Sunday, July 28, 2024

Serikali Yalifungia Kanisa la Mchungaji Dominic Kiboko ya Wachawi


Wizara ya mambo ya ndani imeagiza kufungwa kwa kanisa la christian life linaloongozwa na mchungaji Dominic Dibwe anaefahamika kwa jina la "Kiboko ya Wachawi", lililopo Buza kwa Lulenge jijini Dar es salaam.

Barua kutoka wizara hiyo kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya kiraia inamuelekeza mwenyekiti wa kanisa la Christian Life na Mchungaji Dominic kufunga tawi la kanisa hilo linaoendeshwa na pasta huyo.

miongoni mwa sababu za kufungwa kwake ni mafundisho yanayodaiwa kusababisha hofu katika jamii na mahubiri yanayopingana na maadili, desturi na utamaduni wa Mtanzania.

tuhuma nyingine ni pamoja na kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu madhabahuni, kutoa mahubiri ya uchochezi na kuhimiza waumini wa kanisa kuua watu kwa tuhuma za uchawi.

Barua hiyo ambayo inaonekana kusainiwa na Msajili Emanuel Kihampa inaeleza kuwa tuhuma hizo ni kinyume na imani ya kikristo, katiba ya kanisa na kanuni ikiwa ni pamoja na kuweka ada ya 500,000 kwa waumini kupata huduma ya maombi

Saturday, July 27, 2024

RAIS SAMIA ASISITIZA UMUHIMU WA UHURU WA HABARI


* Amuagiza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa kusimamia utekelezaji wa R4

* Awakumbusha wanahabari kuwa hakuna uhuru usio na mipaka


Julai 27, 2024

Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa uhuru wa habari na kuvitaka vyombo vya habari nchini vizingatie mipaka ya uhuru huo.

Rais Samia alitoa kauli hiyo jana Ikulu, Dar es Salaam, baada ya kumuapisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa.

"Wizara ya Habari ni muhimu sana katika utekelezaji wa ile falsafa yetu ya R4. Na hapa nitagusia uhuru wa habari kwamba lazima uendelee kusimamiwa kikamilifu," alisema.

Hata hivyo, Rais Samia alisisitiza kuwa "hakuna uhuru usiokuwa na mipaka yake. Kwa hiyo uhuru wa habari with (pamoja na) mipaka ya uhuru huo."

Rais Samia amemuagiza Silaa ashirikiane na wadau wa sekta ya habari katika majukumu yake mapya.

"Watu wa sekta ya habari ni muhimu sana, sana, sana kwa taifa hili. Vyombo vyote vya habari ni muhimu sana kwa taifa letu," alisisitiza.

Kauli ya Rais Samia inakuja huku Tanzania ikiwa imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazolinda uhuru wa vyombo vya habari kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa mwaka 2024.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya mwaka huu ya taasisi ya kimataifa ya Reporters Without Borders (RSF).

Ripoti hiyo inaonesha kuwa Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 143 kwa mwaka 2023 hadi nafasi ya 97 mwaka huu.

Kupanda huko kwa nafasi 46 ndani ya mwaka mmoja kunatokana na mafanikio makubwa ya kuimarika kwa mazingira ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania kulinganisha na nchi zote za Afrika chini ya uongozi wa Rais Samia.

Kwa kushika nafasi ya 97 kati ya nchi 180 duniani, Tanzania imekuwa kinara wa nchi zote za Afrika Mashariki kwa uhuru wa habari mwaka huu.

Tanzania iko vizuri kwenye uhuru wa habari kuliko Kenya (102), Burundi (108), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (123), Uganda (128), Sudani Kusini (136), Rwanda (144) na Somalia (145).

Utafiti wa RSF umeangalia masuala kadhaa muhimu, ikiwemo misingi ya kisheria, hali ya kiuchumi, hali ya kisiasa, usalama wa wanahabari na dhana ya kijamii na kitamaduni.

Tangu alipoingia madarakani Machi 2021, Rais Samia ameimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini kama sehemu ya falsafa yake ya R4.

Falsafa ya R4 ya Rais Samia inazingatia maeneo ya Reform (mageuzi), Reconciliation (maridhiano), Resilience (ustahamilivu) na Rebuilding of the nation (kujenga upya).

Serikali ya Raia Samia imefungulia magazeti yaliyokuwa yamefungiwa na kuimarisha mazingira ya waandishi wa habari na vyombo vya habari kufanya kazi zao nchini.

Tangu Rais Samia alipoingia madarakani, matukio ya vyombo vya habari kufungiwa, kupigwa faini, waandishi kukamatwa au kuuwawa wakiwa katika majukumu yao ya kazi yametoweka nchini.

Kisa Yanga Fei Toto Ashindwa Kusajiliwa Kaizer Chiefs na Mamelodi



KISA YANGA FEI TOTO ashindwa kununuliwa MAMELOD na KAIZER CHIEFS

Kiungo wa Azam Feisal Salum Abdallah (Fei Toto) amejikuta akipitwa na bahati za kucheza kwenye timu kubwa za Afrika kwasababu ya Kigezo kilichowekwa na Yanga kwenye mkataba wake wa kwenda Azam

Klabu ya Yanga na Azam walikubaliana kwamba Endapo Fei toto atauzwa na Azam kwenda timu yoyote basi Azam wanatakiwa wailipe YANGA Shilingi Billion 1 za Kitanzania, kitu ambacho kimefanya iwe kazi ngumu kwa Feitoto kuuzika kwasababu dau lake linaanzia Billion 1

Klabu mbalimbali zikiwemo MAMELOD SUNDOWNS na KAIZER CHIEFS zilituma maombi ya kumtaka Mzanzibari huyo lakini bei waliyopewa wenyewe wakashangaa😂😂😂

Ikumbukwe sio kwamba Azam wanataja bei kubwa kwa kupenda ila ni mkataba ndo unawafunga mpaka pale miaka 3 itakapoisha

Je, miaka 3 ikishaisha bado fei atahitajika nje ya nchi???
.

RPC Katabazi akabidhi vitimwendo 20 vilivyotolewa na BAKWATA.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara SACP George Katabazi amekabidhi viti mwendo 20 kwa watu wenye uhitaji maalumu vilivyotolewa na Baraza la  waislamu mkoa wa Manyara BAKWATA.

Kamanda Katabazi amewaomba watumiaji wa hizo viti mwendo wazingatie Sheria za Barabarani kwasababu baiskeli hizo zitakuwa zinatumika Barabarani ambapo kutakuwa na watumiaji wengine wa Barabara ili waweze kuepuka ajali za Barabarani.

Pia ameendelea kusemakuwa jeshi la polisi lipotayari kuwalinda kwasababu jukumu la jeshi la polisi ni kulinda raia na Mali zao lakini ulinzi huo siyo wa jeshi la polisi pekee hata viongozi wa dini wadau mbalimbali Taasisi pia wanajukumu la kuwalinda watu hao wenye uhitaji

Naye shekhe wa mkoa wa Manyara Mohamed Kadidi amewahasa walezi wa watu hao kuwa watunzaji wa viti hivyo ili kuweza kudumu navyo kwa muda mrefu huku akiendelea kusema kuwa Taasisi na wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kusaidia wenye uhitaji

Friday, July 26, 2024

Maana ya ‘SANDA’ iliyopo jezi ya Simba SC

 

Maana ya 'SANDA' iliyopo jezi ya Simba SC

Sababu ya jezi za Simba kuandikwa neno Sanda zimeelezwa,wahusika wamewatoa hofu waliozitafsiri vinginevyo, kutambua kwamba ni ubunifu walioamua kuja nao msimu ujao.


Alipotafutwa Yusuph Yenga, ambaye ni msemaji wa Sandaland alisema walikaa chini na kuona msimu ujao waje kivingine na jina la Sanda ni la Sandaland mwenyewe, hivyo limefupishwa kwenye jezi.


"Kuna mchakato mrefu unazingatiwa hadi kufikia hatua ya kuzitengeneza. Tumetumia zaidi ya miezi mitatu, Sanda ni blandi kama zilivyo Blandi nyingine, hivyo wanaotafsiri wanavyoona jibu tulilowapa ni hilo," amesema.


Ameongeza: "Tumeona mwitikio ni mkubwa baada ya jezi hizo kuzitangaza, tumewahisha mapema tofauti na vipindi vingine ambavyo mashabiki walikuwa wanalalamika zinachelewa."


Msemaji huyo alitoa sababu nyingine kwamba wafanyabiashara wamekuwa wakipoteza pesa nyingi kuzalisha vitu vizuri, lakini hujitokeza wanaotengeneza feki zenye jina kama lao.


"Kuamua kufupisha jina na kutumia Sanda pia linatulinda kimaslahi, hivyo naamini kwa ufafanuzi huo, mashabiki watakuwa wameelewa," amesema.


Uzinduzi wa jezi hizo ulifanyika juzi katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo kulikuwa na mwitikio mkubwa wa Wanasimba.


Video ya kijana wa Kipakistani Akipigwa na Polisi wa Manchester Mbele ya Mamaye yazua hasira

 

Video ya kijana wa Kipakistani Akipigwa na Polisi wa Manchester Mbele ya Mamaye yazua hasira

Video ya kijana wa Kipakistani akipigwa na Polisi wa Manchester mbele ya mamaye yazua hasira

VIDEO:

Mbunge Rahhi awapa Vijana na Wanawake mbinu za kujiajiri.

Na John Walter-Babati 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Mheshimiwa Yustina Rahhi ameendelea kuwawezesha Vijana na Wanawake mkoani humo kwa kugharamia Mafunzo yatakayowawezesha kuweza kujiajiri na kuacha kutegemea  ajira kutoka serikalini.

Mpaka sasa Mheshimiwa Rahhi ameshawawezesha Vijana na Wanawake wa wilaya za Mbulu, Kiteto, Simanjiro, Hanang'  na sasa wilaya ya Babati.

Mafunzo haya yanatolewa ili kuwajengea uwezo vijana na Wanawake, kuwapa maarifa na kujiajiri katika ujasiriamali.

Akifungua Mafunzo hayo Kata ya Magugu wilayani Babati, Mheshimiwa Yustina Rahhi aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa jitihada zake za kuwakwamua vijana kiuchumi kwa kuwapa maarifa wezeshi yanayowawezesha kupambana na umaskini kupitia shughuli za ujasiriamali kwa kuwapatia mikopo isiyokuwa na riba ili wajikwamue kiuchumi.

Mh. Rahhi amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  anapambana kuhakikisha Watanzania wanaingia kwenye uchumi wa kati ili Kiwango cha pato la mtanzania kifike angalau dola 10 kwa siku.


Amesema bidhaa ndogo ndogo kama karanga na  keki zinatumika kila siku hivyo wajasiriamali waliopatiwa Mafunzo hayo wazalishe kwa wingi bidhaa hizo.

Mh.Rahhi amewataka vijana hao kuyatumia maarifa waliyoyapata kwa weledi na kwa faida yao na jamii kwa ujumla ili kufikia azima ya serikali na ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Ujumla.

Source

Thursday, July 25, 2024

Msichana Aliyemkata Uume Mchumba Wake Akamatwa Mpakani Tanzania



Polisi katika Wilaya ya Kyotera Mkoa wa Kati nchini Uganda wanamshikilia, Harriet Ampayire (23) kwa tuhuma za kukata sehemu za siri za mchumba wake na kusababisha kifo chake.

Harriet inadaiwa alifanya uhalifu huo kwa aliyekuwa mpenzi wake Reagan Karamagi, Jumapili Julai 21, 2024 kisha kutoroka.

Msemaji wa Polisi Kanda ya Kusini, Twaha Kasirye amethibitisha kukamatwa kwa Harriet na kueleza kuwa atakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya upelelezi kukamilika.

"Mtuhumiwa alitaka kukimbia kwa kuvuka mpaka wa Mutukula ili kuingia Tanzania. Hata lakini tulifanikiwa kumkamata Jumanne," amesema Kamanda Kasirye.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mutukula, David Mujaasi amesema mpaka huo unatumika na wahalifu wengi kutoroka nchini humo baada ya kufanya matukio ya uhalifu.

"Tunaiomba Serikali ituchukulie hatua kuimarisha ulinzi kwa sababu tuko katika eneo ambalo wahalifu wanalitumia kupita," amesema.

Source

DMI YASHIRIKI MAONESHO YA VYUO VIKUU TANZANIA VISIWANI PEMBA


CHUO Cha Bahari Dar es Salaam ni miongoni mwa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi katika Maonesho ya Vyuo Vikuu Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Gombani - Pemba.

Maonesho hayo ni mfululizo wa maonesho ya vyuo vikuu yanayoandaliwa na kuratibiwa na NACTVET ambapo mwaka huu 2024 yalianzia jijini Arusha kufuatiwa Unguja na sasa kuhitimishwa katika kisiwa cha Pemba - viwanja vya Gombani.

DMI ikiongozwa na wataalam mbalimbali wa tasnia ya Bahari wapo mahiri kuelezea Kozi mbalimbali zitolewazo na DMI lakini pia pamoja na fursa zitokanazo na Bahari.

DMI katika Banda lao wamejipanga kutoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na usajili wa papo Kwa papo.

Karibu DMI chuo pekee chenye Kozi za kipekee nchini Tanzania na Afrika mashariki.

Wednesday, July 24, 2024

SERIKALI KUCHUKUA HATUA MADHUBUTI KUKABILIANA NA HOMA YA INI


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Kuelekea siku ya Homa ya Ini,Barani Afrika kuna Watu milioni 60 wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina B huku Watu milioni 10 wakiwa wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina C.

Aidha hapa nchini inakadiriwa kiwango cha ushamiri wa ugonjwa wa Homa ya Ini ni asilimia 3.5 (aina B) na asilimia 1 (aina C).

Kutokana na hali hiyo,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itandelea kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo Kujumuisha huduma za homa ya ini pamoja na magonjwa ya ngono kwenye Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ugonjwa wa UKIMWI (NACP).

Hayo yamelezwa leo Julai 24,2024 Jijini hapa na Mkuu wa Programu za UKIMWI,Ngono,Ini,Malaria,Kifua Kikuu,Uelimishaji mifumo ya afya,Dkt.Catherine Joakim wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa hivi sasa mpango huo unajulikana kama NASHCoP ambao ulizindiliwa mwezi Novemba mwaka 2023.

Ameeleza kuwa lengo ni kuimarisha upatikanaji wa chanjo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kuimarisha upatikanaji wa matibabu ya homa ya ini .

"Takwimu za Shirika la Afya Duniani za mwaka 2021 zinaonyesha kuwa Duniani kuna watu wapatao milioni 296 ambao wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina B na watu milioni 58 wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina C, " amesema

Ameeleza kuwa mbali na mikakati mbalimbali iliyopo Serikali itaendelea kuelimisha wananchi kuhusu ugonjwa wa homa ya ini.

"Kila Mwaka tarehe 28 ya mwezi Julai, Tanzania huungana na nchi nyingine Ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Homa ya Ini Duniani lengo ni kuongeza uelewa wa homa ya ini ambao husababisha ini kuvima na hivyo kupelekea uwezo mkubwa wa kupata ugonjwa kwenye ini au kansa ya ini, "amesema.

Licha ya hayo ameeleza kuwa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini yamepangwa kufanyika Sinza darajani, Uwanja wa TP, Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Julai, 2024 kuanzia saa 02:00 asubuhi. Kilele cha maadhimisho haya kitakuwa tarehe 28 Julai,2024 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa afya Ummy Mwalimu .

Ametaja huduma zitakazotolewa kuwa ni pamoja na kuhusiana na Virusi vya Homa ya Ini, VVU na lishe Upimaji wa maambukizi ya ini, Chanjo za homa ya Ini
Kuunganishwa na matibabu baada ya kukutwa na maambukiziUpimaji wa VVU,Upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza(kisukari na shinikizo la damu.

Pamoja na Mambo mengine kauli mbiu ya mwaka huu wa 2024 inasema "Ni Wakati wa Kuchukua Hatua" ikiyataka mataifa kuongeza kasi na juhudi makusudi katika huduma za kinga, uchunguzi na tiba ili kupunguza vifo vitokanavyo na maambuki ya virusi vinavyosababisha homa ya ini.

TRA SHINYANGA YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA DIDIA, PUNI KUSIKILIZA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIPA KODI

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga imekutana na wafanyabiashara na wajasiriamali waliopo mji mdogo wa Didia na Puni kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto wanazokumbana nazo sambamba na kutoa elimu.
Kikao hicho kimefanyika leo Julai 24, 2024 kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Kaimu Meneja wa Kodi kutoka TRA Shinyanga Ramadhan Omary ameeleza faida za matumizi ya mashine za risiti za kielektroniki (EFD) kwa wafanyabiashara na umuhimu wa kudai risisti kwa mteja aliyenunua bidhaa.

"Sisi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA jukumu letu ni kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa risiti kwa wateja na wanunuzi wanadai risiti halali ya bidhaa waliyonunua ndio maana leo tumekuja kutoa elimu na kusikiliza changamoto za walipa kodi wetu ili kuboresha utoaji huduma kwenye mamlaka yetu", amesema Ramadhan Omary.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Josephat Mwaipaya amesisitiza matumizi ya mashine za risiti za kielektroniki (EFD) wakati wa kufanya manunuzi kwa wafanyabiashara kwani ni takwa la kisheria.

"Sheria ya kodi inamtaka mnunuzi adai risiti halali kutoka kwa mfanyabiashara na asipofanya hivyo atakuwa amevunja sheria hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kutambua kuwa kudai na kutoa risiti halali ni wajubu wake, lengo likiwa ni kujenga nchi yetu kupitia mapato tunayokusanya", amesema Josephat Mwaipaya. 

Nao baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka mji mdogo wa Didia na Puni wameishukuru Mamlaka ya Mapato kwa kutoa elimu ya umuhimu wa matumizi ya mashine za risiti za kielektroniki (EFD) na kusikiliza changamato wanazokumbana nazo wakati wa ulipaji wa kodi.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Josephat Mwaipaya akizungumza wakati wa kikao hicho.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Josephat Mwaipaya akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kaimu Meneja wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Ramadhan Omary akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Mji Mdogo wa Didia akizungumza wakati wa kikao hicho.

Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Mji Mdogo wa Didia akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Mji Mdogo wa Didia akizungumza wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali waliojitokeza kwenye kikao hicho.
Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga wakitoa huduma kwa wateja.


Source

WORLD VISION TANZANIA YAKABIDHI VIFAA TIBA NA VITENDEA KAZI VYA MILIONI 159.2 SHINYANGA, RC MACHA AHAMASISHA WANANCHI KUPIMA AFYA


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shirika la World Vision Tanzania limekabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga ili kupunguza mahitaji na kuboresha huduma za afya katika jamii.

Vifaa tiba hivyo vimekabidhiwa leo Jumatano Julai 24,2024 na Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Shirika hilo Mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Kaihura amesema kwa kushirikiana na Serikali Idara ya Afya ya Mkoa wa Shinyanga na wilaya za Kishapu na Shinyanga yalibainika mahitaji ya vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma vilivyopo ndani ya eneo la Miradi ya Shirika la World Vision hivyo kufanikiwa kununua vifaa ili kupunguza mahitaji na kuboresha huduma za afya zinazotolewa.


"Tunapokabidhi rasmi vifaa hivi vyenye thamani ya shilingi 159,229,248.52/= muhimu kwako Mhe. Mkuu wa Mkoa kama Serikali vinawakilisha siyo tu maendeleo ya Kiteknolojia, bali pia ahadi yetu ya kusaidia mahitaji ya afya ya jamii yetu. Katika nyakati hizi ambapo mahitaji ya huduma bora za afya yanazidi kuongezeka, ushirikiano wetu na serikali unakuwa muhimu zaidi",amesema Kaihura.
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura (wa pili kushoto) akikabidhi moja ya vifaa tiba kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

Amevitaja vifaa tiba hivyo kuwa ni CHW Working gear (rain boot, rain coat, document bag & umbrella), Power bank,pico projectors, MUAC tapes for adult and children,baby weigh scale, weigh scale for adult,biscycles for CHWs and Peernetworks, T- shirts for CHWs, Peer networks, Sports gears – Football and Netball, Working gears for CHWs peer networks, mobile phone for CHWs, Umbrella Large size, Rain boot and coat, haemocue mashines.

Vingine ni Sodium chloride injection 0.9% for IV,500ML 24 BT, Suction device (penguin sucker) silcon material R, cotton wool absorbent 500mg, Gauze absorbent folder cotton 16 PLY, Apron Theatre Plastic, Gloves surgical latex rubber sterile size 7.5, screen kit for HPV – Speculum Vaginal cusco medium, screen foulding with curtains, Examination bed, Forceps sponge holding straight 20CM, Sterile cotton swab stick for specimen collection, galli pot medium 150CC, Screen kit for HPV – Speculum vaginal cusco small & Large.
Sehemu ya Vifaa tiba na vitendea kazi vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga

"Kwa maafisa wa serikali hasa watoa huduma za afya wanaopokea vifaa hivi, tunatumaini kuwa vitachangia sana katika juhudi zenu za kutoa huduma za afya zinazopatikana na zenye ufanisi kwa jamii zetu. Tukio hili la leo lizidi kuimarisha ushirikiano wetu kati yetu World Vision na Serikali ili kuwezesha kuendelea kuboresha maisha ya wale tunaowahudumia",ameongeza Kaihura.

Meneja huyo wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa amesema shirika hilo ambalo limejikita kufanya kazi na watoto, familia na jamii ili kupambana na umaskini na ukosefu wa haki limeendelea kuishirikisha jamii katika uboreshaji wa huduma kupitia miradi mbalimbali ya afya, lishe, elimu, uzalishaji mali na utetezi wa kijinsia ili kuhakikisha kuna ustawi wa mtoto.

"Katika Mkoa wa Shinyanga, Shirika la World Vision lina miradi katika wilaya za Shinyanga, Kishapu na Kahama likishirikiana na serikali na jamii kutoa huduma za jamii. Miradi hiyo ni Mpango wa Eneo Kilago uliopo Kahama, Mpango wa eneo Mwakipoya, Mpango wa eneo Lagana, Mradi wa NOURISH katika wilaya ya Kishapu na Mradi wa GROW ENRICH unaofanya kazi katika wilaya ya Kishapu na Shinyanga",ameeleza.
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura.

"Leo tumekutanishwa na miradi ya GROW ENRICH ambao unafadhiliwa na nchi ya Ujerumani na NOURISH unafadhiliwa na nchi ya Ireland. Miradi hii inafanya kazi ya kuboresha lishe, afya ya mama na mtoto, afya ya uzazi kwa vijana balehe katika wilaya za Kishapu na Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wetu Shirika la Kivulini",amebainisha Kaihura.

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amelishukuru Shirika la World Vision Tanzania na KIVULINI kwa namna wanavyoshirikiana na serikali kuboresha lishe, afya ya mama na mtoto na afya ya uzazi kwa jamii.

"Tumeshuhudia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha afya ya jamii, tunawashukuru wadau kwa namna mnavyounga mkono juhudi za serikali kuboresha sekta ya afya. Kupitia World Vision tuna historia ya kupokea vifaa na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, na vifaa hivi vipya tulivyopokea leo tutavitumia kama inavyotakiwa",amesema Mhe. Macha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

Mkuu huyo wa Mkoa pia amewahamasisha wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao ili kuchukua hatua za mapema akitilia mkazo kupima Saratani ya Mlango wa kizazi, Presha na Tezi dume.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amesema mashirika la World Vision na KIVULINI yamekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha afya ya jamii na kwamba utoaji huo wa baiskeli 73 utakuwa chachu ya watoa huduma ngazi ya jamii kuzifikia kaya kuhamasisha matumizi ya kujua viashiria vya hatari ngazi ya jamii na kuhamasisha kazi za CHF kaya kwa kaya, kuelimisha masuala ya lishe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally amesema Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa World Vision Tanzania limetoa baiskeli 73 ambazo zitakwenda kuwezesha watoa huduma za afya ngazi ya jamii kwenda nyumba kwa nyumba , Kijiji kwa Kijiji kutembelea zahanati, vikundi vya wanawake vijana lengo ni kutoa elimu ya afya na lishe na kutembelea mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kuhamasisha lishe na afya.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Jumatano Julai 24,2024 wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Jumatano Julai 24,2024 wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura akizungumza wakati World Vision Tanzania ikikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura akizungumza wakati World Vision Tanzania ikikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza wakati World Vision Tanzania ikikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati World Vision Tanzania ikikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza akipokea vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania.
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura ( wa pili kushoto) akikabidhi moja ya vifaa tiba kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura ( wa pili kushoto) akikabidhi moja ya vifaa tiba kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia) akiangalia moja ya vifaa tiba/vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mratibu wa Mradi wa GROW ENRICH kutoka Shirika la World Vision Tanzania, Shukrani Dickson (katikati) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha juu ya vifaa tiba na vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia) akiangalia moja ya vifaa tiba/vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mratibu wa Mradi wa GROW ENRICH kutoka Shirika la World Vision TanzaniaShukrani Dickson (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha juu ya vifaa tiba na vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Muonekano sehemu ya Vifaa tiba na vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akipokea vitendea kazi (baiskeli) zilizotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza wakati akikabidhi baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza wakati akikabidhi baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Sehemu ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Sehemu ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiendesha moja kati ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiendesha moja kati ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiendesha moja kati ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii mkoa wa Shinyanga.
Zoezi la kusaini nyaraka za makabidhiano likiendelea
Zoezi la kusaini nyaraka za makabidhiano likiendelea
Zoezi la kusaini nyaraka za makabidhiano likiendelea

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...