Wednesday, August 21, 2024

Rammy Galis: Masogange Alinitia Hasira Kutafuta Pesa

 

Rammy Galis: Masogange alinitia hasira kutafuta pesa

"Bado nakumbuka, nilipokua na uhusiano na dada mmoja hivi mwaka 2017 aliniambia nikamchukue kati ya kumbi za starehe maarufu sana. Kufika nilipotaka kuingia, akaniambia "Usiingie", nitatoka Nikamuuliza kwanini? Akaniambia hautaweza kuvumilia uone meza niliokaa nimekaa na watu wanaotumia pesa nyingi ili kuwafurahisha marafiki zangu.


"Nikasema sawa, nimepaki hapa nje toka utaona Vitz yangu hapa mlangoni. Alichonijibu niliumia sana, kwani aliniambia nitoe gari hapo nje, nikapaki upande wa pili, kwani hataki marafiki zake na watu wengine wamuone kwenye gari lile langu.


"Sikua na jinsi, nilifanya hivo, Nilipopaki upande wa pili alikuja huku ana angalia huku na kule, Alipoingia kwenye gari nilikua na hasira sanaa na kunyamaza safari nzima ya kuelekea nyumbani.


Tukiwa barabarani pia hakuniacha, Aliniambia babe unajua jinsi ulivyo, unatakiwa utafute sana pesa ili uendane na muonekano wako vinginveyo hautaendana na jinsi ulivyo.


"Wengi wenu mtasema hakua mtu sahihi, kwangu lakini alinisaidia kuniamsha na kunipa hasira ya maisha na kufikia hatua nyingine. #RipAgness;" kupitia Facebook ameandika Rammy Galis, mwigizaji wa filamu aliyekuwa mpenzi wa Agnes Masogange.


Agnes ambaye alikuwa video queen na socialite maarufu, alifariki dunia 2018 baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...