa jopo la Tuzo ya Daudi Mwangosi wakiwa ukumbini.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro.
Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi UTPC wakiwa ukumbini
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) Kadama Malunde, na Katibu wa wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Ali Lityawi wakiwa ukumbini.
Viongozi wa klabu za waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa klabu mpya ya waandishi wa habari mkoa wa Songwe (wa tatu kutoka kushoto).
Picha ya pamoja meza kuu na wenyeviti wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania.
Picha ya pamoja meza kuu na makatibu wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania.
Picha ya pamoja meza kuu na waweka hazina wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania.
Picha ya pamoja meza kuu na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi UTPC
Picha ya pamoja meza kuu na wajumbe wa jopo la Tuzo ya Daudi Mwangosi 
Picha ya pamoja meza kuu na wafanyakazi wa UTPC
Kushoto ni Rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo,Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting,Makamu wa Rais UTPC,Jane Mihanji na kurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC) ,Abubakar Karsan wakifurahia jambo
Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting akiteta jambo na Makamu wa Rais UTPC,Jane Mihanji.
Mwenyekiti wa SPC,Kadama Malunde akipiga selfie na Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs Tanzania - UTPC) ,Abubakar Karsan,Makamu wa Rais UTPC,Jane MihanjiRais wa UTPC,Mkuu wa Idara ya Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallsting na rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo.

- Picha zote na Kadama Malunde na Emmanuel Msumba - Malunde1 blog & Msumba News blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...