Friday, January 29, 2021

Picha : THUBUTU AFRICA YATAMBULISHA MRADI WA 'UTU WA MSICHANA' KUJENGA CHOO CHA KISASA SHULE YA WANAFUNZI NA WALIMU WANACHANGIA CHOO KIMOJA

Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga itakayofanywa na fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Thubutu Africa Initiaves (TAI) limetambulisha mradi wa 'Utu wa Msichana' wenye lengo la kujenga choo cha kisasa chenye matundu 8 na sehemu ya kujistiri kwa wanafunzi wa kike katika shule ya Msingi Mwamangunguli 'A' iliyopo katika kijiji cha Mwamagunguli kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Ujenzi huo wa vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa kike ni sehemu ya utatuzi wa changamoto iliyopo katika shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' yenye jumla ya wanafunzi 400 ambapo kati yao wasichana ni 200 ambao wamekuwa wakilazimika kutumia tundu moja la choo na wavulana 200 wakitumia matundu mawili na walimu katika tundu moja ndani ya choo kimoja.

Uzinduzi na utambulisho huo wa mradi wa 'Utu wa Msichana' ambao umeenda sanjari na kuanzisha rasmi ujenzi wa choo cha kisasa umefanyika leo Ijumaa Januari 29,2021 katika shule hiyo.

Akitambulisha mradi wa 'Utu wa Msichana', Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama amesema tayari ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya Mwamagunguli "A" umeanza ambapo tayari shimo la choo limechimbwa, matofali yameshafyatuliwa na shirika hilo limesaini mkataba na Fundi Ujenzi Robert Kayange kwa ajili ya kazi ya ujenzi.

"Mradi huu wa ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' unaotekelezwa na shirika la Thubutu Africa Initiaves, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia Januari ukigharimu shilingi milioni 16.5 ambazo tumefadhiliwa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania",ameeleza Manyama.

"Tulipata kilio cha changamoto ya vyoo katika shule hii ofisini kwetu kupitia kwa Moses Mshagatila aliyesoma katika shule hii akituomba tusaidie ujenzi wa vyoo kwani hali ni mbaya katika shule hii nasi tukaanza kutafuta mdau wa kutushika mkono ndiyo tukampata Balozi wa Marekani nchini akakubali kutusaidia",ameongeza.

Akielezea kuhusu sifa za choo cha kisasa chenye vigae wanachojenga, amesema kitakuwa na matundu 8 ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa kike,chumba maalum cha kujistri watoto kike,choo maalumu kwa watu wenye ulemavu,sehemu ya kunawia mikono,masinki yenye koki na tanki kwa ajili ya maji ya dharura.

Manyama amesema tayari shirika hilo limepeleka matofali 1,500,mifuko 120 ya saruji na litaendelea kupeleka mahitaji mengine kwa ajili ya ujenzi wa choo na kwa upande wa wananchi watashiriki kwa kuongeza nguvu kazi ikiwemo kupeleka maji.

Amefafanua kuwa lengo la shirika lake ni kuhakikisha linaunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha mazingira shuleni.

Manyama ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi ,wanafunzi na walimu kutunza miundo mbinu ya choo hicho cha kisasa ili idumu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa kata ya Kolandoto, Mwakaluba Wilson alilishukuru shirika la Thubutu Afric Initiatives kwa msaada huo wa choo huku akiwaomba wadau wengine kusaidia kutatua changamoto zingine zilizopo katika shule hiyo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mwamagunguli Makoye Shindayi ameahidi kusimamia kikamilifu ujenzi wa choo hicho huku akimpongeza Kijana Moses Mshagatila kwa kutoa kilio cha changamoto ya vyoo kwa shirika la Thubutu Africa Initiatives ambalo bila kusita limejitokeza kusaidia ujenzi huo.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' Adam Mbega amesema kujengwa kwa choo hicho kutapunguza adha ya wanafunzi kutumia muda mrefu kupanga foleni kwenda kujisaidia wakati wa mapumziko lakini pia kuwaondoa katika hatari ya kupata magonjwa kutokana na kutumia choo kimoja kujisaidia.

"Shule hii iliyopata usajili mwaka 1993 ina walimu 7, wanafunzi 400. Tunatumia choo kimoja walimu na wanafunzi kwani tuna choo kimoja chenye matundu manne, mawili wanatumia wavulana 200, tundu moja wanatumia wanafunzi wa kike 200 na tundu moja tunatumia walimu. Kawaida tundu moja la choo linapaswa kutumiwa na wanafunzi 20 wa kike na kwa upande wa wavulana 25 kwa tundu moja",ameeleza Mwalimu Mbega.

Naye aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, Moses Mshagatila aliyeanza kusoma darasa la kwanza mwaka 1999 wakitumia choo cha mabua na mwaka 2000 kikajengwa choo chenye matundu manne kinachotumika sasa, amelishukuru shirika la Thubutu Africa Initiatives kwa kuanzisha ujenzi wa choo cha kisasa katika shule hiyo ambapo ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuona wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki ndiyo maana akaamua kupiga hodi katika shirika hilo ili lisaidie.

Nao wanafunzi wa shule hiyo wameeleza kufurahishwa na ujio wa choo cha kisasa wakibainisha kuwa wakati mwingine wanachelewa kuingia darasani baada ya kipindi cha mapumziko kutokana na foleni kubwa lakini pia afya zao zinakuwa hatarini kutokana na kutumia choo kimoja tu.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama (aliyesimama) akitambulisha Mradi wa 'Utu wa Msichana' leo Januari 29,2021 katika shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Mradi huo una lengo la kujenga choo cha kisasa  katika shule hiyo.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama (aliyesimama) akitambulisha Mradi wa 'Utu wa Msichana' leo Januari 29,2021 katika shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama (aliyesimama) akitambulisha Mradi wa 'Utu wa Msichana' leo Januari 29,2021 katika shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga itakayofanywa na fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto ( wa kwanza kushoto). Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto Mwakaluba Wilson akishuhudia zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi. 
Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwamagunguli, Makoye Shindayi akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga itakayofanywa na fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akimkabidhi Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga fundi ujenzi Robert Kayange (kushoto).
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akimkabidhi Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama (katikati) akiangalia shimo la choo lililochimbwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa choo cha kisasa kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa choo chenye matundu manne kinachotumiwa na walimu na wanafunzi katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni sehemu inayotumiwa na wanafunzi wa kike 200, kushoto ni choo kinachotumiwa na walimu.
Muonekano wa choo chenye matundu manne kinachotumiwa na walimu na wanafunzi katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' na eneo panapojengwa choo kipya cha kisasa na Shirika la Thubutu Africa Initiatives.
Shughuli ya kusafisha eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' ikiendelea.
Shughuli ya kusafisha eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' ikiendelea.
Mchanga ukiwa eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A'.
Shughuli ya kuleta matofali eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' ikiendelea.
Muoenekano wa sehemu ya matofali
Shughuli ya kusoma matofali eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' ikiendelea.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' Adam Mbega akizungumza ambapo amesema kujengwa kwa choo hicho kutapunguza adha ya wanafunzi kutumia muda mrefu kupanga foleni kwenda kujisaidia wakati wa mapumziko lakini pia kuwaondoa katika hatari ya kupata magonjwa kutokana na kutumia choo kimoja kujisaidia.
Afisa Mtendaji wa kata ya Kolandoto, Mwakaluba Wilson akilishukuru shirika la Thubutu Afric Initiatives kwa msaada wa ujenzi wa choo katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' huku akiwaomba wadau wengine kusaidia kutatua changamoto zingine zilizopo katika shule hiyo.
Diwani wa kata ya Kolandoto, Musa Elias akilishukuru shirika la Thubutu Afric Initiatives kwa msaada wa ujenzi wa choo katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A'.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mwamagunguli, Godfrey Majija akizungumza wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti  wa kijiji cha Mwamagunguli Makoye Shindayi akizungumza wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti  wa kijiji cha Mwamagunguli Makoye Shindayi akimpongeza Moses Mshagatila (kulia) kwa kupeleka kilio cha changamoto ya vyoo katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' na kuamua kuanzisha ujenzi wa choo cha kisasa.
Aliyekuwa mwafunzi wa shule ya msingi Mwamagunguli 'A' Moses Mshagatila mkazi wa kijiji cha Mwamagunguli, akizungumza wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya wanafunzi wa kike wakifuatilia matukio wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...