Thursday, December 12, 2019
Waziri Hasunga awataka wakandarasi wa mradi wa umwagiliaji wakajisalimishe polisi
Na Ahmad Mmow, Lindi.
Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga amewataka wakandarasi wanaojenga miundombinu ya skimu ya mradi wa umwagiliaji wa Nanganga, wakajisalimishe kituo cha polisi iwapo watashindwa kumaliza kazi hadi tarehe 4, Januari, 2020 kama walivyohaidi.
Waziri Hasunga ametoa agizo hilo kwa wakandarasi hao leo katika kijiji cha Nanganga, wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi baada ya kupokea taarifa za ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na kampuni za D&L(T) Ltd na Haricom International Ltd.
Hasunga alisema nijambo lisilokubalika kusikia wakandarasi hao wameshindwa kumaliza kazi kwa wakati kwa mujibu wa mkataba. Ingawa waliongezwa muda mara mbili. Hatahivyo hadi leo hawajamaliza ujenzi huo.
Alisema wakandarasi hao( D&L(T)Ltd na Haricom International Ltd) ambao wote wamehaidi kumaliza kazi hiyo tarehe 4, Januari, 2020 wasipofanya hivyo wasisubiri kukamatwa. Bali waende kituo cha polisi kwa hiari yao. Huku akimtaka mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ahakikishe hilo linafayika iwapo hadi muda huo watakuwa hawajamaliza na kukabidhi kazi hiyo.
Waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo aliyeonesha kuchukizwa na ucheleweshaji huo aliweka wazi kwamba miradi mingi ya umwagiliaji haiendi vizuri. Ingawa serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia ujenzi wake. Hata hivyo haikamiliki.
'' Wakandarasi acheni utani na serikali. Hata waandisi wa kutoka tume ya umwagiliaji. Muda huu uliobaki hautoshi kumaliza ujenzi huu. Hata hivyo kwakuwa mmehaidi wenyewe basi msipo maliza nendeni polisi wenyewe," Hasunga alisema.
Waziri Hasunga alibainisha kwamba lengo la serikali nikuona miradi yote ya umwagiliaji inakamili ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao ya kilimo. Kwani nchi inauwezo wa kuuza chakula nje iwapo azima ya serikali itatimizwa kikamilifu kupitia miradi hiyo.
Mbali na hilo, waziri Hasunga alitilia shaka makadirio ya kazi na malipo ya kazi hizo kwa wakandarasi. Kwani kazi zinakuwa ndogo kuliko malipo. Nakuongeza kusema; "Huku kwenye miradi ya umwagiliaji kuna shida. Haiwezekani mita moja ya mtaro ichimbwe na kujengwa kwa shilingi laki tano. Ni bora mngewapa wananchi wangechimba kwa gharama nafuu,''.
Aidha aliwataka wakulima kuanza kuzalisha mazao kwakutumia sikimu hiyo ili serikali ishawishike kupeleka fedha nyingine kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo. Huku akiwataka wataalamu wa tume ya umwagiliaji wasaidie kuzifanya sikimu hizo ziwe za mfano katika uzalishaji.
Katika hatua nyingine waziri huyo amewataka maofisa wa idara ya ushirika wahakikishe wakulima wa korosho waliouza korosho zao katika chama cha msingi cha ushirika cha Nanganga( Nanganga AMCOS) ambao hawajalipwa kwa zaidi ya siku kumi tangu zinunuliwe, wawe wamelipwa ndani ya siku tatu kuanzia leo.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...