Thursday, September 12, 2024

Airtel Africa Foundation yazindua ‘Airtel Africa Fellowship Program’ kuwawezesha wanafunzi wa IIT Madras Zanzibar


Airtel Africa Foundation imezindua programu maalum ya uanazouni iitwayo 'Airtel Africa Fellowship' itakayowanufaisha  wanafunzi wa shahada ya kwanza ya IIT Madras Zanzibar ambayo ni kampasi ya kigeni ya kwanza kuwahi kuanzishwa na IIT.
 
Programu ya 'Airtel Africa Fellowship'  inalenga kuwasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye uchumi na jamii mbalimbali ambao wanastahiili kujiunga na shahada ya sayansi ya TEHAMA Pamoja na kujifunza maswala ya akili mnemba yanayotolewa na taasisi ya teknolojia ya Madras (IITM) visiwani Zanzibar. Kwa hatua ya awali Airtel imeanza na  dola za kimarekani $500,000, programu hii  itawanufaisha wanafunzi 10 wa shahada ya kwanza katika kipindi chote cha miaka minne ya masomo yao.
 
Programu ya 'Airtel Africa Fellowship' imeanza rasmi mwaka huu 2024 ikiwa na lengo kusaidia maendeleo ya Afrika ambapo Airtel Africa Foundation imedhamiria kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha na kidijitali katika maeneo mbalimbali kwa kuzingatia zaidi sekta ya elimu na utunzaji wa mazingira.

Programu hii ya uanazuoni ni mpango wa kwanza kuwahi kutekelezwa ili kuboresha fursa za elimu kwa ajili ya wanafunzi wanaostahili, hususani wale wanaotoka kwenye hali duni, ambao wamejiunga na IITM Zanzibar.
 
Programu hii imeundwa kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kutoka nchi 14 za Afrika ambazo ni Nigeria, Kenya, Malawi, Uganda, Zambia, Tanzania, Rwanda, DRC, Niger, Congo Brazzaville, Chad, Gabon, Madagascar na Seychelles.
 
Wanufaika wa udhamini huu watajulikana kama  'Airtel Africa Fellows' ambao watapokea asilimia 100 ya ada zao za chuo ambazo ni dola za kimarekani $12,000 kulingana na mchanganuo wa ada ya taasisi hiyo kwa ajili ya programu ya miaka minne. Pia watapatiwa dola za kimarekani $500 kwa ajili ya gharama za kujikimu ambazo zitatolewa kwa wanafunzi wanaostahili.

Mpango huu unalenga kubadilisha maisha na kuwaandaa viongozi wa baadae ambao watachangia katika ubunifu wa teknolojia na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.

Akizungumzia mpango huo wa uanazuoni, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar, Mheshimiwa, Lela Mohamed Mussa alisema, "IITM Zanzibar imeandaa utaratibu bora wa elimu ya kiufundi katika ukanda huu. Kutoa elimu ya hali ya juu kwa wanafunzi nchini Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla ambao wamefanya vizuri katika michakato ya usahili na mitihani, msaada kifedha ni kipaumbele muhimu kwetu. Tunashukuru kwa msaada huu kutoka Airtel Africa Foundation ambao utaboresha jitihada zetu binafsi kupitia mwelekeo huu."
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Airtel Africa Foundation, Dkt Olusegun Ogunsanya alisema, "Tunafuraha ya kushirikiana na IITM Madras Zanzibar kutoa fursa kwa vijana wa kiafrika waweze kupata elimu bora. Mpango huu unalenga kuchangia katika ukuaji wa bara la Afrika. Tunatarajia kuendelea kutengeneza fursa nyingi zaidi kwenye elimu pamoja na ujumuishi wa huduma za kifedha  kidijitali na kulinda mazingira.
 
Naye Mkurugenzi wa IIT Madras, Prof Veezhinathan Kamakoti alisema, "IIT Madras imejidhatiti kwa kuanzisha kampasi yenye ubora duniani visiwani Zanzibar. Tunafarijika kuaona  Airtel Africa Foundation imetuunga mkoni  katika jitihada hizi. Tunatarajia kukaribisha awamu ya pili ya wanafunzi kujiunga na kampasi ya IITM Zanzibar mwaka huu. Tunaishukuru sana Airtel Africa Foundation kwa kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya hawa viongozi wa taifa la baadae."

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...