Wednesday, August 11, 2021

Fisi agongwa na gari barabara kuu ya Babati-Singida






Na John Walter -Babati. 

Baadhi ya Wananchi katika Kata ya Ayalagaya (Dareda) katika wilaya ya Babati mkoani Manyara wameshuhudia mnyama fisi akiwa amekufa barabarani  baada ya kugongwa na gari.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wanapita katika eneo hilo wamedai kuwa fisi huyo amegongwa na gari usiku wa kuamkia leo agosti 11 mwaka huu japo hawajui ni gari gani.

Mwananchi mmoja mkazi wa Gajal ambae hakutaja jina lake amesema eneo hilo lina fisi wengi ambao hudhuru watu na mifugo haswa nyakati za usiku.

Taarifa iliyotolewa mwaka 2020 na mtafiti wa Simba wa Ikolojia ya Manyara-Tarangire Dr Bernard Kissui alisema kila siku mnyama mmoja anagongwa na gari ambapo katika uchambuzi wao walibaini aina tofauti 50 hugongwa na magari wengi wakiwa ni wanyama wanaozaa (Mamalia) na wanaotaga mayai.

Dr Kissui alisema katika mwaka huo Wanyamapori 380 walikufa kwa kugongwa na magari katika mapito ya wanyama, yanayopitiwa na barabara kuu ya Arusha-Babati.

Mara nyingi katika bara bara ya Babati-Singida wanyama wanaonekana kufa kwa kugongwa ni Mbwa,na huwa ni  nadra sana fisi kuonekana barabarani wakiwa wamegongwa ukizingatia kuwa bara bara hiyo haina hifadhi ya wanyamapori.

 


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...