Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza wakati
wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kushoto aliyekaa ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada
Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxoakizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada akieleza jambo wakati wa halfa hiyo
Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamunguakizungumza wakati wa halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo mara baada ya makabidhiano hayo kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwasha moja ya magari hayo
WAFUGAJI  nchini wametakiwa kubadilika na kuachana na  ufugaji wa mazoea bali wafuge kisasa kwa ajili ya kupata mazao mengi  lakini yenye ubora ambayo yataweza kuuzika kwa faida na hivyo kuongeza  mchango wa pato la Taifa.
Ushauri  huo umetolewa na Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba  Ndaki wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka  shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa  Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo  Jijini Tanga.
Alisema  kuwa licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi lakini sekta hiyo mchango  wake kwenye pato la taifa ni asilimia 7.9% pekee  kutokana na ufugaji wa  kimazoea  ambao hautoi matokeo bora.
Akizungumzia  uzalishaji wa maziwa nchini Waziri Ndaki alisema ni lita Bil 3.01 huku  kati ya hizo lita Mil 2.1 zinatokana na ng'ombe wa asili Mil 31 huku  ng'ombe wa kisasa Mil 2 wanatoa lita bil 0.9. 
"Kutokana  na uzalishaji mdogo wa maziwa hata kiwango cha unywaji wa maziwa kwa  mwananchi mmoja mmoja kimekuwa kidogo kwani kwa mujibu wa takwimu ni  lita 54 kwa mwaka sawa na kijiko kimoja kwa siku" alisema Waziri Ndaki.
Nae  Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu alisema kuwa uwepo wa mradi  umesaidia kuongeza kasi ys uanzishwaji wa viwanda vya maziwa hadi  kufikia vitano ambavyo vinazalisha maziwa kwa kutumia teknolojia ya UHT.
Alisema  kuwa bado kumekuwepo na changamoto katika eneo la ukusanyaji wa maziwa  kwani kuna kiasi kikubwa yanakuwa hana kosa ubora kabla ya kufika soko  hivyo kuwa hasara kwa mfugaji.
Kwa  upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji na masoko kutoka  wizara ya mifugo na uvuvi Steven  Maiko alisema kuwa kutokana na  tathimini waliyoifanya 2016/17 inaonyesha kuwa ifikapo mwala 2030/31  sekts hiyo itakabiliwa na upungufu mkubwa raslimali zake za nyama na  maziwa kutokana na ongezeko la idadi ya watu.
Hivyo  kutokana na changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na wahisani  waliamua kuja na mradi huo ili  kuongezs uzalishaji, kudhibiti magonjwa  ya mifugo lakini.na kuongeza mnyororo wa thamani wa maziwa ikiwemo kuweka mazingira safi ya kufanyabiashara.
Nae   Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la  Helfer Mark Tsoxo alisema kuwa lengo la mradi wa TMPP kuongeza kipato  kwa wafugaji wapatao 50, 000 nchi nzima na kwa kipindi cha miezi mitatu  pekee tayari wameweza kuwafikia wafugaji 45, 000 kwa kuwapa mafunzo ya  ufugaji wa kisasa ili waweze kupata mazao bora na ambayo yataweza kuuza  kwa urahisi.
Alisema kwa  upande wa wasindikaji waweze kuwawezesha vifaa ili kuhakikisha  wanaboresha ukusanyaji wa maziwa na kudhibiti ubotevu wake ili  kumuhakikishia mfugaji  soko lenye uhakika.
Nae  Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah  Mhada alisema kuwa benki hiyo imewawezesha wafugaji mkopo wa zaidi ya  sh Mil 396 pamoja na mitamba bora.
"Ili  kuongeza kipato kwa wafugaji wadogo tumewawezesha kupata mitamba ya  kisasa na kiwaunganisha ns masoko ili kuongeza thamani na kuchoches  kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini" alisema Mhada.