Thursday, September 26, 2024

LALJI FOUNDATION YAKABIDHI MADAWATI 100 KWA SHULE 2 ZA WILAYA YA KISARAWE


Taasisi isiyo ya kiserikali ya LALJI FOUNDATION imetoa msaada wa madawati 100 kwa shule za msingi 2 Wilayani Kisarawe ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha mazingira ya sekta ya elimu nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madawati hayo kwa shule za msingi Msanga na Bembeza makamu Mwenyekiti taasisi ya LALJI FOUNDATION Mohamed Damji amesema kuwa wametoa madawati hayo kwaajili ya kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kuboresha miundombinu na mazingira ya elimu nchini.

Aidha Bw. Damji amewataka wanafunzi wa shule hizo kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao ikiwemo kuwa viongozi bora na kufanya kazi katika fani mbalimbali hapa nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mh. Zuberi Kizwezwe ameishukuru taasisi ya LALJI FOUNDATION kwa kutoa msaada huo na kutoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano kutoka taasisi hiyo kutoa misaada mbalimbali katika6 jamii.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Petro Magoti amesema Wilaya ya Kisarawe itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wa maendeleo katika mambo mbalimbali huku akishukuru na kuipongeza taasisi ya LALJI FOUNDATION kwa kuendelea kusaidia jamii ya watu wenye uhitaji.

Airtel Money yawazawadia wateja bonasi ya 20,000


Katika jitihada endelevu za kuboresha huduma za mawasiliano kwa wateja wetu nchini, Airtel Tanzania leo imezindua promosheni mpya ya 'JiBoost na Airtel Money' ambayo inawapa nafasi watumiaji wa Airtel Money kujipatia shilingi 20,000 taslim ya supa bonasi kupitia miamala ya kila siku watakayofanya. Mpango huu ni sehemu ya maono ya kampuni ya Airtel kupanua huduma ya Airtel Money na kujenga huduma za kifedha jumuishi na wezeshi kwa wateja wake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba alieleza furaha yake kuhusu kampeni ya JiBoost na Airtel Money akisema kuwa, "Tunafurahia kuitambulisha kampeni hii ya "JiBoost na Airtel Money' ili kuleta thamani kwa wateja wetu.

Promosheni hii imetengenezwa kuwazawadia wateja wetu kila wanapotumia huduma za Airtel Money katika Maisha yao ya kila siku kama manunuzi ya vifurushi vya muda wa maongezi, intaneti, au malipo ya serikali kama vile LUKU. Wateja wetu watakuwa wakinufaika zaidi na kila muamala watakaofanya. Tunajivunia kuwa vinara wa kutoa huduma suluhishi kupitia Airtel Money kwa wateja wetu."

Akielezea kampeni ya JiBoost na Airtel Money, Balozi wa Airtel Tanzania, Diamond Platnumz alieleza furaha yake kuhusu kampeni hiyo.

"Airtel Money siku zote imekuwa ikirahisisha maisha. Jiboost inakupa wepesi wa kufanya miamala pamoja na kurejeshewa fedha kwenye akaunti yako. Hii ni fursa kwetu sote ya kutunza na kupata fedha wakati tukiendelea kufanya matumizi. Najivunia kuwa sehemu ya mapinduzi haya," alisema.

Kwa upande wake, Joti ambae alivaa uhusika wa Mr Money, alisema, "Kama Mr Money, naweza kukuambia kuwa kampeni hii ni mahususi kwa ajili ya kurudisha pesa kwenye mfuko wako. Kila utakapofanya malipo ya TV, umeme na kununua muda wa maongezi, unakuwa unajipa nafasi kubwa zaidi ya kupata bonasi. JiBoost ipo hapa kwa ajili ya kufanya miamala yako ya kila siku iwe ya furaha na yenye zawadi."

Kampeni ya JiBoost ya Airtel Money inamruhusu Mteja kuweza kupata supa bonasi ya shilingi 20,000 kupitia muamala unaotumwa Kwenda kwa mtu mwingine, kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi, malipo ya LUKU, malipo ya serikali na kununua vifurushi vya king'amuzi. Wateja pia wanaweza kupata bonasi hiyo kwa kufungua App ya Airtel Money.

Kila mteja atakapokamilisha muamala unaostahili, atapokea ujumbe wa maandishi ukithibitisha kuwa amepata bonasi. Kila mteja atakapokuwa akifanya malipo atakuwa anapata gawio la bonasi hadi itakapofikia thamani ya shilingi 20,000. Kila bonasi atakayopata mteja itaonekana kwenye akaunti yake ya Airtel Money ikiambatana na ujumbe wa SMS utakaoonyesha mwenendo wa bonasi hizo. 

Ili kuweza kunufaika na ofa hii, wateja wa Airtel wanaweza kupiga *150*60# au kutumia App ya MyAirtel kukamilisha miamala na kuanza kujizolea bonasi kupitia kampeni ya JiBoost na Airtel Money.


Source

Wednesday, September 25, 2024

JKT yatangaza nafasi kwa vijana kujiunga na Mafunzo ya JKT ya kujitolea

 


Jeshi la kujenga Taifa JKT limetangaza nafasi za mafunzo kwa vijana wa kujitolea kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo huku likitoa rai kwa vijana hao kuwa JKT haitoa ajira wala kuwaunganisha na taasisi nyingine kutapa ajira mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo bali mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwajengea uzalendo na stadi za maisha.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT. Kanali Juma Mrai amesema Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawaarifu vijana wote wa kitanzania wa bara na visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea.

Ameongeza kuwa " utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za wakuu wa Mkoa na Wilaya ambapo muombaji anaishi" amesema.

Amesema usaili wa vijana hao kujiunga na mafunzo ya JKT utaanza Oktoba mosi mwaka huu kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT kuanzia tarehe 01/11 hadi tarehe 03/11 mwaka 2024.

Ameongeza kuwa "JKT linapenda kuwaarifu vijana watakaopata fulsa hiyo kuwa JKT halitoi ajira, pia halihusiki kuwatafutia ajira katika asasi, vyombo vya ulinzi na usalama na mashirika mbalimbali ya serikali na yasiyokuwa ya kiserikali" Amesema.


Amesema JKT hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao JKT na likibainisha kuwa sifa za muombaji  na maelekezo ya vifaa vinavyotakiwa Kwenda navyo yanapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz.

Amesema Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote watakaopata fulsa hiyo kuja kujiunga na vijana wenzao ili kujengewa Uzalando, Umoja wa kitaifa, Stadi za Maisha na utayari wa kulijenga Taifa.

 

MWANAMUZIKI LINAH AVURUGWA KUITWA BIBI KIZEE

MWANAMUZIKI LINAH AVURUGWA KUITWA BIBI KIZEE


Msanii wa Bongo Fleva, Esterina Sana maarufu kama Linah amewajia juu baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimchamba mitandaoni kuwa amezeeka.


Kupitia Insta Story yake Linah ameandika; "Nashangazwa sana na watu wanavyoshambulia wenzao kuhusu kuzeeka dah, tena mtu anacheka kabisa 'Umezeeka' swali ni kwamba kwani wenzetu nyinyi mpo palepale?umri hausogei au mlishushwa tu hamkuzaliwa".


"Yaani mtu baada kumshukuru Mungu unaishi miaka mingi unaanza kutia kasoro duh, nina furaha na miaka 34 yangu kikubwa pumzi jamani".

MSIGWA: CHADEMA NI MAKAMANDA WA MITANDAONI TU HAWANA LOLOTE


Kupitia mitandao yake ya Kijamii, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mch. Peter Msigwa ameonesha kushangazwa na mwitikio mdogo wa watu waliokuwa wakihamasisha wananchi kujitokeza kwenye maandamano ya @ChademaTz yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana Jumatatu Jijini Dar es salaam.

"Watu wanapenda kujiita makamanda hapa kwa mitandao (keyboar heros) wamemuacha mwamba anaandamana pekee yake hata watu hamsini hawakufika magomeni.Wapi mwita , Catherine, maranja, Lutembeka, mwenyekiti wa kanda ya Nyasa wapi Taita! Wapi Big Mungai!?.... Hata kama mtachukia hii inasema kitu.
Tuna Tanzania ya kuijenga.
Niltegemea wale watoa matusi hapa wangekuwa wa kwanza kufika magomeni🤣🤣🤣"

Wakati Msigwa akisema hayo mtumiaji mwingine wa mitandao ya Kijamii Onesmo Mushi, ameandika;

"Mimi nina theory kwamba pengine Mhe. Mbowe hakutaka wafuasi wa CHADEMA watunishiane misuli na polisi (kwa kuogopa kuwa silaha za jeshi la polisi na kutokujali kwao kungeweza kumwaga damu za wengi wasiokuwa na hatia) na hivyo akaamua asimobilize watu au akapitisha taarifa chini chini watu wasijitokeze akiamini kuwa yeye mwenyewe angetosha kufanikisha lengo pasipo kuathiri wafuasi wengi?🤔🤔

..... Hii ni moja ya strategy zilizotumiwa na wanajeshi wengi zamani; rejea kisa cha Achilles na Hector pale kwenye geti la Troy au hata Daudi na Goliathi kwenye biblia.

Ni nadharia tu, sitaki kukubaliana kirahisi kuwa "watu hawakutoka kwa sababu Mbowe ushawishi" wakati juzi tu mwezi wa kwanza walitoka kwa maelfu, achilia mbali vitisho vilivyokuwepo." Amesema.

Source

Tuesday, September 24, 2024

Mawakala feki Watano wapandishwa Kizimbani Dar


Na. Mwandishi wetu. 24 septemba, 2024

WATU  watano wamepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na mashtaka 23 likiwemo la kuongoza genge la uhalifu na wizi wa fedha kiasi cha Sh 3,600,000.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Wangina Chacha(21), Erick Mushi(28), Shabani Msuya(36), Baraka Lunanja (32) na Kassim Dyamwale(34).

Wakili wa Serikali, Nitike Mwaisaka alidai hayo hapo jana tarehe 24 Septemba, 2024  alipokuwa akiwasomea washtakiwa hao mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kemilembe Josiah washtakiwa hao walipofikishwa mahakamani hapo.

Mwaisaka alidai katika mashtaka ya kwanza ya kuongoza genge la uhalifu na kuingilia mfumo wa kompyuta kwa lengo la kufanya uhalifu linawakabili washtakiwa wote ikiwa walitenda kosa hilo Julai, 28,2024 wakiwa katika maeneo ya Mabibo Mwisho, Wilaya ya Ubungo Dar es salaam.

Aliendelea kudai kuwa Julai 28, 2025 katika eneo la Mabibo Mwisho Wilaya ya Ubungo mshtakiwa namba mbili na tatu walijiwasilisha kuwa ni wafanyakazi huru wa kampuni wa mtandao wa simu Airtel kwa Wilbard Simon wakijua kuwa sio kweli.

Pia Julai 28,2024 washtakiwa wote wakiwa katika eneo la Mabibo Mwisho, waliingilia mfumo wa kompyuta kinyume cha sheria kwa kutumia namba ya simu ambayo mmiliki ni Pius Mpanduli.

Alidai kuwa kosa la kutumia kifaa haramu na kuingilia mfumo kinyume na sheria linawakabili mshtakiwa namba moja, mbili, nne na tano, kati ya Septemba 8 hadi 11, 2024 washtakiwa walikutwa wana kifaa kilichoitwa "Screen recorder Unlimited".

Washtakiwa hao walitenda kosa hilo wakiwa katika wilaya tofauti ndani ya Mkoa wa Dar es salaam na Tanga wakiwa wakitumia simu aina ya  Infinix smart plus, Itel A05S, Samsung Galaxy A15, na Infinix smart 8.

Aliendelea kudai kuwa Julai 28,2024 washtakiwa wote wakiwa katika eneo la Mabibo Mwisho Wilaya ya Ubungo waliingilia akaunti ya Airtel Money inayomilikiwa na Paul Mpanduli kinyume cha sheria kwa lengo la kuiba.

Pia katika tarehe na eneo hilo washtakiwa wote waliiba fedha kiasi cha Sh 3,600,000 kutoka katika namba ya airtel inayomilikiwa na Paul Mpanduli.

Alidai mashtaka 11 ya kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine inawakabili mshtakiwa namba moja, mbili, tatu na tano, washtakiwa walidaiwa kufanya  kosa hilo kati ya Julai 7, 2024 na Septemba 9, 2024 wakiwa katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Dar es salaam na Tanga.

Pia mashtaka ya mwisho yanawakabili washtakiwa wote watano, ilidaiwa kuwa Julai 28, 2024 wakiwa katika maeneo ya Mabibo Mwisho Wilaya ya Ubungo washtakiwa wote waliingilia data za kompyuta kinyume cha sheria kwa kuingilia mjumbe mfupi wa mfumo wa mawasiliano ya Pius Mpanduli.

Mwaisaka alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 9,2024 kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, washtakiwa wote hawakupata dhamana, hivyo walirudishwa rumande hadi tarehe iliyopangwa ya kutajwa.

Gekul awataka Vijana waipende nchi yao.



Na John Walter -Babati 

Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Mheshimiwa Paulina Gekul amewataka Vijana waipende nchi yao kwa kuwa wazalendo na kutii mamlaka zilizopo.

Gekul ametoa Rai hiyo kwa Vijana wa kata ya Mutuka na Nangara Jimboni humo akiwa katika ziara yake ya kugawa vifaa vya michezo kwenye mitaa na vijiji kuelekea Dr. Samia & Gekul Cup yenye lengo la kuibua vipaji vipya vya soka na hatimaye kupata timu ya mpira wa miguu itakayowakilisha mji wa Babati kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Gekul amewataka Vijana hao kujituma kwa kufanya kazi halali waweze kujimudu na familia zao na kuwaepuka baadhi ya watu wasioitakia mema nchi ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Gekul amegawa mipira na jezi, vifaa ambavyo amevikabidhi kwa Vijana hao kupitia Viongozi wao ili vitunzwe na kutumiwa na wengine siku zijazo.

Uzinduzi wa michuano ya  Dkt Samia & Gekul Cup 2024, itazinduliwa Rasmi Oktoba 5, mwaka huu katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati.

Aidha Mashindano hayo yataenda sambamba na uhamasishaji wa vijana na Wanawake kushiriki na kugombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na kujiandikisha kwenye mfumo wa Kieletroniki Chama cha Mapinduzi.

Gekul amesema hakuna Chama cha siasa kinachoweza kumsaidia Kijana zaidi ya chama cha Mapinduzi na kwamba hata nchi nyingi za Afrika zimesaidiwa kupata uhuru na Chama hicho tawala.

Hata hivyo Vijana wa Chem Chem na Mutuka wamempongeza Mbunge kwa kuwakumbuka katika Soka huku wakimuahidi kutumia mashindano hayo kuonesha vipaji vyao.

Wasimamizi wa mashindano hayo Chama cha Soka wilaya ya Babati kupitia kwa mwenyekiti Gerald Mtui wamesema watahakikisha wanasimamia kanuni na Sheria zote za Soka ili lengo la Mbunge kupata vipaji vipya vya soka litimie.

Mtui amesema pia katika michuano hiyo watachukua Vijana wadogo wenye umri chini ya miaka 15 na wale wenye umri chini ya miaka 20.

RAIS SAMIA : NATOA MIEZI MITATU MAJI YAWAFIKIE WANANCHI, TULIAHIDI KUMTUA NDOO MAMA KICHWANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma

Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Mtyangimbole leo Jumanne Septemba 24,2024 Mhe. Rais Samia amesema: "Mradi huu unakwenda kuhudumia vijiji vitatu ndio makusudio lakini maji yatabaki, yatakwenda kwenye Kijiji kingine cha nne. Kwa hiyo ndugu zangu nimeona mradi nimeona maendeleo. Nimewaambia Waziri na Katibu Mkuu wake ambao ni wachapakazi wazuri sana na watendaji wao, ninawapa miezi mitatu tu, siku 90 za kazi, mwezi mmoja kufanya yale ambayo mmechelewa kukamilisha, maji yatoke kwa wananchi hawa".

"Mnakumbuka wakati wa kampeni, tuliahidi kumtua ndoo mama kichwani. Sasa tumekwenda kuifanyia kazi ahadi ile. Tumeifanyia kazi kwa kusambaza miradi ya maji nchi nzima. Kama mnavyoona tulivyofanya Ruvuma na nchi nzima ni hivyo hivyo. Kwa hiyo tunatarajia ikifika mwaka kesho 2025 tuwe tumetimiza lile lengo tulilotumwa na Chama Cha Mapinduzi kwamba vijiji vyote vya Tanzania vipate maji kwa asilimia 85 tutakuwa tumelitimiza au kupita kidogo", amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024. 

Monday, September 23, 2024

Wanafunzi 48 Simanjiro wapata ujauzito ndani ya mwezi mmoja.



Na John Walter -Manyara 

Wanafunzi 48 wa shule mbalimbali za sekondari wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamebainika kupata ujauzito ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita. 

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo wilayani Simanjiro na kuzungumza na wakuu wa shule za sekondari za mkoa huo katika Mji wa Mirerani. 

Mkuu wa Mkoa ameeleza kusikitishwa na hali hiyo, akilaani tabia ya baadhi ya wanafunzi na wazazi kuficha ujauzito kwa kudai kuwa watoto ni watoro. 

Amewasisitiza wazazi na walimu kutekeleza wajibu wao ipasavyo katika malezi ya watoto na kuhakikisha wanaume wanaowadanganya wanafunzi, wakati kuna wanawake wazima wamejaa mitaani, wanachukuliwa hatua kali.

EDWIN BALUA AZUMGUMZIA UGUMU WA BAO LAKE CAFCC

 

EDWIN BALUA AZUMGUMZIA UGUMU WA BAO LAKE CAFCC

 EDWIN BALUA AZUMGUMZIA UGUMU WA BAO LAKE CAFCC

NYOTA wa Simba kiungo Edwin Balua aliyewazima wapinzani wao kwenye anga la kimataifa jioni amefichua alichoambiwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kabla ya kuingia kwenye mchezo huo.

Septemba 22 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-1 Al Ahli Tripoli huku mabao ya Simba yakifungwa na Kibu Denns dakika ya 36, Leonel Ateba dakika ya 45 na Balua dakika ya 89 muda mfupi baada ya Simba kufanyiwa shambulizi la hatari na mfungaji wa bao la kwanza kwa Tripoli Cristivo Mabululu.

Balua aliingia kwenye mchezo huo akitokea benchi alifunga bao lililowavuruga Waarabu hao wa Libya mpaka mpira unagota mwisho walikuwa wakilalamika jambo lililopelekea mwamuzi wa kati kumuonyesha kadi nyekundu mfungaji wa bao laTripoli Mabululu.

Kiungo huyo alifunga bao hilo kwa utulivu mkubwa ambapo alikuwa na nafasi ya kutoa pasi kwa wachezaji wawili wa Simba waliokuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga ikiwa ni pamoja na Ateba ila chaguo lake ilikuwa kufunga mwenyewe.

"Mwalimu anajua namna ya kuelekeza wachezaji na aina ya mchezo ambao tunacheza ambacho alisema ilikuwa anahitaji kuonatunapata ushindi hivyo nilivyoingia nilikuwa ninawaza ushindi hakuna kingine.

"Ukiwa umefungwa ama ukiwa unaongoza lakini kuna nafasi ya kufungwa hapo presha inakuwa kubwa lakini tulipofunga bao la tatu naona tulikuwa tumemaliza kabisa mchezo na ushindi ukawa kwetu, mashabiki tunawashukuru wamejitokeza kwa wingi."

Saturday, September 21, 2024

MPANZU TAYARI NI MALI YA SIMBA, BOSI DEWJI KAWEKA MPUNGA MWINGI SANA..


MPANZU TAYARI NI MALI YA SIMBA, BOSI DEWJI KAWEKA MPUNGA MWINGI SANA..
Mashabiki wa Simba kaeni chonjo Elie Mpanzu yupo tayari kujiunga na Simba kwenye dirisha dogo la mwezi January Kama Kila kitu kitaenda vizuri.

Mazungumzo ya moja kwa moja Kati ya Simba na Mpanzu yamefanyika wiki hii na Nyota huyo anaitaka jezi nyekundu. Mshahara wake umetajwa kuwa ni milioni 27 za kitandania kwa mwezi na hela ya usajili au transfer fees ya dola Mia mbili.....

Source

TAEC kuwa mlezi wa programu maalumu ya diploma ya masomo ya teknolojia ya nyuklia


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) PROF. NAJAT KASSIM MOHAMMED amesema taasisi hiyo itakuwa mlezi wa programu maalumu ya diploma ya masomo ya teknolojia ya nyuklia itakayoanzishwa na chuo cha ufundi Arusha (ATC).

Prof. Najat ameyasema hayo katika ofisi za TAEC kanda ya kaskazini eneo la Njiro jijini Arusha baada ya kufanya kikao cha pamoja Kati ya uongozi wa TAEC na uongozi wa chuo cha ufundi Arusha kwa lengo la kuanza maandalizi ya kuanzisha diploma hiyo ya masomo ya nyuklia ambapo TAEC itakuwa mlezi kwa kutoa wataalamu wake watakaoongoza mchakato wa kuwezesha mtaala wa masomo hayo kufanikiwa.

Prof. Najat ameongeza kuwa TAEC kwa kuwa ina wataalamu wa teknolojia ya  nyuklia imetenga muda wa mwaka mmoja kwa kushirikiana na chuo cha ufundi Arusha kwa ajili ya kuwaandaa walimu wa chuo hicho kwa kuwapatia mafunzo kwa njia ya nadharia na vitendo ili kuwajengea uwezo  walimu watakaokuwa na   dhamana ya  kufundisha masomo hayo.

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania ndiyo taasisi pekee ya serikali iliyopewa dhamana ya kusimamia matumizi salama ya mionzi nchini, kuhamasisha na  kuendeleza teknolojia ya nyuklia katika sekta mbalimbali kama vile afya, kilimo, mifugo, nishati, migodi, viwanda, maji na kufanya tafiti mbalimbali kwa kutumia Teknolojia ya Nyuklia sambamba na kutoa ushauri kwa serikali juu ya mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusisha matumizi salama ya  teknolojia ya nyuklia.

Friday, September 13, 2024

UTUNZAJI WA MAZINGIRA KWENYE VYANZO VYA MAJI WAIKOSHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MAJI NA MAZINGIRA

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Maji na Mazingira Jackson Kiswaga katika akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika chanzo cha Maji Mabayani Jijini Tanga wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo
MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia akimueleza jambo Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika wakati akiwasili na kamati hiyo kwa ajili ya ziara ya siku moja



Na Oscar Assenga,TANGA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) imepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge Maji na Mazingira kwa utunzaji mzuri wa mazingira katika maeneo yanayozunguka kwenye vyanzo vya maji ikiwemo Bwala la Mabayani Jijini Tanga.

Kamati hiyo imekagua chanzo cha maji cha Mabayani ambacho ni chanzo kikubwa kunacho hudumia jiji la Tanga na mtambo wa kutibu na kuzalisha maji wa Mowe

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jackson Kiswaga wakati wa ziara ya siku moja ya kutembelea vyanzo vya maji ambapo wakiwa kwenye eneo hilo walieleza kufurahishwa na utunzaji wa mazingira yanayozunguka vyanzo vya maji

Mwenyekiti huyo alisema lengo la ziara hiyo ni kuona namna fedha zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika kutekeleza miradi ya maji na kuelezwa kuridhishwa kwa namna utekelezaji wake unavyofanyika.

"Tumefurahishwa na utekelezaji wa miradi hivyo tuhakikisha wananchi tunawapa maji na utekelezaji wa mradi wa hatifungani uanze haraka ili kutimiza azma ya Rais Dkt Samia Suluhu Kumtua mama ndoo kichwani " Alisema Kiswaga

"Lakini kubwa sha Tanga Uwasa kwa ubunifu na uuzaji wa hatifungani ya kijani ambayo imeweze upatikanaji wa fedha kiasi cha sh.Bilioni 53.12 ambazoo zinakwenda kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya Tanga ,Mkinga,Muheza na Pangani"Alisema

Hata hivyo waliipongeza Wizara ya Maji na Mammlaka yAmeipongeza Wizara ya Maji na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwapeleka huduma ya maji wananchi ili kuondosha tatizo la uhaba wa maji katika jiji la Tanga.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Waziri wa Maji Jumaa Aweso alisema baada ya kupatikana kwa fedha kiasi cha Bilioni 54 kutokana na mradi wa maji Hatifungani tayari wameshampata mkandarasi kwa ajili ya kuboresha mradi wa maji wa tanga Uwasa na wananchi zaidi ya laki sita watanufaika.

Waziri Aweso alisema mpaka sasa wakandarasi tayari wamekwisha kupatikana ambao ni China Railway Co Limited na STC Construction Co Limited huku akieleza hivi sasa ni muda wa kuanza rasmi utekelezaji wa mradi huo ambao umelenga kuongeza uzalishaji wa maji kutoka Lita Milioni 45 hadi Milioni 60 na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Octoba 2025.

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alisema hali ya upatikanaji wa maji kimkoa ambapo alisema maeneo mengi yanapata maji kwa asilimia 59 mpaka 60 kwenye wilaya nane za mkoa huo na juhudi za kuhakikisha wanapata maji zinaendelea.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema ni matarajio yao baada ya mradi huo kukamilika Tanga Jiji watapata maji kwa zaidi ya asilimia 98 na kuwafikia wananchi zaidi ya laki sita.

Wilaya ambazo zitanufaika na mradi huo wa maji ni Jiji la Tanga, Muheza, Pangani na Mkinga


Dickson Job Afunguka 'Nilihisi Sitokuja Kuona Tena'

Dickson Job Afunguka 'Nilihisi Sitokuja Kuona Tena'


Beki wa Taifa Stars, Dickson Job aliumia dakika ya tisa ya mchezo wa Taifa Stars baada ya kugongana na kiungo wa Guinea na kulazimika kutolewa dakika ya 11 nafasi yake ikichukuliwa na Bakari Mwamnyeto. Akizungumza jana, Job alisema baada ya kukutana na ajalih iyo ndani ya uwanja wakati anatolewa alipata wasiwasi kama hataweza kuona tena kufuatia kushindwa kuona kitu kwa takribani dakika moja.

.

Job alisema hakuwa anaona kitu mbele hali iliyomshtua ambapo bado hafahamu aligongwa na kitu gani kwenye kichwa chake kiasi cha kupoteza netiweki hadi alipopatiwa huduma ya kwanza

.

"Sikuwa naona kitu, kuna rangi ambazo hadi sasa sizitambui zilikuwa zinanijia mbele halafu ilikuwa kama dakika hivi sielewi kitu gani nakiona mbele, kiukweli ilinitisha sana," alisema Job. Hata hivyo, Job alisema baada ya matibabu alipo-tolewa hali yake ilianza kuimarika na macho yake kurudi kwenye ufanisi wake.

.

"Nipo sawa sasa naona vizuri, mashabiki wasiwe na wasiwasi nitarudi kazini kwenye majukumu yangu, hadi sasa ninavyojisikia naona nitaweza kuwa sehemu ya timu yangu ya Yanga kwenye mechi inayofuata kule Addis Ababa."

Video Mpya : INAGA MDOGO - KIPINDU PINDU

 

DKT. YONAZI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA PSARP


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na wageni kutoka Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (Protective Security & Attack Response Programme – PSARP) chini ya Ubalozi wa Uingereza kuhusu uwezekano wa kuandaa Mpango wa Kuimarisha Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Maafa walipomtembelea Ofisini kwake tarehe 12 Septemba, 2024 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na ujumbe kutoka Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) wakiongozwa na Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) - Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. John Spencer (kushoto kwake)na kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya utafiti wa maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi.
Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) - Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. John Spencer akizungumza jambo wakati wa kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.

NA. MWANDISHI WETU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (Protective Security & Attack Response Programme – PSARP) chini ya Ubalozi wa Uingereza kuhusu uwezekano wa kuandaa Mpango wa Kuimarisha Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Maafa.

Amekutana nao mwishoni mwa wiki walipomtembelea Ofisi kwake Jijini Dodoma, na kueleza kuwa PSARP inalengo la kuimarisha uwezo wa Wataalam katika kukabiliana na maafa nchini.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Yonazi ameshukuru uongozi huo kwa kumtembelea na kutumia fursa hiyo kujadili majukumu ya msingi ya Ofisi yake ya kuratibu Shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na uratibu wa masuala ya maafa nchini ambalo ndilo eneo walilolenga kuzungumza na kuona namna bora ya kushirikiana na Serikali.

Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) - Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. John Spencer ameipongeza Serikali kwa namna inavyoendelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo suala la menejimenti ya maafa huku akielea lengo la Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi ambao umejikita katika kuimarisha utendaji wa polisi katika operesheni za dharura na kuona fursa katika kushirikiana na nchi ya Tanzania ili kuimarisha utendaji wa pamoja wa taasisi zinazohusika na kukabiliana na maafa.

Aliongezea kuwa wapo tayari kushirikiana ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuimarisha uwezo wa kukabiliana na maafa kwa kuwajengea uwezo wataalam wa maafa katika eneo la mfumo jumuishi wa utendaji wa pamoja wakati wa dharura.




HALMASHAURI YA BARIADI YAKABIDHI MAJENGO KWA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATUMIKE KUFUNDISHIA TAALUMA YA WANYAMAPORI






Na Anangisye Mwateba- Bariadi Simiyu

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) leo tarehe 12 Septemba 2024 amepokea majengo 9 kutoka Halmashauri ya Bariadi ili yatumike kuendeshea mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi watakaokuwa wanasoma kozi za usimamizi wa wanyamapori na waongoza watalii kupitia Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.

Majengo hayo ambayo awali yalikusudiwa kutumika kama sekondari ya wasichana yamejengwa katika eneo linalokabiliwa na changamoto ya uvamizi wa tembo; hivyo ili kuepusha athari hiyo kwa wanafunzi wa kike, na vilevile kufuatia kujengwa kwa shule mpya ya wasichana katika wilaya ya Bariadi; serikali ya mkoa wa Simiyu ilifikia maamuzi ya kutoa majengo ya shule tarajali ya wasichana Matongo kwa wizara ya maliasili na utalii ili yatumike kama taasisi ya kutoa mafunzo ya uhifadhi wa maliasili nchini.

Katika hotuba yake Naibu Waziri Kitandula alisema kuwa kutumika kwa eneo hilo lililopo kata ya Giliya kuendeshea mafunzo ya vitendo kupitia Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi kutatoa fursa ya kiulinzi katika eneo husika na maeneo inayopakana nayo, hivyo kuwahakikishia ulinzi wananchi waliokuwa wanavamiwa na wanyama wakali na waharibifu mara kwa mara, na wakati mwingine wanyama hao kusababisha vifo.

Mhe. Kitandula aliongeza kuwa uwepo wa Chuo cha Taaluma ya Uhifadhi wa maliasili katika wilaya ya Bariadi pia kutatoa fursa kwa jamii kujifunza na kutumia mbinu za kuzuia wanyama wakali na waharibifu

Aidha, Mhe. Kitandula alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wataalam wa halmashauri zote nchini kuacha tabia ya kuanzisha shughuli za kijamii kwenye maeneo ya mapito ya wanyama (shoroba) au karibu na hifadhi za taifa au mapori ya akiba. Mhe. Kitandula asisisitiza kuwa nilazima wakati wote uanzishwaji wa shughuli za maendeleo uzingatie mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Simon Simalenga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alisema moja ya Mipango ya Mkoa wa Simiyu ni kujenga uwanja wa Ndege ambao utatumika kuleta watalii wa Nje na ndani hivyo kuchochea mapato yangiayo kupitia uhifadhi na utalii.

Shule ya sekondari ya Wasichana-Matongo ilianza kujengwa tangu enzi za awamu ya nne. Shule hii pamoja na kukamilika haikuwahi kudahili wanafunzi kutokana na kuwepo kwa changamoto ya Wanyamapori wakali na waharibifu kama tembo ambao mara kwa mara wamekuwa wakivamia eneo husika na kusababisha madhara kwa wakazi wa maeneo hayo na wakati mwingine kusababisha vifo.

Msanii Profesa Jay Ajitokeza Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuzushiwa Kifo...Asema Haya

Msanii Profesa Jay Ajitokeza Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuzushiwa Kifo...Asema Haya


Mbunge wa zamani wa Mikumi na msanii mkongwe wa muziki wa hip hop nchini Tanzania, Profesor Jay, amejitokeza kwa mara ya kwanza kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kuzushiwa taarifa za kifo. Kwenye posti hiyo, Professor Jay alimshukuru Mungu kwa zawadi ya uzima na kusema kuwa yupo tayari kwa mapambano ya maisha, akithibitisha kuwa hali yake ni nzuri.

Kwenye ujumbe wake, aliandika: "Asante sana Mungu kwa zawadi ya uzima, na kunilinda siku zote za maisha yangu, nipo kamiligado tayari kwa mapambano." Alimalizia posti hiyo kwa alama za ushindi na hashtag ya #KataaUtekaji, akijiunga na Watanzania wengine kulaani matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea kutokea nchini.


Mashabiki wake wengi wamejitokeza kumpongeza na kumpa maneno ya faraja, wakifurahia kuona kuwa msanii wao bado yupo salama na mwenye nguvu za kuendelea na mapambano.

Dodoma Jiji FC yazidi kumpa wakati mgumu Mwinyi Zahera Namungo FC


Na John Walter -Babati 

Dodoma Jiji FC imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Namungo FC goli 1-0.

Kabla ya ushindi wa Leo timu hiyo ilikuwa imecheza mechi mbili na kuambilia sare mechi moja sawa kichapo iliyopokea.

Mechi hizo ilikuwa dhidi ya Mashujaa FC katika uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma ambapo ilifungwa goli 1-0 kisha ikatoka suluhu dhidi ya Pamba Jiji FC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Katika mchezo dhidi ya Namungo FC ambayo imepigwa kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara dakika 45 zilianza kwa kasi ambapo Dodoma Jiji FC ndio walinufaika mapema kabisa.

Dakika ya kwanza kupitia kwa Paul Peter ambaye alimalizia mpira wa uliotemwa na kipa wa Namungo FC,Beno Kakolanya baada ya kupangua mpira uliopigwa na Idd Kipagwile.

Licha ya Namungo FC kupambana kutaka kusawazisha lakini uimara wa safu ya ulinzi wa Dodoma Jiji FC ambayo ilikuwa inaongozwa na Joash Onyango na Augustino Nsata kudhibiti kabisa washambuliaji Fabrice Ngoy na Pius Buswita na kushindwa kumletea madhara kipa Alain  Ngeleka na kupelekea dakika 45 za kwanza kukamilika kwa Dodoma Jiji kuongoza kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili Namungo FC ni kama haikufanyia kazi namna ya kugeuza magoli nafasi ambazo wanazitengeneza licha ya Dodoma Jiji FC kuonekana kurudi nyuma na wao kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini wakashindwa kabisa kufanya hivyo.

Na kupelekea dakika 90 kukamilika kwa ushindi kwa Dodoma Jiji FC huku mchezaji Idd Kipagwile akichaguliwa mchezaji bora wa mchezo.

Kipigo kutoka kwa Dodoma Jiji FC inamweka pabaya kocha wa Namungo FC,Mwinyi Zahera kwani katika mechi tatu ambazo timu yake imecheza haijaonja ladha ya ushindi au hata sare kwa maana ya kupoteza zote.

Ilianza kwa kichapo mechi mbili nyumbani katika uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi ikipotea 2-1 kutoka kwa Tabora United,kisha ikachapika 2-0 kwa Fountain Gate FC.



Source

Thursday, September 12, 2024

Makabila Yenye Wanaume Wenye Sura Nzuri Tanzania

Makabila Yenye Wanaume Wenye Sura Nzuri Tanzania


Tanzania ni nchi yenye utajiri wa utamaduni na makabila mbalimbali, kila moja likiwa na sifa na historia zake za kipekee. Hapa tunachunguza baadhi ya makabila ambayo yana sifa ya kuwa na wanaume wenye sura nzuri nchini Tanzania. Wanyakyusa


Wanyakyusa wanapatikana katika maeneo ya kusini mwa Tanzania, hasa mkoani Mbeya. Wanaume wa kabila hili wanajulikana kwa kuwa na miili yenye nguvu na umbo zuri kutokana na maisha yao ya kikazi, hasa katika kilimo na ufugaji.


Sura zao zimejengeka kutokana na mazoezi ya asili, wakionekana wenye afya na mvuto wa kipekee. Aidha, tabia yao ya heshima na utu inafanya waonekane wa kuvutia zaidi.


Wachaga Wachaga wanatoka kwenye milima ya Kilimanjaro na wanajulikana kwa juhudi zao katika kazi na biashara. Wanaume wa kabila hili wanavutia kwa sura nzuri pamoja na tabia ya kufanya kazi kwa bidii, jambo ambalo linawafanya kuwa wa kuvutia mbele ya watu wengi.


Pia, kwa sababu ya mazingira ya baridi wanamoishi, ngozi zao huwa nzuri na zenye afya, jambo linaloongeza uzuri wao wa asili.


Wamasai Wamasai ni kabila maarufu sana kwa utamaduni wao wa kipekee na ujasiri. Wanaume wa Kimasai wanajulikana kwa miili yao yenye nguvu, umbo la kipekee, na urefu wao unaovutia.


Mavazi yao ya kiasili pamoja na mapambo ya shanga huongeza mvuto wao, na kufanya wawe na haiba ya kipekee ambayo inatambulika sio tu Tanzania bali pia duniani kote. Ujasiri wao wa kiasili na heshima wanayopewa katika jamii ni sifa zinazowafanya wawe warembo kwa namna yao.


Wahaya


Wahaya wanatoka Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, hasa mkoani Kagera. Wanaume wa Kihaya wanajulikana kwa sura nzuri na tabia zao za kistaarabu. Wahaya ni watu wenye elimu na wengi wao wamepata mafanikio katika nyanja mbalimbali.


Hili limeongeza haiba yao, kwani wengi wanavutia kutokana na mchanganyiko wa sura nzuri na akili timamu. Pia, ngozi zao nzuri zinazovutia ni sifa moja kuu wanayojivunia.


Wazaramo Wazaramo ni kabila linalopatikana maeneo ya Pwani, hasa karibu na jiji la Dar es Salaam. Wanaume wa kabila hili wanajulikana kwa uzuri wao wa asili na ujasiri wao wa kijamii.


Wanajivunia kuwa na miili iliyokonda na yenye nguvu, na pia wanajua kuzungumza vizuri na kutabasamu, jambo linaloongeza mvuto wao. Ukarimu na tabia zao za kuishi na watu kwa amani huwafanya kuwa wapenzi wa wengi.


Wasukuma


Wasukuma, kabila kubwa zaidi Tanzania, wanatokea mikoa ya Kanda ya Ziwa kama Mwanza, Shinyanga, na Simiyu. Wanaume wa Kisukuma wana sifa ya kuwa na sura nzuri pamoja na miili yenye nguvu kutokana na maisha yao ya kilimo na ufugaji.


Ni watu wa upole na heshima, jambo linaloongeza mvuto wao kwa watu wanaokutana nao. Pia, wana ujasiri wa asili na wanajulikana kwa kuwa wachapa kazi, sifa zinazowafanya kuwa wa kuvutia zaidi.

Dkt Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka IFAD


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo - IFAD wanaosimamia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika ukumbi wa Ofisi hiyo leo 12 Septemba, 2024 Jijini Dodoma. 


  


Airtel Africa Foundation yazindua ‘Airtel Africa Fellowship Program’ kuwawezesha wanafunzi wa IIT Madras Zanzibar


Airtel Africa Foundation imezindua programu maalum ya uanazouni iitwayo 'Airtel Africa Fellowship' itakayowanufaisha  wanafunzi wa shahada ya kwanza ya IIT Madras Zanzibar ambayo ni kampasi ya kigeni ya kwanza kuwahi kuanzishwa na IIT.
 
Programu ya 'Airtel Africa Fellowship'  inalenga kuwasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye uchumi na jamii mbalimbali ambao wanastahiili kujiunga na shahada ya sayansi ya TEHAMA Pamoja na kujifunza maswala ya akili mnemba yanayotolewa na taasisi ya teknolojia ya Madras (IITM) visiwani Zanzibar. Kwa hatua ya awali Airtel imeanza na  dola za kimarekani $500,000, programu hii  itawanufaisha wanafunzi 10 wa shahada ya kwanza katika kipindi chote cha miaka minne ya masomo yao.
 
Programu ya 'Airtel Africa Fellowship' imeanza rasmi mwaka huu 2024 ikiwa na lengo kusaidia maendeleo ya Afrika ambapo Airtel Africa Foundation imedhamiria kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha na kidijitali katika maeneo mbalimbali kwa kuzingatia zaidi sekta ya elimu na utunzaji wa mazingira.

Programu hii ya uanazuoni ni mpango wa kwanza kuwahi kutekelezwa ili kuboresha fursa za elimu kwa ajili ya wanafunzi wanaostahili, hususani wale wanaotoka kwenye hali duni, ambao wamejiunga na IITM Zanzibar.
 
Programu hii imeundwa kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kutoka nchi 14 za Afrika ambazo ni Nigeria, Kenya, Malawi, Uganda, Zambia, Tanzania, Rwanda, DRC, Niger, Congo Brazzaville, Chad, Gabon, Madagascar na Seychelles.
 
Wanufaika wa udhamini huu watajulikana kama  'Airtel Africa Fellows' ambao watapokea asilimia 100 ya ada zao za chuo ambazo ni dola za kimarekani $12,000 kulingana na mchanganuo wa ada ya taasisi hiyo kwa ajili ya programu ya miaka minne. Pia watapatiwa dola za kimarekani $500 kwa ajili ya gharama za kujikimu ambazo zitatolewa kwa wanafunzi wanaostahili.

Mpango huu unalenga kubadilisha maisha na kuwaandaa viongozi wa baadae ambao watachangia katika ubunifu wa teknolojia na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.

Akizungumzia mpango huo wa uanazuoni, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar, Mheshimiwa, Lela Mohamed Mussa alisema, "IITM Zanzibar imeandaa utaratibu bora wa elimu ya kiufundi katika ukanda huu. Kutoa elimu ya hali ya juu kwa wanafunzi nchini Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla ambao wamefanya vizuri katika michakato ya usahili na mitihani, msaada kifedha ni kipaumbele muhimu kwetu. Tunashukuru kwa msaada huu kutoka Airtel Africa Foundation ambao utaboresha jitihada zetu binafsi kupitia mwelekeo huu."
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Airtel Africa Foundation, Dkt Olusegun Ogunsanya alisema, "Tunafuraha ya kushirikiana na IITM Madras Zanzibar kutoa fursa kwa vijana wa kiafrika waweze kupata elimu bora. Mpango huu unalenga kuchangia katika ukuaji wa bara la Afrika. Tunatarajia kuendelea kutengeneza fursa nyingi zaidi kwenye elimu pamoja na ujumuishi wa huduma za kifedha  kidijitali na kulinda mazingira.
 
Naye Mkurugenzi wa IIT Madras, Prof Veezhinathan Kamakoti alisema, "IIT Madras imejidhatiti kwa kuanzisha kampasi yenye ubora duniani visiwani Zanzibar. Tunafarijika kuaona  Airtel Africa Foundation imetuunga mkoni  katika jitihada hizi. Tunatarajia kukaribisha awamu ya pili ya wanafunzi kujiunga na kampasi ya IITM Zanzibar mwaka huu. Tunaishukuru sana Airtel Africa Foundation kwa kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya hawa viongozi wa taifa la baadae."

VIDEO: Tyla Amkatalia Usher Asimkamatie Kiuno Chake LIVE Walipokuwa Wakiicheza wakicheza WATER


VIDEO: Tyla amkatalia Usher asimkamatie kiuno chake LIVE walipokuwa wakiicheza wakicheza WATER



Source

WANAHARAKATI- ELIMU ITOLEWE YAKUTOSHA KUTOKOMEZA MILA ZINAZOMKANDAMIZA MWANAMKE KWENYE JAMII


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIKA Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) zilizofanyika Septemba 11, 2024, wanaharakati wa jinsia walisisitiza umuhimu wa elimu katika kupambana na mila potofu zinazokandamiza haki za wanawake.

Akizungumza katika GDSS, Elizabeth Kiteleko, mwanaharakati kutoka Manzese, alisisitiza kwamba baadhi ya mila potofu bado zinakandamiza haki za wanawake, alitolea mfano mila zinazohusiana na urithi, ambapo mwanamke anapokuwa mjane au yatima, mara nyingi hana haki ya kurithi mali kutoka kwa wazazi au mume.

Aidha Kiteleko alishauri kwamba mila hizi zinahitaji kuboreshwa ili ziendane na wakati wa sasa na kuhakikisha kwamba wanawake wanapata haki zao za msingi kama ilivyo kwa watu wengine.

Kwa upande wake mwanaharakati kutoka Mbagala, Omary Makota alibainisha kwamba mila nyingi bado zinamkandamiza mtoto wa kike, huku akisema kwamba ukosefu wa elimu ndio sababu kuu inayowezesha mila hizi potofu kuendelea.

Pamoja hayo, Makota alitoa wito kwa jamii kuongeza elimu kuhusu haki za wanawake na watoto wa kike ili kuhakikisha kuwa mila hizi zinasahihishwa.

Elimu ni muhimu katika kupinga mila potofu na kuhakikisha usawa wa haki kwa wanawake. Wanaharakati wanakubaliana kuwa kuboresha mitaala ya elimu na kuelimisha jamii ni hatua muhimu katika kuhakikisha haki za wanawake na watoto wa kike zinaheshimiwa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...