Friday, April 30, 2021

Kilimo cha Mchicha

 

Mchicha ni mboga za majani ambazo zina faida lukuki katika miili yetu. Ukiachilia mbali faida hizo pia kilimo cha mchicha kina faida lukuki hasa pale mtu anapoamua kujiweza katika kilimo hiki. Kilimo hiki ni kizuri kwa sababu huwa hakichukui muda mwingi katika upandaji hadi uvunaji.

Hali ya hewa na udongo kwa  kwa ajili ya ulimaji wa kilimo hiki.

Mchicha unahitaji maji ya kutosha katika kipindi chake chote cha ukuaji hadi kuvuna. Vilevile mchicha huhitaji udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye kuhifadhi maji.

Utayarishaji wa shamba.
Tengeneza shamba la mchicha kwa kutifua ardhi na kulainisha udongo wenye kina cha sentimeta thelathini. Weka mbolea ya samadi debe moja katika kila mita moja ya mraba. Panda mchicha katika matuta yenye upana wa 90cm-100cm.

Aina za mbegu
Amaranthus hybridus huu ni mchicha wenye majani mekundu na mbegu zake ni nyeusi.
Amarantus africana ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni ni nyeusi.
Amaranthus hypochondriacus ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni njano hasa mbegu zake hutumika kutengeneza uji wa watoto wachanga.
Amaranthus dubius ni mchicha wa kienyeji na Aspinosus ni mchicha wenye miba mingi.

Upandaji
Mchicha upandwe katika tuta kwa mistari yenye nafasi ya sentimita thelathini.
Funika mbegu kwa kutumia udongo uliolaini na tandaza nyasi kavu baada ya kupanda ili kutunza unyevunyevu na toa matandazo baada ya siku tatu hadi tano tangu siku ya kupanda.
Pandikiza mchicha kwa nafasi ya sentimeta kumi na tano kwa ishirini.
Mwagilia maji ya kutosha.

Namna ya kukuzia.
Tumia mbolea ya samadi iliyolowekwa kwenye maji kwa muda wa masaa ishirini na nne kumwagilia mchicha wako ili kupata mavuno mengi zaidi. Tumia kiasi cha debe moja kwa kila mita moja ya mraba.

Namna ya kudhibiti wadudu waaribifu.
Adui mkubwa wa mchicha ni wadudu aina ya mafuta au kitaalamu zaidi huitwa spinach aphids ambao hufyonza utomvu wa mchicha na kusababisha majani kujikunja , mchicha kusinyaa na kunyauka. Kudhibiti wadudu hawa mwagilia mchicha wako kutumia chombo kinachotoa maji mithili ya mvua kitaalamu kinaitwa "watering can" ili kuwadondosha wadudu hao.

Wadudu wengine ni kitambazi ambacho hula majani ndani kwa ndani hivyo tumia mwarobani kunyunyuzia majani ili kuwaua wadudu hao waharibifu.

Mavuno
Mchicha huwa tayari kuvunwa baada ya majuma 3 hadi 6 tangu kupandwa au kupandikizwa. Uvunaji huweza kuendelea kwa muda wa miezi 2 hadi 3 kutegemeana na namna utakavyoamua kuuvuna mchicha wako.

Kiasi cha mavuno
Kila mita moja ya mraba huzalisha kiasi cha 4kg hadi 5kg za mchicha. Hii inamaanisha kuwa utapata kiasi cha tani 20 hadi 40 kwa hekta moja ya mchicha.

Harmonize achora Tattoo ya Hayati Magufuli


 Msanii Harmonize ambaye anafanya vizuri kwasasa ndani na nje ya Afrika kupitia wimbo wake 'Attitude' huenda akawa anamkumbuka Hayati Magufuli kwa staili ya pekee kwani amechora tattoo ya sura yake mguuni kwake.

Harmonize ama Jeshi ameichora tattoo hiyo kwenye mguu wake wa kulia akiwa Lagos nchini Nigeria, ikiambatishwa na nukuu ya maneno ambayo Hayati Magufuli alikuwa akipenda kuyatumia "Nime Sacrifice Maisha yangu kwaajili ya Watanzania Masikini"

Harmonize_tz ni mmoja wa wasanii pendwa wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano nchini Tanzania Hayati John Pombe Magufuli, aliwahi kumtaka agombee Ubunge wa jimbo la Tandahimba.

Hayati JPM alifariki dunia Machi 17, 2021. Daima tutamkumbuka.


SIMBA SC KUCHAPANA NA KAIZER CHIEFS YA AFRIKA KUSINI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


Timu ya Simba SC ya Tanzania itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya droo iliyopangwa leo Jijini Cairo nchini Misri.

Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri nao watamenyana na wapinzani kutoka Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.

Mshambuliaji Mtanzania, Simon Happygod Msuva yeye timu yake, Wydad Casablanca itamenyana na MC Alger ya Algeria. CR Belouizdad ya Algeria pia yenyewe itamenyana na vigogo wengine wa Afrika, Esperance ya Tunisia.

Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 14 na 15 na marudiano ni Mei 21 na 22, Simba SC wakianzia nyumbani Dar es Salaam.

ROBO FAINALI
Al Ahly vs Mamelodi Sundowns.
MC Alger vs Wydad Casablanca.
CR Belouizdad vs Esperance.
Kaizer Chiefs vs Simba SC.

NUSU FAINALI
MC Alger / Wydad Casablanca VS Kaizer Chiefs / Simba SC.
CR Belouizdad / Esperance VS Al Ahly / Mamelod Sundowns.

Via Binzubeiry blog

Meli ya kubeba ndege ya China yapitia mpaka wa Japan


Meli ya kubeba ndege ya Wachina "Liaoning" ilipita kati ya mkoa wa kusini mwa Japan wa Okinawa na kisiwa cha Miyakojima.

Kulingana na taarifa ya shirika la habari la umma la Japan NHK kwa kuzingatia vyanzo vya Wizara ya Ulinzi, iliarifiwa kwamba meli ya Liaoning ilisafiri karibu na Okinawa, kusini mwa Japan, ikiongozana na meli 5.

Ikipita kati ya mkoa wa kusini wa Okinawa na kisiwa cha Miyakojima, meli ya Liaoning ilielekea kaskazini na kuingia Bahari ya China Mashariki, kwa mujibu wa taarifa ya Kikosi cha Ulinzi wa Bahari (MSDF).

Wakati wa msafara wa meli za kijeshi, Japan haikukiuka sheria za mipaka ya bahari ya eneo hilo.

Sheria ambayo ilianza kutumika nchini China mnamo Februari 1, inampa mamlaka mlinzi wake wa pwani kutumia silaha dhidi ya meli za kigeni ambazo hazizingatii sheria.

Shirika la Kyodo lilisema kwamba sheria hii inaidhinisha China kulenga meli za Japan zinazozunguka Visiwa vya Senkaku vinavyozozaniwa katika Bahari ya China Mashariki.

Visiwa vya Mashariki mwa Bahari ya China, ambayo Japan inaita "Senkaku" na China inaita "Diaoyu", ina visiwa 5 na miamba 3.

MANISPAA YA SHINYANGA KUANZISHA MASHINDANO YA USAFI WA MAZINGIRA

 

Mkuu wa idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Kuchibanda Snatus, akisoma taarifa ya mpango wa kuanzisha mashindano ya usafi wa mazingira kwenye Baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi. Picha zote na Marco Maduhu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.

***
Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, inatarajia kuanzisha mashindano ya usafi wa mazingira, kwa ajili ya kuuweka mji huo katika hali ya usafi, pamoja na kupambana na magonjwa yatokanayo na uchafu kikiwemo kipindupindu.

Akisoma taarifa ya mpango huo leo wa kuanzisha mashindano ya usafi wa mazingira, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga, Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa hiyo Kuchibanda Snatus, kwa niaba ya Mkurugenzi, alisema lengo la mashindano hayo ni kuhakikisha mji unakuwa safi muda wote.

Alisema mashindano hayo yatajumuisha kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga, Mitaa 55, vijiji 17, Taasisi zote za umma, na binafsi, zikiwamo Shule za Msingi na Sekondari, Masoko, viwanda, ambayo yanatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

"Maeneo yatakayokaguliwa kwenye mashindano hayo ni usafi wa Kaya, Shule, Masoko, Mitaro, Barabara, Viwanda, na Maeneo ya wazi na utekelezaji utasimamiwa na viongozi wa Serikali za vijiji, mitaa na Kata, kwa kufanya ukaguzi wa usafi wa mazingira kwenye maeneo yote,"alisema Snatus.

"Mshindi wa mashindano haya ngazi ya Kaya na Shule atapewa zawadi ya vifaa vya usafi, Kiwanda na Kata itakayo ongoza watapewa Ngao, Mtaa utapewa Cheti, na watakaofanya vibaya watapewa Kinyago,"aliongeza.

Aidha alisema faida za mashindano hayo ni kuboresha hali ya usafi wa mazingira kwenye maeneo mbalimbali ya Manispaa, kupunguza madharia ya Mbu, pamoja na kutokomeza magonjwa ya kuhara na kipindupindu.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, alisema mpango huo ni mzuri na utasaidia kuondoa kero za uchafu mjini Shinyanga, ambapo mji utakuwa msafi pamoja na kuzolewa uchafu wa kwenye Maghuba kwa wakati, huku akitoa wito kwa madiwani wakatoe elimu ya usafi kwa wananchi.

Nao Madiwani wa Manispaa hiyo ya Shinyanga, walipongeza mpango huo wa mashindano ya usafi wa mazingira kuwa utaleta hamasa kubwa ya kuufanya mji huo kuwa msafi huku kila mmoja akijingamba kupata ushindi.

Pia Baraza hilo la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, limefanya kikao cha siku mbili kujadili ajenda mbalimbali, kwa ajili ya mstakabali wa maendeleo ya Manispaa hiyo.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Bwalya: Tutafanya Maajabu Kimataifa… Droo Ya CAF Leo




KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Larry Bwalya amesema kuwa timu hiyo ina nafasi kubwa ya kufanya maajabu katika Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo inatarajiwa kupangwa leo Ijumaa.

 

Bwalya alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu baada ya kiwango chake kufurahishwa na mabosi wa timu hiyo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaakuelekea kwa droo hiyo ambapo Simba ndiyo itajua mpinzani wake, Bwalya alisema: "Imekuwa heshima kwangu na timu pia kuona tunafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya kimataifa.



"Kwa sasa tunasubiri ratiba na timu ambayo tutacheza nayo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

"Bado tunayo nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kutokana na maandalizi mbalimbali ambayo tunaendelea kufanya, " alisema Bwalya.

 

Katika droo ya leo Simba inatarajiwa kupangwa na wapinzani kati ya hawa, CR Belouizdad au MC Alger zote za Algeria au Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini

Stori: Leen Essau,Dar es Salaam

DANIEL CHONGOLO KATIBU MKUU WA CCM, SHAKA ACHUKUA NAFASI YA HUMPHREY POLEPOLE


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya viongozi wake wakuu kitaifa ikiwemo nafasi ya Katibu Mkuu iliyokuwa inashikiliwa na Bashiru Ally pamoja na nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi iliyokuwa inashikiliwa na Hamphrey Polepole.

Katika Mabadiliko hayo, CCM imempitisha Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu Mpya wa chama hicho, huku nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ikichukuliwa na Shaka Hamdu Shaka.

Breaking : LAZARO NYALANDU AIKACHA CHADEMA NA KUREJEA CCM


Lazaro Nyalandu akitangaza kurejea CCM leo
**
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu ametangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) akisema ameamua kurejea nyumbani na kwamba Wimbo wa bwana hauimbiki katika nchi ya ugenini.

Nyalandu ametangaza kurejea CCM leo Ijumaa Aprili 30,2021 wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi Dodoma.

Mara baada ya kutangaza uamuzi wake huo mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais  Samia Suluhu Hassan katika mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma,Nyalandu ametoa shukrani zake kwa Mwenyekiti wa chama hicho kumpokea ,kumsamehe na kumruhusu kumrejesha katika chama hicho.


"Ninampongeza rais kwa uongozi wako shupavu. Nakushukuru kwa kukubali kunipokea na kunisamehe pamoja na kuniruhusu kurejea chamani. Hakuna furaha izidiyo furaha ya mtoto arejeapo nyumbani. Wimbo wa bwana hauimbiki katika nchi ya ugenini, Mzee Sumaye , Lowassa na Dk Slaa ni mashahidi wa hilo", amesema Nyalandu.

Nyalandu ambaye ni Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya awamu ya nne alijitoa CCM Oktoba 30, 2017 na baadaye alijiunga CHADEMA ambako alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati.

Nyalandu alichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa tiketi ya CHADEMA, Lazaro Samwel Nyalandu hata hivyo aliangushwa na Tundu Lissu.

LIVE: Mkutano Mkuu Maalum Wa CCM, Dodoma

 LIVE: Mkutano Mkuu Maalum Wa CCM, Dodoma



Thursday, April 29, 2021

Namna ya kujitibu tatizo la kutokwa na damu puani

 

Kutokwa na damu puani ni jambo la kawaida sana kwa kila mtu na mara nyingi huwa sio hatari sana isipokuwa kama linaambatana na dalili nyingine hatari. Tatizo ili huweza kusababishwa na kuumia ndani au nje ya pua, kuchokonoa pua mara kwa mara, shinikizo la damu, matumizi dawa za aspirini, ukosefu wa vitamini K, pombe kupita kiasi, na mabadiliko ya hormoni kwa wajawazito.

Jinsi ya kujitibu tatizo hili;
1. Simama wima na inamisha kichwa kwa mbele, kusimama itakusaidi kupunguza kasi na presha   katika mishipa ya damu puani wakati unapoinamisha kichwa kwa mbele huzuia kumeza damu ambayo italeta shida tumboni.

2. Weka pamba au kitambaa chenye uwezo wa kufyonza damu nje ya pua na bana pua kwa muda wa dakika 15 huku ukitumia mdomo kupumua, kubana pua hurudisha damu katika mishipa ya pua na kuzuia kuvuja.

3. Kuzuia damu isitoke tena usichokonoe pua wala kuinamisha kichwa mbele kwa nguvu na kwa muda mrefu.

4. Kama damu inaendelea kutoka bana pua kwa kutumia kitambaa chenye ubaridi au barafu itasaidia kusinyaa kwa mishipa ya damu na kuzuia damu.

5. Nenda hosipitali kama damu puani inatoka na kuumia kichwani, haijakata kwa muda wa dakika 20 na kama pua imeumia au kuvunjika

JAMAA AJIUA GESTI

Jamaa mmoja amepatikana amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni (lojing'i'/ Guest) mjini Thika nchini Kenya kwa kile kilichoshukiwa kuwa alijitia kitanzi.

 OCPD wa Thika Mohammed Kofa alisema jamaa huyo aliyetambuliwa kama Joseph Nyutu mwenye umri wa miaka 45 aliingia chumbani humo akiwa pekee yake Jumatatu, Aprili 26,2021 kulingana na ripoti ya The Standard.

Alisema kuwa awali ripoti zilionyesha kwamba aliaga dunia baada  kunywa sumu lakini kiini haswa cha kifo chake kitadhibitishwa baada ya upasuaji wa maiti kufanywa.

 Mwili wa marehemu ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Thika General Kago.

 Hii sio mara ya kwanza kwa maafa kuripotiwa katika vyumba vya kukodisha vya kulala kwani awali kiliripotiwa kisa kingine ambapo jamaa mwenye umri wa makamo alipatakana ameaga dunia ndani ya lojing'i eneo la Maua, kaunti ya Meru.

 Iliarifiwa kuwa marehemu alionekana akijivinjari na wanawake katika kilabu moja maarufu eneo hilo kabla ya kukodi chumba hicho cha kulala ambapo aliingia na warembo hao.

 Watatu hao waliingia katika kilabu hiyo Jumanne, Januari 12 kabla ya mwanamume huyo kupatikana uchi akiwa ameaga dunia kitandani. 

Wanawake hao walihepa lakini maafisa wa polisi waliofika eneo la tukio walipata mipira ya kondomu chumbani walimokuwa watatu hao.

Kwingineko mwanamume mwenye umri wa miaka 35 kutoka mtaani Dandora, Nairobi alizimia na kufariki dunia ghafla akila uroda na mpenziwe Jumatano, Januari 6. 

Robert Maina, mfanyikazi wa hospitali ya kitaifa ya Kenyatta alikuwa akila mahaba na mpenziwe Joyce Maina Wangare wakati alipoteza fahamu na kukata roho. Ripoti ya polisi katika kituo cha Dandora ilionesha kwamba Wairimu aligutushwa na tukio hilo ambapo alikimbia kwenda kupiga ripoti.

CHANZO - TUKO NEWS

Mume asakwa akituhumiwa kumuua mkewe


Zerrin Mwanakatwe (33) mkazi wa kijiji cha Mbuza wilayani Kalambo mkoani Rukwa ameuawa baada ya mumewe kumpiga na gogo kichwani.


Akizungumza leo Alhamisi Aprili 29, 2021 kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Theopister Mallya amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano Aprili 28, 2021 kijiji cha Mbuza wilayani Sumbawanga na kwamba mwanamke huyo alikuwa mjamzito.


Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kuibuka kwa mvutano kati ya mwanamke huyo na mumewe, Cravery Makwangu (53) na walikuwa wamekunywa pombe.


Inaelezwa kuwa mwanamke huyo aliochukua gogo akitaka kumpiga mumewe lakini mwanaume huyo alimzidi nguvu na kumnyang'anya kisha kumpiga nalo mwanamke huyo aliyeanguka chini na kufariki.


Amesema baada ya tukio hilo majirani walichukua mwili wa mwanamke huyo na kuupeleka hospitali ambapo alitolewa mtoto akiwa amekufa.


"Baada ya tukio mwanaume huyo ametokomea kusikojuliana polisi wanaendelea kumsaka ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria," amesema.


Source

MHUBIRI ROBERT BURALE ASEMA MAPENZI HAYACHAGUI UMRI...WATU WAPENDANE


Tunafahamu watu maarufu kadhaa wameoana au kuolewa na wapenzi wanaowazidi kwa umri, mwanamuziki Bahati, Emmy Kosgei na Guardian Angel ni miongoni mwao.

Mashabiki mitandaoni wamekuwa wakiwashambulia, kuwatusi na kuwakashifu kwa kuoa wapenzi wakubwa kwa umri.

Mtaalamu wa Mapenzi Mhubiri Robert Burale kwa kauli yake amehoji kwamba hakuna mtu yeyote anastahili kutusiwa wala kukashfiwa kwa kuwa na mpenzi anayemzidi kwa umri mradi ana miaka 18.

 Burale amekuwa mstari wa mbele kuwatetea watu maarufu ambao wamekuwa wakikejeliwa na kukosolewa mitandaoni kwa ajili ya kuwa uhusiana wa kimapenzi na watu wa umri mkubwa. 

 Burale ambaye ni baba wa mtoto mmoja alisema kila mtu anapaswa kuishi maisha anayotaka, wale wanaochambua maisha ya wengine wanapaswa kujipatia shughuli.

 " Watu wawili ambao wamekomaa kiakili wakiamua kuoana, hakuna haja ya mtu kupinga uamuzi wao wala kukejeli na kuwakashifu hasa kama mmoja anamzidi mwingine kwa umri, kama hivyo ndivyo wanafurahia maisha na iwe hivyo." Alisema Burale.

 " Ni jambo la kukera sana kuona watu wakiingilia maisha ya wengine, kila mtu anafaa kuishi maisha yake," Aliongeza Burale. 

Kwenye taarifa ambazo zinahusiana na hii, mwanamuziki Emmy Kosgei amekuwa akikejeliwa sana kwa kuolewa na mwanaume ambaye anamshinda mara dufu kwa miaka. 

Emmy alisema alifanya uamuzi huo kwa sababu mumewe anaheshimu muziki wake, marafiki , mashabiki wake na kila mara yeye humsaidia katika kila hali anapokwama.

CHANZO - TUKO NEWS

Sasa Twitter bila VPN Tanzania… Watumiaji wafurahia uhuru huo


Watumiaji wa Mtandao wa Twitter Tanzania wameanza kuutumia mtandao huo leo bila kuhitaji kujiunga kwanza na Virtual Private Network (VPN) ambayo wamekua wakiitumia kwa zaidi ya miezi mitano sasa, tweets mbalimbali zimeandikwa na baadhi ya Watumiaji kuonesha kufurahishwa na maamuzi hayo.

Kuanzia mwishoni mwa October 2020 Mtandao huo wa Twitter kwa upande wa Tanzania haukuwa unafanya kazi katika mfumo wa kawaida hivyo iliwalazimu Watumiaji wote kuweka application za VPN kwenye simu zao kwanza ndio waweze kuutumia, miongoni mwa Watumiaji wa Twitter waliofurahia hatua hii ya leo ni Mwanzilishi wa Nala Money Benjamin Fernandes.

Benjamin ameandika "Happy Twitter Independence Day Tanzania 29/4/2021 finally, 7 months later Twitter unblocked in Tanzania"

Chuo kikuu cha Kenya chakanusha kutoa shahada ya uchawi

 


Chuo kikuu kimoja kilichopo mashariki mwa Kenya kimekanusha taarifa kuwa kinawaandikisha wanafunzi wa shahada ya uchawi.

Chuo kikuu cha Machakos kimesema taarifa hizo ni za uongo.

Makala iliyoandika katika blogu moja ya Kenya kuhusu kuanzishwa kwa kozi ya uchawi katika chuo hicho.

Suala hilo liliwafanya watu kuwaandikia chuo kikuu cha Machakos kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu taarifa hiyo.

Azam FC Wakataa Kumuachia Dube




UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa hawapo tayari kumuuza staa wao, Mzimbabwe, Prince Dube, kwenda Simba na badala yake ataendelea kubaki kikosini kwao.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu ziwepo tetesi za Simba kuwa kwenye mipango ya kumnasa mshambuliaji huyo anayeongoza kwa mabao Ligi Kuu Bara akiwa amepachika 12.

 

Taarifa zilizopo kwa sasa ni kwamba, hivi karibuni mshambuliaji huyo ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Azam, hivyo atakuwa hapo hadi 2024.Akizungumza na Spoti Xtra,Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin 'Popat' alisema Dube hataenda timu yoyote hapa nchini, bali atabaki Azam.



Popat aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo kama akiondoka Azam, basi atakwenda kucheza soka nje ya Tanzania."Kwa kifupi Dube hatakwenda popote ndani ya nchi hii, ataendelea kubaki Azam.

 

"Dube kama akiondoka hapa Azam, basi atakwenda kucheza soka nje ya Tanzania na siyo kwenye klabu za hapa.

 

"Hizo timu zinazomtaka hata watoe dau kubwa kiasi gani, sisi Azam hatutalipokea, hivyo nao waende kutafuta wachezaji bora nje ya nchi kama sisi tulivyokwenda kumtafuta Dube," alisema Popat.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

 

Marekani imerudi kwenye mkondo sahihi - Rais Biden

 


Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa nchi hiyo ipo tena kwenye mkondo sahihi, na akatoa mwito wa matrilioni ya dola kwa ajili ya kuwasaidia watu wa tabaka la kati kuanza upya maisha ya baada ya janga la corona. 

Matamshi hayo ameyatoa wakati akilihutubia Bunge la Marekani, na kuongeza kuwa fedha hizo pia zitawapa maisha mapya wafanyakazi ambao anasema walikuwa wamesahaulika. 

Huku akisifia mafanikio yaliyopatikana katika kampeni kabambe ya kutoa chanjo kwa umma dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, Biden ameliambia Bunge na taifa kupitia televisheni kuwa Marekani kila mara huwa inajikwamua yenyewe. 

Kuhusu sera za kigeni, Biden ambaye anaadhimisha siku 100 tangu aingie madarakani, amesisitiza kurejea kwa Marekani katika ushirikiano wa kimataifa uliokuwa umeharibiwa chini ya utawala wa Trump.



Source

Israel yaongoza kwa kutoa bei rahisi za Bando za Internent

 


Nchi ya Israel imekuwa namba moja Duniani kwa kutoa bei rahisi za Bando za Internent ambapo GB 1 inagharimu USD 0.05 (Tsh. 116.19), hii ni kwa mujibu wa Mtandao wa Cable wa Uingereza, kwenye tano bora ya Dunia ya bei rahisi ya Bando ipo pia Sudan (USD 0.27).

Waziri Kalemani Atoa Maagizo Shirika la Viwango Tanzania (TBS)


Na Teresia Mhagama, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuhakikisha kuwa uwekaji wa vinasaba kwenye mafuta kama vile petroli na dizeli unafanyika kuanzia kwenye matenki yanayohifadhi mafuta hayo badala ya magari ili kuhakikisha kuwa mafuta yote yanayosambazwa nchini yanakuwa na ubora na Serikali inapata kodi stahiki.

Dkt.Kalemani alitoa agizo hilo tarehe 28 Aprili, 2021 mara baada ya kufanya ziara kwenye maghala ya mafuta ya kampuni za Camel Oil na Oil Com, Kurasini mkoani Dar es Salaam na kukuta wataalam kutoka TBS wakifanya kazi ya uwekaji wa vinasaba kwenye magari ya kusafirisha mafuta ya kampuni tajwa.

"Nataka muanze kupima mafuta kuanzia kwenye matenki yenyewe, hadi kwenye vituo, siyo tu kusubiri pale wanapopakia kwenye magari, Je ikitokea wamepakia wakati hampo, mtajuaje kuwa mafuta husika yana ubora?"Alisema Dkt.Kalemani

Dkt.Kalemani alieleza kuwa, amefanya ukaguzi wa kazi ya uwekaji wa vinasaba kwenye mafuta ili kujiridhisha kama TBS wanafanya kazi husika kwa ufanisi baada ya kukabidhiwa kutekeleza jukumu hilo ambalo awali lilikuwa likifanywa na mkandarasi binafsi ambaye alikuwa akilipwa takriban shilingi Bilioni Tano kwa mwezi.

Aliongeza kuwa, Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kumlipa mkandarasi binafsi kuweka vinasaba kwenye mafuta badala ya TBS ambayo ndiyo yenye dhamana ya kuhakikisha kuwa mafuta yanayouzwa nchini yanakuwa na ubora stahiki.

"Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa, mafuta yanakuwa na ubora, kodi zinapatikana na pia tunajenga uwezo wa watu wetu kufanya kazi husika na Taasisi zetu zisimamie kazi hii badala ya kutegemea watu kutoka nje ya nchi." Alisisitiza Dkt.Kalemani

Katika ukaguzi huo, Dkt.Kalemani aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kuhakikisha kuwa, wanasimamia kikamilifu kazi ya uwekaji wa vinasaba kwenye mafuta nchini kwani TBS ina jukumu la kupima mafuta hayo na EWURA ndiye mwenye jukumu la kumsimamia mpimaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya alimhakikishia Waziri wa Nishati kuwa, TBS ina uwezo wa kufanya kazi ya uwekaji vinasaba kwenye magari na kwamba mafuta yote yanayosambazwa nchini yanakuwa na vinasaba.

Katika ziara yake kwenye maghala hayo ya mafuta mkoani Dar es Salaam, Waziri wa Nishati aliambatana na Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Sebastian Shana, na Wakuu wa Taasisi za Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), TBS na EWURA.




Uhispania yaweka sheria ya karantini ya lazima kwa wasafiri wanaoingia nchini kutoka India

Serikali ya Uhispania imeamua kuweka sheria ya karantini ya lazima ya siku 10 kwa wasafiri wote wanaoingia nchini kutoka India.

Kama tahadhari dhidi ya aina mpya ya virusi vya corona (Covid-19), abiria wote kutoka India kuja Uhispania kuanzia Mei 1, watawekwa katika karantini kwa siku 10.

Abiria watatekeleza karantini hiyo katika nyumba zao au vyumba vya hoteli. Hawataruhusiwa kuondoka sehemu hizo ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kufanya ununuzi wa mahitaji ya kimsingi.

Wale ambao watafanyiwa vipimo vya PCR siku ya 7 ya karantini na kupata matokeo hasi, hawatatengwa kabla ya kutimiza siku 10.

Waziri wa Afya wa Uhispania Carolina Darias alisema kuwa aina ya mpya ya virusi vya Covid-19 nchini India inaonekana kuwa na athari ndogo nchini Uhispania na inaweza kudhibitiwa kwa hatua kama hizo.

 

Mwanamke bora katika maisha ya ndoa hujengwa na mambo haya

 

Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo;

Uvumilivu
Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung'uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo.

Upendo wa dhati
Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. Wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni upendo wa dhati na uhalisia.

Utii kwa jamii
Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka  ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii  kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa.

Uaminifu katika jamii
Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote.

Unyenyekevu wa kweli
Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima.

Uwajibikaji wa dhati
Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake.

Ushirikiano wa dhati
Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora.

Utaratibu wa kazi/mpangilio
Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako.

Wednesday, April 28, 2021

Zijue athari za kuvaa viatu virefu wakati wa ujauzito

Kipindi cha ujauzito ni wakati wa kubadili mambo mengi katika mfumo wa maisha wa mjamzito. Moja ya mambo makubwa ni pamoja na tabia ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu. Mjamzito hashauriwi kuvaa viatu vyenye visigino virefu kutokana na athari zinazoweza kutokana na aina hizi za viatu.

Zifuatazo ni athari za kuvaa viatu vyenye visigino virefu wakati wa ujauzito:

Maumivu ya misuli ya mapaja.
Wadada hupenda kuvaa "high heels" husababisha misuli ya mapaja kukaza na kuwa na muonekano mzuri. Katika ujauzito, mabadiliko ya homoni huweza kupelekea misuli hii kuwa na maumivu tofauti na ilivyokua kabla ya ujauzito.

Maumivu ya mgongo.
Wakati wa ujauzito, uzito mkubwa huhamia mbele na misuli ya nyonga hulegea. Mabadiliko haya ya kimsawazo huweza kusababisha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo na kiuno.

Hatari ya kuanguka.
Ni wazi kuwa uzito huongezeka wakati wa ujauzito na mabadiliko ya vichocheo vya mwili huweza kupelekea kizunguzungu cha hapa na pale. Hii huongeza hatari ya kuanguka iwapo utavaa "high heels" na kupelekea majeraha kwako na kwa mtoto aliyeko tumboni.

Uvimbe miguuni.
Ni jambo la kawaida miguu kuvimba wakati wa ujauzito. Kuvaa viatu vyenye visigino virefu na vyenye kubana huweza kuongeza tatizo hilo na kupelekea maumivu.

Mimba kutoka.
Mjamzito akivaa viatu vyenye visigino virefu anakua katika hatari kubwa ya kuanguka. Hii huweza kusababisha majeraha makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni hali inayoweza kusababisha mimba kutoka.

Lakini, iwapo kuna ulazima sana wa kuvaa viatu hivyo, unapaswa kuzingatia yafuatayo:
Ni salama kuvaa viatu hivi katika muhula wa kwanza wa ujauzito (Miezi mitatu ya mwanzo).
Viatu visiwe virefu sana na visigino viwe imara.
Vaa viatu visivyo na bugdha na usivikaze sana.
Epuka visigino vyembamba sana.
Usivae siku nzima. Vitoe mara kwa mara kupumzisha miguu.
Epuka kutembea au kusimama muda mrefu ukiwa umevivaa.
Ukihisi maumivu kwenye misuli ya mapaja jaribu kufanya mazoezi ya kujinyoosha na kujikanda.

Prof Jay afunguka kuhusu deni kubwa analodaiwa



Mkongwe wa muziki wa HipHop Bongo Proffesor Jay, amesema ana deni kubwa sana analodaiwa kutoka kwa mashabiki zake ambao walim-miss kipindi yupo Bungeni anatumikia wananchi wa Jimbo la Mikumi.


Katika kulipa deni hilo msanii huyo ametangaza kuja na Album yake mpya itakayotoka mwaka huu ambayo itakata kiu ya mashabiki wake ambao wamem-miss kwa kipindi kirefu alichokaa bila kutoa wimbo.


"Nilikuwa nina deni kubwa kwa mashabiki, nataka niwape furaha waliyo-miss kwa muda mrefu, nitakuja na Album mwaka huu, mimi ni Shule pia Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Kitaa na nitawaletea Album ambayo itakuwa kama kitabu na nyimbo zake zitakuwa kama Chapter"


"Napenda kuimba wimbo ambao unagusa maisha ya jamii zaidi kuliko mimi, kati ya nyimbo zangu zote chemsa biongo ningeipa tuzo za Grammy" ameongeza Prof Jay


Kwa sasa Prof Jay anatamba na wimbo wake mpya wa 'utaniambia nini' ambao unafanya vizuri kwenye vituo vingi vya Radio na TV pamoja na Digital Platform.


Source

Watu 9 wafariki kwenye shambulizi la silaha lililotokea nchini Nigeria


Watu 9 waliuawa na wengine wengi walijeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa na watu wenye silaha katika jimbo la Anambra nchini Nigeria.

Msemaji wa Polisi wa Anambra, Tochukwu Ikenga alisema kuwa vikosi vya usalama vilitumwa eneo la tukio.

Ikenga aliongezea kusema kuwa hali ya usalama ilidhibitiwa katika mkoa huo.

Katika taarifa kwenye vyombo vya habari vya kitaifa, ilidaiwa kuwa watu 19 walikufa katika shambulizi hilo.

Kwa upande mwingine, ilani ya marufuku ya kutoka nje ilitangazwa kutokana na visa vya vurugu katika mkoa huo.



Source

WEZI WAIBA KENGELE YA KANISA YENYE KILO 500

Watu wasiojulikana wameripotiwa kuiba kengele ya kanisa la Virgin Mary Orthodox lililoko eneo la Limuru kaunti ya Kiambu nchini Kenya ambapo tayari maafisa wa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo. 

Kulingana na Katibu wa kanisa la Virgin Mary Ordhodox  James Warari alisema genge la wezi lilivamia kanisa hilo Alhamisi, Aprili 22,2021 na kuiba kengele hiyo ambayo inasemekana kuwa na uzito wa kilogramu 500. 

"Kisa hicho kilitokea Alhamisi Usiku, tuliamka asubuhi na tukagundua kwamba kengele hiyo haikuwepo. Mtu mmoja hawezi akabeba kengele hiyo kwa sababu ni nzito sana. Tunajua kulikuwa na watu kadhaa walishirikiana kubeba," Warari alisema. 

Warari alisema kengele hiyo ilikuwa imetengenezwa na shaba na ilikuwa ikitumiwa kuwakumbusha waumini saa za kuomba na pia kupanga ratiba ya kanisa hiyo.

Inasemekana kengele hiyo ilinunuliwa kutoka ng'ambo na Warari amemrai Mkenya yeyote ambaye atataka kuuziwa asiinunue bali awasiliane na wasimamizi wa kanisa hiyo.

 "Tungependa mtu yeyote ambaye ataiona kengele hiyo awasiliane nasi, nisingependa inunuliwe na mtu yeyote, naomba ipelekwe afisi yoyote ya chifu ilioko eneo la Limuru, kengele hiyo ulinunuliwa ng'ambo na hatuwezi ipata nyingine kama hiyo hapa Kenya," Wariru alisema.


Bocco Amwaga Wino Msimbazi




NAHODHA wa Simba John Raphael Bocco 'Papaa' naye amemwaga wino kuendelea kutumikia mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Simba.

 

Kupitia ukurasa wa Simba kwenye mtandao wa Instagram wame share picha za mshambuliaji huyo akisaini mkataba.



Hii imekuja muda mfupi baada ya beki Mohamed Hussein kuongeza kandarasi jipya kuendelea kuitumikia Simba.


Giggs Ashitakiwa Kuwanyanyasa Wanawake




MENEJA wa Klabu ya Wales, Ryan Joseph Gigs anashitakiwa makosa matatu ya unyanyasaji dhidi ya wanawake wawili. Anashutumiwa kwa kusababisha madhara ya mwili kwa mwamke aliye na umri wa miaka zaidi ya 30 na unyanyasaji wa kawaida dhidi ya mwanamke mwingine mwenye umri wa zaidi ya miaka 20 katika eneo la Salford, Novemba 2020.

 

Giggs (47), wa Worsley, pia anashitakiwa kwa kosa la kulazimisha au tabia ya kuthibiti. Amepewa dhamana ya kufika katika makakama za hakimu mkazi za Manchester na Salford, Aprili 28. Giggs alisema katika taarifa yake kwamba atakana mashitaka mahakamani.

 

"Ninaheshimu kabisa mchakato wa shetia na ninafahamu ukubwa wa madai," alisema.

"Ninasubiri kusafisa jina langu."

 

Polisi wa Manchester Police walisema maafisa wa polisi waliitwa saa nne na dkika tano za usiku tarehe 1 Novemba kutokana na taarifa za usumbufu zilizotokea katika eneo la Worsley.

 

Polisi walisema kuwa mwanamke mwenye miaka zaidi ya 30 alitibiwa majeraha madogo katika eneo la tukio. Giggs pi anashutumiwa kwa tabia ya kulazimisha na mienendo ya kudhibiti anayodaiwa kutekeleza katika miezi ya Disemba, 2017 na Novemba, 2020.

 

Shirikisho la Soka la Wales (FAW) limethibitisha meneja msaidizi Robert Page h atachukua usukani wa timu hiyo kuanzia msimu huu wa Championi Lig.

 

FAW lilisema kutakuwa na mkutano wa bodi ya klabu hiyo "kujadili suala hilo na athari yake kwa shirikisho na timu ya taifa ".

 

Katika taarifa yake, Bw Giggs alioneza kuwa: "Ningependa kumtakia Robert Page, makocha, wachezaji na mashabiki kila mafanikio katika michuano ya Eropa msimu huu."

 

Winga huyo wa zamani wa Manchester United ni mmoja wa wacheza waliotunukiwa tuzo zaidi nchini Uingereza baada ya miaka 24 ya mchezo wake katika Old Trafford na aliteuliwa kuwa OBE mwaka 2007 kabla ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC mwaka 2009.

 

Pia alishinda kofia 64 za mchazaji bora wa Wales kati ya mwak 1991 na 2007 na aliteuliwa kuwa meneja wa taifa wa Wales Januari,2018, ambapo aliongoza timu ya taifa hilo kufuzu michezo ya Ulaya 2020, ambayo iliahirishwa kwasababu ya Covid-19. Pia ni mmiliki mwenza wa timu ya Ligi ya daraja la pili ya Salford City.


Serikali Yasitisha Matumizi ya Vitamin C Kutibu COVID-19




WIZARA ya afya nchini Uganda imesitisha matumizi ya vitamin C katika kutibu virusi vya Covid-19 kutokana na matumizi mabaya ya wagonjwa.

 

Vitamni C ndiyo moja ya dawa zilizokuwa zinatumiwa kWa wagonjwa wa covid-19 nchini Uganda kwa sababu zinasaidia kuendeleza chembe hai nyeupe(White blood cell) kupambana kuondoa virusi.

 

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya afya wanaoshughulika na masuala ya utafiti, wanadai vidonge vya vitamn C vinapatikana kwa urahisi na hivyo watu hutumia kiholela kupita kiasi na kuleta madhara.

 

Daktari Misaki Wanyegera ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kupambana na virusi vya corona katika wizara ya afya nchini Uganda, amesema walichukua hatua ya kuondoa Vitamic C baada ya wagonjwa hospitalini kukutwa wakitumia hovyo vitamin hizo na kusababisha figo kushindwa kufanya kazi kutokana na matumizi mabaya.

 

Kulingana na ushauri wa madaktari, matumizi ya Vitamin C kwa mgonjwa wa mafua ni tembe 2 kila baada ya saa 8, lakini watu wanatumia mara tatu ya hizo. Mwezi Januari kulikuwa na ukosefu wa Vitamin C za Gramu 100 kote nchini humo kutokana na matumizi mabaya.


Kirusi Kipya cha Covid 19 ni Hatari Zaidi




SHIRIKA  la Afya duniania WHO limesema aina ya virusi vya corona ambavyo vinahofiwa kuchangia wimbi la visa vya maambukizi nchini India vimebainika katika mataifa mengine kadhaa duniani.

 

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kirusi aina ya B.1.617 vya Covid-19 ambavyo kwa mara ya kwanza viligundulika India, kwa rekodi za jana vilibainika katika mataifa mengine takribani 17.

 

Taarifa hiyo ilisema idadi kubwa ya visa vyake vya maambukizi vimetokea Uingereza, Marekani na Singapore.

 

Kwa namna inavyotambulishwa aina hiyo ya virusi inaonesha kuwa ni hatari zaidi kuliko ile ya awali ikioneshwa kuwa na uwezo wa kuwa na kasi ya maambukizo au kuweza kukwepa kinga za chanjo.

 

Mlipuko wa maambukizi wa India kwa rekodi za jana pekee umesababisha visa vipya 350,000, hali inayosababisha rekodi mpya ya maambukizo duniani kufikia watu milioni 147.7 na vifo zaidi ya milioni 3.1.


Rosa Ree Akiri Kulizwa na Mapenzi






RAPA mkali wa kike Bongo, Rosary Robert 'Rosa Ree' amekiri kulia kwa ajili ya mapenzi.

 

Akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, Ree anasema kuwa, sababu ya yeye kulia ni kitendo cha kuwa na mpenzi aliyekuwa akimsaliti wakati yeye alikuwa akimuamini kinoma hivyo hakuweza kuamini alichofanyiwa.

 

"Mapenzi yanauma asikwambie mtu, mimi nilishawahi kulia kwa ajili ya mpenzi wangu ambaye alini-chit (kusaliti). Nilikuwa nikimuamini sana," anasema Ree.



JAMAA AKUBALI KUMUOA ALIYEKUWA KAHABA NA KUZAA WATOTO 10 WA BABA TOFAUTI


Jaribu kuweka taswira ya picha ya siku ya harusi yako kila kitu kimeandaliwa lakini una wasiwasi kwa sababu haujawahi kukutana na mwanaume ambaye anataka kukuoa.

Kando na hali hiyo kuonekana nadhimu, hii ni hadithi ya Janet, ambaye alikutana na mume wake Jackson siku Spesheli ya harusi yao. 

Akizungumza kwenye mahojiano na Afrimax, Janet alisema mume wake ambaye alikuwa anaishi Marekani, alimjua baada ya video yake kusambaa akisimulia namna alivyoacha ukahaba na kuokoka.

Alisema video hiyo ilimfanya kudhalilishwa hususan baada ya kuchapishwa bila ruhusa yake lakini ilimvutia mwanaume mmoja ambaye aliguswa na ushuhuda wake. 

"Aliona ushuhuda wangu na aliguswa. Alihisi kwamba tunatakiwa kuishi pamoja milele," alisema.

 Alitafuta nambari zake za simu akiwa Marekani na baada ya kuzipata alimpgia na kuanza urafiki na kisha wakaishia kuwa wapenzi kisha mipango ya harusi ilianza akiwa bado ughaibuni 

Walikuwa wakizungumza kila siku na wakati mapenzi yao yalikolea na kuwa dhabiti, alimposa kupitia simu na kisha punde si punde mipango ya harusi ilianza.

 Jamaa huyo hakubabaishwa na ukweli kuwa mama huyo ana watoto 10 ambao aliwazaa akiwa kahaba.

 Badala ya kubabaishwa na maisha yake ya zamani, alichagua kumuoa mwanamke ambaye alikuwa anajaribu kuishi maisha mapya. 

Janet alisema alikumbana na pingamizi kutoka kwa kanisa lake kwa kumuona kama mwenye dhambi kubwa zaidi kufanya harusi lakini alikumbatiwa na kanisa lingine ambalo liliidhinisha ndoa yake Disemba 2020.

Siku ya harusi hiyo, ndege ya bwana harusi ilitua na kukutana na mke wake kwa mara ya kwanza na kisha wawili hao walibadilishana viapo vya ndoa. Baada ya kubadilishana viapo vya ndoa, wapenzi hao walikaa pamoja kwa wiki kadhaa kabla ya mwanamume huyo kurejea Marekani na kuanza mipango ya Janet kuhamia nchini humo.


Tuesday, April 27, 2021

Hali ya Mzee King Kikii Bado ni Tete “Nisaidieni”




GLOBAL TV imemtembelea msanii Mkongwe wa muziki wa dansi nchini aliyetamba zaidi na kibao chake cha 'KITAMBAA CHEUPE', Mzee King Kiki, ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maradhi ambayo yamemsababishia kukaa nyumbani na kushindwa kuendelea na kazi zake.

 

NGULI huyo amekumbwa na maradhi ya uti wa mgongo.

Unaweza kumchangia fedha kwa ajili ya matibabu kupitia nambari hii

( 0713 50 50 62 au 0757 50 50 62 – JINA COSTANSIA KALANDA)


JSC yampendekeza Martha Koome kuwa Jaji mkuu nchini Kenya

 


Koome ana uzoefu wa miaka 33 katika tasnia ya sheriana pia amewahi kuhudumu kamamtetezi wa haki za binadamu

Tume ya huduma kwa idara ya mahakama JSC imempendekeza jaji Martha Koome kuwa Jaji mkuu ajaye nchini Kenya ili kuichukua nafasi ya David Maraga aliyestaafu .

Kaimu mwenyekiti wa tume hiyo Olive Mugenda ametangaza kwamba uamuzi huo umeafikiwa na makamishna wote wa tume hiyo .Koome ana uzoefu wa miaka 33 katika tasnia ya sheria na pia amewahi kuhudumu kama mtetezi wa haki za binadamu . Iwapo rais Uhuru Kenyatta ataidhinisha uteuzi huo Koome atakuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kama Jaji mkuu nchini Kenya .


Source

Makampuni yasiyolipa waajiri kutangazwa hadharani


Na Maridhia Ngemela, MWANZA

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, sera na Ajira, Patrobas Katambi.

 ,amewataka  waajiri kuwathamini wafanyakazi kwani wao ndo hufanya kazi na kuinua uchumi wa taasisi husika  hivyo ni vyema kuona thamani ya mwajiri na kumpatia sitahiku zake kwa wakati.

Ameongeza kuwa,wananchi kutambua,walioshikilia uchumi wa nchi ni wafanyabiashara wa kati kushuka chini,ndio maana serikali imeamua kuwawezesha,hivyo vijana,kina mama na baba wafanye kazi na sio kusubiri ajira ambazo upatikanaji wake umekuwa ni watabu.

Katambi alisema hayo jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na waajiri ,chama cha wafanyakazi pamoja wakala wa usalama afya  na mahali pa kazi ( Osha)  katika  maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahala pa kazi Duniani ambayo yalianza Aprili 26 mwaka huu hadi Aprili 28/2021 ambayo ndio itakuwa siku ya kilele,

"Waajiri wapo wanaowanyima haki wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi,natoa rai andapo wakibainika sisi tutawashughulikia,hivyo wale wote walioyo na madai walioumizwa na wanasumbuliwa na waajiri kupata haki yake wafike wizarani tutatatua madhira hayo,"alisema Katambi.

Katika maazimisho hayo zaidi ya wajasiliamali 600 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa walipatiwa mafunzo ya usalama,Afya mahala pakazi kwa kipindi cha wiki mbili,ambayo yamegharimiwa na serikali maana wananchi ili afanye kazi anategemea afya na usalama ikiwa ni kuleta mafanikio ndani ya familia na Taifa kwa ujumla

 Naye mkurugenzi mtendaji wa OSHA Khadija Mwenda,alisema, adha kubwa wanayokutana nayo katika usimamizi wa sheria ni uelewa mdogo wa kukabiliana na athari kazini kumepelekea matatizo,hivyo wananchi watambue mtaji wao ni usalama na afya,hivyo akipata madhara hawezi kujikomboa kiuchumi kutokana na maumivu au kilema alichokipata kutokana na mazingira ya kazi

Aidha mwenda alisema bado kunachangamoto katika mfumo  ya kuwalinda wafanyakazi mpaka sasa ni asilia 40 tu ndio kubwa wako salama mahala la kazi.

Kwa upande wake wakili mwandamizi  chama cha waajiri Tanzania Mercy Sevya amesema waajiri  wawaelimishe  kuhusiana  na namna ya kuishi salama na kutoa mfumo samala kwaajili ya wafanyakazi  mahala pa kazi .

AWESO ATOA SIKU 10 MRADI WA MAJI MWAKITOLYO SHINYANGA UKAMILIKE

 

Waziri wa Maji Jumaa Aweso (mwenye shati la bluu katikati) akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi wa Maji Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Ukaguzi ukiendelea.


Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea ujenzi wa mradi wa maji Mwakitolyo uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga huku akitoa siku 10 mradi huo uwe umekamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Amesema kati ya miradi ya maji 177 ambayo ni kero hapa nchini, mmoja wapo ni mradi huo wa Mwakitolyo hivyo kuagiza hadi ifikapo Mei 5 mwaka huu ndani ya siku 10 zijazo, uwe tayari umeshakamilika.

"Mradi huu wa maji Mwakitolyo nina historia nao, ni kati ya miradi ya maji kichefuchefu hapa chini, hivyo naagiza hadi ifikapo Mei 5 uwe tayari umeshakamilika"

"Nakumbuka nilikuja hapa miaka ya nyuma mradi hiu ulikuwa ni changamoto nikaupa jina kichefu chefu kwa sababu haiwezekani zitokea fedha Bilioni 1.4 lakini mwananchi hana maji "Alisema

Waziri Aweso alisema mradi huo ni miongoni mwa 177 ambayo waliianisha ambayo ilikuwa inachafua wizara na maelekezo yalikuwa ni kuhakikisha miradi kichefu chefu yote inakwamuliwa na kati ya miradi 177 miradi 85 wameikamilisha ikiwemo huo wa Mwakitolyo .

Alisema hivi sasa hapo hakuna kisingizio kwa sababu fedha zimekwisha kutolea milioni 400 na mabomba yameshajengwa hivyo ndani ya Mei 10 mwaka huu wananchi wanakwenda kupata huduma ya maji.

"Hapa visingizio hakuna tena tutakwenda kugombana kwa hali ninavyoiona mambo ni mzuri kubwa ninaloliona pamoja na wananchi wa mwakitolyo kupata maji lakini na mwakitolyo maeneo ya jirani inakuwa kwa kasi sana kwa hiyo tutafute eneo la mlima tutengeneze tenki la lita laki tano"Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa, ambao ndiyo watekelezaji wa mradi kwa kushirikiana na (RUWASA),alimhakikishia Waziri Aweso kuwa utakamilika ndani ya siku hizo 10.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...