Saturday, August 31, 2024
KINACHOENDELEA FAINALI LIGI YA DR. SAMIA - KATAMBI CUP
A to Z Mawakili wa Yanga Wakipangua Hoja za Magoma Mahakamani
Akifafanua hoja ya kwanza, wakili Rashid (wa Yanga) amedai kuwa uamuzi ambao kina Magoma wameukatia rufaa ni uamuzi mdogo ambao kwa mujibu kifungu cha 74 (2) cha Sheria ya Mashauri ya Madai (CPC), Sura 33, haukatiwi rufaa.
Huku akirejea uamuzi wa kesi moja iliyowahi kuamuriwa na aliyekuwa Jaji Mkuu, Francis Nyalali, Wakili Rashid kwa kuwa hauamui haki za msingi za wadaawa na wala hauhitimishi shauri la msingi, bali hudumisha hali iliyopo kusubiri uamuzi wa shauri la msingi.
Amedai kuwa haki za msingi za wadaawa ziliamuriwa katka shauri la marejeo ambapo warufani walikuwepo wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo na waliwakilishwa ma nawakili wao.
Kuhusu hoja ya pili, wakili Rashid amefafanua kuwa rufaa hiyo imeshapitwa na wakati kwa kuwa tukio linatokana na uamuzi wanaoukatia rufaa (shauri la maombi ya marejeo) lilishapita, kwani shauri hilo la marejeo tayari lilishatolewa uamuzi, hivyo hakuna kinachoweza kubadilishwa.
Amesema kuwa nafuu za msingi walizoziomba Mahakama ya Kisutu ilisikilizwa mbele ya warufani pamoja na mawakili wao.
Ameongeza kuwa na uamuzi wa shauri la marejeo walilolifungua namba 17939/2024 kati ya Bodi ya Wadhamini wa Yanga dhidi ya Juma Ally na Mwaipopo na Abeid Abeid baada ya kuruhusiwa ulitolewa Agosti 9, 2024 Katika shauwi la maombi namba.
"Mheshimiwa Jaji kwa mujibu wa hoja hizo ni maombi ya mrufaniwa wa kwanza (Bodi ya Wadhamini wa Yanga) kwamba rufaa hii iitupilie mbali kwa gharama", amesema wakili Rashid.
Akijibu hoja hizo, Wakili Mashenene amepinga pingamizi hilo huku akitoa maana ya uamuzi au amri ambazo hazipaswi kukatiwa rufaa (interlocutory orders) kwa kuirejesha mahakama hiyo katika uamuzi wa Mahakama ya Rufani kwenye kesi ya Seif Sharif Hamad dhidi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Amesema kuwa huo ni uamuzi au amri ambayo inahusiana na shauri masuala yanayohusiana na shauri husika lakini haitoi hitimisho la shauri hilo.
Wakili Mashenene pia akirejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika mashauri mbalimbali amesema kuwa mahakama hiyo imeweka vigezo vya kupima kama uamuzi au amri hiyo ndogo, akibainisha kuwa ni pamoja na aina ya nafuu zinazotokana na amri hizo, kama hazihitimishi shauri.
Amesema kuwa katika kumbukumbu za Mahakama ya Kisutu shauri la Yanga la kuongezewa muda lilikuwa ni shauri linalojitegemea na kwamba nafuu zilizoombwa ni pamoja na kuongezewa muda kufungua shauri la marejeo.
Hivyo amedai kuwa uamuzi wa nafuu hizo ulihitimisha kabisa shauri hilo hapakuwa na shauri lingine mahakamani lililouwa linasubiriwa kusikilizwa (kabla ya Yanga kufungua shauri la marejeo)
Kuhusu hoja ya pili amedai kuwa si tu kwamba haina msingi lakini pia haifai kuwa pingamizi la awali kwa sababu, haikidhi matakwa ya kisheria ambayo yanataka hoja hiyo iwe ni ya kisheria na si ya kiushahidi.
Amesisitiza kuwa kwa kuzingatia hoja hizo hoja ya pili haifai kuwa pingamizi la awali kwa kuwa inahitaji Mahakama kuchunguza kama uamuzi huo unaolalamikiwa hauna athari kwa—-na kama ulitokana na shauri la msingi na kwamba hilo linaweza kuamuriwa wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo.
"Hivyo, kwa kuzingatia mawasilisho hayo tunaomba mahakama hii iitupilie mbali hoja zote za pingamizii na kwa gharama", amesema wakili Mashenene.
Lakini wakili Rashid naye amepinga hoja za wakili Mashenene huku akidai kuwa katika baadhi ya hoja ametoa tafsiri isiyo sahihi akirejea muktadha wa uamuzi wa kesi ya Seif Sharif Hamad na SMZ.
Badala yake alifafanua uamuzi wa kesi hiyo akisisitiza kuwa unaakisi hoja zake katika hoaj zinazobishaniwa
Kwa hiyo mahakama inapaswa kuzingatia matokeo ya mwisho ya uamuzi unaokatiwa rufaa Katika kuamua.kama ni Interlocutory, na sisi tunasema ndio.
Friday, August 30, 2024
TCB yathibitisha kuendelea kushirikiana na Serikali kupanua biashara nje ya nchi
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kupanua wigo wa uwekezaji nje ya mipaka ya nchi. Hayo yameelezwa wakati wa kikao kazi cha siku tatu kinachohitimishwa hivi leo jijini Arusha.
Kikao hicho kilichofunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan na kuwakutanisha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma kujadiliana mikakati mbalimbali ya mageuzi ndani ya taasisi za umma na uwekezaji wenye tija.
Kauli mbiu ya kikao kazi hicho "Mikakati ya Taasisi na Mashirika ya Umma Nje ya Tanzania" inagusia namna ambavyo taasisi na mashirika ya umma yanaweza kupanua wigo nje ya soko la ndani.
Kauli mbiu hii ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais katika kikao kazi kama hicho kilichofanyika mwaka jana, kuwataka wakuu wa taasisi za umma kutafuta fursa za kimataifa. Kikao hiki kimetoa fursa nzuri kwa wenyeviti na watendaji wakuu wa taasisi za umma kutathimini maboresho waliyofanya toka kikao kilichopita na kuainisha mikakati mipya ya mipango ijayo.
Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Adam Mihayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB alisema, "Ili kufanikiwa nje ya mipaka ya Tanzania, ni lazima tulitambue soko lengwa kwa kufanya tafiti za kina ili kubaini mianya ya fursa na kutengeneza bidhaa na huduma zetu kadri ya mahitaji ya soko la kimataifa."
Alisisitiza pia umuhimu wa mashirika hayo kuunda ubia wa kimkakati, ushirikiano, na muungano ili kutumia mtandao wao wa ndani na utaalamu. Aliongeza kuwa, "Muundo wetu wa kibiashara unatakiwa uwe wa kibunifu na wenye uwezo wa kubadilika kuendana na mazingira, ili kukabiliana na mahitaji tofauti tofauti ambayo ni muhimu ili kufanikiwa katika soko la kimataifa."
Mihayo aliendelea kufafanua kuhusu umuhimu wa ushirikiano baina ya taasisi za umma. "Ni muhimu kutumia uwezo wa mashirika yetu kufanya kazi tukiungana pamoja kwa kushirikishana takwimu, kupanga mikakati pamoja, na kusadiana katika utoaji wa huduma.
Kwa kufanya hivyo, tutaboresha rasilimali zetu na pia tutawapa wateja wetu huduma bora kulingana na mahitaji yao na kujenga imani yao kwetu." Alibainisha kuwa ushirikiano wa kimkakati katika tafiti na kubadilishana takwimu baina ya taasisi zinazotegemeana zinaweza kuwasaidia kufikia malengo yao na kuzifanya taasisi hizo kufanya vizuri sokoni.
Akielezea utekelezaji uliofanywa na Benki ya TCB, Mihayo aliwaelezea washiriki mafanikio ya hivi karibuni ya benki hiyo ikiwemo uzinduzi nchini Comoro wa huduma za kibenki kwa Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora Banking).
"Hii inaonyesha dhamira yetu ya kutoa huduma za kibenki nje ya mipaka na kuyafikia mahitaji ya
Watanzania wote dunia nzima. Katika dhamira hii, tunatarajia kuwa katika miaka miwili jayo tutaipeleka TCB katika Soko la Hisa (Dar es Salaam Stock Exchange), hivyo kumpa kila Mtanzania fursa ya kumiliki hisa na kuwa sehemu ya mafanikio ya taasisi hii," alisema.
Akihitimisha hotuba yake, Mihayo alitoa wito kwa taasisi na mashirika ya umma kutobweteka na soko la ndani, bali kuiga mfano wa mataifa yaliyofanikiwa kujipenyeza nchini mwetu na kuanzisha biashara zinazostawi. "Wametuonyesha kwamba inawezekana kufanya hivyo, ni wakati wetu sasa kuthubutu na kutumia fursa hii.
Tushirikiane pamoja, tuwe wabunifu, na kupanga mikakati pamoja ili kuhakikisha kwamba taasisi na mashirika ya umma yanajitegemea, yanachangia pato la taifa lakini pia yanakuwa mojawapo kati ya mashirika makubwa duniani."
BENKI YA CRDB YAKABIDHI MADAWATI SHULE YA SEKONDARI MAGANZO
Benki ya CRDB tawi la Maganzo imekabidhi madawati kwenye shule ya sekondari Maganzo yenye thamani ya Shilingi Milioni 3.
Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika leo Agosti 30, 2024 katika shule ya sekondari Maganzo wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo CRDB benki imekabidhi viti pamoja na meza 44 ikiwa ni asilimia 1 inayorudishwa kwenye jamii.
Akisoma taarifa ya shule hiyo Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Maganzo Evalist Luhende amesema kumekuwa na changamoto ya meza na viti kwa wanafunzi wawapo shuleni kutokana na idadi kubwa ya wananfunzi waliopo shuleni hapo.
"Shule yetubina jumla ya wananfunzi 1237 wavulana 611 na wasichana 626 kabla ya kupokea msaada huu kutoka benki ya CRDB uhitaji wa meza na viti ni 1237 huku yaliyopo ni 834 hivyo uhitaji ni 403, tunawashukuru sana wadau wetu wa elimu benki ya CRDB tawi la Maganzo kwa kutupatia msaada huu, na kufanya kufikia idadi ya madawati 878 hivyo uhitaji bado ni mkubwa kulingana na wanafunzi waliopo, tunawaahidi kuendelea kufanya vizuri na kutunza madawati haya ili yaweze kutumika kwa vizazi na vizazi vijavyo", amesema Mwl. Luhende.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Udhibiti wa Benki ya CRDB, Madaha Mayega Chabba, ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya juhudi za benki hiyo kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi nchini.
Amebainisha kuwa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonyesha kuwa asilimia 49.1 ya Watanzania ni watoto wenye umri chini ya miaka 18, na wengi wao wanahitaji huduma bora za elimu ili kufikia malengo yao ya maisha.
"Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii kwa miaka mingi, tumekuwa tukisaidia miradi mbalimbali ya kijamii, hususan katika sekta ya elimu, mazingira, na afya kila mwaka, tunatenga asilimia moja ya faida yetu baada ya kodi kwa ajili ya kusaidia miradi ya kijamii, na leo tunakabidhi madawati haya 44 ili kuwasaidia wanafunzi wa Sekondari ya Maganzo kupata mazingira bora ya kusomea," amesema Chabba.
Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya madawati shuleni hapo amesema benki ya CRDB imeendelea kuiunga mkono serikali kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuchangia vifaa mbalimbali vya kujifunzia ujenzi wa madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kufanya vizuri kwenye masomo yao na kufikia malengo.
"Sisi Benki ya CRDB tumeweka utaratibu wa asilimia 1 ya faida tunayoipata tunairudisha kwa jamii ambapo hivi karibuni tulikabidhi madarasa mawili pamoja na madawati katika shule ya msingi Kiloleli, jambo hili ni muendelezo kama tulivyosikia kwenye taarifa iliosomwa hapa kuwa zipo changamoto zinazoikabili shule ya sekondari Maganzo ni waahidi kuwa tutaendelea kufanya hivyo pindi bajeti itakapo ruhusu lengo likiwa ni kuongeza ufaulu na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto mashuleni", amesema Jumanne Wagana.
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Katibu tawala wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka wanafunzi kutunza madawati hayo huku akiipongeza CRDB kwa kuiunga mkono serikali na kuwasihi wadau wengine kuiga mfano huo.
"Niwapongeza sana benki ya CRDB kwa kutoa msaada huu wa madawati ambayo yatakwenda kuwasaidia watoto wetu kuweza kujifunzia, mmekuwa mkifanya hivyo sehemu mbalimbali kupitia faida mnayopata tunawashukuru sana, na nitoe wito kwa taasisi zingine kuiga mfano huu kwani jukumu la kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora ni la kila mmoja wetu, lakini pia niwasihi wanafunzi na waalimu wa shule ya sekondari Maganzo kutunza madawati haya ili yaweze kudumu kwa muda mrefu", amesema Bi Fatma.
Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Maganzo Evalist Luhende akisoma taarifa wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Diwani kata ya Maganzo Mhe. Lwinzi Kidiga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Afisa tarafa ya Mondo Bi. Atka Haji akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Udhibiti wa Benki ya CRDB, Madaha Mayega Chabba akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Udhibiti wa Benki ya CRDB, Madaha Mayega Chabba akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Katibu tawala wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Katibu tawala wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 |
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania
Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier League – Msimamo NBC Tanzania Premier League NBC 2024/2025 Table Standings,Msimamo ligi kuu NBC Premier League NBC 2024/2025 Tanzania, Ratiba NBC Premier League,
Msimu wa 2023/2024 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania umekamilika kwa kishindo, Yanga SC wakiibuka mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo. Wanajangwani hao walimaliza kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 80 baada ya kucheza mechi 30, wakishinda mechi 26, wakitoa sare mbili, na kupoteza mbili pekee. Azam FC na Simba SC walimaliza nafasi ya pili na ya tatu mtawalia, zote zikiwa na pointi 69, huku Azam FC ikiwazidi Simba kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Msimu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa zaidi, huku timu zikifanya usajili wa nguvu na kujiandaa kwa ajili ya kuwania taji la ubingwa. Je, Yanga SC wataweza kutetea ubingwa wao?
Mashabiki wa soka Tanzania wana kila sababu ya kutazamia msimu uliojaa msisimko, ushindani mkali, na mshangao mwingi. Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 inaahidi kuwa msimu ambao hautakumbukwa tu kwa matokeo yake, bali pia kwa ubora wa soka litakalochezwa.
Udakuspecially.com Inakuletea live Msimamo wa Ligi kila siku Hapa chini:
Maskini..Hii Hapa A to Z Michael Jackson Alivyouawa na Illuminati , Kumbe Ilipangwa Muda Mrefu
Wanasema ilianzia kwenye video ya wimbo wa 'BLACK OR WHITE'
Ujumbe wa siri unao patikana kwenye wimbo huo ni kwamba Michael Jackson anawaambia Illuminati wao na yeye sasa ni basi.
Katika wimbo huo Michael Jackson anaonekana akitakaswa na maji matakatifu, sauti ya shetani akiwa amekasirika inasikika, Michael Jackson anazaliwa mara tatu kama alama ya 'kuzaliwa upya, kuwa mtu mpya na kuachana na mambo ya kale, kisha najipongeza mwenyewe kwa hilo, anapiga magoti mbele ya Mungu na kuwa huru kutoka kwenye mikono ya illuminati.
Kisha kachukua maji matakatifu na kuyamwagia kwenye alama ya 'ROYAL ARMS' na 'Royal' ikiwa na maana ya 'Royal Bloodline' ambazo nazo zipo 13. Mwishowe Michael anabadilika na kuwa 'panther'. Lakini kabla ya hapo alivunja kioo cha gari kilicho andikwa 'NIGGER GO HOME' na na ndani ya maneno hayo nambari '666' ikiwa imefichwa ndani yake.
Akavunja bango la 'KKK' ambapo 'K' ni herufi 11 kwenye alfabeti,hivyo 11x3=33, lakini pia 'KKK' inasimama badala ya jina la Ku Klas Klan, ambalo ni jina la kikundi cha Illuminanti, kilicho undwa na Albert Pike mwana masonia wa daraja la 33, kikundi hichi ni cha kibaguzi na kinahusishwa na kila aina ya uchafu unao fanywa na Illuminanti dhidi ya watoto, wanawake na watu wa matabaka mengine.
Mwishoni Michael Jackson alipogeuka 'Panther' ambapo panther inawakilisha, nguvu, uhuru, kuzaliwa upya baada ya mateso, yaani kuwa mtu mpya. Miaka 3 baada ya wimbo huo hadithi ya Michael Jackson kwenye vyombo vya habari ikabadilika.
Miaka 17 iliyo fuata Illuminanti walikuwa kwenye vita kali na Michael Jackson, kwa miaka yote hiyo walifanya kazi kubwa ya kuibomoa taswira yake kwenye vyombo vya habari na kwenye macho ya walimwengu.
Hawakutaka kumuua kipindi hicho kwa sababu hilo lingezindua watu, walimwengu wangeona kuna ambacho hakipo sawa, hivyo ilihitaji mpaka muda maalum, wakati muafaka.
Ingawa Michael Jackson hakung'ara na kupanda chati kwa sababu ya 'ku-sale his soul to the devil' lakini kwa sababu ya kipaji chake, lakini hata hivyo Illuminati hawakupoteza malengo yao, walimtumia Michael Jackson kwenye kazi zake kutukuza na kutangaza ushetani.
Wimbo kama ule wa 'Thriller' na 'Beat it' utakuta kwenye mashairi yake kumebeba vionjo vya kishetani.
Kwa Illuminati 'mtu mweusi' ni sawa na mnyama, yaani thamani yake ni ndogo, yaani siyo binaadam kamili, hili linahitaji mtiririko wa post kadhaa iliuweze kuelewa, lakini unapotizama filamu za Hollywood, unapotizama sera za nchi za Ulaya dhidi ya nchi za kiafrika, unapotizama matukio ya ubaguzi kote duniani, hutachelewa kuona kuna tatizo la makusudi la kutengenezwa dhidi ya matabaka na rangi za watu.
Hivyo Michael Jackson naye 'weusi' wake ulikuwa ni shida kwenye kipaji chake, 'baniani mbaya kiatu chake dawa.'
Vipi basi mtu mweusi awe 'KING OF POP' na abakie kama kama mtu mweusi, na akumbukwe kama mtu mweusi, hapana hili hata kidogo haliwezekani, hata kidogo haifai mtu mweusi kuwa 'king of pop' kazi ya ziada ikafanyika na Michael Jackson akaambukizwa au akatiwa ugonjwa wa ngozi unao fahamika kama 'VITILIGO.'
Kwenye mahojiano ya mwaka 1993, Michael akasema kuwa 'Baba aliniambia kuwa ugonjwa wa ngozi wa Vitiligo upo kwenye damu ya familia yetu"
Lakini ajabu ugonjwa ulimpata Michael Jackson peke yake ambaye ametokea kuwa ni King of Pop.
Kabla ya 'Thriller' MTV, walikataa kuonesha kwa watazamaji wake wimbo wowote wa Michael Jackson.
Kwanini?
Michael Jackson ni MWEUSI.
Rais w CBS Records Walter Yetnikoff aliwatishia MTV na kuwaambia "Sitawaletea tena video na ninakwenda hadharani na **** kuwambia watu kwamba hamtaki kuonesha video za watu weusi"
Nafasi ya Walter iliwafanya MTV waanze kurusha vidio ya 'Billie Jean' na 'Beat it'.
Bahati mbaya ni kuwa Thriller ilikuwa ni kama barabara ya kumfanya Michael kuwa kikaragosi cha Illuminati, kuanza kumtumia Michael na kipawa chake kuingiza maono ya kishetani kwa umma. Safari hiyo ilikuwa ni muhimu kufanyika kabla hawajamfanya Michael kuwa 'White Man' yaani kabla hawajampatia ugonjwa wa vitiligo ulio badilisha ngozi yake.
Dada yake na Michael, Latoya Jackson alikuwa na haya ya kusema kuhusu kifo cha kaka yake.
"I believe Michael was murdered," she said. "I felt that from the start. Not just one person was involved, rather it was a conspiracy of people. He was surrounded by a bad circle. Michael was a very meek, quiet, loving person. People took advantage of that. People fought to be close to him, people who weren't always on his side."
"He had needle marks on his neck and on his arms and more about those will emerge in the next few weeks," she said. " I cannot discuss that any further as I may jeopardize the investigation. I can, however, say that I have not changed my mind about my feeling that Michael was murdered."
"I am going to get down to the bottom of this," she said. "I am not going to stop until I find out who is responsible. Why did they keep the family away? It's not about money. I want justice for Michael. I won't rest until I find out what and who killed my brother."
Yaani kwa kiswahili.....
"Namini Michael aliuwawa, nilihisi hilo tokea mwanzo, sio mtu mmoja tu alihusika pasi na shaka ni kikundi cha watu, alizungukwa na kundi baya, Michael alikua mkimya na mpole na mwenye upendo,kwaio walitumia nafas hio vibaya kwake,,watu walipigana kua karibu nae,sio kila mara watu walikua upande wake. Alikua na majeraha ya sindano kwenye shingo na kwenye mikono,japo siwezi kuzungumzia hilo kwa kina nitaharibu upelelezi, lakini siwezi kamwe kubadili msimamo wangu na ninachoamini kwamba Michael walimuua. Sitapumzika hadi nihakikishe nani alihusika, kwanini wameitenga familia, sina shida ya pesa,nataka haki itendeke kwa Michael, sitapumzika.hadi nijue nani alimuua kaka.yangu".
Michael Jackson alifahamu kuwa Illuminati wanataka kumuua. Mwili wake ulipatikana na majeraha kadha ikiwemo shingoni na magotini, pia inaonesha kuwa alidondoka sakafuni kabla ya kifo chake, yaani alikuwa akipambana dhidi ya muuaji kuokoa uhai wake.
Latoya alipoulizwa ni nani aliyemuuwa Michael alijibu ....
"Doctor unaye muona, anaye tajwa kama msababishi wa kifo, ni kinga, yupo nyuma yake watu waliotaka Michael Jackson afe."
Wakati wa shitaka la mara ya pili la Michael lililomalizika Juni 13 2005, wazazi wa Michael walimuita rafiki yake na Michael Dick Gregory, ambaye alikuwa ni rafiki mzuri wa Michael, walimuomba amtembelee Michael maana hayupo vizuri hata kidogo.
Baada ya siku chache Gregory alirudi na Michael kwenye jumba lake la Neverland. Michael alimkumbatia na kumuambia tafadhali usiniache wanataka kuniuwa.
Gregory akamuuliza Michael lini ilikuwa mara yake ya mwisho kula maana anaonekana kudhoofu, Michael akamjibu, " wanataka kuniuwa kwa sumu", akamuuliza ni lini mara ya mwisho amekunywa maji, Michael akamjibu, "Wanataka kuniua"
Gregory akamchukua Michael na kwenda naye kwenye hospitali ya karibu lakini mbali na Neverland bila kumuarifu mtu yeyote kwamba anakuja hapo na Michael Jackson, na akatundikiwa dripi kutoka 11:30 jioni mpaka 11:30 asubuhi na siku iliyofuata kwa masaa 24 akawa kwenye drip bila kupumzika, Dr. Aliyekuwa akimuhudumia akasema lau asingefika kwa wakati basi masaa mengine 12 angelikufa.
Utaona hapo kuwa Juni 2005, illuminati walikuwa wakifanya jaribio la kumuuwa Michael tena, lakini lilishindikana, lakini Juni 2009 walifanikiwa kutekeleza azma yao baada ya kumtumia mtu ambaye Michael alimuamini zaidi, Daktari wake, Conrad Murray.
Michael alikuwa na nguvu za kutosha, dokumentari kadhaa zimetolewa zikimuonesha wiki kabla ya kifo chake, alionekana yuko safi, na akifanya maandalizi ya 'tour' yake ya London aliyoipatia jina la 'THIS IS IT', Tetesi ni kuwa kwenye Tour hiyo Michael kati ya mengi aliyo kuwa nayo ilikuwa ni kuufumbua macho ulimwengu kuhusiana na madhila na ubaya wa Illuminati, lakini jamaa nao walishaiona hatari hiyo na hawakuwa na muda wa kupoteza, ndipo daktari ambaye pia ni Freemason alipochukua jukumu hilo zito la kumuangusha King of Pop.
Thursday, August 29, 2024
MATOKEO Yanga Vs Kagera Sugar Leo 29 August 2024
MATOKEO Yanga Vs Kagera Sugar Leo 29 August 2024
Kagera Sugar inacheza na Young Africans kwenye Uwanja wa Ligi Kuu Bara wa Tanzania Bara Agosti 29. Mechi hiyo itaanza saa 19:00 kwa saa za kwenu.
Kagera Sugar na Young Africans (ambazo kwa kawaida huitwa Yanga au Yanga SC) zinakutana tena miezi 4 baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo Young Africans ilishinda 1-0. Kagera Sugar wanakaribia kucheza mechi hiyo baada ya kufungwa na Singida Black Stars Jumamosi iliyopita. Kocha na wachezaji huenda wakaweka nguvu ya ziada kwenye safu ya ulinzi kwani wamekuwa wakiruhusu mabao kwa mechi 6 mfululizo sasa.
Kwa upande mwingine, Young Africans wanakaribia kucheza wakiwa katika hali nzuri ya kupata ushindi katika michezo 4 mfululizo dhidi ya VitalO, VitalO, Azam na Simba wakiendeleza wimbi lao la kutopoteza hadi mechi 15.
Udaku Special inaangazia Kagera Sugar dhidi ya Young Africans kwa wakati halisi, ikitoa mtiririko wa moja kwa moja na matokeo ya moja kwa moja ya mechi, safu za timu, takwimu kamili za mechi, maoni ya mechi ya moja kwa moja na muhtasari wa video rasmi. Tunashughulikia mechi zote za Tanzania Ligi Kuu Bara kwa wakati halisi na kutoa utiririshaji wa moja kwa moja inapowezekana
WAZAZI WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI KWA KUDUMISHA TAMADUNI KWA WATOTO
Wednesday, August 28, 2024
Fei Toto Agoma Kuongeza Mkataba Kuitumikia Azam Mkataba Ukiisha
Sunday, August 25, 2024
TANZANIA YAZISIHI NCHI ZA AFRIKA KUSHIRIKIANA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOLIKABILI BARA LAO
Source
Azam Huruma Tupu Pamoja na Fei Toto Wao Watupwa nje ya Mashindano ya CAF
Thursday, August 22, 2024
WEKENI TAKWIMU SAHIHI KWENYE MIFUMO KULETA MAGEUZI YA UTENDAJI - MHA. MWAJUMA WAZIRI
Wednesday, August 21, 2024
Eng Hersi "Mimi Sio Mfanyakazi Wa Yanga Na Sipati Hata shilingi Kutoka kwao"
"Mimi Sio Mfanyakazi Wa Yanga Na Sipati Hata shilingi Kutoka Yanga, hata Kwenye Mfumo Wa Mishahara Ya Wafanyakazi Wa Yanga Mimi Sipo
Rammy Galis: Masogange Alinitia Hasira Kutafuta Pesa
"Bado nakumbuka, nilipokua na uhusiano na dada mmoja hivi mwaka 2017 aliniambia nikamchukue kati ya kumbi za starehe maarufu sana. Kufika nilipotaka kuingia, akaniambia "Usiingie", nitatoka Nikamuuliza kwanini? Akaniambia hautaweza kuvumilia uone meza niliokaa nimekaa na watu wanaotumia pesa nyingi ili kuwafurahisha marafiki zangu.
"Nikasema sawa, nimepaki hapa nje toka utaona Vitz yangu hapa mlangoni. Alichonijibu niliumia sana, kwani aliniambia nitoe gari hapo nje, nikapaki upande wa pili, kwani hataki marafiki zake na watu wengine wamuone kwenye gari lile langu.
"Sikua na jinsi, nilifanya hivo, Nilipopaki upande wa pili alikuja huku ana angalia huku na kule, Alipoingia kwenye gari nilikua na hasira sanaa na kunyamaza safari nzima ya kuelekea nyumbani.
Tukiwa barabarani pia hakuniacha, Aliniambia babe unajua jinsi ulivyo, unatakiwa utafute sana pesa ili uendane na muonekano wako vinginveyo hautaendana na jinsi ulivyo.
"Wengi wenu mtasema hakua mtu sahihi, kwangu lakini alinisaidia kuniamsha na kunipa hasira ya maisha na kufikia hatua nyingine. #RipAgness;" kupitia Facebook ameandika Rammy Galis, mwigizaji wa filamu aliyekuwa mpenzi wa Agnes Masogange.
Agnes ambaye alikuwa video queen na socialite maarufu, alifariki dunia 2018 baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...