Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la World Vision Tanzania limekabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga ili kupunguza mahitaji na kuboresha huduma za afya katika jamii.
Vifaa tiba hivyo vimekabidhiwa leo Jumatano Julai 24,2024 na Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Shirika hilo Mjini Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Kaihura amesema kwa kushirikiana na Serikali Idara ya Afya ya Mkoa wa Shinyanga na wilaya za Kishapu na Shinyanga yalibainika mahitaji ya vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma vilivyopo ndani ya eneo la Miradi ya Shirika la World Vision hivyo kufanikiwa kununua vifaa ili kupunguza mahitaji na kuboresha huduma za afya zinazotolewa.
"Tunapokabidhi rasmi vifaa hivi vyenye thamani ya shilingi 159,229,248.52/= muhimu kwako Mhe. Mkuu wa Mkoa kama Serikali vinawakilisha siyo tu maendeleo ya Kiteknolojia, bali pia ahadi yetu ya kusaidia mahitaji ya afya ya jamii yetu. Katika nyakati hizi ambapo mahitaji ya huduma bora za afya yanazidi kuongezeka, ushirikiano wetu na serikali unakuwa muhimu zaidi",amesema Kaihura.
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura (wa pili kushoto) akikabidhi moja ya vifaa tiba kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
Amevitaja vifaa tiba hivyo kuwa ni CHW Working gear (rain boot, rain coat, document bag & umbrella), Power bank,pico projectors, MUAC tapes for adult and children,baby weigh scale, weigh scale for adult,biscycles for CHWs and Peernetworks, T- shirts for CHWs, Peer networks, Sports gears – Football and Netball, Working gears for CHWs peer networks, mobile phone for CHWs, Umbrella Large size, Rain boot and coat, haemocue mashines.
Vingine ni Sodium chloride injection 0.9% for IV,500ML 24 BT, Suction device (penguin sucker) silcon material R, cotton wool absorbent 500mg, Gauze absorbent folder cotton 16 PLY, Apron Theatre Plastic, Gloves surgical latex rubber sterile size 7.5, screen kit for HPV – Speculum Vaginal cusco medium, screen foulding with curtains, Examination bed, Forceps sponge holding straight 20CM, Sterile cotton swab stick for specimen collection, galli pot medium 150CC, Screen kit for HPV – Speculum vaginal cusco small & Large.
Sehemu ya Vifaa tiba na vitendea kazi vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga
"Kwa maafisa wa serikali hasa watoa huduma za afya wanaopokea vifaa hivi, tunatumaini kuwa vitachangia sana katika juhudi zenu za kutoa huduma za afya zinazopatikana na zenye ufanisi kwa jamii zetu. Tukio hili la leo lizidi kuimarisha ushirikiano wetu kati yetu World Vision na Serikali ili kuwezesha kuendelea kuboresha maisha ya wale tunaowahudumia",ameongeza Kaihura.
Meneja huyo wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa amesema shirika hilo ambalo limejikita kufanya kazi na watoto, familia na jamii ili kupambana na umaskini na ukosefu wa haki limeendelea kuishirikisha jamii katika uboreshaji wa huduma kupitia miradi mbalimbali ya afya, lishe, elimu, uzalishaji mali na utetezi wa kijinsia ili kuhakikisha kuna ustawi wa mtoto.
"Katika Mkoa wa Shinyanga, Shirika la World Vision lina miradi katika wilaya za Shinyanga, Kishapu na Kahama likishirikiana na serikali na jamii kutoa huduma za jamii. Miradi hiyo ni Mpango wa Eneo Kilago uliopo Kahama, Mpango wa eneo Mwakipoya, Mpango wa eneo Lagana, Mradi wa NOURISH katika wilaya ya Kishapu na Mradi wa GROW ENRICH unaofanya kazi katika wilaya ya Kishapu na Shinyanga",ameeleza.
"Leo tumekutanishwa na miradi ya GROW ENRICH ambao unafadhiliwa na nchi ya Ujerumani na NOURISH unafadhiliwa na nchi ya Ireland. Miradi hii inafanya kazi ya kuboresha lishe, afya ya mama na mtoto, afya ya uzazi kwa vijana balehe katika wilaya za Kishapu na Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wetu Shirika la Kivulini",amebainisha Kaihura.
Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amelishukuru Shirika la World Vision Tanzania na KIVULINI kwa namna wanavyoshirikiana na serikali kuboresha lishe, afya ya mama na mtoto na afya ya uzazi kwa jamii.
"Tumeshuhudia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha afya ya jamii, tunawashukuru wadau kwa namna mnavyounga mkono juhudi za serikali kuboresha sekta ya afya. Kupitia World Vision tuna historia ya kupokea vifaa na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, na vifaa hivi vipya tulivyopokea leo tutavitumia kama inavyotakiwa",amesema Mhe. Macha.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amewahamasisha wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao ili kuchukua hatua za mapema akitilia mkazo kupima Saratani ya Mlango wa kizazi, Presha na Tezi dume.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amesema mashirika la World Vision na KIVULINI yamekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha afya ya jamii na kwamba utoaji huo wa baiskeli 73 utakuwa chachu ya watoa huduma ngazi ya jamii kuzifikia kaya kuhamasisha matumizi ya kujua viashiria vya hatari ngazi ya jamii na kuhamasisha kazi za CHF kaya kwa kaya, kuelimisha masuala ya lishe.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally amesema Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa World Vision Tanzania limetoa baiskeli 73 ambazo zitakwenda kuwezesha watoa huduma za afya ngazi ya jamii kwenda nyumba kwa nyumba , Kijiji kwa Kijiji kutembelea zahanati, vikundi vya wanawake vijana lengo ni kutoa elimu ya afya na lishe na kutembelea mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kuhamasisha lishe na afya.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Jumatano Julai 24,2024 wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Jumatano Julai 24,2024 wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura akizungumza wakati World Vision Tanzania ikikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura akizungumza wakati World Vision Tanzania ikikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza wakati World Vision Tanzania ikikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati World Vision Tanzania ikikabidhi vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza akipokea vifaa tiba na vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 159.2 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania.
Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura ( wa pili kushoto) akikabidhi moja ya vifaa tiba kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision TanzaniaMeneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jacqueline Kaihura ( wa pili kushoto) akikabidhi moja ya vifaa tiba kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia) akiangalia moja ya vifaa tiba/vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mratibu wa Mradi wa GROW ENRICH kutoka Shirika la World Vision Tanzania, Shukrani Dickson (katikati) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha juu ya vifaa tiba na vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia) akiangalia moja ya vifaa tiba/vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mratibu wa Mradi wa GROW ENRICH kutoka Shirika la World Vision Tanzania, Shukrani Dickson (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha juu ya vifaa tiba na vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Muonekano sehemu ya Vifaa tiba na vitendea kazi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akipokea vitendea kazi (baiskeli) zilizotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza wakati akikabidhi baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza wakati akikabidhi baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamiiSehemu ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Sehemu ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiendesha moja kati ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiendesha moja kati ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiendesha moja kati ya baiskeli 73 zilizotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ufadhili wa shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii mkoa wa Shinyanga.
Zoezi la kusaini nyaraka za makabidhiano likiendelea
Zoezi la kusaini nyaraka za makabidhiano likiendelea