Friday, September 13, 2024

Dodoma Jiji FC yazidi kumpa wakati mgumu Mwinyi Zahera Namungo FC


Na John Walter -Babati 

Dodoma Jiji FC imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Namungo FC goli 1-0.

Kabla ya ushindi wa Leo timu hiyo ilikuwa imecheza mechi mbili na kuambilia sare mechi moja sawa kichapo iliyopokea.

Mechi hizo ilikuwa dhidi ya Mashujaa FC katika uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma ambapo ilifungwa goli 1-0 kisha ikatoka suluhu dhidi ya Pamba Jiji FC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Katika mchezo dhidi ya Namungo FC ambayo imepigwa kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara dakika 45 zilianza kwa kasi ambapo Dodoma Jiji FC ndio walinufaika mapema kabisa.

Dakika ya kwanza kupitia kwa Paul Peter ambaye alimalizia mpira wa uliotemwa na kipa wa Namungo FC,Beno Kakolanya baada ya kupangua mpira uliopigwa na Idd Kipagwile.

Licha ya Namungo FC kupambana kutaka kusawazisha lakini uimara wa safu ya ulinzi wa Dodoma Jiji FC ambayo ilikuwa inaongozwa na Joash Onyango na Augustino Nsata kudhibiti kabisa washambuliaji Fabrice Ngoy na Pius Buswita na kushindwa kumletea madhara kipa Alain  Ngeleka na kupelekea dakika 45 za kwanza kukamilika kwa Dodoma Jiji kuongoza kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili Namungo FC ni kama haikufanyia kazi namna ya kugeuza magoli nafasi ambazo wanazitengeneza licha ya Dodoma Jiji FC kuonekana kurudi nyuma na wao kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini wakashindwa kabisa kufanya hivyo.

Na kupelekea dakika 90 kukamilika kwa ushindi kwa Dodoma Jiji FC huku mchezaji Idd Kipagwile akichaguliwa mchezaji bora wa mchezo.

Kipigo kutoka kwa Dodoma Jiji FC inamweka pabaya kocha wa Namungo FC,Mwinyi Zahera kwani katika mechi tatu ambazo timu yake imecheza haijaonja ladha ya ushindi au hata sare kwa maana ya kupoteza zote.

Ilianza kwa kichapo mechi mbili nyumbani katika uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi ikipotea 2-1 kutoka kwa Tabora United,kisha ikachapika 2-0 kwa Fountain Gate FC.



Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...