Friday, July 26, 2024

Maana ya ‘SANDA’ iliyopo jezi ya Simba SC

 

Maana ya 'SANDA' iliyopo jezi ya Simba SC

Sababu ya jezi za Simba kuandikwa neno Sanda zimeelezwa,wahusika wamewatoa hofu waliozitafsiri vinginevyo, kutambua kwamba ni ubunifu walioamua kuja nao msimu ujao.


Alipotafutwa Yusuph Yenga, ambaye ni msemaji wa Sandaland alisema walikaa chini na kuona msimu ujao waje kivingine na jina la Sanda ni la Sandaland mwenyewe, hivyo limefupishwa kwenye jezi.


"Kuna mchakato mrefu unazingatiwa hadi kufikia hatua ya kuzitengeneza. Tumetumia zaidi ya miezi mitatu, Sanda ni blandi kama zilivyo Blandi nyingine, hivyo wanaotafsiri wanavyoona jibu tulilowapa ni hilo," amesema.


Ameongeza: "Tumeona mwitikio ni mkubwa baada ya jezi hizo kuzitangaza, tumewahisha mapema tofauti na vipindi vingine ambavyo mashabiki walikuwa wanalalamika zinachelewa."


Msemaji huyo alitoa sababu nyingine kwamba wafanyabiashara wamekuwa wakipoteza pesa nyingi kuzalisha vitu vizuri, lakini hujitokeza wanaotengeneza feki zenye jina kama lao.


"Kuamua kufupisha jina na kutumia Sanda pia linatulinda kimaslahi, hivyo naamini kwa ufafanuzi huo, mashabiki watakuwa wameelewa," amesema.


Uzinduzi wa jezi hizo ulifanyika juzi katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo kulikuwa na mwitikio mkubwa wa Wanasimba.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...