Friday, January 29, 2021

Mkuu wa Usalama bara barani aipongeza TANROADS Manyara kwa kuweka alama Maeneo hatarishi

 Na John Walter Manyara

Kamishna msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Polisi ambaye pia ni Mkuu wa  Usalama bara barani nchini Tanzania Wilbroad Mutafungwa,  amepongeza wakala wa bara bara mkoa wa Manyara (TANRODS) kwa kazi kubwa walioifanya ya kuweka alama zote zinazohitajika katika maeneo hatarishi ya bara bara.


Amesema kuwepo kwa alama hizo kunasaidia kutoa ishara kwa madereva na watembea kwa miguu pindi wawapo bara barani na kupunguza ajali.


Mutafungwa ameyazungumza hayo wakati  akizungumza na kituo hiki  akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla.


"Kama mnavyofahamu bara bara hizi za mkoa wa Manyara zina Mlima, Kona kali na miteremko, tumepita kuona namna ambavyo magari yanatembea na madereva wanavyozingatia sheria za usalama bara barani" alisema Mutafungwa.


"Kusema kweli nichukue nafasi hii kuwapongeza wenzetu wa Tanroads ambao wamefanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba wameweka alama kwenye maeneo yote ambayo ni hatarishi katika bara bara za mkoa huu" alisema Mutafungwa.


Amesema katika ukaguzi wao walifika katika eneo hatarishi lenye kona kali lijulikanalo kama  Logia katika bara bara ya  Babati Singida ambapo wamejionea madereva wakizingatia sheria kwa kufuata alama zilizowekwa na Tanroads.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...