Tuesday, December 4, 2018

CHINA YAPIGA MARUFUKU HARUSI

Mamlaka za China zipo mbioni kudhibiti ongezeko la harusi za kifahari amabazo zimekuwa zikishamiri katika miaka ya karibuni.

Kwamujibu wa maafisa wa serikali, harusi za kisasa si tu ni za gharama kubwa bali zinaenda kinyume na misingi ya kijamaa ya nchi hiyo.

Harusi za Kichina ambazo hufungwa kimila, hauambatana na sherehe ambazo kwa sasa mamlaka zinadai kuwa zimekuwa kubwa mno.

Sasa serikali ya Beijing inajipanga kuja na namna ya kuzifanya ziwe sawa kwa kufanyika kwa sherehe zenye kiasi.

Wachina kama ilivyo kwa raia wa nchi nyengine duniani wamekuwa wakishindana na jirani, marafiki na jamaa katika kuandaa sherehe kubwa na za kupendeza za harusi. Na harusi kubwa tayari zimeshakuwa fasheni nchini humo.

Harusi hizo huambatana na karamu kubwa, nguo za kifahari na safari za ughaibuni kupiga picha za harusi.

Chanzo:Bbc
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...