Thursday, August 12, 2021

Kiongozi wa mbio za mwenge awafunda vijana wa Kibaha kuchangamkia fursa

 


Na Victor Masangu, Kibaha. 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amewataka vijana kubadilika kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali mbali mbali ikiwemo kilimo ili kuweza kujikwamua kiuchumi. 

Kauli hiyo ameitoa wakati alipokwenda kutembelea na kukagua shamba la mikorosho samba na kupanda miti.  

Aliongeza kuwa kwa Sasa sekta ya kilimo inasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwasaidia vijana kuondokana na umasikini kupitia fursa mbali mbali za ajira. 

 Aidha alifafanua kwamba endapo vijana wakajikita zaidi katika kujishugulisha na kilimo Cha mikorosho kutaweza kuwaongezea zaidi kujiongezea kipato. 

Mbali na kutembelea mradi huo wa kilimo Cha mikorosho alikwenda kutembelea katika kituo Cha afya mlandizi na kunionea jinsi ya mfumo wa Tehama unavyofanya kazi na kuwaagiza watendaji kuhakikisha wanasimia vizuri ukusanyaji wa mapato.

Kadhalika akielezea juu ya mapambano dhidi ya marelia alisema kuwa ni vema wataalamu wa afya wakaweka mipango madhubuti ambayo itasaidia kupungua kasi ya maambukizi hayo.


Awali mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ambaye aliupokea mwenge huo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alibainisha kuwa miradi 13 itatembelewa.  

Pia alisema kuwa miradi yote hiyo imegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 2  ambayo itakuwa katika sekta mbali mbali.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...