Menya embe bichi, likate vipande na kuviweka katika chombo, au tengeneza juice changanya na unga wa pilipili manga pamoja na asali, kisha tafuna vipande hivyo vyenye mchanganyiko huo.
Mchanganyiko wako utategemea kiwango cha vipande vya embe lako. Hata hivyo, usile zaidi ya embe mbili kwa kutwa moja. Endelea na tiba hii muda wa siku tatu.
Kuharisha ni kitendo cha kujisaidia kinyesi chenye majimaji mara kwa mara. Hali hiyo hutokea baada ya utumbo mdogo kuwa na maji mengi ambayo yanashindwa kutoka mwiilini kwa njia za kawaida kama ya mkojo na jasho hivyo yanatelemka kwenye utumbo mkubwa usio na uwezo wa kutunza maji.
Yakiwa huko mtu hujikuta anajisikia hali ya kutoa haja na ndipo maji hayo hutoka kupitia haja kubwa. Kimsingi utumbo mdogo una uwezo wa kupokea zaidi ya lita nane za maji kutoka kwenye vyakula au vinywaji vinavyopitia mdomoni na mengine kutoka sehemu mbalimbali katika mwili.
Tatizo la kuhara linaweza kusababishwa na kula kupita kiasi, kula mchanganyiko wa vyakula vya aina mbalimbali, kuwa na hofu, hasira au wasiwasi, kuchacha chakula ndani ya tumbo, kula sumu, bakteria, virusi au vijidudu wenye vimelea.