Sunday, August 30, 2020

ANGALIA PICHA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM 2020... JPM AAHIDI MAKUBWA KWA WATANZANIA

Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza na Wanamuziki wa Bendi ya TOT mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

(PICHA IKULU NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-DODOMA)
******
Na Majid Abdulkarim, Dodoma
Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hivi karibuni watanzania wataanza kuona faida kupitia mavuno ya miradi waliyoanza kutekeleza ndani ya miaka mitano ambayo ni Mavuno ya reli ya SGR, Umeme wa Bwawa la Nyerere, barabara mbalimbali, ujenzi wa Meli katika maziwa mbalimbali.

Aidha Dkt. Magufuli ameaidi watanzania kuwa wakimrudisha madarakani kazi yake ya kwanza atakayoifanya ni kujenga uwanja mkubwa wa michezo katika Jiji la Dodoma.

Dkt. Magufuli amebainisha hayo katika Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kitaifa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma

Dkt. Magufuli ameeleza kuwa Kazi alizofanya ndani ya miaka mitano ndizo zimewafanya kurudi kuomba tena ridhaa ili waweziendeleze zisije kukwama, wamenunua Ndege mpya 11, nane zimefika na tatu zinatengenezwa, katika Ilani mpya ya Uchaguzi amesema watanunua Ndege nyingine tano mpya ndani ya miaka 5 ikiwemo ya mizigo.

"Mkituchagua tumepanga kununua ndege nyingine tano, mbili za masafa ya mbali, mbili masafa ya kati na moja ya mizigo hivyo Tupeni kura za ndio tukakamilishe haya yote" amessema Magufuli.

"Mwaka 2015 Watanzania walitaka mabadiliko na Serikali ya awamu ya 5 imejitahidi kukata kiu zao, tumerudisha nidhamu Serikalini sasa hivi maofisini mnahudumiwa vizuri,tumedhibiti rushwa na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na waliofikishwa Mahakamani sio dagaa ni samaki wakubwa"ameeleza Dkt. Magufuli.

"Tutahamasisha pia wataalamu wetu wanaoweza kutibu magonjwa kwa kutumia dawa za kienyeji ili watambuliwe kikamilifu badala ya kuwapuuza, tutaongeza fedha kwa ajili ya utafiti na kusomesha Watanzania kwenye Vyuo bora" amesisitiza Dkt. Magufuli

Katika hatua nyingine Dkt. Magufuli amesema kuwa wamepanga kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia Mil 5 2025, na mapato kutoka Dola Bil 2.6 hadi Dola Bil 6, kupanua wigo wa vivutio vya Utalii, ikiwemo kukuza Utalii wa mikutano na uwindaji wa Wanyamapori na kuimarisha utalii wa fukwe.

Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watanzania kuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu azidi kuliongoza na kulisimamia taifa ili hatimaye kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa amani na usalama na huku watanzania kubaki wamoja.

" 2015 Watanzania walitaka mabadiliko ya kuona vitendo vya rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za umma unakomeshwa na walitaka mabadiliko ya kuona rasilimali za nchi zinalindwa na walitaka mabadiliko ya uchumi wa nchi ukue kwa kasi", ameongeza Dkt . Maguful.

Pia Dkt. Magufuli amesema kuwa Watu wengi wanadhani yeye kutosafiri sana nje ya nchi basi uhusiano wa kidiplomasia umepungua, kitu ambacho si kweli na badala yake umeongezeka zaid , Balozi nane za Tanzania katika nchi 8 zimefunguliwa na mataifa mawili yamefungua Balozi zao mbili hapa nchini .

Lakini pia Dkt. Magufuli ameeleza kuwa mradi mkubwa wa FAR jijini Dodoma unatekelezwa , mradi huu utatatua changamoto ya upatikanaji wa maji Dodoma .

"Hadi sasa vijiji 9570 nchini vimeunganishwa na huduma ya umeme kutoka vijiji 2018 mwaka 2015, na hii ni kutokana na serikali kupunguza gharama ya kuunganisha umeme kutoka Sh. 177,000 hadi kufikia shilingi elfu 27 tu " ameweka wazi Dkt. Magufuli

Hata hivyo Kuhusu usafiri wa anga tumekamilisha ujenzi wa Jengo jipya la Terminal 3, kule Dar es Salaam. Kwa hapa Dodoma tumepanga kujenga uwanja mkubwa ndege eneo la Msalato, uwanja huo utakua na Kilomita 3, hapa ndio makao makuu ya Nchi, kutakua na Ndege zinazoruka kutoka hapa Kwenda Ulaya"amesema Dkt. Magufuli

Kwa upande wake Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Mhe. Samia Suluhu ameeleza kuwa Katika miaka mitano wameweza kutekeleza kwa kishindo na wanaweza .

Huku Mgombea urais CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ally Mwinyi amesema kuwa atafanya kazi na kuendeleza pale alipoishia Rais Ally Mohamed Shein. Nitakwenda kwa 'speed".

"Natoa wito kwa watanzania wote kulinda amani kwani bila amani hakuna maendeleo , hivyo tulinde amani yetu watanzania", ametoa wito Dkt. Mwinyi

Katibu Mkuu CCM, Ally Bashiru amesema Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 inakurasa zaidi ya 300 Ikieleza Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka tano iliyopita na Uelekeo wa Miaka tano ijayo.

"CCM tunayo majimbo 18 kibindoni wagombea wetu wamepita bila kupingwa na sasa wanasubiri kuapishwa tu. Pia, tunazo kata zaidi ya 400 ambapo wagombea wetu wamepita bila kupingwa, mitambo imewashawashwa, moto uliowashwa atakayebabuka tusilaumiane," ameeleza Dkt. Bashiru

Dkt. Bashiru ameendelea kusema kuwa Miaka mitano ijayo, CCM itaendeleza kuhimiza wananchi kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kufanya kazi kwa uadilifu, bidii na maarifa kama msingi imara wa maendeleo ya taifa .

"CCM inatambua kuwa nchi yetu ina watu wenye uwezo na rasilimali za kutosha kama vile ardhi, madini, gesi asilia,misitu, wanyama, malikale, bahari, maziwa na mito" amesema Dk. Bashiru .

"CCM itaendelea kulinda na kuimarisha umoja, mshikamano, amani, utulivu, ulinzi na usalama, kulinda, kuimarisha, kudumisha uhuru, Mapinduzi matukufu ya Zanzibar na muungano wa Tanzania", Dk. Bashiru

"Ndugu zangu wana Dodoma tunayo kila sababu ya kumchagua Magufuli kampeni yetu ya safari hii kwa sababu Madiwani wengi wamepita bila kupingwa na baadhi ya majimbo Wabunge wamepita moja kwa moja iwe ya Rais tu na iwe ya Nyumba kwa Nyumba" amesisitiza Spika Ndugai

Spika Ndugai ameeleza kuwa wengine lazima awape ripoti kazi yao ni kuzira, kununa na kutoka nje Bungeni,hivyo hadhani kama wananchi wanachagua watu kwenda Bungeni au kutoka, badala ya kuwa mali ya wananchi wanakuwa mali ya hivyo vyama.

Ikumbukwe Dkt. Magufuli anasimama jukwani kupeperusha Bendera ya CCM kwa mara ya Pili, ambapo Mara ya Kwanza ilikuwa ni Mwaka 2015.
 
Mgombea Mwenza kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. 

Mgombea Urai wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi akizungumza katika mkutano huo.


Mbunge Mteule kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Mh George Simbachawene akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.


Mbunge Mteule wa jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde naye akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni.

Mbunge Mteule wa jimbo la Kongwa Mh. Job Ndugai naye amezungumza machache katika mkutano huo
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa wamenyanyua mikono yao juu na Wananchi wa Dodoma hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. 
Picha mbalimbali zikionesha umati wa wananchi wa jiji la Dodoma na viunga vyake walivyojitokeza kwa wingi ili kumsikiliza mgombea kupitia CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.

 
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza na Wanamuziki wa Bendi ya TOT mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza na wasanii wa bendi ya TOT wakati alipowasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kumsalimia Rais wa Zanzibar na Makamo Mwenyekiti wa CCM alipowasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiimba na viongozi mbalimbali hawapo pichani alipowasili katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuuwa CCM Dk. Bashiru Ali katika uwanja wa mpira wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Urais, Wabunge na Madiwani nchi nzima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanjwa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwa na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kushoto katika uzinduzi wa kampeni kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafuMh. Fredrick Sumaye.
viongozi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Mzee Philip Mangula akiwasili uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwa ameketi jukwaani kulia ni Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa na Katikati ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Ali Idd. 

(PICHA IKULU NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-DODOMA)

Thursday, August 27, 2020

Wakenya Waendelea Kuishukia Serikali yao Sakata la Kuzuia Abiria Kutoka Tanzania...


This is now getting messy and it is NOT healthy at all.


While in the past I was hard on TZ this time round we are on the wrong and we should quietly swallow our pride and fix this problem.


As long as we continue to exclude TZ from the list of the countries that can visit Kenya without being quarantined then they will continue doing this and I won't be surprised if this ended with border closure.


Firstly that list we gave out has a condition in that everyone must present a Covid free certificate which should have been issued less not more than 96 hours, why did we exclude TZ? It was an ill adviced move.


Now folks we cannot have our cake and at the same time eat it. If TZ are not good enough to be on the list then they just did the natural thing of stopping us also. We cannot be going to a neighbour as we wish but choose not to reciprocate.


Irony is that maids , trucks and bus drivers move without any restrictions at cross border points.


I feel for investors in the aviation industry...I feel for airlines.... I feel for our national carrier KQ. Our national carrier has its own challenges then add this where they cannot fly to a lucrative Nbi Dar route.


Finally it is not in our position to judge TZ on how they have handled the Corona crisis....we opted for more stringent measures which I support ...Sweden adopted a TZ similar approach as well and TZ continue with life. Last weekend popular simba sports club unveiled new players at parked Benjamin Mkapa Stadium where they played Vital O SC of Burundi.


KLM. Qatar. Emirates. Ethiopian.....all fly to Dar and Kili eating  lunch meant for KQ as immediate neighbours.


TZ is our biggest trading partner and we share one of the longest borders and we speak the same national language. 


I appeal to H.E to step in and help resolve this... with one call I believe he can do it. 


Mohammed Hersi

Chairman

Kenya Tourism Federation


Source

Aua mchepuko na mtoto baada ya kuufumania nyumbani kwake na rafiki yake

Na Clavery Christian Bukoba Kagera.
Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia kijana mmoja aitwaye Derick Dambuve mwenye umri wa 26 kwa kumuua mkwe wa mtu, Helda Amon (28) na mwanae Gradnes Amon (2) baada Helda kufumaniwa akifanya tendo la ndoa na Kajere Ibrahim (mchepuko mwingine) nyumbani kwa Derick.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa tukio hilo limetokea Agosti 22, mwaka huu kijiji cha Mukoma wilaya ya Ngara mkoani Kagera na uchunguzi wa awali umebainisha kuwa Helda alikuwa mke wa mtu, yeye na mwanae Gradnes walikwenda kijiji cha Mukoma kwa ajili ya kushiriki mnada wa gulio, akiwa gulioni hapo aliingia kwenye kilabu cha pombe ambako ndiko alikokutana na Derick na kuanzisha mahusiano.

"Baada ya kuanzisha mahusiano siku hiyo hiyo walikubaliana kuwa wangekuwa pamoja usiku huo, ndipo Derick alipomkabidhi Helda kwa rafiki yake (Alex Gray) ili mpeleke nyumbani kwake atamkuta baada ya kumalizia kufanya kazi ya ujenzi ambayo alikuwa hajaikamilisha.

Derick aliacha amewanunulia pombe akaenda kumalizia kibarua chake, walipomaliza kinywaji Alex alimpeleka Helda nyumbani kwa Derick na kufikisha salama akamuacha akimsubiria mwenyeji wake," alisema Malimi.

Malimi alisema wakati Helda na mwanae wanaendelea kumsubiri Derick nyumbani hapo ndipo Kajere alipofika ambaye naye alimuomba Helda waanzishe mahusiano ombi ambalo lilikubaliwa na kuanza kutenda tendo la ndoa.

"Wakati wakiendelea kutenda tendo la ndoa nyumbani kwa Derick ndipo Derick mwenyewe aliporudi nyumbani na kuwakuta bado hawajamaliza na baada ya Kajere kugundua kuwa wamefumaniwa alifanikiwa kumkimbia na kumuacha Helda.

Kufuatia fumanizi hilo, Derick alimpiga Helda kwa kutumia silaha mbalimbali ikiwemo kifaa cha mazoezi cha kunyanyua kwa ajili ya kutunisha kifua na kumsababishia mauti.

Baada ya Derick kuwa tayari amemuua Helda, naye mtoto Gradnes alianza kulia jambo lililosababishia Derick hasira na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na kifaa hicho cha mazoezi na kusababisha kifo cha mtoto huyo."

Malimi alisema kwa sasa Derick anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Helda na mtoto wake Gradnes na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wednesday, August 26, 2020

Nilikuwa Nadanga Sana Kabla ya Kuolewa...Haitham Afunguka


HAITHAM Kim ni moja kati ya wasanii wanaokuja kwa kasi kunako anga la Bongo Fleva, amefanya vizuri kupitia ngoma zake kama Ananichora, Yaishe na Nionyeshe.

Risasi Jumamosi limezungumza naye, ambapo pamoja na mambo mengine, amezungumzia suala la yeye kujihusisha na uuzaji wa mwili wake (kudanga)

Risasi: Umeshawahi kudanga?

Haitham: Ndiyo, nimeshawahi kudanga kabla sijaolewa.

Risasi: Changamoto gani ambazo ulizipitia kipindi unadanga?

Haitham: Yaani unakuta unaenda na mtu mnakubaliana kiasi fl'ani, ikifika asubuhi kakukimbia au anakuambia ngoja niende Bank nakurudia, lakini harudi, jambo lingine unaweza ukakopwa na usilipwe. Kwa hiyo, hayo mambo yapo na nilikuwa napitia wakati mgumu sana.

Tuesday, August 25, 2020

Sababu na athari zitokanazo na kitambi

Utafiti  umegundua  kwamba  kuna  idadi  kubwa  sana  ya wanawake  na  wanaume  wanao  sumbuliwa  na  tatizo  la  kuwa  na matumbo  makubwa  kiasi  ama  vitambi  kwa  lugha  nyingine. Uchunguzi wetu  umetuwezesha  kubaini  kuwa  katika  watu  kumi  wanao  tembea bararani  angalau  watatu  kati yao  wanasumbuliwa na  tatizo la kitambi.

Sababu  kuu  za tatizo la  kitambi  ni  pamoja  na;

  • Ulaji  mbovu  wa  vyakula ( Ulaji usio zingatia  mlo  kamili ).
  • Ulaji  mbovu  wa  vyakula  unajumuisha   ulaji  wa  vyakula  vya  aina moja  kwa  wingi  kupita  kiasi  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo, mfano  ulaji  wa  vyakula  vya  mafuta  mafuta  kwa  wingi kupita kiasi.
  • Unywaji  wa  pombe  kupita  kiasi
  • Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo pamoja  na  sababu  nyinginezo.


Athari  za  tatizo  la  kitambi  ni  pamoja  na :

  • Kuwa  katika  hatari ya  kushambuliwa  na  magonjwa  ya  hatari kama  vile  kisukari, moyo  na  presha.
  • Kutokuwa  na  uwezo  wa  kumudu  tendo  la  ndoa (  kwa  wanaume )
  • Kupunguza   mvuto  wa  kimapenzi (  kwa  wanawake na  hata  wanaume  pia  )
  • Kupoteza  fedha  na  muda  mwingi  katika  kuhangaika  kutafuta tiba  ya  tatizo   pamoja  na  athari  nyinginezo  lukuki.


Ndejembi, Kibajaji wapitishwa Ubunge Chamwino na Mvumi, waahidi kampeni za kistaarabu

 

BAADA ya kupitishwa na Chama chao cha Mapinduzi (CCM) na kisha kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa leo wagombea wa Ubunge, Deo Ndejembi wa Jimbo la Chamwino na Livingstone Lusinde 'Kibajaji' wa Mvumi wamerudisha fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Dodoma, Athuman Masasi.


Wagombea hao wote majimbo yao yapo katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo wameahidi kufanya kampeni za kistaarabu huku wakiahidi kushughulika na kero za wananchi.


Akizungumza baada ya kurudisha fomu mgombea wa ubunge Chamwino, Deo Ndejembi amesema anaamini kwa mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dk John Magufuli ni wazi watapata kura nyingi za ndio kutokana na imani kubwa ambayo serikali imejenga kwa wananchi.


" Nakishukuru chama changu kwa kunipitisha niwaahidi ndugu zangu wa Chamwino kwamba ninakuja kufanya kazi ya kuwatumikia nyinyi, ninakuja kushirikiana na serikali yetu kuwaletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi," Amesema Ndejembi.


Kwa upande wake Lusinde amewataka watanzania kumpigia kura nyingi za ndio Rais Magufuli ili kumpa heshima kwa utendaji wake uliovunja rekodi nchini na nje ya Nchi.


" Wananchi wenzangu wa Chamwino ni ahadi yetu kwenu kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuwatumikia, mmeona namna ambavyo Rais wetu amefanya kazi kubwa ikiwemo kuifanya Nchi yetu kuwa na uchumi wa kati hata kabla ya 2025 ambapo tulikua tumejiwekea malengo," Amesema Lusinde.

Sunday, August 23, 2020

Picha : DIAMOND PLATINUMZ, MO DEWJI NA MANARA GUMZO SIMBA DAY


Diamond Platinumz na wanenguaji wake wakitoa burudani kwa mashabiki kwenye tamasha la SIMBA DAY leo katika uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji akishiriki kutoa burudani kwenye jukwaa pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz kwenye tamasha la SIMBA DAY leo katika uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mo Dewji akisakata burudani

Helikopta iliyowabeba Diamond Platinumz na Haji Manara ikiwa inazunguka uwanja wa Mkapa kabla ya kutua
Mashabiki wa Klabu ya Simba waliojitokeza kuipa sapoti timu yao kwenye tamasha la SIMBA DAY
Wachezaji wa timu hiyo wakifanya mazoezi kabla ya kuanza mchezo 
Msanii Diamond Platinumz akitoa burudani 
Msafara wa Diamond Platinumz na Haji Manara ukiteremka kwenye Helikopta katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kwenye tamasha la SIMBA DAY
Mchezaji Shomari Kapombe akipasha misuli kabla ya mchezo
Helikopta ikitua uwanjani hapo
Madencer wa Diamond Platinumz wakitoa burudani kwa mashabiki waliojitokeza uwanjani 
Picha kwa hisani ya Simba SC Tanzania

Thursday, August 20, 2020

Ujumbe wa Mwana FA baada ya kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Muheza Tanga



Baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kamati yake kupitisha majina ya wagombe wa Ubunge, Udiwa na viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi CCM hivi leo.

Baadhi ya wadau wa muziki wameteuliwa ambao ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva Mwana FA na meneja wa Diamond Platnumz Bbutale.


Baada ya uteuzi huo Mwana FA  ameandika ujumbe huu 

"Mungu ni mwema sana, Leo ni miongoni mwa zile siku chache, mimi nimeishiwa na sina la kusema, alama nyingine kuhusu ukubwa wa Mungu"



Mtoto Mwingine Atupwa Chooni Kagera



MTOTO mwingine wa kike mwenye umri wa siku tatu, ameopolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye choo cha Zahanati ya Mshikamano wilayani Ngara mkoani Kagera akiwa hai.

Hilo ni tukio la pili kutokea wilayani humo, kwani Mei 21 mwaka huu, mtoto Isabela aliopolewa akiwa hai kwenye choo cha Shule ya Msingi Murganza wilayani humo na jeshi hilo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, Hamis Dawa, amesema walipata taarifa ya kutupwa kwa kichanga hicho katika choo cha Zahanati ya Mshikamano kupitia kwa Jeshi la Polisi wilayani humo.

"Baada ya taarifa hiyo, tuliwatuma askari wawili ambao ni ZM 3338 Sajenti Bahati Rudisha na FC 3802 Amos Mwita, ambao walifanikiwa kumuokoa mtoto huyo akiwa hai.

"Mtoto huyo tumemkabidhi kwenye Hospitali ya Mshikamano kwa ajili ya matibabu wakati huo Jeshi la Polisi likiendelea kumtafuta mama wa mtoto huyo aliyemtupa kwenye shimo la choo," alisema kamanda Hamisi Dawa.

Kwa mujibu wa Kamanda Dawa, kichanga hicho ambacho kilikuwa bado hakijakatika kitovu, kiliopolewa katika choo hicho kilichokuwa kinatumika, hivyo baada ya askari hao kubomoa mfuniko wa choo, walikiona kikiwa kinaelea.

"Mtoto hakukutwa na majeraha, bali alikuwa na afya njema, hivyo wahudumu wa afya hospitalini, wanaendelea kumfanyia uchunguzi wa kitabibu

"Tunashirikiana na watu wa Ustawi wa Jamii na wahudumu wa afya kitengo cha afya ya uzazi, ili kuweza kutoa elimu kwa akina mama ambao ndiyo wanaobeba ujauzito, jinsi ya kulea na kukabiliana na changamoto za kifamilia zinazowasababishia kutenda ukatili kwa watoto kama huu," alisema Kamanda Dawa.


Source

Picha : ASKOFU SANGU AONGOZA IBADA YA MASIFU YA JIONI

Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu,leo Jumatano Agosti 19,2020 ameongoza Ibada ya masifu ya jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kutoa daraja Takatifu la Upadre kwa Mashemasi sita ambapo watatu ni wa jimbo la Shinyanga ,wawili ni wa shirika la Mtakatifu Agustino na Mmoja ni wa shirika la SMA.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na Mapadre,Watawa,na Waamini kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya jimbo Katoliki.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu ameongoza Ibada ya masifu ya jioni .PICHA KWA HISANI YA RADIO FARAJA FM STEREO

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...