Na Maridhia Ngemela, MWANZA
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, sera na Ajira, Patrobas Katambi.
,amewataka waajiri kuwathamini wafanyakazi kwani wao ndo hufanya kazi na kuinua uchumi wa taasisi husika hivyo ni vyema kuona thamani ya mwajiri na kumpatia sitahiku zake kwa wakati.
Ameongeza kuwa,wananchi kutambua,walioshikilia uchumi wa nchi ni wafanyabiashara wa kati kushuka chini,ndio maana serikali imeamua kuwawezesha,hivyo vijana,kina mama na baba wafanye kazi na sio kusubiri ajira ambazo upatikanaji wake umekuwa ni watabu.
Katambi alisema hayo jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na waajiri ,chama cha wafanyakazi pamoja wakala wa usalama afya na mahali pa kazi ( Osha) katika maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahala pa kazi Duniani ambayo yalianza Aprili 26 mwaka huu hadi Aprili 28/2021 ambayo ndio itakuwa siku ya kilele,
"Waajiri wapo wanaowanyima haki wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi,natoa rai andapo wakibainika sisi tutawashughulikia,hivyo wale wote walioyo na madai walioumizwa na wanasumbuliwa na waajiri kupata haki yake wafike wizarani tutatatua madhira hayo,"alisema Katambi.
Katika maazimisho hayo zaidi ya wajasiliamali 600 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa walipatiwa mafunzo ya usalama,Afya mahala pakazi kwa kipindi cha wiki mbili,ambayo yamegharimiwa na serikali maana wananchi ili afanye kazi anategemea afya na usalama ikiwa ni kuleta mafanikio ndani ya familia na Taifa kwa ujumla
Naye mkurugenzi mtendaji wa OSHA Khadija Mwenda,alisema, adha kubwa wanayokutana nayo katika usimamizi wa sheria ni uelewa mdogo wa kukabiliana na athari kazini kumepelekea matatizo,hivyo wananchi watambue mtaji wao ni usalama na afya,hivyo akipata madhara hawezi kujikomboa kiuchumi kutokana na maumivu au kilema alichokipata kutokana na mazingira ya kazi
Aidha mwenda alisema bado kunachangamoto katika mfumo ya kuwalinda wafanyakazi mpaka sasa ni asilia 40 tu ndio kubwa wako salama mahala la kazi.
Kwa upande wake wakili mwandamizi chama cha waajiri Tanzania Mercy Sevya amesema waajiri wawaelimishe kuhusiana na namna ya kuishi salama na kutoa mfumo samala kwaajili ya wafanyakazi mahala pa kazi .