Friday, August 13, 2021

WACHAWI WAZUA GUMZO BAADA KUTUPA JENEZA LENYE VITU VYA AJABU MLANGONI

Wenyeji wa kijiji cha Karando nchini Kenya wameingiwa na hofu baada ya kuamka asubuhi na kukuta jeneza lililokuwa na kuku na rozari likiwa limetupwa katika nyumba ya mmoja wao.

Wenyeji hao waliamkia kisa hicho mnamo Alhamisi, Agosti 12,2021 asubuhi. Kando na kuku aliyekuwa hai na rosari, jeneza hilo pia lilikuwa na konokono na vitu vingine vya ajabu.

Mmiliki wa boma hilo Silvestor Okero alisema waliamka asubuhi na kupata jeneza hilo likiwa limetupwa nyumbani kwake.

Okero aliingiwa na wasiwasi na kumwita mmoja wa majirani zake aje kushuhudia kile alichokiona nyumbani kwake.

"Jeneza lilikuwa limefungwa kwa hivyo sikulifungua lakini nikampigia mmoja wa majirani zangu aje kunisaidia kuhusiana na suala hilo zito," Okero alisema.

Mwanaume huyo alisema maishani mwake hajawahi kushuhudia vituko kama hivyo namkuongeza kwamba amekuwa akiishi kwa amani na watu na wala hana uadui wowote na yeyote.

"Sina tatizo lolote na mtu yeyoye lakini nashuku huenda kisa hiki kimetekelezwa na mmoja wa jamaa zangu ambaye tunazozania shamba," aliongeza.

Mmoja wa majirani zake alisema kwamba alikwenda nyumbani humo alipopigiwa simu, akaona jeneza, na kuripoti jambo hilo kwenye kituo cha polisi cha Riat; jeneza hilo baadaye lilifunguliwa.

Alidokeza kwamba wenyeji waliliondoa jeneza hilo bomani mwake na kisha wakaliteketeza na tunguri zilizokuwa ndani. Wakazi hao walishuku huenda kikawa ni kisa cha uchawi na kuwataka maafisa wa polisi kuanzisha uchunguzi.

Walilalamikia kuongezeka kwa visa vya uchawi katika eneo hilo, wakisema vimelemaza maendeleo na kuwanyima usingizi.

CHANZO - TUKO NEWS

Source

Kumekucha..Sabaya Awataja Magufuli, Dk Mpango na Gavana BoT Kuwa Walifahamu Operesheni Aliyokuwa Akiifanya Arusha.



Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amewataja Hayati John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa akiifanya Arusha.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Ijumaa Agosti 13, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amewataja Hayati John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa akiifanya Arusha.

Sabaya amesema hayo wakati akitoa utetezi mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Odira Amworo kuwa alichokuwa anakifanya Arusha Februari 9, 2021 haikuwa operesheni yake ya kwanza kuagizwa na hayati Rais Magufuli 

Diwani wa CCM aangua kilio mahakamani akisimulia namna Sabaya alivyomtisha kwa bastol

Akiongozwa na Wakili anayemtetea Mosses Mahuna, wakati alipoanza kujitetea mahakamani hapo amesema kesi hiyo ni ya kutengeneza na yeye hajaiba wala kumtishia mtu yoyote kwa silaha.

Sabaya alisema siku ya tukio Februari 9, 2021 alipomaliza kuongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Hai, alipokea simu ya Dk Magufuli aliyemwelekeza kazi ya kufanya katika mkoa wa Arusha ambapo pia alipaswa kuwapitia watu wengine wanne katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo watu hao walikuwa na maelekezo juu ya kazi hiyo wanayoenda kufanya.

"Hiyo haikuwa kazi ya kwanza kwa sababu miezi michache iliyopita tulipewa zoezi la kukamata mitambo inayotengeneza noti bandia na tulifanikiwa kukamata mitambo na fedha Sh 800 Milioni bandia eneo la Chanika wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam ,Gavana wa BoT anajua na aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa wakati huo Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa sasa pia anafahamu,"

IGP Sirro akemea wanaojihusisha na dawa za kulevya



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameitaka jamii kujiepusha na kuacha vitendo vya udhalilishaji na biashara ya dawa za kulevya kwani vyombo vya dola vitatumia sheria zilizopo kuwashughulikia wanaojihusisha na vitendo hivyo.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa Cheo cha Sajenti wa Polisi yaliyofanyika kwa muda wa miezi miwili katika Chuo cha Polisi Zanzibar ambapo jumla ya wahitimu 1297 walihitimu mafunzo hayo na kupandishwa vyeo.

Kina Mbowe waigeuzia kibao Serikali, Hakimu atoa agizo



Freeman Mbowe akiwa mahakamani Kisutu
KIONGOZI wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania-Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iwasilishe ombi lao Mahakama Kuu ya Tanzania la kupinga matamshi yaliyotolewa na Taasisi ya Serikali, dhidi ya mashtaka ya kula njama za kufanya ugaidi yanayowakabili mahakamani hapo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi hilo limewasilishwa mahakamani hapo leo Ijumaa, tarehe 13 Agosti 2021 na mawakili upande wa utetezi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba.

Akiwasilisha ombi hilo, Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala, amedai matamshi hayo ambayo hakuyataja, yataathiri mwenendo wa kesi hiyo.

Amedai, wateja wake wanayaona matamshi hayo kama hukumu, hivyo hawana imani kama mashtaka yao yataendeshwa kwa uhuru mahakamani.


"Tumeleta taarifa ya kusudio la kuiomba mahakama ipeleke Mahakama Kuu kama suala la kikatiba, matamshi yaliyotolewa na taasisi fulani hapa nchini, watu wote wanaifahamu, wamesikia.

"Tunachosema maneno yale au matamshi yale kwa maoni yetu sisi na wateja wetu, yameingilia uhuru wa mahakama. Sio mahakama hii tu, lakini mahakama itakayokwenda kusikiliza shauri la ugaidi linalowakabili washtakwia," amedai Kibatala.

Katika maombi hayo, Mbowe na wenzake, wanaiomba Mahakama Kuu iangalie kama matamshi hayo yameingilia uhuru wa mahakama na kama itabainika yameingilia uhuru wa mhimili huo, kesi husika ifutwe.


"Kwa kuwa mamlaka ile yenye nguvu naishawishi basi matamshi yale kwa namna yalivyotamkwa, yamewafanya wateja wetu kuona tayari wamehukumiwa na kwamba hakuna namna yoyote wanaweza wakapata fair trial, tumeomba iangalie matamshi yale kama yameingilia uhuru wa mahakama," amesema Kibatala.

Kibata ameongeza "na iwapo au la matamshi yale yamesababisha kesi isiwe na mantiki tena na hakuna la kufanya isipokuwa kufutwa."

Kibatala amesema hayo nje ya Mahakama hiyo baada ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe 27 Agosti 2021.

Awali, Wakili wa serikali Pius Hilla, alisema kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini washtakiwa wameshinmdwa kufikishwa mahakamani kutokana na kukosekana usafiri jambo lililopingwa na Kibatala, akisema walipaswa kuletwa mahakamani na si kama walivyofanya.

STEVE NYERERE : MSISIKILIZE WAPOTOSHAJI KUHUSU CHANJO KACHANJENI



Na Magrethy Katengu - Dar es salaam
Wanzania wamehimizwa kupuuza maneno ya upotoshaji yanayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wanasiasa na watu maarufu viongozi wa dini kuhusu chanjo ya UVIKO -19.

Wito huo umetolewa leo na Balozi wa uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19 ambaye pia mwenyekiti wa taasisi ya Wazalendo kwanza Steve Mengele Nyerere wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo amesema wapo watu wanahamasisha wananchi kutokuchanja kwa kueleza madhara ambayo siyo ya kweli.

"Ukifanya ubishi wa hili jambo fanya mwenyewe usiwashawishi wengine kaa kimya nyumbani kwako kwakuwa ukibainika unanashawishi watu wasichanje usijutie mdomo wako",alisema Steve.

Aidha amewahimiza vijana ambao ndio taifa la kesho kuwekeza nguvu zao katika kulisaidia Taifa kukua kiuchumi na sio kujiingiza kwenye makundi ya mitandao jamii inayolenga kuchafua serikali na kurudisha nyuma jitihada za Rais Samia ambaye amejielekeza katika kujenga uchumi na kusaida jamii kujikwamua katika lindi la umasikini.

Kwa upande wake Asha Baraka ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kujali wananchi wake Kwa kuwaletea  chanjo na kuigawa bure kwa kila mmoja ili kusaidia hata wasio na uwezo wapate chanjo

Aidha Wazalendo kwanza wanasisitiza kuwa ugonjwa wa UVIKO -19 upo na unaua hivyo bi muhimu wananchi waliopo kwenye kundi la umri waliopewa kipaumbele kujitokeza na kuchanjwa kwa hiyari zao ili kunusuru maisha yao dhidi ya ugonjwa huo.

Source

Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri Afariki Dunia


Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri amefariki dunia leo Ijumaa Agosti 13 alfajiri, akiwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia hiyo, Mzee Abri atazikwa leo baada ya Swala ya adhuhuri katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

"Hakutakuwa na mikusanyiko kwa tutakaokuwa Iringa, tafadhali tutumie zaidi teknolojia za habari kutoa pole na shughuli nyingine," imeeleza taarifa hiyo.



Source

ULEGA ATAKA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUKOMESHWA NCHINI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga (hawapo pichani) mara baada ya kufika katika wilaya hiypo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Mkoani Tanga. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga na kutoa maagizo ya kukomeshwa kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji kote nchini, mara baada ya kufika katika wilaya hiyo kwa ziara ya kikazi ya siku moja.  (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi).


Na. Edward Kondela

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewataka viongozi wa maeneo mbalimbali nchini kuanzia ngazi ya kijiji kuhakikisha wanasimamia haki na amani na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji.

 

Naibu Waziri Ulega amebainisha hayo (12.08.2021) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga na kuibainisha hayoa kwenye kikao chake na uongozi wa wilaya hiyo na kuwataka pia wataalam wa sekta ya mifugo washirikiane vyema na viongozi katika kutoa pia elimu juu ya umuhimu wa makundi hayo mawili ya wakulima na wafugaji.

 

Mhe. Ulega amesema wafugaji lazima waishi kwa upendo maeneo walipo pamoja na wafugaji wengine na wakulima kwa kuwa ni dhambi kubwa kuchukua mifugo na kuingiza kwa makusudi kwenye shamba la mkulima.

 

"Kitendo cha ng'ombe kupelekwa kwenye mashamba ni jinai kama jinai nyingine siyo haki kwa mkulima au mfugaji kuchukua hatua kinyume na taratibu na viongozi wa kijiji wawe wasimamizi wa haki na amani na wasifanye upendeleo pamoja na kufanya vitendo vyovyote vya rushwa." amesema Mhe. Ulega

 

Naibu Waziri Ulega amelazimika kutoa maelekezo hayo baada ya kupokea taarifa ya uongozi wa Wilaya ya Handeni kuwa kumejitokeza migogoro baina ya wakulima na wafugaji hadi kusababisha vifo vya baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo hali ambayo imekuwa ikisababisha hofu ya mahusiano baina ya makundi hayo mawili.

 

Katika taarifa hiyo wameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inaweka mikakati mbalimbali ya kukomesha migogoro hiyo ambayo imekuwa ikisababisha hofu, ukizingatia Wilaya ya Handeni ina mifugo mingi na imekuwa ikifanya biashara ya kupeleka mifugo ndani na nje ya nchi.

Chama kujiunga na Klabu ya RS Berkane ya Morocco


CLATOUS Chama kiungo namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho anatajwa kujiunga na Klabu ya RS Berkane ya Morocco kwa dili la miaka mitatu.


Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge ambaye alikuwa anafundisha AS Vita anatambua vema uwezo wa Chama kwa kuwa alikutana naye kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 nyota huyo alitengeneza jumla ya pasi 15 na alifunga mabao nane akiwa ni namba moja kwa utengenezaji wa pasi ndani ya ligi.

Taarifa zimeeleza kiungo huyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao wa 2021/22.

Mbali na Chama pia nyota wao Luis Miquissone yupo kwenye hesabu za mwisho kutua nchini Misri kwa ajili ya kujiunga na Klabu ya Al Ahly ya Misri.

Tayari jezi namba 11 ambayo aliyokuwa anavaa Luis amekabidhiwa kiungo mpya Peter Banda ambaye anatajwa kuwa mbadala wa nyota huyo.

Simba imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22 ambapo Luis hakuwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kipo kambini.

 

Serikali ya Canada kuanzisha kutoa hati ya chanjo kwa ajili ya safari za kimataifa

 Waziri wa Uraia na Uhamiaji wa Canada Marco Mendicino, alitangaza kuwa wale ambao wamechomwa dozi mbili za chanjo dhidi ya corona (Kovid-19) watapewa hati ya chanjo itakayotumika katika safari za kimataifa.

Mendicino, ambaye hakutoa tarehe halisi, alisema kuwa mpango huo utatekelezwa katika siku za kwanza za msimu wa vuli.

Akielezea kuwa serikali yake inafanya kazi na nchi zingine kutambua hati za chanjo, Mendicino alisema kuwa watu wa Canada waliopata chanjo kikamilifu wataweza kupata hati ya serikali ambayo itathibitisha historia yao ya chanjo ya Kovid-19 kwa sababu za kusafiri kimataifa.

Mendicino pia alisisitiza kuwa hati ya chanjo itakayotolewa itajumuisha data juu ya aina, tarehe na mahali pa chanjo zilizotolewa, na kubainisha kuwa utumiaji wa hati iliyoandaliwa kwa safari za kimataifa baina ya nchi imeachwa kwa uamuzi wa serikali za majimbo.

Mfumo wa hati ya chanjo, ambao unaendelea kutumika Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Denmark, Ujerumani, Ugiriki, Croatia na Poland, pia ulianzishwa huko Japan mnamo Julai.

Wale wanaotumia programu ya ArriveCAN, ambayo Canada ilizindua mnamo Julai, wameondolewa ulazima wa kukaa karantini wanapoingia nchini ikiwa watathibitisha maelezo yao na kujaza data zinazohitajika kwenye programu.

MAGAZETI TA LEO 13.8.2021














 

Thursday, August 12, 2021

Manara avuruga mashabiki Unguja



BAADHI ya mashabiki wa mpira wa miguu Unguja wamesema msimu wa 2021-2022 wa Ligi Kuu Bara hautakuwa na msisimko mkubwa kutokana na kung'atuka kwa aliyekuwa msemaji wa Simba,Haji Manara.

Haji Bakari Haji, shabiki wa Yanga alisema: "Japo Manara alikuwa akitukera na baadhi ya kauli zake, lakini alikuwa anachangamsha sana ligi hususan zikikutana timu mbili Simba na Yanga,"

"Zile kauli za Manara zilikuwa zinawafanya wachezaji wetu wapambane kweli, lakini sasa hivi hayupo sijui msimu unaokuja itakuwaje, ila tutammisi,"

Ali Juma na Haji Issa ambao ni mashabiki wa Simba walisema walikuwa wakivutiwa na kauli za Manara hususan akiwa anawatania watani zao, Yanga.


 
"Hakuna binadamu ambaye hana upungufu hata Manara anayo yake, lakini kwenye usemaji aliitendea haki Simba hata ukisikiliza vipindi vya redio vya michezo siku ambayo kuna sauti yake vinanoga kweli, lakini hatuwezi kupinga kilichotokea," alisema Ali.

WAZIRI UMMY AZINDUA MPANGO MKAKATI WA PILI MIAKA MITANO WA TARURA JIJINI DODOMA


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy Mwalimu,akizungumza wakati wa uzindua Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma
Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),David Silinde ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Prof.Riziki Shemdoe ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma
Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki pamoja na viongozi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy Mwalimu,(hayupo pichani) wakati wa uzindua Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy Mwalimu,akizindua rasmi Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma

…………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy Mwalimu, amezindua Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) wenye thamani ya Sh.Trilioni 3.6.

Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma Waziri Ummy amesema kuwa Mpango huo unaanza mwaka huu 2021/22 hadi 2025/26.

Mhe.Ummy ameeleza kuwa mpango huo utaongeza mtandao wa barabara kutoka kilometa 2,404.90 hadi 3,855.65, changarawe kutoka kilometa 29,116.57 hadi 102,358.14 na madaraja kutoka 2,812 hadi 6,620 na fedha zitakazotumika ni Sh.Trilioni 3.6.

"Mpango huu kwa miaka mitano unahitaji Sh.Trilioni 3.6 sidhani kabisa Rais Samia kama atashindwa kwa kuwa anauwezo wa kuzitafuta ndani ya miaka mitatu, twendeni tukaoneshe kazi yenye ubora na ufanisi,"amesema.

Waziri Ummy amesema serikali itaupatia Wakala huo magari 122 na mchakato wa kuomba ajira za Wahandisi unaendelea na wataajiri Maofisa manunuzi kwa ajili na kutoa ajira za muda.

Aidha Ummy, amesema kuwa kwenye miji hiyo zitajengwa kilometa tano za barabara ya lami huku akisema kuna andiko litaandaliwa kwa ajili ya miji ambayo haitapata.

Hata hivyo Ummy ametoa angalizo kwa Wakala huo kuhakikisha kazi za ujenzi wa barabara zifanyike kwa ufanisi kwa kuwa ni kipimo chao kwa watanzania.

"Tunataka tuone tija katika suala zima la ukarabati wa barabara mijini na vijijini, ndugu zangu mnakazi kubwa mwaka huu mmoja ndio mwaka wa kuwapima je, kile kisingizio cha kuwa hamna fedha kilikuwa kisingizio au hamna uwezo na ubunifu na utashi wa kazi mnazotakiwa kuzifanya,"amesema.

Amesema matarajio ya serikali kwa Tarura ni makubwa sana hivyo wasiiangushe na waoneshe kuwa ni taasisi sahihi ya kufungua barabara za mijini na vijijini.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, David Silinde, amesema TARURA katika historia ya nchi kwa mara ya kwanza imetengewa fedha nyingi.

"Nipongeze Bunge kupitia kwa Spika wetu Job Ndugai kwa kupitisha kiwango cha fedha, ambacho Tarura itaweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, malengo na mikakati tuliyojadili hapa itatekelezwa kama ilivyokusudiwa,"amesema.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe, amesema mkutano huo wa siku wa tatu mbali na kuzindua kauli mbiu, watapitia utekelezaji wa Mkakati wa kwanza wa miaka minne na kupitia Mkakati wa Pili wa mwaka 2021/22 hadi mwaka 2024/25.

Awali Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff ,amesema katika utekelezaji wa Mpango Mkakati kuanzia mwaka 2017 hadi Juni mwaka 2021, jumla ya Sh. trilioni 1.3 zimetumika kutengeneza kilomita 24,979.24, ambapo kilomita 955.35 zimetengwa kwa kiwango cha lami, kilomita 16,857.82 za kiwango cha changarawe.

"Madaraja 231 yamejengwa hivyo kuwa na ongezeko la madaraja kutoka madaraja 2,960 hadi kufikia madaraja 3,191 na makaravati 1,325 yamejengwa hivyo kufikia makaravati 69,317 kutoka makaravati 67,992 ya awali"amesema Mhandisi Seff

Mafuriko yasababisha vifo vya watu 52 Niger

 Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Niger iliongezeka hadi 52.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani, ilielezwa kuwa watu 50,305 waliathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kutoka Juni hadi Agosti 11.

Katika taarifa hiyo, iliripotiwa kuwa nyumba  5,694 ziliharibiwa, watu 52 walipoteza maisha na watu 34 walijeruhiwa katika janga la mafuriko.

Wakati mji mkuu wa Niamey ulikuwa moja ya miji iliyoathiriwa zaidi na mafuriko, ilisisitizwa kuwa kipimo cha 70 hadi 140 cha mvua kwa kila mita ya mraba zilinyesha katika sehemu nyingine za jiji wakati wa usiku wa kuamkia Jumanne hadi Jumatano.

Wakati wa msimu wa mvua, ambao huanza Juni hadi Septemba huko Niger, mafuriko hutokea mara kwa mara.

Katika kipindi kama hicho cha mwaka jana, watu 350,000 waliathiriwa na mafuriko na watu 73 walipoteza maisha.

Nicole "Ningekuwa Najiuza Ningekuwa Tajiri Sana NATUMIA Dola 800 Kwa Siku"



Mrembo mwenye shape yake hapa Africa @nicolejoyberry kupitia interview aliyoifanya na channel ya Millardayo amewatolea povu wale watu wanaodhani yeye anajiuza:

"Wanaotaka kuninunua sidhani kama wanapesa za kunilipa so far....i think hata hapa unanifanyia interview you can see its not more money...I spend over 800 Dollars a day inamaanisha kama najiuza nilipwe that means they have to pay me....kiukweli ningekua najiuza ningekua tajiri sana" - Alisema Nicole


Ole Sabaya na wenzake wawili wakutwa na kesi ya kujibu


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili Sylevester Nyegu, Daniel Mbura, hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea kesho Ijumaa Agosti 13, 2021.


Sabaya na wenzake wawili wanatuhumiwa kutenda makosa matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha.



Kiongozi wa mbio za mwenge awafunda vijana wa Kibaha kuchangamkia fursa

 


Na Victor Masangu, Kibaha. 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amewataka vijana kubadilika kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali mbali mbali ikiwemo kilimo ili kuweza kujikwamua kiuchumi. 

Kauli hiyo ameitoa wakati alipokwenda kutembelea na kukagua shamba la mikorosho samba na kupanda miti.  

Aliongeza kuwa kwa Sasa sekta ya kilimo inasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwasaidia vijana kuondokana na umasikini kupitia fursa mbali mbali za ajira. 

 Aidha alifafanua kwamba endapo vijana wakajikita zaidi katika kujishugulisha na kilimo Cha mikorosho kutaweza kuwaongezea zaidi kujiongezea kipato. 

Mbali na kutembelea mradi huo wa kilimo Cha mikorosho alikwenda kutembelea katika kituo Cha afya mlandizi na kunionea jinsi ya mfumo wa Tehama unavyofanya kazi na kuwaagiza watendaji kuhakikisha wanasimia vizuri ukusanyaji wa mapato.

Kadhalika akielezea juu ya mapambano dhidi ya marelia alisema kuwa ni vema wataalamu wa afya wakaweka mipango madhubuti ambayo itasaidia kupungua kasi ya maambukizi hayo.


Awali mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ambaye aliupokea mwenge huo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alibainisha kuwa miradi 13 itatembelewa.  

Pia alisema kuwa miradi yote hiyo imegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 2  ambayo itakuwa katika sekta mbali mbali.


Raia wa Zambia wanapiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali

 Mamilioni ya raia wa Zambia wanapiga kura leo, Alhamisi katika uchaguzi mkuu wa rais huku hali ya kiuchumi ikiwa imezorota.

Polisi na wanajeshi wanafanya doria nchi nzima katika vituo vya kupigia kura na idadi kubwa ya waangalizi wa kimataifa watakuwa wakifuatilia mchakato huo.

Rais Edgar Lungu anawania kutawala kwa muhula wa pili huku akikabiliana na ushindani mkubwa kutoka kutoka kwa Hakainde Hichilema, mgombea wa chama kikuu ya upinzani nchini humo.

Huku wapiga kura wengi wakiwa wanataka hali ya uchumi kuboreshwa na fursa za ajira kupatikana. Tume ya uchaguzi nchini Zambia imehaidi uchaguzi wa uwazi na haki.


Source

Umoja Wa Afrika Kuipatia Tanzania Chanjo Milioni 17 Za Corona




Umoja wa Afrika umeitengea Tanzania dozi milioni 17 za chanjo za UVIKO- 19 kupitia mpango wa Umoja huo wa kuzisaidia Nchi wanachama kupata chanjo kwa ajili ya Wananchi wake.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo Addis Ababa Nchini Ethiopia alipokutana kwa mazungumzo na Jumuiya ya Watanzania waishio Nchini Ethiopia (Diaspora) waliotaka kufahamu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na UVIKO -19 ikiwa ni pamoja na suala la chanjo.

Aidha Balozi Mulamula amewataka Watanzania wanaofanya kazi katika Mashirika na Taasisi mbalimbali za Kimataifa kusaidia upatikanaji dozi nyingine za chanjo ya UVIKO 19 ili kuwawezesha Watanzania wengi  kupata chanjo hiyo kutokana na  mwamko wa Watanzania kuongezeka mara  baada ya kuzinduliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ethiopia Mhe Sahle – Work Zewde Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo Tanzania na Ethiopia zimekubalina kuendelea kutumia ndege za shirika la Ethiopia kutangaza vivutio na kusafirisha Watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja Tanzania.

Aidha Balozi Mulamula amemhakikishia Rais Sahle – Work Zewde kuwa Tanzania itaendelea kutekeleza maeneo yote ya ushirikiano ambayo Rais Zewde alikubaliana na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ziara ya Rais huyo Chato nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na suala la kuwarejesha Nchini Ethiopia wahamiaji wanaoshikiliwa katika magereza mbalimbali.

Kwa upande wake Rais wa Ethiopia  Mhe. Sahle – Work Zewde amesisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Nchi hiyo hususani katika kutatua changamoto zinazozuia maendeleo miongoni mwa Mataifa hayo.

Baba Levo Amuonya Rayvanny Kuhusu kuoa "Usiwe Kama Umechanganyikiwa"



Msanii Baba Levo amemkatalia Rayvanny kuoa haraka kama mtu aliyechanganyikwa baada ya Rayvanny kuweka hisia zake za kufanikisha jambo hilo siku za hivi karibuni.

Kupitia Insta Story ya Rayvanny amezua gumzo baada ya kuandika kwamba hawezi kusubiri kuhusu suala la ndoa yake "I can't wait for my wedding"

Muda mfupi uliopita Baba Levo akamjibu kwenye ukurasa wake Instagram baada ya kupost picha ya Rayvanny kisha kuandika maneno yafuatayo.

"Dogo hapana kuoa haraka haraka kama mtu aliyechanganyikiwa, unakimbilia wapi tulia kwanza mdogo wangu".

Kwa sasa Rayvanny yupo kwenye mahusiano na Paulah ambaye ni mtoto wa staa wa filamu Kajala Masanja.

Nimemkuta Mume Wangu Akifanya Ngono na House Girl wa Jirani Yetu

Juzi nilikuwa naenda kazini nikamuacha mume wangu
nyumbani anaangalia TV, gari langu likazima ghafla kiasi cha
kilomita moja toka nyumbani.

Nikaona nitembee mpaka nyumbani kumwomba mume wangu aje anisaidie kutengezagari, kwa mshangao wangu nilipofika nyumbani nikamkuta mume wangu yuko chumbani na msichana wa kazi wa nyumba ya jirani. Mume wangu ana miaka 43, mimi nina miaka 39 na msichana huyo ana miaka 19 hivi.Tumekuwa katika ndoa kwa miaka 10. Nilipomuuliza mume wangu alikubali kuwa uhusiano wao umekuwa ukiendelea kwa miezi sita sasa, nifanye nini mimi?

NISHAURINI NIFANYAJE NDUGU ZANGU...
SHARE HII TAFADHALI

Wednesday, August 11, 2021

Fisi agongwa na gari barabara kuu ya Babati-Singida






Na John Walter -Babati. 

Baadhi ya Wananchi katika Kata ya Ayalagaya (Dareda) katika wilaya ya Babati mkoani Manyara wameshuhudia mnyama fisi akiwa amekufa barabarani  baada ya kugongwa na gari.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wanapita katika eneo hilo wamedai kuwa fisi huyo amegongwa na gari usiku wa kuamkia leo agosti 11 mwaka huu japo hawajui ni gari gani.

Mwananchi mmoja mkazi wa Gajal ambae hakutaja jina lake amesema eneo hilo lina fisi wengi ambao hudhuru watu na mifugo haswa nyakati za usiku.

Taarifa iliyotolewa mwaka 2020 na mtafiti wa Simba wa Ikolojia ya Manyara-Tarangire Dr Bernard Kissui alisema kila siku mnyama mmoja anagongwa na gari ambapo katika uchambuzi wao walibaini aina tofauti 50 hugongwa na magari wengi wakiwa ni wanyama wanaozaa (Mamalia) na wanaotaga mayai.

Dr Kissui alisema katika mwaka huo Wanyamapori 380 walikufa kwa kugongwa na magari katika mapito ya wanyama, yanayopitiwa na barabara kuu ya Arusha-Babati.

Mara nyingi katika bara bara ya Babati-Singida wanyama wanaonekana kufa kwa kugongwa ni Mbwa,na huwa ni  nadra sana fisi kuonekana barabarani wakiwa wamegongwa ukizingatia kuwa bara bara hiyo haina hifadhi ya wanyamapori.

 


Source

Balozi Agnes Kayola aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya Makatibu Wakuu wa SADC

Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu ni miongoni mwa vikao vya awali kuelekea Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 17 hadi 18 Agosti 2021 jijini Lilongwe, Malawi.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu unaongozwa na Mratibu Mkuu wa Kitaifa wa masuala ya SADC, Balozi Agnes Kayola ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine.

Viongozi wengine walioambatana na  Balozi Kayola kwenye mkutano huo ni pamoja na: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban ambaye ameongoza Kikao cha Kamati ya Fedha katika kikao hicho cha Makatibu Wakuu; na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa.

Aidha, mkutano huu utafuatiwa na mikutano mingine ya awali ikiwamo Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utafanyika tarehe 13 hadi 14 Agosti, 2021 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2021 ambao utajadili hali ya ulinzi na usalama katika kanda kwa kipindi cha Agosti 2020 hadi Agosti 2021. Mkutano huu utahusisha nchi tatu (3) za SADC Organ Troika ambazo wajumbe wake ni Botswana, Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Afrika Kusini, Mwenyekiti ajaye wa Organ; na Zimbabwe, Mjumbe aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ambaye ataambatana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwakilishi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mikutano hii ya awali pamoja na mambo mengine inajukumu la kuandaa, kupitia na kuwasilisha mapendekezo ya masuala mbalimbali ya kikanda yatakayofanyiwa maamuzi kwenye Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 17-18 Agosti 2021 jijini Lilongwe.

Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu ulianza tarehe 9 Agosti 2021 na unatarajiwa kumalizika leo tarehe 11 Agosti 2021. Kumalizika kwa mkutano huu kunaruhusu kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

 

Majibu ya Gigy Money Kuhusu Kurudiana na Mo Jay






MSANII Gigy Money amejibu madai ya taarifa za kurudiana na mzazi mwenzie Mo Jay baada ya kuonekana wakiwa pamoja na mtoto wao Mayra.

 

Gigy Money amekanusha hilo kwenye 'Insta Story' yake kwa kueleza hajarudiana na mtu hivyo watu wasidanganywe na trending za story hizo mitandaoni, kilichotokea ni Mayra alikuwa anaumwa na baba yake kaenda kumuona.

 

"Sijarudiana na mtu jamani, naona natrend huko wanawadanganya tu, Mayra anaumwa na baba yake kaja kumuona nimependa jinsi wamecoperate kwa hiyo sioni kama ni kosa, mniache". comment ya Gigy Money

CCM yaijia juu gazeti la Uhuru


Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa na upotoshwaji mkubwa uliyofanywa na gazeti la Uhuru toleo Namba 24084 la leo Jumatano 11 Agosti, 2021, gazeti hili limepotosha sehemu ya mahojiano aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan na BBC.

Katika habari yake kuu limeandika kichwa cha habari "Sina wazo kuwania urais 2025- Samia" Huu ni upotoshwaji mkubwa na kumlisha maneno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan hakusema kabisa maneno hayo, hili ni kosa kubwa linalokwenda kinyume na sera inayoongoza vyombo hivyo, jambo ambalo halitavumiliwa hata kidogo hivyo HATUA KALI za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika katika uandaaji wake.

Gazeti la Uhuru ndiyo "Adam na Hawa" wa magazeti yote hapa nchini, linawajibika kuonesha weledi wa hali ya juu na sio vinginevyo.

Tunawaomba Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na watanzania kwa ujumla kupuuza habari hiyo kwani imeandikwa na watu wenye maslahi yao binafsi.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan fikra na nguvu zake kwa sasa zimejikita katika kuwatumikia watanzania na si vinginevyo" Shaka Hamdu Shaka

Watu 24 wa familia moja wafariki dunia kwa kula sumu waliodhani ni chumvi





 
Watu 24 wa familia moja wamefariki baada ya kula chakula kinachoshukiwa kuwa na sumu kaskazini magharibi mwa Nigeria. Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Danzanke - katika jimbo la Sokoto.

Kamishna wa Afya wa jimbo Ali Inname aliwaambia waandishi wa habari kwamba familia hiyo ilitumia kimakosa kemikali ya mbolea ambayo ilionekana kama chumvi wakati wa kuandaa chakula siku ya Jumatatu. Alisema wafanyakazi wa afya walijaribu kuokoa maisha ya wahanga bila mafanikio.

Hata hivyo watu wawili wa familia ambao walionja tu chakula hicho sasa wanapata matibabu hospitalini. Kufuatia tukio hilo, maafisa wameshauri tena watu kuweka vitu vyenye sumu mbali na maghala yao ya chakula kwa sababu za usalama.

Matukio kama hayo yanayohusu familia kufa kwa kula sumu yametokea huko Nigeria lakini idadi ya waliokufa katika tukio hili la hivi karibuni ni kubwa sana.


Serikali Yazindua Mpango Wa Kukopesha Wananchi Katika Urasimishaji


 Na. Hassan Mabuye, Mbeya
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amezindua mpango wa kitaifa wa kuwakopesha wananchi fedha za kufanya urasimishaji wa maeneo yao kwa kipindi cha miaka miwili.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo katika kata ya Igawa wilayani Mbarali mkoa wa Mbeya wakati akizindua Mpango wa maalumu wa kukopesha wananchi gharama ya kupanga, kupima na kupewa hati kwa kushirikiana na Benki ya NMB.

Lukuvi amesema mpango huu ni wa nchi nzima ambao umeanzia hapa Mbarali kwa kuwamilikisha wananchi zaidi ya 52,000 kwa kuwa mazoezi mengi ya urasimishaji yameshindwa kufanikiwa kwa sababu baadhi ya wananchi wameshindwa kupata fedha kwa mkupuo kugharimia shilingi 150,000 za upimaji na umilikishaji.

"nimeamua kuanzisha mpango huu kwa kushirikiana na NMB ambao watawakopesha fedha za kupanga, kupima na kuandaa hati ambazo Benki italipa 100% kwa mkupuo kisha nyinyi mtalipa taratibu na kwa awamu kwa muda wa miezi 24 yaani miaka miwili" Amesema Waziri Lukuvi.

"baadhi ya wananchi wamekwamisha kazi hii ya urasimishaji katika maeneo mengi kwa kuwa wachache ndio wameweza kupata fedha za kugharimia upangaji, upimaji na umilikishaji kwa wakati. Sasa NMB leo hapa Mbarali wamekuja kuwakopesha wananchi gharama zote. Na ninataka zoezi kama hili lifanyike nchi nzima na wengine waige kwa kuafuata utaratibu huu" Ameongeza Waziri Lukuvi.

Amesema pia 90% ya wananchi wa Mbarali walikuwa hawakopesheki kwa sababu ya ardhi yao ilikuwa haijapangwa wala kupimwa. Lakini kwa mpango huu pia watakuwa na haki ya kukopeshwa na benki yoyote hapa nchini kwa kuwa watakuwa na dhamana inayotambulika kisheria ambayo ni hatimiliki ya ardhi.

Naye Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB Bwana Benedicto Baragomwa amewataka wananchi kuchangamkia fursa hii kufanya urasimishaji kupitia Benki ya NMB ambayo itafanya zoezi hili kwa kutumia matawi yake yote 226 nchi nzima  kujipatia mkopo huu na kujiwezesha kiuchumi.

Kwa upande Mwingine Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Mary Makondo amewahakikishia wananchi kwamba Wizara yake itasimamia kikamilifu mpango huu ambao wananchi watapewa hatimiliki za ardhi za miaka 99 na watamilikishwa kisheria.


Moses Iyobo Atoa Siri "Sikuwa na Mpenda Aunty Ezekiel Nilimtamani tu Nikapita nae"



Dancer Wa Diamond Platnumz (@moseiyobo ) Amefunguka kuwa Hakuwahi kumpenda Mama Wa Mtoto wake Ambaye Ni Aunty Ezekiel Ila Alimtamani Tuuu.

"Ukweli sikuwahi Kumpenda Yule mdada Ila Nilikuwa Namtamani Tuuu nikimtazama kwenye Movie Nikaamua Tuuu Nimtongoze Na Yeye Akajaa Basi na Mimi nikapitanae"-Ameongea
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...