Wizara ya mambo ya ndani imeagiza kufungwa kwa kanisa la christian life linaloongozwa na mchungaji Dominic Dibwe anaefahamika kwa jina la "Kiboko ya Wachawi", lililopo Buza kwa Lulenge jijini Dar es salaam.
Barua kutoka wizara hiyo kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya kiraia inamuelekeza mwenyekiti wa kanisa la Christian Life na Mchungaji Dominic kufunga tawi la kanisa hilo linaoendeshwa na pasta huyo.
miongoni mwa sababu za kufungwa kwake ni mafundisho yanayodaiwa kusababisha hofu katika jamii na mahubiri yanayopingana na maadili, desturi na utamaduni wa Mtanzania.
tuhuma nyingine ni pamoja na kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu madhabahuni, kutoa mahubiri ya uchochezi na kuhimiza waumini wa kanisa kuua watu kwa tuhuma za uchawi.
Barua hiyo ambayo inaonekana kusainiwa na Msajili Emanuel Kihampa inaeleza kuwa tuhuma hizo ni kinyume na imani ya kikristo, katiba ya kanisa na kanuni ikiwa ni pamoja na kuweka ada ya 500,000 kwa waumini kupata huduma ya maombi