Wednesday, August 28, 2024

Fei Toto Agoma Kuongeza Mkataba Kuitumikia Azam Mkataba Ukiisha

Fei Toto Agoma Kuongeza Mkataba Kuitumikia Azam Mkataba Ukiisha



Kiungo mshambuliaji wa Azam Fc Feisal Salum Abdallah Fei Toto amegoma kuongeza mkataba kuitumika Klabu yake ya Azam Fc mara baada ya mkataba wake huo utakapokwisha rasmi.

Zipo taarifa tumeletewa na chanzo cha ndani kikidai mchezaji huyo kwa sasa hana mpango tena wa kuendelea na timu hiyo huku taarifa zikisema anaweza kutua Simba Sports Club ingawa kuna offer lukuki za kumuhitaji zipo mezani moja ikiwa kutoka kwa Timu ya Kaizer Chiefs ya nchini South Africa.

Kocha Mohamedi Nasreedine Nabi yupo nchini Tanzania 🇹🇿 kwa sasa kufanya mazungumzo na kiungo huyo lengo ikiwa kumshawishi kujiunga na timu yake ambayo anafundisha kwa sasa nchini South Africa Kaizer Chiefs.

Offer ambayo Kaizer Chiefs imeweka mezani kwa kiungo huyo mzawa wa Tanzania 🇹🇿 ni dola 300,000 na mshahara wa milioni 45 kwa mwezi mmoja Kocha huyo bado yupo nchini Tanzania kuhakikisha anamaliza kila kitu kwa kiungo huyo fundi na bora kwa sasa kabla hajaondoka na kurudi South Africa.

Taarifa nyingine inasema Klabu ya Simba huwenda wakaongeza nguvu katika kuinasa saini ya kiungo huyo kama asipoongeza mkataba na klabu yake ya awali.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...