Monday, May 31, 2021

Faida ya Embe bichi kiafya

 

Unaweza usiamini nikikuambia embe bichi ni tiba ya ugonjwa furani, lakini amini kuwa kweli ni tiba, tena iliyo makini. Embe bichi linasaidia sana kwa mgonjwa wa maradhi ya kuhara. Tumia embe bichi kumaliza tatizo hilo.

Menya embe bichi, likate  vipande na kuviweka katika chombo, au tengeneza juice changanya na unga wa pilipili manga pamoja na asali, kisha tafuna vipande hivyo vyenye mchanganyiko huo.

Mchanganyiko wako utategemea kiwango cha vipande vya embe lako. Hata hivyo, usile zaidi ya embe mbili kwa kutwa moja. Endelea na tiba hii muda wa siku tatu.

Kuharisha ni kitendo cha kujisaidia kinyesi chenye majimaji mara kwa mara. Hali hiyo hutokea baada ya utumbo mdogo kuwa na maji mengi ambayo yanashindwa kutoka mwiilini kwa njia za kawaida kama ya mkojo na jasho hivyo yanatelemka kwenye utumbo mkubwa usio na uwezo wa kutunza maji.

Yakiwa huko mtu hujikuta anajisikia hali ya kutoa haja na ndipo maji hayo hutoka kupitia haja kubwa. Kimsingi utumbo mdogo una uwezo wa kupokea zaidi ya lita nane za maji kutoka kwenye vyakula au vinywaji vinavyopitia mdomoni na mengine kutoka sehemu mbalimbali katika mwili.

Tatizo la kuhara linaweza kusababishwa na kula kupita kiasi, kula mchanganyiko wa vyakula vya aina mbalimbali, kuwa na hofu, hasira au wasiwasi, kuchacha chakula ndani ya tumbo, kula sumu, bakteria, virusi au vijidudu wenye vimelea.

CCM yazidi kuwanoa wanachama wadai lengo kuu tangu kuzaliwa ni kushika dola milele


Na Amiri Kilagalila,Njombe.

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimewataka wanachama wa Chama hicho kujua  malengo makubwa  ya kuanzishwa  kwa Chama hicho kuwa ni pamoja na  kushika dola milele na kuwaagiza wanachama kuendelea kujenga chama hicho pamoja na jumuiya zake.

Hayo yamebainishwa na katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi  mkoa wa Njombe Ndugu,Erasto Ngole wakati akitoa elimu ya ukuaji na uimarishaji wa Chama kwa viongozi wa mashina,tawi,kata na wilaya katika wilaya ya Ludewa ilipofika Sekretarieti ngazi ya mkoa wilayani humo kwa ajili ya kukagua uhai wa Chama na jumuiya zake,kukagua utekelezaji wa Ilani (miradi mbali mbali ya Maendeleo) pamoja na utekekelezaji wa maagizo mbali mbali kutoka ngazi ya juu ya Chama.


"CCM ilianzishwa kwa lengo moja tu la kushika dola,yaani lengo la CCM ilianzishwa ili yenyewe ishike dola milele katika hii nchi.Kwa hiyo kama lengo ni kushinda chaguzi na kushika dola basi yeyote atakayeleta kikwazo huyo ni adui"alisema Erasto Ngole

Aidha amewataka wanaccm kufutilia shughuli za maendeleo ndani ya maeneo yao na kuhakikisha zinatekekeleza ili kulinda kata zinaongozwa na chama chicho.

Naye katibu wa Jumuiya ya wazazi Agatha Lubuva ametoa wito kwa wanachama kuendelea kuhamisiashana katika jamii ili kuhakikisha wanachama wanaongezeka kwa njia zozote ikiwemo ushawishi.

"Hata ukiwa nyumbani muulize jilani yako ana kadi ya chama,iwe ya vijana ya wazazi au UWT na umueleze kadi inakopatikana na gahalama zake ili tuhakikishe wanachama wanaongezeka"alisema Agatha Lubuva

Kwa upande wake katibu wa UWT mkoa wa Njombe Bi,Frola Kapalie ametoa rai kwa wanachama kuongeza nguvu katika ulipiaji wa kadi pamoja na ada ya uanachama,

"Tujitafakari na kuhakikisha sisi wenyewe kwanza tumelipia kadi ndio unamfuata Yule mwanachama mwingine ili nae alipie kadi kwasababu ulipaji wa ada ni muhimu katika uhai wa Chama"alisema Frola Kapalie

Katibu wa Jumuiya ya vijana UVCCM mkoa wa Njombe Amos Kusakula ameelekeza vijana walioaminiwa kwenye nyadhifa mbali mbali kwenye chama na seriakali wakiwemo madiwani,kufanya kazi kwa kujituma na kwa juhudi ili kulinda imani kwa vijana wengine.

"Vijana mnaopewa nafasi lazima muangalie na vijana wengine wanao kuja kwa kuhakikisha mnafanya kazi vizuri ili tuiendelee kuaminiwa"Alisema Kusakula


Kwa upande wake  katibu wa CCM mkoa wa Njombe  Bi,Amina Imbo ambaye ndiye kiongozi wa semina na kikao kazi kinachoendelea mkoani Njombe ameshukuru namna utekelezaji wa ilani unavyoendelea katika wilaya hiyo huku akiagiza kuongezwa vyanzo vya mapato katika jumuiya na Chama.

"Wilaya ya Ludewa tupo chini katika swala la kiuchumi,tuzidi kushirikiana kuleta wawekezaji mpaka kwenye matawi ili tuweze kupata kipato lakini kipato pia kinaazia kwenye ulipaji wa ada,ada hazilipwi ndio maana uchumi unakuwa chini"alisema Amina Imbo

Nao baadhi ya washiriki katika kikao kazi hicho cha kawaida akiwemo diwani wa kata Ludende bwana Vasco Mgimba wamesema wapo tayari kufikisha maelekezo hayo ya chama ngazi ya mkoa kati maeneo yao ili kuzidi kuimarisha chama chao.

 

MSIMBE ATEULIWA KUWA ASKOFU JIMBO LA MOROGORO


Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Lazarus Vitalis Msimbe, S.D.S kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Monsinyo Msimbe alikuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Morogoro.

 Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Lazarus Vitalis Msimbe, S.D.S., alizaliwa tarehe 27 Desemba 1963 huko Homboza, Jimbo Katoliki la Morogoro.

 Baada ya masomo yake ya msingi na sekondari, alijiunga na masomo ya falsafa kwenye Seminari kuu ya Kibosho, Jimbo Katoliki la Moshi.

Baadaye aliendelea na masomo ya taalimungu, Seminari kuu ya Segerea, iliyoko Jimbo kuu la Dar es Salaam. Baada ya majiundo yake ya kitawa, tarehe 8 Desemba, 1987, Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, akaweka nadhiri zake za daima na hatimaye, kupewa daraja Takatifu ya Upadre tarehe 21 Juni 1998.

 Askofu mteule Msimbe aliendelea na masomo ya juu kwenye Chuo kikuu cha "Heythrop College" huko London, Uingereza na kujipatia Shahada ya Uzamili katika Sheria za Kanisa kutoka katika Chuo Kikuu cha Uingereza.

 Baadaye pia alijiendeleza na hatimaye kujipatia shahada kwenye Sheria za Kimataifa kutoka katika Chuo Kikuu cha West-England, kilichoko Bristol, Uingereza.

Baada ya kurejea nchini Tanzania, alipangiwa utume wa kuwa ni mlezi wa Wapostulanti na Wanovisi wa Shirika la Mungu Mwokozi, maarufu kama Wasalvatoriani. Kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2012 alichaguliwa kuwa Padre Mkuu wa Kanda ya Shirika la Mungu Mwokozi, nchini Tanzania.

 Baada ya kumaliza muda wake wa uongozi, ameendelea kuwa ni mlezi wa Shirika kimataifa katika nyumba ya malezi "Mater Salvatoris" iliyoko Jimbo Katoliki la Morogoro.Tarehe 13 Februari 2019 aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Morogoro.

 Tarehe 30 Desemba 2020 akateuliwa tena kuwa Msimamizi wa Kitume "Sede Vacante ad nutum Sanctae Sedis" Jimbo Katoliki la Morogoro. Yaani kama Msimamizi wa Kitume, alikuwa anawajibika moja kwa moja na Vatican katika masuala yote ya uongozi wa Jimbo Katoliki la Morogoro.




Wizara ya Kilimo yaweka msukumo kuzalisha Pembejeo nchini


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha.

WIZARA ya Kilimo imesema kwa sasa imeweka msukumo kwa wawekezaji kuzalisha pembejeo hapa nchini ili kurahisisha upatikanaji wake.

Aidha, imeeleza inapambana kutafuta masoko ili bei za bidhaa mbalimbali za mazao zipande na kuwa zenye tija kwa mkulima.

Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha jana tarehe 30 na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa kupitia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na maelekezo ya  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo hivi karibuni kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija.

Amebainisha kwa sasa wanaweka msukumo kwa wawekezaji kuzalisha pembejeo hapa nchini ambapo katika kufanikisha hilo hivi karibuni alitembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu kuhakikisha kinafanya upanuzi na kuongeza uzalishaji.

"Kuna kiwanda kingine kinajengwa Dodoma, kuna viwanda viwili vya viuatilifu vinajengwa hapa Arusha na tunataka kuwahakikishia wawekezaji hao kwamba tutawapa kipaumbele katika kununua pembejeo," Amesema

Ameeleza kuwa baadhi ya maeneo matumizi ya mbolea yanahitaji kuwekwa chokaa ili iweze kuwa na tija katika kilimo hivyo kwa sasa wanaongeza juhudi za kupima afya ya udongo na aina yake.

Aidha, amesema yatafanyika mafunzo rejea mengi kwa mabwana shamba ili kutoa ushauri wa matumizi ya mbolea sehemu ambayo inahusika.

Amesema licha ya kutokuwa na shida ya soko la mafuta nchini kwakuwa ipo ardhi ya kutosha kuotesha alizeti, michikichi, pamba lakini bado yanaagizwa kutoka nje ya nchi.

"Tunakidhi mahitaji ya mafuta ya kula kwa asilimia 47 tu nchini na hiyo inatokana na tija ndogo ya uzalishaji kiasi kwamba inakuwa ni bei rahisi zaidi kuagiza mafuta kutoka Malaysia, Indonesia, kuliko kuchukua mafuta ya mawese au ya alizeti.

Kwa hiyo suala hapa kubwa ni tija na soko kwenye mafuta ya kula lipo, kwenye ngano lipo, takribani tani 800,000 mpaka milioni moja  humo ndani tunazalisha tani 77000, soko la ngano lipo, uzalishaji ni mdogo na tija ni ndogo kiasi kwamba ngano inayokuja kutoka nje inaonekana ni bei ndogo zaidi kuliko inayotumika hapa nchini," Amesema.

Ameeleza unaweza kwenda na zao moja hado jingine ukagundua kuwa changamoto iliyopo ni tija na kwamba wamegundua ili kupambana na changamoto hiyo ni lazima kufanya utafiti ili kuwa na mbegu bora.

"Sasa kuna mbegu zimegunduliwa pale Kibaha kwenye kituo cha utafiti ambapo ikitumika kwa hekta moja unaweza ukapata kuanzia tani 22 mpaka 50 za mihogo.

Sasa hivi tunapata wastani wa tani 8 mpaka 3 kwahiyo hata soko la China ambalo tunataka kupeleka mihogo sasa hivi tunashindwa kufanya hivyo kukidhi mahitaji ya soko kwa sababu tija ni ndogo"

Ameongeza:"Lakini vilevile, mihogo inazalisha Starch, tunaagiza Starch toka nje kwa sababu hatujazalisha mihogo ya kutosha kuzalisha Starch hapa nchini kwa utafiti na mbegu bora tunaweza tukajitegemea kwenye vitu vingi, Lakini chamngamoto kubwa kwetu ni pembejeo kwa sababu nyingi zinaagizwa nje na kwa gharama kubwa,".

Pia Waziri Mkenda amesema kuwa, kunapokuwepo changamoto ya soko la mazao ni lazima gharama za uzalishaji zitakuwa kubwa na matokeo yake mkulima halimi kwa faida.

Amesisitiza kuwa kwa sasa wanapambana na masoko kwakuwa ni suala ambalo lazima walivalie njuga na wanafanya hivyo ili bei ianze kupanda.

"Tunafuatilia bei za mahindi kwa mfano Ruvuma huko, Mbeya ziko chini sana ukilinganisha na gharamaza uzalishaji," Amesisitiza

 

Prof. Mkumbo: Serikali Inaendelea Kuboresha Mazingira Ya Biashara Mpakani, Wafanyabiasha Zingatieni Sheria Na Taratibu Za Kufanya Biashara.


Na Eliud Rwechungura
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (Mb) amewahakikishia Wafanyabiashara kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ili kuhakikisha wanafanikiwa huku akiwahasa wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya kuzingazia Sheria na taratibu zilizowekwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuondokana na vikwazo ambavyo vimekuwa vikiwekwa  kutoka na kutozingatia Sheria na taratibu za kufanya biashara mipakani.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo 30 Mei 2021 alipoambatana na Mawaziri wa Kenya na Tanzania kutembelea Mpaka wa Namanga kujionea jinsi biashara na shughuli za upitishaji wa bidhaa na huduma zinafavyofanyika katika Mpaka huo baada ya nchi hizo kukubalina kuondoa vikwazo 30 vya biashara visivyokuwa vya kiushuru.

"Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anataka kuona Maisha ya Watanzania yanaboreka na biashara zinafanyika vizuri, niwahakikishie wafanyabiashara wa Watanzania, Serikali yenu ipo na nyie na itaendelea kuwaunga mkono na kuwapa msaada ili kuona mnafanikiwa lakini kwa upande wenu tunaomba katika kufanya kwenu biashara mzingatie sheria na taratibu zilizopo kwasababu nchi zetu zinaongozwa na utawala wa sheria" ameeleza Prof. Mkumbo

Ameongeza kuwa, lengo la ziara hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Waheshimiwa Marais wa Tanzania na Kenya ya kuhakikisha mahusiano ya wananchi wa nchi mbili yanaboreka lakini muhimu Zaidi biashara hazikwami ndo maana wamekutana Mawaziri kutatua mambo mengi yaliyokuwa yanakwamisha biashara ikiwemo changamoto ya mahindi hapa mpakani wameweza kuizungumzia  na anashukuru imetatuliwa na mambo mengine mengi yalikuwepo pande zote mbili za Tanzania na Kenya.

Aidha, Prof. Mkumbo amewapongeza wataalam wa pande zote mbili za Tanzania na Kenya kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya huku akiwahasa kuendelea kuimalisha mahusiano mazuri kwa kukaa Pamoja na kujadiliana kwa kuzitatua changamoto kwasababu ni jambo kubwa na la muhimu viongozi wetu wanalotaka kuliona

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Wajasiliamali nchini Kenya Mhe. Betty Maina amefurahishwa na kuona changamoto 30 kati ya 64 zimetatuliwa na hizo nyingine zilizobaki wamejiwekea muda wa miezi mitatu kuzifanyia kazi huku akiwataka wafanyabiashara wa pande mbili kuendelea kuzingatia sheria ambazo zimewekwa kwa pande zote mbili za Kenya Tanzania wakati wa ufanyaji biashara.


Nuh Mziwanda aitwa polisi



 Msanii wa muziki nchini Nuh Mziwanda ameitwa na jeshi la polisi katika kituo cha  Oysterbay . Taarifa hiyo ameitoa msanii huo kwenye ukurasa wake wa instagram bila kutoa sababu iliyofanya aitwel

Aidha, Nuh ameeleza kuwa anaheshimu wito huo na atafika kituoni hapo.

Ajenda Kuu Ya Serikali Ni Kujitegemea Katika Uzalishaji Mbegu-waziri Mkenda


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Katika kuendeleza ushirikiano na Sekta binafsi, ambalo ni jukumu la kisheria la Serikali kuhamasisha sekta binafsi katika uzalishaji wa Mbegu Bora, Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda katika ziara yake Jijini Arusha, leo tarehe 30 Mei 2021 ametembelea moja ya kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO

Waziri Mkenda pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao wa Wizara ya Kilimo Ndg Nyasebwa Chimagu wamepata fursa ya kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo binafsi hasa katika suala zima la uchakataji na utunzaji wa Mbegu Bora unavyofanywa na kampuni hiyo kutoka hatua za awali Mbegu zinapotoka shambani, zinapopokelewa, kuchakatwa, kupimwa na kupakiwa tayari kwa kumfikia mkulima.

Katika ziara hiyo Waziri Mkenda amesema kuwa moja ya ajenda kuu ya Wizara ya Kilimo ni kuhakikisha nchi inazalisha mbegu za kutosha za kilimo kupitia sekta binafsi kadhalika Mamlaka ya Mbegu ya Serikali (ASA) ili kufikia hatua ya kujitosheleza katika uzalishaji mbegu na kuanza kuuza nje ya nchi.

Amesema kuwa serikali inahimiza Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) pamoja na Taasisi zote zinazojihusisha na utafiti hususani wa mbegu kuhakikisha kuwa zinazendelea kufanya utafiti wa mbegu bora na zitakazo ongeza tija katika kilimo.

"Tunataka mtu aweze kuzalisha kiasi kikubwa zaidi kwa Hekari moja ili nguvu ya mkulima iwe inazaa matunda makubwa na vilevile itatusaidia sana kwenye masoko kwa sababu ukizalisha kwa wingi hata kama bei ya mazao imeshuka lakini kipato kinakuwa kikubwa" Amekaririwa Prof Mkenda

Waziri Mkenda amesema kuwa pamoja na juhudi za serikali za kutumia taasisi ya utafiti (TARI) na mamlaka ya Mbegu (ASA) ambayo ina kazi ya kuchukua mbegu bora na kuzalisha kwa wingi ili kuzipeleka kwa mkulima lakini pia serikali inafanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ikiwemo kampuni ya mbegu ya SEED.CO

Prof Mkenda ameipongeza kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO kutokana na uzalishaji wa mbegu bora ambazo zimekuwa na matokeo mazuri kwa wakulima ambapo amewahakikishia hitaji lao kubwa la kukodi mashamba ya serikali kwa ajili ya uzalishaji mbegu bora linafanyiwa kazi kwa haraka iwezekanavyo.

"Lakini nimewaahidi endapo watajenga maabara kubwa ya kisasa kwa ajili ya shughuli za mbegu hapa Tanzania, nitajitahidi kuhakikisha kuwa wanapata mashamba makubwa angalau mawili kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mbegu" Amesema Mkenda

Amewasihi kuongeza zaidi uzalishaji wa mbegu ikiwa ni pamoja na kuanzisha uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali badala ya Nafaka na Mbogamboga pekee, Kwa kufanya hivyo kutakuwa na uwezekano wa kuongeza mbegu bora na zenye tija kwa wakulima nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mbegu (TASTA) Ndg Bob Shuma amepongeza Serikali kwa kuamua kulichukulia kwa msisitizo swala la uzalishaji wa mbegu bora nchini ambapo ameeleza furaha yake na kumuhakikishia Waziri wa Kilimo kuwa umoja huo unaendelea na mkakati madhubuti katika uzalishaji wa mbegu bora na kwa wingi.

Hata hivyo amerejea msisitizo wa Waziri wa Kilimo kuyaomba mashirika mengine nchini na nje ya nchi kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya mbegu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa karibu na serikali kupitia taasisi ya TARI na ASA ili kuongeza ufanisi katika sekta ya mbegu.


Yanga Yathibisha Carlinhos Kuondoka




Uongozi wa Yanga umethibisha kufikia makubaliano na Carlinhos ya kusitisha mkataba wao kuanzia sasa.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Carlinhos kuwasilisha maombi ya kusitisha mkataba wake, uongozi wa Yanga umesema, baada ya majadiliano na kwa kuzingatia maslahi mapana ya pande zote, uongozi umeafiki ombi lake.


Mshukiwa wa utapeli wa mamilioni ya pesa akiwa Marekani kufikishwa mahakamani Kenya





Stacey Marie Parker anatuhumia kuwatapelli Wakenya mamilioni ya fedha huku akidai watapata faida zaidiImage caption: Stacey Marie Parker anatuhumia kuwatapelli Wakenya mamilioni ya fedha huku akidai watapata faida zaidi
Mwanamke anayeshukiwa kuwa ndiye msimamizi wa mpango wa utapeli ambao ulitumiwa kuwalaghai Wakenya mamia ya mamilioni ya pesa amekamatwa mwishoni mwa wiki na atafikishwa mahakamani leo.

Stacey Marie Parker mwenye umri wa miaka 50, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumamosi alipowasili kutoka Marekani.

Mshukiwa alikamatwa kufuatia uchunguzi ulioendeshwa na idraa ya makosa ya Jinai nchini Kenya baada ya kuhusishwa na sakata hiyo ya ulaghai iliyopora pesa wawekezaji ambao hawakujua kwamba wanahadaiwa.

Katika mpango ulioratibiwa na kupangwa vizuri, wawekezaji walidanganywa kuwekeza pesa zao katika programu ya mtandaoni inayojulikana kama Amazon Web Worker, kwa kudhani kuwa watapata faida kubwa ya hadi 38% kwa amana inayodumu kwa siku 7 tu.

Kumbi za mitandao ya kijamii zilikuwa zimejaa matangazo yaliyowashawishi Wakenya kujiunga na mpango huo ili wapate faida .

Wakenya wasio ambao hawakujua kwamba mpango huo ulikuwa utapeli walipakua programu kwa wingi na wakasajiliwa huku wengi wakiweka amana zao. Wengine waliwapeleka wapendwa wao , watoto na marafiki wa karibu kwenye mpango huo, kwa nia ya kupata utajiri wa haraka.

Hadi wakati programu hiyo ilipofutwa kutoka mtandaoni bila taarifa kwa wawekezaji , ndipo wawekezaji walipogundua walikuwa wamedanganywa.

Walishtuka kujua kwamba programu hiyo haikuhusishwa kwa njia yoyote na Amazon, kampuni ya teknolojia ya kimataifa iliyo nchini Marekani Programu hiyo ilizama na amana zenye thamani ya mamia ya mamilioni ya pesa .

Jay Z kwa mara ya kwanza afunguka kuikataa Tuzo ya Grammy kisa marehemu DMX

 


Jay Z kwa mara ya kwanza afunguka kuikataa Tuzo ya Grammy kisa marehemu DMX

VIDEO:

Wakazi Achafukwa Waopiga Kampeni Diamond BET Award


ANAANDIKA Wakazi

Nimesikitishwa na comment za watu za kusema hawataki kum-support Diamond BET kwa sababu akishinda ataitumia kama fimbo kuwa mahasimu wake na wengine wanasema hawawezi kum-support msanii ambae alikuwa CCM.

Diamond mimi sio hata rafiki yangu na huwa nina m-criticize mara nyingi tu kama ninavyofanya kwa wengine, lakini penye pongezi apewe, na hii ya BET ina manufaa kwa TZ nzima.

Akiwa nominated na akashinda, basi awareness ya Tanzania katika ulimwengu wa muziki inaongezeka, na ikiongezeka basi nafasi ya msanii unayempenda kupata fursa inaongezeka pia. So hata kama ningekuwa nina mchukia jamaa (which I don't), naelewa umuhimu wa nafasi aliyopo kwetu Wasanii na kwa Taifa pia.

Tujifunze kujenga UMOJA kupitia TOFAUTI zetu. Badala ya kudumisha CHUKI, basi tutafute suluhu ambazo zina manufaa kwa wengi kama sio wote.

Ni kama hili swala la Ushindani na Ushabiki tumelielewa vibaya hapa Tanzania. Niliwahi ku-rap "SIMBA na YANGA ni wapinzani wa Jadi, ila ukiweka Simba na Yanga unapata TAIFA STARS". Meaning hapa ndani sawa tushindane, ila huko nje tuungane kwa maslahi zaidi.

Ni kweli akishinda atapata bichwa, hata ungekuwa wewe hilo halipingiki, ILA bado nasi tunanufaika.

Na ukisema kisa ali-support CCM, unakuwa huna tofauti na ambao wanamnyima fursa @wakazi Jhikoman, Vitali Maembe, @officialbabalevo kisa nao walikuwa Upinzani. Basi ningewaona bora zaidi kama mtatu-support sisi tuinuke, na sio kutumia nguvu kumshusha mwingine. Just saying….

"Two wrongs don't make it right" hata kama yeye kaongea mbovu. Na it's okay kama hum-support ILA kufanya kampeni kabisa waziwazi, we better than that. Tasnia yetu ina matatizo mengi, ila nadhani tiba ya kwanza inabidi iwe UPENDO.

The Leader.

Wakazi Achafukwa na Waopiga Kampeni Diamond Asishinde BET Award "Hatumkomoi Diamond Tunajikomoa Wenyewe"



Nimesikitishwa na comment za Watu za kusema hawataki kum-support Diamond BET kwa sababu akishinda ataitumia kama fimbo kuwa mahasimu wake na wengine wanasema hawawezi kum-support msanii ambae alikuwa CCM.

Diamond mimi sio hata rafiki yangu na huwa nina m-criticize mara nyingi tu kama ninavyofanya kwa wengine, lakini penye pongezi apewe, na hii ya BET ina manufaa kwa TZ nzima. Akiwa nominated na akashinda, basi awareness ya Tanzania katika ulimwengu wa muziki inaongezeka, na ikiongezeka basi nafasi ya msanii unayempenda kupata fursa inaongezeka pia. So hata kama ningekuwa nina mchukia jamaa (which I don't), naelewa umuhimu wa nafasi aliyopo kwetu Wasanii na kwa Taifa pia.

Tujifunze kujenga UMOJA kupitia TOFAUTI zetu. Badala ya kudumisha CHUKI, basi tutafute suluhu ambazo zina manufaa kwa wengi kama sio wote.

Ni kama hili swala la Ushindani na Ushabiki tumelielewa vibaya hapa Tanzania. Niliwahi ku-rap "SIMBA na YANGA ni wapinzani wa Jadi, ila ukiweka Simba na Yanga unapata TAIFA STARS". Meaning hapa ndani sawa tushindane, ila huko nje tuungane kwa maslahi zaidi.

Ni kweli akishinda atapata bichwa, hata ungekuwa wewe hilo halipingiki, ILA bado nasi tunanufaika.

Na ukisema kisa ali-support CCM, unakuwa huna tofauti na ambao wanamnyima fursa @wakazi Jhikoman, Vitali Maembe, @officialbabalevo kisa nao walikuwa Upinzani. Basi ningewaona bora zaidi kama mtatu-support sisi tuinuke, na sio kutumia nguvu kumshusha mwingine. Just saying....

"Two wrongs don't make it right" hata kama yeye kaongea mbovu. Na it's okay kama hum-support ILA kufanya kampeni kabisa waziwazi, we better than that.

Tasnia yetu ina matatizo mengi, ila nadhani tiba ya kwanza inabidi iwe UPENDO.

The Leader

Njia sahihi za kuongeza maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha

 


Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea wakina mama wengi kushindwa kuzalisha maziwa mengi kwa ajili ya kuwanyonyesha watoto zao. Hata hivyo kama wewe ni mama na una tatizo hilo basi unatakiwa kufanya yafuatayio ili utengeneze maziwa kwa wingi;

1. Nyonyesha mara kwa mara.Nyonyesha angalau mara nane kwa siku. Kadri unavyonyonyesha, ndivyo utatengeneza maziwa zaidi.

2.Tumia vinywaji vya kutosha na kula zaidi. Epuka kukosa mlo wowote wa siku.

3. Pumzika mara kwa mara.Iwapo baba na wanafamilia wengine watasaidia na kazi zingine za nyumbani, mama atamhudumia mtoto vizuri zaidi.

4. Hakikisha maziwa yametoka yote wakati wa kunyonyesha au unapokamua. Usiache maziwa yako kujaa kwa muda mrefu. Hata kama uko mbali na mtoto hakikisha unakamua maziwa.

5. Hakikisha mtoto amenyonya maziwa yote mara mbili kila unaponyonyesha

6. Kwa kina mama ambao hawana maziwa ya kutosha wanaweza kuongea na daktari akawaandikia dawa za kusaidia kuzalisha maziwa.

MKE WA PASTA ACHAPANA MAKONDE NA MWANAMKE MWENZAKE LIVE KANISANI


Video moja inasambaa kwenye mtandao wa kijamii ikiwaonyesha wanawake wawili wakipigana kanisani katika eneo la Umuahia, jimbo la Abia nchini Nigeria.

Kulingana na Sunday Ogirima, ambaye alichapisha video hiyo kwenye mtandao wa Facebook, kati ya wanawake hao mmoja ni mke wa pasta na muumini wa kanisa hilo. 

Ogirima ambaye anaonekana kuwa mwandishi wa habari, alisema hawezi kunyamazia kitendo hicho kwa sababu ni cha aibu na ndio maana alianika video hiyo mtandaoni.

Katika video hiyo, mwanamke aliyevalia rinda la blu ndiye mke wa pasta Akaa na anayepokezwa kichapo ni binti ya shemasi wa Kanisa la AG Worship Center.

 Ogirima alifichua kuwa sababu za wawili hao kupigana kanisani ni kwamba Bi Akaa alikuwa amepanga njama na kundi la TAG kunyakuwa kanisa hilo kimabavu lakini mume wake alikataa kushirikiana naye.

Kutokana na kuhofia, shemasi na binti yake walikwenda kufunga kanisa hilo ili kumzuia Bi Akaa kuuza kanisa hilo kwa TAG.

 Bi Akaa aliwakaripia shemasi na bintiye kwa kumzuia kuuza kanisa hilo kwa TAG na kutaka kusalia katika kundi la TST.

 Kisha baada ya kurushiana maneno, mke wa pasta alianza vita na kumtupa chini binti ya shemasi.

Via Tuko news

Sunday, May 30, 2021

Hussein Machozi ajibu madai ya kuolewa Italy







Msanii Hussein Machozi ameikataa kauli ya watu wanaomsema amefungiwa ndani na mwanamke nchini Italy huku wengine wakimwambia kwamba yeye ndio ameolewa na mwanamke huyo.


Akizungumzia hilo kupitia EATV & EA Radio Digital Hussein Machozi amesema watanzania wanapenda sana maneno hasa wakiona mtu anaishi nje ya nchi au kupata mwanamke aliyemzidi kipato.



"Watanzania wakiona mtu amepata mwanamke mwenye pesa utaambiwa umeolewa, Ben Pol aliambiwa kaolewa na mwanamke Mkenya na Dogo Janja nae aliambiwa ameolewa na Irene Uwoya, hawajui mtu ametoka nae wapi wanasema ameolewa, mimi nilienda Ulaya kwa mambo yangu" ameeleza Hussein Machozi



"Hakuna mwanaume anayeolewa wanaume wote wanaoa, Mtanzania huwa hataki kuona mtu anafanikiwa, maneno yao huwa wanayatoa  Instagram wanaamini mtu akienda Ulaya anaenda kuishi vizuri" ameongeza



Msanii huyo amekuwa akiishi nchini Italy kwa kipindi cha miaka 7 ambapo amefanikiwa kupata mwanamke na mtoto mmoja wa kike.

Wakulima ufuta watakiwa kulinda ubora

 


Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga amewataka wakulima wa ufuta,  washiriki kikamilifu kulinda na kudhibiti ubora wa ufuta ili kupata soko la uhakika.


  Ndemanga ametoa wito huo akiwa   katika kijiji cha Kilangala B, jimbo la Mchinga.


Amesema ili kulinda na kupata soko zuri,  ni vyema wakulima wakazingatia  usafi wa mazao yao. Pia  aliwataka wanunuzi wazingatie na kutekeleza kwa vitendo makubaliano,  ikiwamo kuwalipa wakulima kwa wakati kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kuhusu muda wa malipo baada ya kushinda mnada.


Ndemanga pia amekitaka chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao kuhakikisha kina vifungashio vya kutosha ili ununuzi usisimame.


Mnada huo wa kwanza ni kwa chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao, ambao ni muunganiko wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) vilivyo katika wilaya za Lindi na Kilwa.


kwa upande wake,  Mwenyekiti wa Chama kikuu Lindi Mwambao Ismail Nalinga, amesema  chama hakitawavumilia viongozi na watendaji watakaochafua soko kwa kuchanganya mchanga na ufuta.


''Ipo tabia ya baadhi ya viongozi na watendaji ya kuongeza mchanga kwenye ufuta,  hatutawavumilia na tutawachukulia  hatua za kinidhamu,'' amesema Nalinga.


Mnada wa mauzo  wa ufuta umeanza, huku  tani 1370 zikiuzwa kwa bei ya chini ya Sh2,201  na juu Sh2,345.

Idadi ya walikufa kwa kunywa pombe yenye sumu yaongezeka India


Idadi ya waliokufa kutokana na kunywa pombe yenye na sumu nchini India leo hii imeongezeka na kufikia watu 35 huku polisi ikifanya msako kabambe wa kuwasaka watuhumiwa huko jimboni Uttar Pradesh.


Wakazi pamoja na madereva wa malori katika vijini vitatu tofauti vya wilaya ya Aligharh walianza kuugua baada ya kunywa pombe hiyo, ambapo watu 23 walikufa baada ya kufikishwa hospitali mapema Ijumaa.Mbunge wa Aligarh, Satish Gautam amedai idadi ya waliokufa ni kubwa, huku akiilaumu serikali ya jimbo kwa kuficha ukweli. 


Vyombo vya habari katika maeneo hayo vimesema takribani watu 58 wamefariki.Mamia ya watu, wengi wao kutoka katika familia masikini wanakufa nchini India kila mwaka kutokana na kunywa pombe zenye sumu. Mwaka uliopita katika jimbo la jirani la Punjab watu 105 walikufa kwa kunywa pombe yenye sumu.

Idara ya uhamiaji yawasimamisha kazi Askari wake watatu kwa kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai

 


Idara ya uhamiaji imewasimamisha kazi Askari wake watatu kwa tuhuma za kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao dhidi ya Mtuhumiwa wa utapeli Alex Raphael Kyai kama ilivyoonekana katika video fupi iliyosambaa.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kulaghai na kupokea fedha kutoka kwa Wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka pia amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo TAKUKURU.

"Hatua ambazo Idara imechukua dhidi ya Askari, tumewasimamisha kazi kupisha uchunguzi wa tukio lenyewe lakini pia Mtuhumiwa tumemfikisha kwenye mamlaka husika ili aweze kuendelea na utaratibu mwingine kisheria" ——— Dr. Anna Peter Makakala, Kamishina Jenerali wa Uhamiaji. 




Waziri Wa Maliasili Na Utalii Dkt.ndumbaro Kuwashawishi Mawaziri Kujifunza Mchezo Wa Gofu


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro aahidi kutumia ushawishi wake kuwahamasisha Mawaziri wenzake pamoja wa watu kawaida  kujifunza mchezo wa gofu kufuatia ombi la Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier kufanya hivyo

Ametoa kauli hiyo jana wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa Mabalozi na Wataalamu wa nchi mbalimbali ambao ni Wachezaji na Wanachama wa Chama wa gofu nchini kufuatia kumalizika kwa mashindano ya Gofu  yaliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania yaliyofanyika Mwezi April mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

 Hafla hiyo ya utoaji zawadi kwa Wachezaji wa gofu imefanyika nyumbani kwa Balozi huyo, Mhe.Frederic Clavier  na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wataalamu mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania  ambao ni Wachezaji wa Gofu na Wanachama wa Gofu nchini Tanzania.

Amesema kufuatia ombi la Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier mbali ya kuwahasisha Mawaziri pia atawahamasisha Wabunge kujifunza mchezo huo ili kuwa timu bora ya Bunge ya mchezo wa gofu  hali itakayopelekea Wabunge hao kuendeleza mchezo huo katika majimbo waliyotoka.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Dkt.Ndumbaro amewapongeza Washiriki hao na kuwaaahidi kuendeleza mchezo huo kwa kuunganisha na utalii wa michezo ili kuhamasisha Mabalozi hao kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.

'" Nawaahidi  kuandaa mashindano mengi zaidi ya Gofu ambayo nitawashirikisha karibu  vivutio vya Utalii ili mkishacheza gofu mbajipumzisha kwa kuwa tembo na simba" alisema Ndumbaro

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier ametoa wito kwa Watanzania kujifunza mchezo wa gofu huo kwani ni mchezo kama michezo mingine

Amewatoa hofu Watanzania kuwa mchezo huo haubagui ni wa watu wote wenye kipato cha chini na cha juu na sio mchezo wa Watu wa Matajiri na Wasomi  pekee

Amesema gofu ni mchezo rahisi sana kujifunza na sio mchezo mgumu, " Jitokezeni kujifunza mchezo wa Gofu ni ajira na pia ni burudani kama ulivyo mchezo wa mpira wa miguu" alisema Mhe.Balozi Frederic Clavier

Katika hatua nyingine amempongeza Waziri Dkt. Ndumbaro kwa kuwa Mwanachama pekee wa Mchezo wa Gofu kati ya Mawaziri wote nchini Tanzania na hivyo kutoa wito kwa Mawaziri wengine kucheza mchezo huo.


KATIBU WA CHAMA CHA WASIOAMINI UWEPO WA MUNGU AJIUZULU

Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Nchini Kenya (AKS) kimepata pigo kubwa kufuatia kujiuzulu kwa katibu wao Seth Mahiga baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja unusu.

Mahiga amejiuzulu kutoka kwa wadhifa wake akisema amekutana na Yesu na hataki tena kuendelea kupiga kampeni za kumkana Mungu nchini.

Katika taarifa Jumamosi, Mei 29, 2021 rais wa chama hicho Harrison Mumia, alimtaja kama kiongozi aliyekuwa amejitolea mhanga na kumtakia kila la heri katika uhusiano wake mpya na Yesu Kristu.

"Tunamtakia Seth kila la heri katika uhusiano wake mpya na Yesu Kristu, tunamshukuru kwa kutumika chama hiki na bidii kwa zaidi ya mwaka mmoja unusu," ilisoma taarifa hiyo.

Chama hicho pia kilitangaza kuwa kiti hicho ki wazi na kuwaalika Wakenya kutuma maombi.

Chama hicho kilitangaza kuwa kiti hicho ki wazi na kuwaalika Wakenya kutuma maombi.

Kujiuzulu kwa Mahiga kulizua hisia mseto mtandaoni huku wanamtandao wengi wakimupa kongole kwa hatua hiyo.

Baadhi walimuhimiza Mumia kufuata mkondo huo wa mwangaza. Hii hapa baadhi ya maoni ambayo TUKO.co.ke imekuchagulia. Jaji Mkuu wa zamani Willy Mutunga alisema: "Rais.Endapo unategemea tu kipengee cha 32(1) cha katiba ambacho kinasema kila mtu ana haki ya kuabudu, dini, mawazo, imani na maono. Haki hii si ya kuchezea."

Maadhimisho ya wiki ya maziwa kitaifa kuanza Juni 1,2021 Jijini Tanga

Msajili wa Bodi ya maziwa nchini Dk. George Msalya amesema kuwa maadhimisho ya wiki ya maziwa ambapo Dunia huadhimisha siku hiyo kila Juni 1 na mwaka huu kitaifa yatafanyika jijini Tanga

Hayo ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari   kuelekea madhimisho ya wiki ya maziwa duniani amesema kuwa uagizaji maziwa kutoka nje ya nchi umekuwa ukiliumiza soko la ndani.

Dk.Msalya mesema  kuwa karibu bilioni 22 zimekua zikitumika katika uagizaji wa maziwa kutoka Nje na kuingia nchini kupitia taasisi zake .

Amesema kuwa suala la unywaji  maziwa kwa watanzania bado linaokena kutokua na hamasa licha ya serikali kutumia juhudi kubwa katika uhamasishaji wa matumizi ya maziwa

"Bado uelewa ni mdogo mtu badala ya kunywa maziwa wanakwenda baa kunywa pombe wakati maziwa ni muhimu kuliko hiyo pombe"amesema

Hata hivyo Dk.Msalya amewataka watanzania kuwa na uzalendo wa kutumia bidhaa za ndani za maziwa ili kuwainua wafugaji, wasindikaji na wachakataji wa bidhaa hiyo kwani zipo bidhaa nzuri za maziwa zinazotengenezwa nchini.

Dk.Msalya amesema kuwa nchi yetu bado ina uzalishaji mdogo wa maziwa kwani inazalisha Lita bilioni 3.4 ambapo ukigawanya kwa idadi ya watanzania, kila mtu atakunywa wastani wa Lita 50 tu kwa mwaka.

Amesisitiza kuwa mujibu wa wataalamu wa Afya mtu anatakiwa kunywa maziwa Lita 200 Kwa mwaka hivyo bado kuna uhitaji mkubwa wa uzalishaji zaidi wa maziwa kwani ni kinywaji muhimu Kwa Afya ya binadamu.

Aidha Dkt.Msalya amesema kuwa  tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 2005 Tanzania imepiga hatua katika uzalishaji wa maziwa kwani mwaka 2015 kushuka chini wastani kila mtu alikuwa anakunywa Lita 40 Hadi 45.

Hivyo kufikia mwaka 2015 hadi 2021 kila mtu anakunywa maziwa Lita 50 kwa mwaka ambapo katika pato la Taifa maziwa yanachangia kwa asilimia 30 huku katika sekta ya mifugo ikichangia Kwa asilimia 7.

Amesema kuwa maadhimisho hayo yatalenga katika kufanya tafiti kuhusu tasnia ya maziwa, kujifunza namna ya kufuga ng'ombe bora wa maziwa na kugawa maziwa katika makundi mahitaji kama wagonjwa katika hospitali mnalimbali.

Wiki ya Maziwa Duniani duniani ilianzishwa baada ya kugundua unywaji  ni mdogo na sasa kuamua kuipigia chapuo ili kuyapa kipaumbele ili kuboresha afya za wananchi Kauli mbinunya mwaka huu ni  "Tunywe Maziwaa ya Kwetu,Uzalishaji na Usindikaji Kazi Iendelee"

 

Jamaa Mgonjwa Atimuliwa Hospitali Baada ya Kumshika Nesi Makalio

 


Jamaa aliyekuwa akipokea matibabu katika hospitali moja eneo la Chogoria nchini Kenya amefukuzwa wodini kabla ya kupata nafuu baada ya kushindwa kula kwa macho akaishia kunyoosha mkono na kumgusa makalio nesi mkuu.


 Inasemekena ilikuwa ni mwendo wa saa mbili usiku ambapo wagonjwa wote walikuwa wamekula wakati nesi aliyekuwa zamuni alipita katikati ya wagonjwa katika wodi kuhakikisha kila mgonjwa anashughulikiwa.

Kwa mujibu wa Taifa leo, nesi huyo alikuwa amevalia sketi fupi mno bila kujali wagonjwa.


 Duru zinaarifu kuwa alipofika alikokuwa jamaa aligundua kuwa kulikuwa na mgonjwa kando yake aliyehitaji msaada. 


Alimuonesha jamaa mgongo kisha akaninama na kufaraghua sehemu yake ya nyuma iliyompagawisha na kumzuzua jamaa. Jamaa alipoona hivyo, akili zilimsimama akawaza na kuibuka na mawazo ya kumgusa nesi bila kujali matokeo yake.


"Samahani dada. Nimeshindwa kuvumilia urembo wako nikaona ni bora niguse," jamaa mgonjwa alisema. 


"Mjinga wewe! Umefaidi nini? Nyie nyinyi vibaka tunaoogopa usiku. Watakaje?" Nesi aliuliza.


 "Niwie radhi dada. Samahani sitarudia tena," jamaa alizidi kujitetea.


 "Kesho utaenda nyumbani kwa maana inaonekana haufai kuwa humu wodini. Wewe ni hatari kwa wagonjwa wengine na wafanyakazi katika hospitali hii," muuguzi mkuu alimwambia jamaa


. Siku iliyofuata mapema asubuhi, jamaa aliamuriwa kuondoka hospitalini, japo hakuwa amepona na jamaa zake walipouliza ni kwa nini waliachwa vinywa wazi walipoarifiwa kuhusu alichomfanyia nesi mkuu usiku uliotangulia. 


"Huyu ni mtu hatari kuendelea kubaki katika wodi kwa sababu anaweza kuwadhuru wagonjwa na wafanyakazi. Tamaa yake imevuka mipaka. Ondokeni naye mkamuuguze nyumbani," waliarifiwa.


 Penyenye zinasema kuwa baadhi yao walitishia kuishtaki hospitali kwa kumfukuza mgonjwa kabla ya kupona lakini naye nesi akawaambia angemshtaki kwa kumdhulumu kimapenzi.


Jamaa hakuwa na lingine ila kuchechemea akiondoka hospitalini humo, haikubainika iwapo jamaa zake walimpeleka hospitali nyingine

Saturday, May 29, 2021

Papa Francis atuma ujumbe Cologne kuchunguza unyanyasaji wa kingono





Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amewatuma wajumbe wawili kwenda katika Kanisa la Cologne, Ujerumani kuchunguza iwapo jimbo hilo lilifanya makosa katika kushughulikia kashfa za udhalilishaji wa kingono. 
Mwakilishi wa Vatican nchini Ujerumani, Nikola Eterovis amesema Papa Francis ameamuru wajumbe hao Askofu wa Stockholm, Kadinali Anders Arborelius na Askofu wa Rotterdam, Johannes van der Hende kuchunguza makosa yanayowezekana kufanywa na Askofu Mkuu wa Cologne, Rainer Maria Woelki.

 Maaskofu hao wataizuru Cologne mwezi ujao na watafanya uchunguzi wao kwa muda wa wiki mbili. Uchunguzi wa kashfa hiyo uligundua zaidi ya visa 300 vya udhalilishaji wa kingono katika kanisa dhidi ya watoto waliokuwa chini ya miaka 14 kati ya mwaka 1975 na 2018. 

Zaidi ya wanyanyasji 200 walihusika kuwadhuru watoto. Ripoti ya mwezi Machi iligundua kuwa maafisa wa kanisa walikiuka majukumu yao katika kukabiliana na visa hivyo.

Serikali kuandaa Sera itakayowawezesha Vijana kiuchumi

 


Na John Walter-Manyara

Katika kuhakikisha lengo la kukuza uchumi wa viwanda linatimia, Serikali ya Tanzania inaendelea kubuni sera na mikakati ya kukuza uwekezaji kupitia wajasiriamali wadogo.


Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Viwanda na biashara Exaud Kigahe wakati akifungua maonesho ya 16 ya SIDO kanda ya kaskazini yanayofanyika katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara.


Amesema serikali inaandaa sera mpya  ya maendeleo ya Viwanda vidogo na biashara ndogo ambayo pamoja na mambo mengine imetazama namna bora ya kuwawezesha wajasiriamali vijana kuingia katika shughuli za kiuchumi.


Aidha amesema serikali inaendelea na hatua mbalimbali za kuwawezesha wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa katika kukuza fursa za masoko kwa kuendelea kupanua wigo mpana wa masoko katika jumuiya ya Afrika Mashariki,nchi za SADC, ambapo pia kwa sasa serikali ipo katika hatua za mwisho kulipia mkataba wa eneo huru la biashara Afrika.


Amewataka wajasiriamali kutumia masoko hayo kikamilifu ili serikali ipate nguvu ya kuendelea kuwatafutia fursa zaidi.


Kagahe amesema sekta ya Viwanda na Biashara nchini imeendelea kuongeza miundombinu ya kufanyia kazi wajasiriamali wadogo katika mitaa ya viwanda vidogo vya SIDO ambapo mpaka sasa imejenga zaidi ya majengo 15 kwenye mikoa ya Manyara, Geita,Kigoma,Mtwara na Dodoma kwa ajili ya uzalishaji, kazi hiyo ni endelevu.


Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya TEMDO iliyo chini ya wizara ya Viwanda na Biashara inayohusika na utafiti,Usanifu na utengenezaji wa Teknolojia mbalimbali Mhandisi Profesa Fredrick Kahimba, amewataka wenye changamoto ya teknolojia kuwasiliana nao ili kupata msaada na biashara zao kupata tija.


Amesema katika kuwafikia wajasiriamali wadogo wanawatembelea katika mikoa mbalimbali na kupitia mtandao wa  SIDO.


Maonesho hayo ya 16 ya SIDO  yanabebwa na kauli mbiu isemayo Maendeleo ya viwanda nuru ya maendeleo kiuchumi,yanatarajiwa kufungwa mei 31,2021 na mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere.

Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo Atembelea Ubalozi Wa Tanzania- Pretoria


Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo,ametembelea Ubalozi wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Jenerali Mabeyo yupo Nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini Jenerali SZ Shoki zilizofanyika kitaifa Jana Mjini Pretoria. Kuhudhuria sherehe hizi,ni utaratibu uliowekwa  na nchi wanachama wa Jumuiya za SADC ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuimarisha  mashirikiano  hususan katika nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi (Defence Diplomacy) na Amani katika eneo Ia nchi za SADC.

Jenerali Mabeyo, alikaribishwa Ubalozini na Mhe. Balozi Mej. Jen. Gaudence Milanzi (Mst) na watumishi wa Ubalozi Mhe. Balozi Milanzi alitoa taarifa fupi ya eneo la uwakilishi ya Afrika Kusini, Botswana na Falme ya Lesotho.

Mhe. Balozi alieeza kuwa hali ya uwakilishi inaridhisha kiulinzi na kiusalama, Ubalozi umeendelea kukuza mashirikiano na nchiza eneo la uwakilishi ikiwa ni pamoja na SADC. Kwa kufuata miongozo ya sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza kuendeleza Diplomasia ya kisiasa na kutekeleza Diplomasia ya uchumi.


Upande wake Jenerali Mabeyo alielezea ziara yake kwa ujumla nchini Afrika Kusini imekuwa ni ya mafanikio, na pia kuna mambo kama ambayo kama Mkuu  wa Majeshi ameona yanafaa kuigwa ili kuboresha utendaji wa Jeshi la Tanzania.

Jenerali Mabeyo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya  Muungano  wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan, amelenga kuendeleza maendeleo ndani na nje ya nchi mfano katika kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania na mwelekeo  unaelekeza kuimarisha  Diplomasia kwa  kujenga mahusiano na nchi duniani kwa   kuimarisha Diplomasia ya siasa na Diplomasia ya uchumi.

Jenerali Mabeyo alimsihi Balozi na watumishi wa Ubalozi kuhakikisha kuwa wanaielewa na kuisimamia dira ya Diplomasia kama ilivyoainishwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ili kuweza kutelekeza majukumu yao kwa wepesi.


 



BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega (katikati) wakipongezana mara baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo jana(28.05.2021) jana katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Kulia kwao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Uvuvi nchini (TAFICO) Bi. esther Mulyila.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kushoto) akiwashukuru na kuwapongeza Viongozi, Wakuu wa idara na vitengo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge jijini Dodoma mara baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo jana (28.05.2021).

Viongozi, Wakuu wa idara na vitengo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakifuatilia hotuba ya bajeti ilivyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mashimba Ndaki juzi (27. 05. 2021) Bungeni jiini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) wakizungumza na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Christine Ishengoma (katikati) muda mfupi baada ya bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo jana (28.05.2021) jijini Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (katikati mbele), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega ( wa nne kutoka kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kutoka kulia), katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (wa nne kutoka kushoto), Wakuu wa idara na vitengo kutoka Wizara ya Mifugo na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma jana (28.05.2021).


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana (28.05.2021) lilipitisha bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyolenga kutekeleza vipaumbele 13 kwa sekta zote mbili za Mifugo na Uvuvi.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo ambapo baadhi ya wabunge walitaka kupata ufafanuzi wa baadhi ya masuala yanayohusu sekta hizo mbili ikiwa ni pamoja na kutaka kujua namna Wizara hiyo ilivyojipanga kuendelea kushughulikia changamoto za wafugaji na wavuvi.

Akizungumza wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai mbali na kuishauri Serikali kuibinafsisha kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ili kuongeza ufanisi zaidi, aliwapongeza viongozi na watendaji wa Wizara hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuimarisha sekta za Mifugo na Uvuvi nchini.

"Kuongoza na kuiendesha Wizara hii sio rahisi kwa sababu inashughulikia kundi kubwa sana la Wananchi na ni miongoni mwa Wizara iliyozalisha ajira nyingi zaidi na ndio maana kutokana na umuhimu wake niliona ni vizuri tuijadili kwa mapana zaidi" Alisisitiza Ndugai.

Ndugai alisema kuwa Bunge lake limekubali kupitisha kiasi chote cha fedha kilichoombwa na Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa sababu linaamini kuwa kama Serikali ikifanya uwekezaji kwenye Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi changamoto ya ukosefu wa ajira kwa Watanzania itapungua kwa kiasi kikubwa na hatimaye kumalizika kabisa.

Awali akianisha maeneo ya kipaumbele ambayo Wizara yake imejipanga kutekeleza kwa mwaka ujao wa fedha kwa upande wa Sekta ya Mifugo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki alisema kuwa Wizara yake imejipanga kuboresha na kutafuta masoko ya mifugo na mazao yake, kuboresha kosaafu za mifugo,kuboresha malisho na upatikanaji wa maji na vyakula vya mifugo.

"Mhe. Spika Wizara yetu pia kwa mwaka wa fedha ujao imedhamiria kuendelea kuimarisha afya ya mifugo, kuwezesha utafiti na mafunzo ya ugani na kutekeleza mpango wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe na kopa mbuzi lipa mbuzi" Aliongeza Ndaki.

Akianisha maeneo ya vipaumbele ambayo Wizara yake imejipanga kuyatekeleza kwa upande wa sekta ya Uvuvi, Ndaki alisema kuwa kwa mwaka ujao wa fedha Wizara imejipanga kujenga bandari ya uvuvi na kununua meli tatu za uvuvi, kuimarisha mialo, masoko, vichanja vya kukaushia samaki, maghala ya ubaridi na mitambo ya barafu, kuweka mazingira wezeshi kwenye uvuvi wa bahari kuu na kuanzisha mashamba darasa ya ufugaji samaki katika Halmashauri 40 kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI.

"Mhe. Spika kwa upande wa sekta ya Uvuvi pia tunakusudia kuongeza uzalishaji wa vifaranga na chakula cha samaki, kuimarisha ulinzi shirikishi na matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi nchini na kuweka mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya utambuzi wa maeneo ya mavuvi" Aliongeza Ndaki.

Bunge limepitisha jumla ya shilingi Bil. 47. 8 zilizoombwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa upande wa sekta ya Mifugo na shilingi Bil. 121. 4 ambazo zitatumika kwa upande wa sekta ya Uvuvi kwa mwaka ujao wa fedha 2021/2022.

WAJASIRIAMALI WAASWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE BORA


Wajasiriamali kote nchini wameaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na kimataifa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya SIDO kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Kwaraa Babati mkoani Manyara.

Naye Meneja wa Uthibiti Ubora wa TBS Bw.Gervas Mwanjabala akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo, alisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya TBS kutoa elimu ya masuala ya viwango kwa wajasiriamali waliokusanyika kutoka sehemu mbalimbali nchini na vilevile n fursa ya kusikiliza maoni na changamoto za wajasiriamali na wananchi kwa ujumla na kutafutia ufumbuzi changamoto hizo.

. "Ushiriki katika haya maonesho umetufanya tuweze kukutana na wadau wenye viwanda,wananchi, wajasiriamali na kuweza kuwaelimisha kuhusu masuala ya viwango pamoja na kusikiliza changamoto zao". Amesema Bw. Mwanjabala.

Aidha Meneja wa kanda ya kaskazini wa TBS, Bi. Happy Brown aliwataka wajasiriamali wote katika kanda hiyo kutosita kutoa taarifa zozote ili waweze kusaidiwa na hata kupatiwa ushauri wa kitaalam ili waweze kuzalisha bidhaaa bora.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa TBS Bi. Deborah Haule amesema muitikio wa watu katika maonesho haya umekuwa mkubwa na wajasiriamali wengi wamejitokeza kutaka kufahamu zaidi kuhusiana na taratibu za kufuata ili kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.

Amesema wajasiriamali wadogo nchini hawaingii gharama zozote bali wanatakiwa kupitia SIDO ili watambulike na wakipata alama ya ubora wanaweza kufikia masoko mbalimbali hasa ya Afrika Mashariki na zitaweza kuvuka mipaka ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote.

Pamoja na hayo Bi. Deborah amesema TBS inawahimiza wahakikishe wanazalisha bidhaa zilizo na ubora hatua itakayosaidia kulinda mitaji yao na kuhimili ushindani kwenye soko la kitaifa na kimataifa.
  

Waziri Ummy Ameagiza Kusimamishwa Kazi Kwa Wakuu Wa Idara Wanne Kupisha Uchunguzi




Angela Msimbira, SHINYANGA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza kusimamishwa kazi wakuu wa Idara Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushindwa kusimamia kwa weledi ukamilishaji wa ujenzi wa Machinjio ya kisasa iliyopo Ndembezi mjini Shinyanga ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili.

Akikagua mradi huo jana katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga Waziri Ummy amesema kuwa amewasimamisha kazi wakuu hao wa idara kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kumshauri Mkurugenzi kuhusu mradi huo na kushindwa kusimamia ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

Amewataja waliosimamishwa kupisha uchunguzi kuwa ni aliyekuwa Kaimu Afisa Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji Bw. Gwakisa Mwaisyeba, Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Tito Kagize, Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Kassim Thadeo na Mkuu wa Kitengo cha manunuzi Bw.Godfrey Mwangailo na amemuagiza Mkuu wa Mkoa Bw.Dkt Philemon Sengati kuhakikisha anaunda tume itakayochunguza ubadhilifu wa fedha ambao umesababisha kusuasua kwa ujenzi wa Machinjio hiyo.

Waziri Ummy amesema kutokamilika kwa Mradi wa Machinjio ni aibu kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na inarudisha nyuma maendeleo ya Manispaa hiyo.

'Ukamilishaji wa machinjio hii kutasaidia kuongeza mapato ya wananchi na Halmashauri kwa ujumla kwa kuwa Halmashauri ikikusanya mapato itaweza kutatua changamoto katika Sekta ya Afya, Elimu na miundombinu ya barabara' alisema

Mbali na kuwasimamisha Wakuu hao wa Idara pia ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwaandikia barua Mkandarasi wa mradi huo , Kampuni ya Home Africa pamoja na Mhandisi mshauri B.J Amour nao wapelekwe bodi ya Mkandarasi ili iwawajibishe.

" Mradi huu haukusimamiwa vizuri na tunawatesa watu wa shinyanga mpaka leo haujakamilika na fedha hazionekani, kuna shilingi milioni 800 zimelipwa kwa wakandarasi bila kuhakikiwa wala kujiridhisha. Huu mradi ni aibu kwa Shinyanga kwa hiyo nawasimamisha kazi kwa wiki mbili ili wapishe uchunguzi" amesema Waziri Ummy

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema kuwa mradi huo ulitengewa kiasi cha shilingi bilioni 5.7 lakini hadi sasa zimetumika kiasi cha shilingi bilioni 5.1 na shilingi milioni 600 hazijulikani zilipo wakati mradi haujakamilika, amesisitiza kuwa katika ripoti ya mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ilieleza kuna ufisadi na mradi haukukamilika vizuri.

Hatua hiyo ya Waziri Ummy imekuja baada ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila kueleza kuwa kamati ya fedha ya halmashauri hiyo kupitia baraza la madiwani walikuwa wameanza kuchukua hatua baada ya kubaini kuwa thamani ya fedha katika mradi huo hairidhishi, huku akibainisha kuwa kupitia vyanzo vya ndani watatenga shilingi milioni 172 kwa ajili ya kukamilisha machinjio hiyo.

Machinjio hiyo ilianza kujengwa mwaka 2018 na ilitazamiwa kukamilika mwaka2019 na kuanza kutoa huduma lakini maendeleo yake yamekuwa yakisuasua na kusababisha baadhi ya viongozi kuilalamikia.

Mawaziri Sekta Ya Biashara EAC Wakubaliana Kuondoa Vikwazo Visivyo Vya Kibiashara


Na mwandishi wetu, Arusha
Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) la Jumuiya ya Afrika Mashariki lakubaliana kuondoa vikwazo visivyo vya kibiashara na kuimarisha biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya hiyo.

Awali akifungua mkutano Jijini Arusha jana Ijumaa, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani utawawezesha mawaziri kupitia na kujadili miongozo ambayo itasaidia kuboresha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo kuondoa vikwazo visivyo vya kibiashara. 

Aidha, Mhandisi Mlote ameongeza kuwa, kwa kuzingatia kanuni na sheria ya Afrika Mashariki, vikwazo visivyo vya kibiasha baina ya nchi na nchi vimekuwa vikizuia ukuaji wa biashara hivyo ni muhimu kupitia mkutano wa baraza la mawaziri kuangalia namna ya kuviondoa ili kuwezesha ukuaji wa biashara ndani ya jumuiya.

Nae Waziri wa Viwanda na Biashara, na Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana mambo mengi ya msingi ikiwemo kuendelea kuondoa vikwazo vya biashara visivyo vya kikodi.

"Tumezungumza pia kuhusu ushiriki wetu katika kufanya biashara na Uingereza kwa kuzingatia kuwa Uingereza siyo sehemu Jumuiya ya Ulaya, lakini pia tumezungumzia suala la EAC kujiunga na jumuiya ya biashara ya Afrika ambayo sisi Tanzania tupo katika hatua kadhaa na kuona kuwa na sisi tunajiunga na jumuiya hiyo mwaka huu," Amesema Prof. Mkumbo

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe amesema kuwa mawaziri wamekubaliana kutoa msukumo wa biashara katika jumuiya ya afrika mashariki lizingatiwe na kupea kipaombele na kuruhusu sekta binafsi kufanya biashara katika nchi mbalimbali.

"Pamoja na mambo mengine, pi tumekubaliana kuondoa vikwazo visivyo vya kiushuru (Non-tarrif barriers) viondolewe kwani vimekuwa vikikwamisha biashara bila sababu za msingi, na kuangalia jinsi ya kuwekeza kwenye eneo la uwekezaji ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa na mikakati ya pamoja ya kuvutia wawekezaji" amesema Mhe. Mwambe   

Miongoni mwa maeneo yaliyojadiliwa ni pamoja na maamuzi ya ripoti ya mawaziri wa fedha, ripoti ya kamati ya forodha, ripoti ya kamati ya biashara, ripoti ya kamati ya viwango ya Afrika Mashariki, ripoti juu ya masuala ya ushindani pamoja na ripoti ya kamati ya uwekezaji.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Kenya Mhe. Betty Maina, Waziri wa Viwanda na Biashara, – Tanzania, Prof. Kitila Mkumbo,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban.

Wengine ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Mhe. Beata Habyarimana, Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushirika wa Uganda, Mhe. Grace Choda, pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Uchukuzi, Viwanda na Utalii wa Burundi, Balozi Jeremie Banigwaninzigo.

Mkutano huu ni maelekezo ya Wakuu wa Nchi na Serikali katika ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini Kenya tarehe 04 hadi 05 Mei, 2021.



Mwenyekiti wa Ccm ahukumiwa kwa kupokea Rushwa

Na John Walter-Manyara

Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Simon Kobelo amemhukumu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Maisaka Kati Mjini Babati, Bakari Khatibu Yangu kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya laki tatu kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mwinjilisti wa Kanisa la KKKT mtaa wa Komoto Daniel Jacob Tango.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu ameyasema hayo mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Makungu amesema Mwenyekiti huyo  ameingia h
atiani baada ya kukiri makosa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Amesema alitenda kosa hilo ili amwachie mwinjilisti huyo kiwanja ambacho Mwenyekiti huyo alikuwa akidai ni mali ya CCM.

Amesema awali, kesi hiyo namba CC 24/2020 ilifikishwa katika mahakama hiyo na mawakili wa TAKUKURU Martin Makani na Evelyne Onditi, Juni 26 mwaka 2020 ambapo mshtakiwa alikana mashtaka yake.

"Baada ya kukana makosa yake mawakili wa TAKUKURU waliwasilisha vielelezo na ushahidi ulioiwezesha Mahakama kumwona mshtakiwa ana kesi ya kujibu mashtaka baada ya kutakiwa kujitetea aliamua kutoisumbua mahakama kwa kukiri makosa yake yote ya kuomba na kupokea rushwa kama alivyoshtakiwa," amesema Makungu.

Amesema baada ya kukiri makosa yake Mahakama ikatoa ikatoa adhabu kwa mujibu wa kifungu cha 15 (2) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 ambapo mshtakiwa Yangu aliweza kulipa faini hiyo ya shilingi laki tatu na hivyo kukwepa kifungo cha miaka miwili kwenda jela.

"Tunatumaini kuwa hukumu hii itakuwa fundisho kwa viongozi ndani ya chama tawala hasa wa ngazi ya chini wenye utajiri wa fikra haba wanapopitapita na kuwaaminisha wananchi kuwa hawawezi kuguswa na TAKUKURU kwa sababu ni chama kilichowaajiri na kinaongoza Serikali," amesema Makungu.

Ametoa rai kwa viongozi wa aina hiyo wakumbuke  kuwa ibara ya 13 (1) ( 5) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza usawa mbele ya sheria kwa watu wote bila kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini jinsia na hali yao ya kimaisha.

Faida Zitokanazo na Kutumia Ukwaju

 


Ukwaju ni tunda maarufu sana ambalo hupatikana katika maeneo yenye uoto wa kitropiki. Kwa kingereza hujulikana kama tamarind, na kwa kitaalamu (botanical name) huitwa tamarindus indica, waarabu huita tamru alhind. Katika baadhi ya maeneo hutumiwa kama kiungo katika mboga.


Ukwaju umetunukiwa viambata muhimu na madini ambayo ni muhimu sana kwa mustakabali wa afya zetu. Una viambata kama calcium, vitamin C, copper, phosphorus, madini ya chuma, magniziam, na pyridoxine. Wataalamu wa afya wanasema kila gramu 100 za ukwaju kuna 36%za thiamin, 35% Iron, 23% magnesium ,na 16%phosphoras.

Pia ukwaju una kiwango kikubwa cha tartic acid Ma citric acid.


Namna ya kuutumia ukwaju, tengeza juisi nzuri ya ukwaju, tumia kama kiungo katika chakula, unaweza kutafuna majani yake yenye ladha ya chumvichumvu, au kuyakausha majani ya mkwaju kivulini na kuweka katika uji, au supu au juisi ya matunda.


Zifuatazo ni faida zitokanazo na matumizi sahihi ya ukwaju;

1. Husaidia kuongeza uwezo wa macho kuona (improving eyesight). Matumizi ya ukwaju kwa kula au kutumia kama juisi huondoa matatizo ya macho na kukufanya uwe na macho yenye afya.


2. Husaidia kwa wenye kisukari, kwa sababu ukwaju unaviambata muhimu kama polyphenols na flavonoids ambavyo ni madhubuti katika kurekebisha sukari mwilini na kupunguza vitambi.


3. Husaidia kwa wenye shinikizo la damu unashauriwa kunywa juisi ya ukwaju Mara kwa mara. Kwasababu ukwaju hupunguza kiwango kikubwa cha lehemu mwilini (cholesterol). Pia unakiwango kikubwa cha madini ya potasiam licha ya hayo ukwaju unafaida ya kusafisha damu.


4. Huondoa tatizo la nywele kukatika, na kuzipa mng'aro halisi, chemsha ukwaju, kisha tumia maji yake, changanya na vijiko viwili vya bizari, oshea nywele zako. Kisha ziache nusu saa na uzioshe kwa maji ya vuguvugu.


5. Kuboresha mfumo wa mmeng 'enyo na kuondoa gesi, tumia juisi ya ukwaju.


6. Mengineyo ni kupunguza uzito


7. Kuboresha ngozi yako

JAMAA ACHOMA MOTO NYUMBA YA MAMA MKWE BAADA YA MKE WAKE KUMTOROKA

Maafisa wa polisi eneo la Kiminini kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya wanamsaka jamaa mmoja mwenye umri wa makamo aitwaye Amos Wanjala ambaye anadaiwa kuvamia makazi ya mamake mkwe na kuchoma malazi yake.

Inaelezwa kuwa Amos Wanjala alitekeleza kitendo hicho baada ya mkewe kumtoroka.

Akiwa mwenye ghadhabu, Wanjala alivamia boma la Mercyline Wanyama Alhamisi, Mei 28,2021 mwendo wa saa tano usiku, alimuasha mama mkwe na kisha kuchoma malazi na baadhi ya nguo zake.

Mama huyo alisema alipoteza mali inayogharimu zaidi ya KSh 6,000 kwenye mkasa huo na hadi kwa sasa anashangaa ni nini kilichomfanya mkwe wake kumvamia.

Mshukiwa anasemekana kumtishia maisha mama huyo, hii ni kulingana na OCPD wa Kiminini Francis Tumbo.

Tumbo alisema mshukiwa akikamatwa, atashtakiwa kwa uharibifu wa mali na pia kumtishia maisha mama huyo.

"Akishakamatwa, atashtakiwa kwa kosa la kuharibu mali," OCPD huyo alisema.

Kwa mujibu wa taarifa za The Standard, mkaaji mmoja aliyetambulika kama Juma Barasa ametaka mshukiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kutokana na kukiuka mila.

"Ni kinyume na ukoo wa Wabukusu kwa mtu yeyote kuwashambulia wakwe zake ama kuharibu mali yao," Barasa alisema.

Mmoja wa majirani amesema kwamba Wanjala atapigwa faini ya mbuzi ambayo itachinjwa kwenye sherehe ya utakaso.

Chanzo - Tuko news
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...