Friday, April 30, 2021

Meli ya kubeba ndege ya China yapitia mpaka wa Japan


Meli ya kubeba ndege ya Wachina "Liaoning" ilipita kati ya mkoa wa kusini mwa Japan wa Okinawa na kisiwa cha Miyakojima.

Kulingana na taarifa ya shirika la habari la umma la Japan NHK kwa kuzingatia vyanzo vya Wizara ya Ulinzi, iliarifiwa kwamba meli ya Liaoning ilisafiri karibu na Okinawa, kusini mwa Japan, ikiongozana na meli 5.

Ikipita kati ya mkoa wa kusini wa Okinawa na kisiwa cha Miyakojima, meli ya Liaoning ilielekea kaskazini na kuingia Bahari ya China Mashariki, kwa mujibu wa taarifa ya Kikosi cha Ulinzi wa Bahari (MSDF).

Wakati wa msafara wa meli za kijeshi, Japan haikukiuka sheria za mipaka ya bahari ya eneo hilo.

Sheria ambayo ilianza kutumika nchini China mnamo Februari 1, inampa mamlaka mlinzi wake wa pwani kutumia silaha dhidi ya meli za kigeni ambazo hazizingatii sheria.

Shirika la Kyodo lilisema kwamba sheria hii inaidhinisha China kulenga meli za Japan zinazozunguka Visiwa vya Senkaku vinavyozozaniwa katika Bahari ya China Mashariki.

Visiwa vya Mashariki mwa Bahari ya China, ambayo Japan inaita "Senkaku" na China inaita "Diaoyu", ina visiwa 5 na miamba 3.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...