Friday, January 29, 2021

Museveni akataa maridhiano na wapinzani

 


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaonya watu wenye lengo la kumpatanisha na wapinzani baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliompa ushindi na kuongoza muhula wa sita.


Upande wa upinzani unaoongozwa na msanii Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine aliyeshika nafasi ya pili, unapinga vikali kuyatambua matokeo hayo.


Kauli hiyo ya Museveni imekuja baada ya kuibuka wasiwasi kwa Taifa na baadhi ya viongozi wa dini kuomba maridhiano kwa Serikali na upinzani na kumuachia Bobi Wine aliyekuwa amezuiliwa nyumbani kwake.


Rais Museveni aliwajibu akisema Serikali ya NRM tayari ilianza maridhiano miaka mingi iliyopita ndiyo sababu katika Serikali yake kuna mtoto wa aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin, mtoto wa Rais wa zamani, Tito Lutwa Okello na wengine wengi.


Kiongozi wa chama cha NUP, Bobi Wine alipokutana na wabunge wake wateule kwa mara ya kwanza, aliwataka wapinge matokeo ya uchaguzi mkuu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...