Sunday, December 29, 2019

Diamond Platnumz Apokelewa Kishujaa Kigoma

Mwanamuziki Diamond Platnumz amepokewa na mabango wakati akiwasili stesheni ya Nguruka Mkoani Kigoma katika kuadhimisha miaka yake kumi katika muziki.

Umati wa watu umejitokeza katika stesheni ya Nguruka Mkoani Kigoma wakiwa na mabango yaliyobeba jumbe mbalimbali kwa mwanamuziki huyo.

Moja ya mabango hayo lilikuwa limeandikwa "Karibu Diamond kwenu Kigoma tuijenge Kigoma, Sisi Nguruka tulishaanza ujenzi wa madarasa saba na vyoo 12. Tunaomba tuunge mkono, watoto 494 hawana pakusoma."

Diamond aliyeanza safari ya kuelekea Kigoma jana Desemba 28, 2019 akiwa na mashabiki wake katika treni lengo lake kubwa ni kujumuika na watu wa mkoa huo kusheherekea miaka kumi tangu kuanza muziki.

Nguruka ikiwa ndio stesheni ya kwanza unapoingia Mkoa wa Kigoma, Diamond alikutana na umati wa watu ukimsubiri.

Baada ya kuwasili eneo hilo Diamond alipanda jukwaani na kuanza kuwaimbisha wakazi hao wimbo wa Baba lao .
Hata hivyo ilifika mahali mzuka ukampanda kweli kama moja ya kibwagizo kilichopo katika wimbo huo kinachosema 'mzuka ukipanda hata nguo nitavua, nivue muone'walipoitikia mashabiki akavua fulana yake aliyokuwa ameivaa ambapo watu wake waliichukia na baadaye kumrudishia



Source

Monday, December 23, 2019

WAJAWAZITO WAIDAI SERIKALI - "TWENDE NA WAUME ZETU KLINIKI"

Na Abby Nkungu - Manyoni
Imeelezwa kuwa moja ya sababu ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kukumbwa na utapiamlo ni kutokana na baadhi ya wanaume kutokuwa na tabia ya kwenda kliniki na wenzi wao pindi wanapokuwa wajawazito ili wakapatiwe elimu na ushauri wa Lishe bora kwa Mama na Mtoto.

Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Muhalala katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida walisema kutokana na mfumo dume katika jamii nyingi ambapo baba ndiye mtoa uamuzi na mmiliki wa kipato katika familia,wengi wa wajawazito hushindwa kupata lishe bora kwa kukosa fedha za kununua mahitaji muhimu kulingana na ushauri wa kitaalamu.

Walisema kuwa hali hiyo husababisha lishe duni isiyokuwa na virutubisho muhimu kwa mtoto aliye tumboni na hata baada ya kuzaliwa hali ambayo walidai huendelea kutokana na wanawake wengi kuishi kwa kuwategemea waume zao ambao hawajui umuhimu wa lishe bora.

"Hebu fikiria kwa baba ambaye ni mlevi kupindukia, utoke kliniki eti ukamueleze unatakiwa upate lishe bora kwa afya yako na mtoto aliye tumboni, hawezi kukuelewa katu", alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Bunku mkazi wa Muhalala Wilayani Manyoni.

Alieleza kuwa tatizo hilo ni moja ya sababu ya baadhi ya watoto kupata utapiamlo kutokana na lishe duni inayochangiwa na baadhi ya wazazi wa kiume kutojua umuhimu wala kuwa na elimu ya lishe bora.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanawake wanasema kuna haja kwa Serikali kutunga Sheria itakayowalazimisha wanaume kwenda na wenzi wao kliniki kabla na baada ya kujifungua.

Walidai kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza tatizo la utapiamlo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano iwapo akinababa, ambao ndio watoa uamuzi, watapata elimu na kujua umuhimu wa lishe bora kwa mama na mtoto.

Ofisa Lishe mkoa wa Singida, Teda Sinde anasema ukosefu wa lishe bora kwa mjamzito husababisha udumavu kwa mtoto aliye tumboni na hata baada ya kuzaliwa huathiri ukuaji wa ubongo na maungo ya mwili wake; hivyo kudumaza maendeleo ya ukuaji wake kwa ujumla.

Takwimu za utafiti wa kitaifa za mwaka 2018 juu ya hali ya lishe mkoani Singida zinaonesha kuwa asilimia 29.8 ya watoto walio chini ya miaka mitano wana udumavu, asilimia 5 ukondefu na asilimia 15 wana uzito mdogo.

Kadhalika, utafiti huo unabainisha kuwa asilimia 27.9 tu ya watoto hao ndio walionyonyeshwa maziwa ya mama kwa kipindi cha miaka miwili kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya na asilimia 3 tu ya watoto walio chini ya miaka miwili ndio angalau hupata mlo unaokubalika katika tafsiri ya lishe bora. 

Friday, December 20, 2019

Mwanamke bora katika maisha ya ndoa hujengwa na mambo haya

Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo;

Uvumilivu
Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung'uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo.

Upendo wa dhati
Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. Wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni upendo wa dhati na uhalisia.

Utii kwa jamii
Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka  ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii  kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa.

Uaminifu katika jamii
Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote.

Unyenyekevu wa kweli
Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima.

Uwajibikaji wa dhati
Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake.

Ushirikiano wa dhati
Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora.

Utaratibu wa kazi/mpangilio
Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako.

Thursday, December 19, 2019

TRUMP APIGIWA KURA NYINGI ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA


Baraza la Wawakilishi la Marekani limepiga kura kuridhia kushtakiwa kwa Rais Donald Trump kwa kutumia vibaya madaraka yake na kuingilia uchunguzi wa Bunge.



Mchakato wa mwisho wa kura utalihusisha baraza la Seneti ambalo litakuwa na mamlaka ya kuamua kama anaweza kuondolewa madarakani au la

Matokeo ya mchakato huo ni kama ulikuwa ukijulikana mapema kutokana na baraza hilo kuwa na wingi wa wabunge wa chama cha Democratic.  


Baada ya majadiliano ya masaa 10, wabunge walipigia kura vifungu viwili vya sheria; Shtaka la kwanza likiwa ni kutumia vibaya mamlaka aliyonayo lililotokana na madai ya kwamba Trump alijaribu kuishinikiza Ukraine kutangaza uchunguzi dhidi ya hasimu wake wa kisiasa na mgombea urais kupitia chama cha Democrats, Joe Biden.

Shtakala pili lilikua ni kuzuia shughuli za bunge la Kongresi kwasababu rais anadaiwa kukataa kutoa ushirikiano katika uchunguzi dhidi yake, kwa kukataa kutoa nyaraka za ushahidi na kuwazuwia wasaidizi wake kutoa ushahidi katika uchunguzi huo.

Kura katika kipengele cha kwanza cha uchunguzi, cha kutumia vibaya mamlaka zilikuwa 230 ndiyo na 197 hapana na kipengele cha pili cha kuzuia utendaji wa Kongresi zikawa 229 ndiyo na 198 hapana.

Baraza la wawakilishi lina nguvu ya kumshitaki rais kwa wingi mdogo wa kura, lakini baraza la Seneti litahitaji wingi wa theluthi mbili kumuondoa rais madarakani, hatua ambayo sio rahisi kufanyika. 

Rekodi zinaonesha kuwa hatua hiyo ni ya mara ya tatu kwa rais wa Marekani kushitakiwa.




MBOWE ADAI KUANZIA MWAKA 2020 CHADEMA HAITATEGEMEA TENA RUZUKU KUJIENDESHA


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimezindua mfumo wake mpya wa Kidigitali wa uendeshaji wa Chama hicho ambapo kitakuwa kikikusanya ada za Uanachama wa wanachama wake na kukifanya kujitegemea.


Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama  hicho uliofanyika leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, amesema mfumo utawasaidia kukusanya karibia Bilioni 15 kwa mwaka.

Mbowe amesema programu hiyo iliyozinduliwa leo Jumatano Desemba 18, 2019 inahusisha uandikishaji wa wanachama kidigitali, kufanya mikutano kidijitali pamoja na kampeni.

"Kila mwaka mwanachama anatakiwa alipie Sh1,000 ya ada, kwenye vikao hivi tunapendekeza iwe Sh2,500 kwa mwaka. Maana yake ni nini? Leo hii chama kinapata ruzuku ya Sh3 bilioni kwa mwaka. Gharama ya kufanya mkutano wa baraza kuu ni zaidi ya Sh1 bilioni kwa hiyo ruzuku peke yake haitoshi."

"Kupitia Chadema Digital tuna digital fund raising, tumekubaliana kuchangia Sh2,500. Asilimia 90 wana Chadema wana simu za mkononi, kila mwanachama akilipa kwa simu tutapata Sh15 bilioni kwa mwaka."

Amesema kupitia vikao vyao wataibadilisha katiba ya Chadema ili kuruhusu mfumo huo ufanye kazi vizuri, "tunahitaji kujenga chama cha kujitegemea na hili msajili usikie, maana yake kuna watu wanafikiri chama kinategemea sana ruzuku."

Amesema kutokaa na mfumo huo, chama hicho sasa hakihitaji tena kufanya mikutano ya hadhara ili kupata wanachama wapya.


Wednesday, December 18, 2019

Mambo 5 ya kuficha unapokuwa kwenye ndoa yako


Yafuatayo ndiyo mambo matano ya kuficha unapokuwa kwenye maisha ya ndoa;

Tendo 
Maisha yenu ya mahusiano ya kimwili  (sex) na mwenzako ni marufuku kumwambia mtu yeyote kwa gharama yoyote. Funga mdomo; iwe ni nzuri au mbaya. Ni mwiko kuwambia watu! (watu ni pamoja na mama yako, ndugu, marafiki, viongozi wa dini, n.k.)

Utamaduni 
Utaratibu wenu wa kufanya mambo na mtindo wa maisha. Kwa mfano, sio lazima kuwaambia watu mambo yenu ya ndani ikiwemo mipango yenu ya baadae ya kifamilia au biashara, mambo ya watoto wenu, n.k. Ikibidi kusema, basi iwe ni kwa sababu maalumu sana ya kujenga watu wengine na kufundisha wengine sio kuanika tu maisha yenu hovyo; hasa mtandaoni. Ni muhimu kuchagua kwa makini kitu cha kuweka hadharani kwa maana ukitoa jambo hutaweza kulirudisha wala kulizuia lisisambae; litaenda hadi usikotaka, litaendea tu!

Ugomvi 
Hakuna faida yoyote ya kusema magomvi yenu ya kwenye ndoa. Mara nyingi, tabia ya kusema magomvi yenu itawapunguzia heshima mbele ya jamii. Mara chache sana tabia hiyo ina faida, ila kila palipo na faida ya kusema magomvi, hasara ni kubwa zaidi kuliko faida. Chagua mwenyewe!

Pesa 
Kipato chenu na pesa zenu ni siri. Wacheni watu waone kazi zenu na jinsi mnavyowasaidia wengine sio kujisifia pesa!

Siri 
Ni mwiko kutoa siri za ndoa! Kama mwenzako kasema, "hii ni siri" au "usimwambie mtu!" Au "nimekwambia wewe tu!", n.k. Hakikisha husemi kwa gharama yoyote, la sivyo hatakuamini tena! Na hasara yake ni kwamba, hatakuamini hata katika mambo mengine mengi tu! Tabia ya kutoa siri ni mbaya na inaweka ufa usiozibika kwa urahisi.

Tuesday, December 17, 2019

Mbinu muhimu za kuzingatia ili kufanikiwa katika biashara


Biashara nyingi zinazoanzishwa haziwezi kufikisha miaka mitano, na hata zinazofikisha huwa hazina maendeleo mazuri.

Hii ni kutokana na sababu biashara nyingi huanzishwa kiholela, kienyeji, kimazoea, ukosefu wa mipango na mikakati ya biashara. Pia, ukosefu wa utafiti wa masoko na kukosa utaalamu na ujuzi mbalimbali katika biashara.

Katika kuanzisha biashara yako unatakiwa kujifunza mbinu na ujuzi mbalimbali kadri unavyozidi kuifanya ili iweze kufanikiwa. Kuna hatua ambazo ukizifuata biashara yako itafanikiwa.

Fanya utafiti
Ukishakuwa na wazo la biashara unayotaka kufanya, kinachofuata ni kuangalia uhalisia, jiulize je, wazo lako lina uwezekano wa kufanikiwa? Unahitaji kuendeleza wazo lako huku ukiendelea kufanya utafiti wa kina ili kupata uhalisia wa wazo lako kabla hujasonga mbele.

Ili biashara ndogo ifanikiwe lazima ilenge kutatua tatizo, kukidhi mahitaji au itoe kitu ambacho soko linahitaji au kuongeza thamani katika biashara husikKuna njia kadhaa zinazoweza kukusaidia kutambua mahitaji hayo, hasa kufanya utafiti na kujaribu.

Kadri unavyotafiti soko, kuna baadhi ya maswali ambayo lazima huyajibu; kuna uhitaji wa bidhaa/huduma yako?; Nani anahitaji?; Kuna mtu au kampuni zinatoa bidhaa/huduma sawa?; Ushindani ukoje? Na namna gani biashara yako itaingia sokoni?

Tengeneza mpango wa biashara
Ili biashara yako iweze kufanikiwa huna budi kuwa na mpango wa biashara wa namna ya kulifanyia kazi wazo lako. Mpango wa biashara ni muongozo utakaokuongoza katika biashara yako kuanzia hatua ya awali hadi inavyokua.

Mpango wa biashara unaweza kukupa dira sahihi ya kile unachotegemea kufanikiwa katika biashara yako na namna gani umepanga kufanya kitu hicho kiuhalisia, unaweza pia kutengeneza mpango kazi katika daftari lako na ukaendelea kuboresha kadri mda unavyosonga mbele.

Pangilia matumizi fedha
Kuanzisha biashara ndogo hakuhitaji fedha nyingi sana, lakini itakuhitaji kufanya baadhi ya uwekezaji muhimu wa mwanzo kama vile ufahamu wa biashara husika na uwezo wa kugharimia kadri unavyoendelea kabla hujaanza kupata faida.

Weka pamoja daftari linaloonyesha makadirio ya gharama ya kuanzisha na kuendeleza biashara yako kama vile vibali, leseni, ada, ushuru, bima, vifaa, utafiti wa soko, matangazo, mshahara wa wewe binafsi na wasaidizi wako, gharama ya pango, uzalishaji, gharama za usafirishaji na usambazaji.

Chagua mfumo wako wa uhasibu
Biashara ndogo zinaendeshwa vyema na kwa mafanikio zaidi ikiwa kuna mifumo rasmi ya kifedha, mapato na matumizi ikifanya kazi kwa weledi na kibunifu. Moja ya mifumo muhimu zaidi katika biashara ndogo ni pamoja na mfumo imara wa uhasibu.

Mfumo wako wa uhasibu ni muhimu ili kuunda na kuongoza bajeti yako, kupanga viwango na bei, kufanya biashara na wengine pamoja na kodi.

Tengeneza eneo la biashara
Kuandaa eneo lako la biashara ni muhimu sana katika uendeshaji wa biashara yako iwe ni kwenye ofisi yako nyumbani, ofisi binafsi ya biashara au eneo lolote biashara yako inafanyika.

Inakubidi ufikirie kwa kina kuhusu eneo, vitendea kazi na mengineyo yote yanayohusika katika biashara yako, hakikisha eneo la biashara yako linafaa kwa aina ya biashara utakayokuwa unafanya.

Andaa timu yako
Ikiwa utakuwa unaajiri watu mbalimbali wa kukusaidia katika biashara yako, basi ni wajibu wako sasa kuanza kutengeneza timu yako.

Hakikisha unapata muda wa kutosha kuainisha nafasi, wajibu na sifa unazozihitaji katika kila kitengo cha biashara yako. Utawala wa biashara ndogo una muongozo rahisi katika kuajiri watu kitu ambacho ni muhimu kwa mwenye biashara ndogo kukua na kufanikiwa.

Tangaza biashara yako
Ikiwa biashara yako tayari imeanza huna budi kuanza kuvuta wateja katika huduma/bidhaa yako. Utahitajika kuanza na mbinu na mikakati ya kimasoko na mauzo ya kipekee sana ili kuweza kufikia wateja.

Hamisi wa Bongo Star Search uwezo wake mdogo



Leo niliangalia marudio ya Bongo Star Search ya Jumapili nimeona kabisa huyo Hamisi uwezo wake wa kuimba ni mdogo sana wakati wenzake uwezo wao ni mkubwa. Na amshukuru Mungu kufika hatua ya 10 Bora, hakustahili kufika hatua hiyo.

Ifike kipindi watanzania tuache unafiki pale Bongo Star Search wanaangalia kipaji na si mtu kutia huruma na washiriki wote wameenda kwa ajili ya kutafuta nafasi ya kuonekana na pia kutafuta maisha kupitia vipaji vyao.

Hitimisho: kiukwel Bongo Star Search ya mwaka huu ndio yenye vipaji vikubwa kuliko Bongo Star Search zote kwa mtazamo wangu

By Innocent Dependent/JF

Saturday, December 14, 2019

Aliyeachiwa kwa msamaha wa Rais azua taharuki stand ya Bukoba auwa mmoja ajeruhi watano



Na Clavery Christian Bukoba Kagera.

Jeshi la polisi mkoani Kagera linaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya watu wawili na majeruhi watano baada ya mtu mmoja anayesadikika kuwa ni mmoja kati ya wafungwa waliotoka jera kwa msamaha wa Rais kuwavamia na kuwashambulia kwa kuwachoma visu katika maeneo mbalimbali ya mwili katika eneo la stand kuu ya mabasi bukoba na kusababisha taharuki kubwa kwa raia.

Majeruhi watano ambao ni wananchi wa kawaida waliojeruhiwa na mtu huyo katika tukio hilo watatu wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa - Bukoba na hali zao zinaendelea vizuri japo kuwa mmoja kati yao alipata majeraha makubwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wanaeleza kwamba jana tarehe 13/12/2019 majira ya saa 03:00 usiku maeneo ya stand kuu ya mabasi Bukoba ghafla mtu mmoja asiyefahamika majina yake majina yake mwenye kati ya umri wa miaka 30-35 jinsia mwanaume alivamia watu waliokuwa hapo stand na kuanza kuwachoma watu visu na mtu wa kwanza kuanza kumchoma alikuwa Godfrey Gobadi miaka 30-35 ni mhaya dereva wa bajaji ambaye alimchoma kisu tumboni na kumsababishia kifo papo hapo.

Aidha mtu huyo alizidi kusababisha hofu na taharuki kubwa kwa watu wa eneo hilo alipoendelea kuwavamia na kuwachoma visu watu wengine na kujeruhi watu watano.

Baada ya mtuhumiwa kufanya vitendo hivyo wananchi wenye hasira kali walimvamia na kuanza kumshambulia na kumuumiza vibaya na baadae askari polisi waliokuwa doria waliweza kufika katika eneo hilo na kufanikiwa kumuokoa mtuhumiwa asiendelee kushambuliwa lakini alifariki wakati akipelekwa hospitalini.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa chanzo cha tukio hilo hakijafahamika na uchunguzi bado unaendelea.

HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA (HKT) YAAZIMIA BENARD MEMBE, MZEE MAKAMBA NA KINANA WAITWE NA KUHOJIWA KWA TUHUMA ZINAZOWAKABILI


CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

TAARIFA KWA UMMA

KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
_______________

Ofisi ya CCM Mkoa, Mwanza
13 Disemba 2019

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Jijini Mwanza chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kabla ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa wajumbe walifanya ziara ya kukagua miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza. Wajumbe pia walipata muda wa kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maandalizi na maudhui ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) inayo ongozwa na Ndugu Rais John Pombe Joseph Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Ndugu Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo mafanikio makubwa ya kimaendeleo yamepatikana.

Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.

Wanachama hao ni;-

1.    Ndg. Januari Makamba (Mb)
2.    Ndg. Nape Nnauye (Mb) na,
3.    Ndg. William Ngeleja (Mb)

Kikao cha HKT kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwamo kufukuzwa uanachama.

Wakati uo huo, Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama wafuatao;-

1.    Abdulrahman Kinana
2.    Mzee Yusuf Makamba na,
3.    Benard Membe

Waitwe na Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.

Awali Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina ya Wagombea wa nafasi za Uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-

1.    Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha

a.    Ndg. Batilda Salha Buriani
b.    Ndg. Zelothe Stephen Zelothe
c.    Ndg. Bakari Rahibu Msangi

2.    Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa

a.    Mafanikio Paulo Kinemelo
b.    Hilary Adelitius Kipingi
c.    Lucas Felix Lwimbo

3.    Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Mtwara

a.    Petro Mwendo Mwendo
b.    Mustafa Nguyahamba Mohamed
c.    Selemani Manufred Sankwa

4.    Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Dodoma

a.    Ndg. Damas Mukassa Kasheegu
b.    Baraka Andrea Mkunda
c.    Christopher Thomas Mullemwah

5.    Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani

a.    Mary Daniel Joseph
b.    Fredrick Gasper Makachila
c.    Samaha Seif Said

Licha ya hamasa kubwa waliyokuwa nayo wajumbe wa HKT kutokana na kazi nzuri ya Serikali ya CCM, Ndg. Magufuli amesisitiza kazi ya Urais ni ngumu sana na yeye ataheshimu utamaduni na desturi za CCM, Kanuni, Katiba ya CCM na Katiba ya Nchi na kwamba CCM ni kiwanda cha kuzalisha viongozi na kwa utaratibu ambao chama kimejiwekea kitampata mtu bora zaidi atakayepokea uongozi baada yake.

Nawashukuru sana viongozi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya Chama chetu kwa kuzisimamia vizuri Serikali zetu mbili na hivyo kuwezesha kupatikana mafanikio makubwa katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM. Tukaendelee kujenga umoja, kuimarisha ujenzi wa Chama chetu na tunapoelekea katika chaguzi zinazokuja tukaepuke makundi, na tuendelee kuisimamia Serikali ikiwamo kukagua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yetu, amesema Ndg. Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na,




HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI

Kanuni za kuandaa kitalu cha mbogamboga



Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m (ama urefu unaoona wewe kuwa unakufaaa ila tu upana ubaki kuwa 1mita) . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.

Weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1 kwenye tuta changanya vizuri na udongo.

Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati wa kusia ili miche isisongamane.

Funika mbegu na weka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo unatakiwa kuwa na unyevu kiasi mpaka mbegu ziote.

Nyasi ziondolewe mara tu mbegu zikiota .

Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe katika hali ya usafi.

Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie umri wa kupandikiza shambani.

Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji.

KUMBUKA:siku za ukaaji wa mbegu kitaruni inategemeana na aina ya mbegu ama zao.

Friday, December 13, 2019

JOSEPH Kusaga "FIESTA Haijawahi Kuingiza FAIDA Miaka Yote..Naambiwa Niandike Barua Kupiga Nyimbo za Wasafi"

JOSEPH Kusaga "FIESTA Haijawahi Kuingiza FAIDA Miaka Yote..Naambiwa Niandike Barua Kupiga Nyimbo za Wasafi"

VIDEO:

VIDEO: Afisa tabibu atimua mbio baada ya kupokea rushwa ya elfu 15/ampa mgonjwa dawa tofauti


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annaclair Shija ameeleza tukio la    Afisa Tabibu  wa hospitali ya wilaya hiyo anayefahamika kwa jina la Kimweri aliyekimbia mbio baada ya kuwekewa mtego kupokea rushwa ya shs. 15,000 na kuipokea  kutoka kwa mama mwenye mtoto mchanga  mgonjwa wakike mwenye umri wa miezi mitano wa kijiji cha Vunta kilichopo ukanda wa milimani mwa wilaya hiyo.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Kabla Hajaingia Kwenye Siasa Mbowe Alikuwa DJ mmoja Matata sana


Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA  Freeman Aikael Mbowe kabla hajawa Mwenyekiti wa chama hiki alikuwa ni DJ Matata sana enzi zake, kwa sasa tunaweza kumuita mstaafu katika hii tasnia ya u DJ. 

Thursday, December 12, 2019

Waziri Hasunga awataka wakandarasi wa mradi wa umwagiliaji wakajisalimishe polisi



Na Ahmad Mmow, Lindi.

Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga amewataka wakandarasi wanaojenga miundombinu ya skimu ya mradi wa umwagiliaji wa Nanganga, wakajisalimishe kituo cha polisi iwapo watashindwa kumaliza kazi hadi tarehe 4, Januari, 2020 kama walivyohaidi.

Waziri Hasunga ametoa agizo hilo kwa wakandarasi hao leo katika kijiji cha Nanganga, wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi baada ya kupokea taarifa za ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na kampuni za  D&L(T) Ltd na Haricom International Ltd.


Hasunga alisema nijambo lisilokubalika kusikia wakandarasi hao wameshindwa kumaliza kazi kwa wakati kwa mujibu wa mkataba. Ingawa waliongezwa muda mara mbili. Hatahivyo hadi leo hawajamaliza ujenzi huo.

Alisema wakandarasi hao( D&L(T)Ltd na Haricom International Ltd)  ambao wote wamehaidi kumaliza kazi hiyo tarehe 4, Januari, 2020 wasipofanya hivyo wasisubiri kukamatwa. Bali waende kituo cha polisi  kwa hiari yao. Huku akimtaka mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ahakikishe hilo linafayika iwapo hadi muda huo watakuwa hawajamaliza na kukabidhi kazi hiyo.

 Waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo aliyeonesha kuchukizwa na ucheleweshaji huo aliweka wazi kwamba miradi mingi ya umwagiliaji haiendi vizuri. Ingawa serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia ujenzi wake. Hata hivyo haikamiliki.

 '' Wakandarasi acheni utani na serikali. Hata waandisi wa kutoka tume ya umwagiliaji. Muda huu uliobaki hautoshi kumaliza ujenzi huu. Hata hivyo kwakuwa mmehaidi wenyewe basi msipo maliza nendeni polisi wenyewe," Hasunga alisema.

 Waziri Hasunga alibainisha kwamba lengo la serikali nikuona miradi yote ya umwagiliaji inakamili ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao ya kilimo. Kwani nchi inauwezo wa kuuza chakula nje iwapo azima ya serikali itatimizwa kikamilifu kupitia miradi hiyo.

Mbali na hilo, waziri Hasunga alitilia shaka makadirio ya kazi na malipo ya kazi hizo kwa wakandarasi. Kwani kazi zinakuwa ndogo kuliko malipo. Nakuongeza kusema; "Huku kwenye miradi ya umwagiliaji kuna shida. Haiwezekani mita moja ya mtaro ichimbwe na kujengwa kwa shilingi laki tano. Ni bora mngewapa wananchi wangechimba kwa gharama nafuu,''.

 Aidha aliwataka wakulima kuanza kuzalisha mazao kwakutumia sikimu hiyo ili serikali ishawishike kupeleka fedha  nyingine kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo. Huku akiwataka wataalamu wa tume ya umwagiliaji wasaidie kuzifanya sikimu hizo ziwe za mfano katika uzalishaji.


Katika hatua nyingine waziri huyo amewataka maofisa wa idara ya ushirika wahakikishe wakulima wa korosho waliouza korosho zao katika chama cha msingi cha ushirika cha Nanganga( Nanganga AMCOS) ambao hawajalipwa kwa zaidi ya siku kumi tangu zinunuliwe, wawe wamelipwa ndani ya siku tatu kuanzia leo.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuongeza safari za treni ya abiria Dar-Moshi



Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema lipo mbioni kuongeza safari za treni ya abiria kati ya Dar es Salaam na Moshi kutoka mbili kwa wiki hadi tatu.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Masanja Kadogosa ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari wakati akizungumzia utendaji wa shirika hilo tangu mwaka 2015.

Amesema Watanzania wamepokea kwa shauku treni hiyo, kwamba kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka wamepata maoni mengi kuhusu kuongezwa kwa safari hizo.

"Hii ni treni ya Watanzania wametoa maoni na tumeyapokea tumeyafanyia kazi, tutaona ni jinsi gani tunajipanga kuhakikisha inakwenda Moshi mara tatu kwa wiki na kurudi Dar mara tatu,"

Kadogosa pia amezungumzia ukarabati wa mabehewa ya shirika hilo na kueleza kuwa wana nia ya kuyafufua na kuyaweka katika hali nzuri ili yatumike.

Kwa sasa treni hiyo inatoka Dar es Salaam kila Ijumaa na Jumanne na Moshi kila Jumatano na Jumamosi.

Treni hiyo ambayo imeongezwa mabehewa ya abiria kutoka saba hadi nane kuanzia Jumatatu iliyopita, ina madaraja matatu.

Behewa la daraja la tatu lina uwezo wa kupakia abiria 80 waliokaa, daraja la pili kukaa abiria 60 na daraja la pili kulala abiria 36 huku nauli ikiwa Sh16,500 (daraja la tatu), Sh23,500 (daraja la pili kukaa) na Sh39,100 daraja la pili kulala.

Aliyeachiwa Huru Kwa Msamaha wa Rais Afanya Tukio Arudishwa Rumande



Na Amiri kilagalila-Njombe

Mtuhumiwa mmoja aliyefahamika kwa majina ya Mstafa Msola maarufu kwa jina la (Hitler) aliyeachiwa huru kwa msamaha wa Rais mkoani Njombe amekamatwa tena na kuludishwa lumande kwa tuhuma za kuvunja nyumba ya kulala wageni kwa minajili ya kuiba.



Akizungumza na vyombo vya habari mjini Makambako mkoani hapa,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema Musa Msola ni mmoja wa wafungwa walioachwa huru siku ya jana mara baada ya msamaha wa Rais uliotolewa disemba 9 siku ya maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika.

"Akiwa mkoani Njombe kwanza aliomba msamaha mbele ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkuu wa mkoa wa Njombe kuwa anawasihi wenzake wawe ni watu wema,lakini ni masaa nane yamepita mtuhumiwa huyu aliyekuwa huru ilifika majira ya  saa tisa usiku,alijikuta ameshawishika kwenda kufanya  tukio la uvunjaji,na alienda kuvunja gesti moja Nang'ano iliyopo mtaa we Mwembetogwa hapa Makambako,na kwa kuwa wananchi wanaelewa jukumu lao la ulinzi waliweza kupeana taarifa usiku ule na alikamatwa"alisema kamanda Hamis Issa.


Kwa upande wake mtuhumiwa Mstafa Msola amesema anashindwa kujitetea kwa kuwa ameshawishika kufanya kosa hilo licha ya kuwa huru kwa msamaha wa Rais.

"Nimefanya kosa kubwa sana nashindwa kujitetea kutokana msamaha ulipotoka nilishkuru hivyo nimejikuta nimeingia tena kwenye kosa"alisema Mstafa

Mstafa Msola ni mmoja kati ya wafungwa 70 walioachiwa huru siku ya jana mkoani Njombe mara baada ya msamaha wa Rais akitokea gereza la Njombe lililoachia huru wafungwa 25

Wednesday, December 11, 2019

VIDEO:Aliyeachiwa kwa msamaha wa Rais aiba tena arudishwa mahabusu


Mtuhumiwa aliyefahamika kwa majina ya Mstafa Msola maarufu kwa jina (Hitlar) miongoni mwa wafungwa 70 aliyeachiwa siku ya jana mara baada ya msamaha wa Rais uliotolewa disemba 9 katika maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika ,aliyekuwa akitumikia kifungo chake gereza la Njombe amekamatwa tena na kurudishwa Lumande kwa tuhuma za kuvunja nyumba ya kulala wageni.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Mkuu Wa Mkoa Wa Mara Asimamia Zoezi La Kuachiwa Huru Wafungwa

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima akiongea na sehemu ya wafungwa 23 walioachiwa katika gereza la Musoma kati ya wafungwa 259 waliofaidika na msamaha wa Rais Mkoani humo.

Mhe Malima, ambae alikuwa ameongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mkoa wa Mara (RAS) Mhe. Carlo Mthaphula,  amewataka wafungwa hao wakamlipe fadhila waliyopewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kwenda kutenda mema na ya maendeleo katika jamii badala ya kuanza uhalifu upya.


Rais Trump asema mkurugenzi wa FBI hawezi kulijenga shirika hilo



Rais Donald Trump wa Marekani amemkosoa vikali Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la nchi yake, FBI, Christopher Wray, kwa kumpa ripoti isiyo sahihi.

Akitumia mtandao wake wa Twitter, Trump ameandika kuwa kamwe Wray hataweza kulijenga tena shirika hilo la ujasusi, ambalo anadai limeharibika vibaya.

Ukosoaji huu wa Trump unakuja siku moja baaa ya wizara ya sheria kusema imekosa ushahidi wa upendeleo wa kisiasa, wakati FBI ilipoanza kuchunguza mawasiliano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi mwaka 2016.

Kwenye mahojiano na kituo cha ABC News hapo jana, Wray alisema licha ya kwamba shirika lake limegundua mapungufu kadhaa, lakini uchunguzi huo ulifanyika kwa njia sahihi.

Monday, December 2, 2019

Mchungaji Msigwa Achaguliwa Uenyekiti Chadema Kanda ya Nyasa



Mbeya. Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa akibainisha kuwa safari ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini kuiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 imeiva.

Msigwa ametoa kauli hiyo leo Desemba Mosi, 2019 wakati akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Kanda ya Nyasa kwa kumchagua.

Msigwa ameibuka mshindi baada ya kupata kura 66 sawa na asilimia 62.5 kati ya kura 107 zilizopigwa na kuwashinda wapinzani wake,  wakili Boniface Mwabukusi  aliyepata kura 26 na Sadrick Malila 'Ikuwo'(14).

Amesema baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo wanaelekeza nguvu kuimarisha misingi imara ya chama hicho ikiwa pamoja na kujenga umoja na mshikamo kuhakikisha viongozi wa kanda hiyo hawayumbishwi kwa kurubuniwa.

 "Niwashukuru sana wajumbe wenzangu kwa kuniamini na kunipa ridhaa hii. Najua mzigo nilioongezewa  lakini niwahakikishie hiki chama kitajengwa na wenye moyo wa kujitoa na kusema hadharani bila woga."

"Adui yetu ni CCM tunapaswa kupambana naye kuanzia sasa na uchaguzi ujao ni mwepesi kwa kuwa kanda yetu hii safu (ya uongozi) mliyotupa ina watu makini," amsema Msigwa.

Mwananchi
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...