Serikali ya Uhispania imeamua kuweka sheria ya karantini ya lazima ya siku 10 kwa wasafiri wote wanaoingia nchini kutoka India.
Kama tahadhari dhidi ya aina mpya ya virusi vya corona (Covid-19), abiria wote kutoka India kuja Uhispania kuanzia Mei 1, watawekwa katika karantini kwa siku 10.
Abiria watatekeleza karantini hiyo katika nyumba zao au vyumba vya hoteli. Hawataruhusiwa kuondoka sehemu hizo ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kufanya ununuzi wa mahitaji ya kimsingi.
Wale ambao watafanyiwa vipimo vya PCR siku ya 7 ya karantini na kupata matokeo hasi, hawatatengwa kabla ya kutimiza siku 10.
Waziri wa Afya wa Uhispania Carolina Darias alisema kuwa aina ya mpya ya virusi vya Covid-19 nchini India inaonekana kuwa na athari ndogo nchini Uhispania na inaweza kudhibitiwa kwa hatua kama hizo.