Monday, May 31, 2021
Prof. Mkumbo: Serikali Inaendelea Kuboresha Mazingira Ya Biashara Mpakani, Wafanyabiasha Zingatieni Sheria Na Taratibu Za Kufanya Biashara.
Na Eliud Rwechungura
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (Mb) amewahakikishia Wafanyabiashara kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ili kuhakikisha wanafanikiwa huku akiwahasa wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya kuzingazia Sheria na taratibu zilizowekwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuondokana na vikwazo ambavyo vimekuwa vikiwekwa kutoka na kutozingatia Sheria na taratibu za kufanya biashara mipakani.
Prof. Mkumbo ameyasema hayo 30 Mei 2021 alipoambatana na Mawaziri wa Kenya na Tanzania kutembelea Mpaka wa Namanga kujionea jinsi biashara na shughuli za upitishaji wa bidhaa na huduma zinafavyofanyika katika Mpaka huo baada ya nchi hizo kukubalina kuondoa vikwazo 30 vya biashara visivyokuwa vya kiushuru.
"Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anataka kuona Maisha ya Watanzania yanaboreka na biashara zinafanyika vizuri, niwahakikishie wafanyabiashara wa Watanzania, Serikali yenu ipo na nyie na itaendelea kuwaunga mkono na kuwapa msaada ili kuona mnafanikiwa lakini kwa upande wenu tunaomba katika kufanya kwenu biashara mzingatie sheria na taratibu zilizopo kwasababu nchi zetu zinaongozwa na utawala wa sheria" ameeleza Prof. Mkumbo
Ameongeza kuwa, lengo la ziara hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Waheshimiwa Marais wa Tanzania na Kenya ya kuhakikisha mahusiano ya wananchi wa nchi mbili yanaboreka lakini muhimu Zaidi biashara hazikwami ndo maana wamekutana Mawaziri kutatua mambo mengi yaliyokuwa yanakwamisha biashara ikiwemo changamoto ya mahindi hapa mpakani wameweza kuizungumzia na anashukuru imetatuliwa na mambo mengine mengi yalikuwepo pande zote mbili za Tanzania na Kenya.
Aidha, Prof. Mkumbo amewapongeza wataalam wa pande zote mbili za Tanzania na Kenya kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya huku akiwahasa kuendelea kuimalisha mahusiano mazuri kwa kukaa Pamoja na kujadiliana kwa kuzitatua changamoto kwasababu ni jambo kubwa na la muhimu viongozi wetu wanalotaka kuliona
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Wajasiliamali nchini Kenya Mhe. Betty Maina amefurahishwa na kuona changamoto 30 kati ya 64 zimetatuliwa na hizo nyingine zilizobaki wamejiwekea muda wa miezi mitatu kuzifanyia kazi huku akiwataka wafanyabiashara wa pande mbili kuendelea kuzingatia sheria ambazo zimewekwa kwa pande zote mbili za Kenya Tanzania wakati wa ufanyaji biashara.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...