Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema dirisha la usajili kwa vilabu vya Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili litafungwa Julai 31, 2019 huku usajili kwaajili ya michuano ya CAF kwa timu za Simba, Yanga, Azam na KMC ukifungwa Julai 10, 2019.
Sunday, June 30, 2019
Polepole Awapa Makavu Wanachama CCM....."Usitumie uongozi kama mali yako"
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema ugonjwa mkubwa ndani ya CCM ni ubinafsi na kuwataka kuacha kupendekeza wagombea ambao wananchi hawawataki.
Aidha aliwataka viongozi wa chama wakiwemo mabalozi wa nyumba 10 kuacha kupanga safu za watu wanaowataka badala yake wahakikishe wanasimamia utaratibu.
Polepole alitoa maaelekezo hayo kwa makamisaa nchini kote kukisema Chama cha Mapinduzi kinachofanya kazi zake chini ya Rais John Magufuli ili wananchi waelewe .Aliyasema hayo jana Jijini Arusha katika kikao maalumu cha kupokea Ilani ya Uchaguzi wa CCM 2015/2020 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha Julai 2018 hadi Machi 2019.
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema anayepanga safu, aliyepangwa katika safu, kanuni za chama zinatoa adhabu kwa wale wote waliosababisha ukiukwaji wa uchaguzi au uteuzi wa wagombea
"Chama hakiangalii mtu kwa sura, mtatandikwa adhabu kali, uongozi ni dhamana usitumie uongozi kama mali yako na wale wabaya nawaambia acheni kupanga safu na tunawakata wale wote wasioheshimu maadili ya chama…
"Acheni kupanga safu za uongozi na nitawasubiri kwenye sekretarieti nitahangaika na wewe ulalo ulalo hadi kieleweke kura hazipigwi na viongozi wa CCM zinapigwa na wanachama wa CCM hivyo achene mambo yenu," alisema.
Alisema kwenye serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wekeni watu wanaokubalika na kama mnaona hawakubaliki kata weka wengine na mwaka kesho kwenye udiwani, madiwani wa CCM wafanye mikutano katika kata zao na wasiofanya mikutano wote watajulikana.
Polepole alisema Tanzania imepata bahati ya kuwa na Rais wa kipekee kwani Rais Magufuli amevunja historia nchini katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi sita rais amejenga hospitali za wilaya 67 na vituo vya afya 353 nchi nzima.
Alisema yapo mengi mazuri Rais Magufuli amefanya ikiwa ni pamoja na kutoa ndege yake kwa ajili ya wananchi kuipanda na amenunua ndege kubwa mbili mpya, ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme wenye uwezo wa kuvuna megawati za umeme zaidi ya 2000.
Mwanaume Amwoa Mwanaume Mwenzake Bila Kujua
Mwanaume mmoja mkoani Mtwara amekaa na mwanaume mwenzake miezi minne bila kujua.
Kwa mujibu wa maelezo mahusiano yalianza baada ya kukosea namba wakafahamiana mpaka wakafikia maamuzi ya kuoana huku akijua ni wa kike.
Baada ya kufata taratibu wawili hao wakaoana lakini tatizo likaja wakati wa kujamiiana mwenzake wakawa kilasiku anasema anaumwa ikawa hivyo ndani ya miezi mitatu ndipo akaja gundua kuwa ni mwanaume mwenzake.
Kuhusu mavazi anasema mwenzake huyo huvaa kama mwanamke na kupika pia anajua hata kujiremba anajiremba hali iliyo mpelekea kutogundua.
DPP Akabidhi Madini, Vito Na Fedha Benki Kuu (BOT ) Zilizotokana Na Kesi Za Uhujumu Uchumi.
Jumla ya madini yenye thamani ya Sh.3,125, 704,456.12 yamekabidhiwa kwa Serikali kupitia Hazina baada ya kutaifishwa kutokana na kubainika yalikuwa yanatoroshwa nchini.
Mbali na kukabidhiwa madini na vito, pia Serikali imekabidhiwa fedha za kigeni ambazo nazo zimetaifishwa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi madini, vito na fedha hizo kwa Katibu Mkuu Hazina Dotto James, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amefananua kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) katika vipindi tofauti kati ya mwaka 2017 na mwaka 2018 imeendesha kesi mbalimbali.
Amesema kesi hizo zilikuwa zinahusiasana na utoroshaji au kukutwa na madini bila kuwa na kibali na katika uendeshaji wa kesi hizo washtakwa walitiwa hatiani na kuamriwa kulipa faini au kutumikia kifungo gerezani pamoja na amri ya kutaifishwa madini na fedha walizokutwa nazo wakati wakisafirisha madini hayo.
"Madini yaliyotaifishwa ni kilo 25.546 za dhahabu ,zaidi ya kilo 76,020.20(tani 76) za Colored gemstone, Tanzanite pamoja na fedha za kigeni za mataifa mbalimbali 15 zenye thamani ya Sh.1,023,608, 515.12.
"Kwa kuwa madini hayo yametunzwa sehemu mbalimbali kiasi kwamba uwezekano wa kupotea au kumbukumbu zake kupotea na kwa kuwa mali zote zinazotaifishwa zinakuwa mali za Serikali na Katibu Mkuu Hazina ndiye msimamizi wa mali hizo" ameeleza.
"Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anakabidhi kilo 25.5 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 913,954.72 sawa na Sh.bilioni 2,102,095,941,"amesema Mganga.
Akifafanua madini na vito, amesema kuna tani 76 na Carrats 2849 zenye thamani ya Dola za Marekani 2,638,349.95 sawa na Sh.bilioni 6,068,204.885 na Carrats 2,849 zenye thamani ya Dola za Marekani 3,803.32 sawa na Sh. milioni 888,409,000.
Pia Tanzanite gramu 888 zenye thamani ya Dola 3,197 sawa na Sh.bilioni 7,353,348 na fedha za kigeni za mataifa 15 ambazo ni sawa na Sh.1,023,608,515.12.

Saturday, June 29, 2019
Mabweni ya Shule ya Mtama Yateketea kwa Moto
MABWENI ya Shule ya Sekondari Mtama, mkoani Lindi, yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo ambapo taarifa za awali zinasema hakuna majeruhi ila vitu vyote vilivyokuwa ndani vimeteketea.
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, kupitia Twitter yake amesema wanafanya tathmini na uchunguzi wa chanzo cha tukio hilo.

Utoaji wa huduma za Afya kwa maskini si hiari ni wajibu - Mkurugenzi wa Ustawi
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dr.Ntuli Angelile Kapologwe amesema huduma jumuishi za afya kwa wananchi maskini si jambo hiari bali ni wajibu wa kila mtoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za Afya Nchini.
Dr. Ntuli amesema hayo wakati alipokutana na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita kuzungumzia masuala mbalimbali ya kiutendaji na namna ya kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa Jamii.
Dr. Ntuli amesema mwananchi masikini hapaswi kubaguliwa kwa sababu tu hawezi kuchangia huduma za Afya ni wajibu wetu kumhudumia kisha kujirdhisha kama kweli hana uwezo wa kulipa kisha kupewa msamaha kwa mujibu wa Sera ya Afya.
"Moja kati ya haki ya msingi za kila binadamu ni kufurahia viwango vya juu vya afya viwezekanavyo na sisi kama watumishi wa Serikali tunalo jukumu la kutoa huduma bora za afya zinazofikika na zinazopatikana kwa watu wote bila ubaguzi.
Msamaha katika huduma za Afya unahusishwa mama mjamzito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano lakini kwa mama yule ambaye ana Bima ya Matibabu inapaswa kutumika ili kuchangia na gharama hizo ambazo zitaenda kusaidia wananchi ambao hawana uwezo hivyo katika hili ni muhimu tuelimishe wananchi ili kuwa na uelewa wa pamoja," Alisema Dr Ntuli.
Aidha Dr.Ntuli aliongeza kuwa msamaha huu pia unalenga wazee wenye zaidi ya miaka sitini na wale wenye magonjwa sugu lakini msamaha huo utatolewa pale ambapo afisa usawi wa jamii wa hospital au kituo husika atajiridhisha pasipo shaka kuwa makundi haya yote yaliyotajwa kwenye msahama hawana kabisa uwezo wa kuchangia huduma za Afya.
"Kila mtoa huduma anapaswa kuelewa vyema kuhusu msamaha na nani analengwa kati msamaha huu, mwananchi yupi anapaswa kuchangia huduma na yupi anapaswa kupewa msamaha na mfahamu fika kuwa utaoji wa msamaha huu si kwa mujibu wa matakwa yetu bali ni Sera ndio imeelekeza hivyo kila mmojawetu atimize wajibu wake katika hili," alisema Dr, Ntuli.
Sambamba na hilo Serikali inaendelea kupanua utoaji wa huduma za afya kila inapowezekana, kuhakikisha upatikanaji wa dawa ni wa uhakika, wataalamu wa afya wanaajiriwa na kuendelezwa kulingana na mahitaji na wanapata motisha: Tunatarajia jitihada hizi zitawezeshe utoaji wa huduma za Afya kuzidi kuimarika kuanzia ngazi ya msingi, ninachowataka ni nyinyi kujituma kwa moyo na kuhakikisha wananchi wanakuwa na Afya njema na mnaokoa maisha ya watanzania alimalizia Dr.Ntuli.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dr. Japhet Simeo amemshkuru Mkurugenzi wa Afya kwa kukutana na watumishi wa Afya, kuskiliza changamoto zao, kutafuta ufumbuzi wa pamoja na kutoa maelekezo ya Serikali katika kuboresha huduma za Afya.
"Nikuhakikishie tu kuwa maelekezo uliyatoa tumeyapokea na tutayafanyia kazi kwa weledi na kufuata miiko ya Taalumu yetu ili kuhakikisha tunafanikisha ile dhana ya upatikanaji wa huduma za Afya kwa wote" alisema Dr. Japhet"
Source
Tundu Lissu Kwenda Mahakamani Kupinga Kuvuliwa Ubunge
Baada ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kusema Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amepoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge, mwanasiasa huyo ambaye anaendelea kuuguza majeraha ya risasi ughaibuni amesema atakwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.
Lissu alisema hayo jana Ijumaa Juni 28, 2019 wakati akizungumza na gazeti la Mwananchi kwa njia ya simu akiwa Ubelgiji, ambapo amesisitiza kuwa, tangu aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa Area D jijini Dodoma Septemba 7, 2019 amekuwa akipata matibabu nje ya nchi.
Amesema kwa hatua ya sasa, "Nitawasiliana na wanasheria wangu haraka iwezekanavyo ili kuona cha kufanya lakini Septemba 7 (mwaka huu) ambayo nilikwisha kusema nitarudi sitabadili, nitarudi na alichokifanya Ndugai ni kukoleza mjadala."
Jana Ijumaa, Spika Ndugai aliliambia Bunge hilo kuwa amewandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha kuwa kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kipo wazi.
Amesema hatua hiyo inatokana na Lissu kutojaza taarifa za mali na madeni na sababu ya pili kutokutoa taarifa kwa Spika mahali alipo.
Mara baada ya kushambuliwa kwa risasi Septemba 7 mwaka 2017 jijini Dodoma, mwanasiasa huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyo akahamishiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambapo alipatiwa matibabu hadi Januari 6, mwaka jana na kisha kuhamishiwa nchini Ubelgiji hadi leo.

Mbinu za kumfanya mwanamke akupende pasipo kumtongoza
Ushawahi kujikuta katika hali ambayo unashindwa kujua utaanza vipi kuongea na mwanamke? Ni mwanamke mzuri ambaye moyo wako unamtamani lakini akili yako inashindwa kutengeneza mawazo ya jinsi utakavyoanzisha stori na yeye.
Unabakiwa ukimuangalia akikupita mbele yako, ama mbaya zaidi anakuja kuchukuliwa na wanaume wasiokuwa na thamani yeyote kwa maisha yake. Unabakia na majutio na mawazo ya "kama ningeweza kujiamini mbeleni si ningem...." Well, tatizo hilo halijawahi kutokea kwako pekee bali kwa kila mwanaume wakati flani katika maisha yake na hatutaki lijitokeze tena mbeleni.
So chanzo cha wewe kutoweza kumtongoza huyu mwanamke ni kuwa akili yako ilikataa kutoa mazungumzo ambayo ungeweza kuyatumia kwa huyo mwanamke. Well, waonaje kwa mara moja tukubaliane na akili yako na tusitumie maongezi kuapproach mwanamke, na badala yake tutongoze kimya kimya?
Kutongoza kimya kimya ni mbinu rahisi sana, mwanzo ni rahisi kwa kuwa unapata kujua kama mwanamke anakupenda au la. So bila kupoteza wakati, hebu tuchambue mpango mzima.
Zifuatazo ndizo mbinu unazopaswa kuzitumia ili mwanamke akupende;
Kwa kutumia macho
Kila mtu anajua nishati inayotokana na kutumia macho. Macho ni kiungo ambacho wanaume wamebarikiwa nacho na akikitumia vizuri kinageuka kama silaha nzito wakati ambapo unaitumia kwa mwanamke. Ushawahi kujiuliza ni kwa nini wakati mwingine mwanamke anashikwa na aibu/haya wakati unapomwangalia? Ama je ushawahi kumskia mwanamke akisema kuwa usimwangalie machoni mwake? Hii ni kwa sababu macho yanaweza kutumika kuongea maneno ambayo mdomo unaweza kushindwa kuongea.
Wakati utajipata ukimwangalia mwanamke, mwangalie machoni halafu utoe tabasamu. Kumuangalia kunaonyesha unajiamini. Kutabasamu unamwonyesha kuwa wewe ni salama na anaweza kuongea na wewe.
Mfanye akugundue kupitia kutangamana kwako
Njia nzuri ya kusimama ili wanawake waweze kukutambua ni kupitia utangamano wako na wengine. Kujizunguka na wanawake wengi (haswa wale warembo) kutaashiria ya kuwa wewe ni aina ya mwanaume ambaye wanawake wanapenda kuwa naye. Hii itawafanya wanawake wengine katika hio sehemu kuwa na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani ambacho kinakufanya wanawake wapende kuwa na wewe. Hii automatically itawafanya wanawake kuwa na umbea kukuhusu, kuvutiwa kwako, na hata kuingiwa na wivu wa kwa nini haujawaingiza katika kundi lako.
Mbinu hii ni moja wapo ya kiutekaji ya wanawake, kimaumbile wanawake hupenda vitu ambavyo wanawake wengine hupenda. Hivyo kama wewe unamtaka mwanamke flani na hutaki kutumia maongezi, anza kutangamana na marafiki wake wote isipokuwa yeye, mwishowe utamwona akijileta yeye mwenyewe, tena ujitayarishe na mapema kwa kuwa atakuja na presha ambayo kama hukujipanga vizuri inaweza ikakulemea.
Mvutie na mwonekano wako
Ukitaka kumvutia mwanamke kiurahisi basi ni muhimu kubadilisha mwonekano wako. Mbinu hii tuliieleza kwa kina katika chapisho la jinsi ya kubadilisha mwonekano wako uwavutie wanawake. Kwa kawaida, wanawake wanapenda kushufu wanaume ambao wanavalia kinadhifu.
Lakini hapa usichukulie makosa. Kubadilisha mwonekano hakumaanishi ya kuwa unapaswa kuvalia nguo ghali ama za thamani ya juu. La hasha. Kubadilisha mwonekano kunamaanisha kuvalia nguo safi, nadhifu na ambazo zinaashiria hulka yako. Usijitese kuvalia nguo ambazo haziwiani na wewe kwani kwa mwanamke ni rahisi kukugundua kama umejeuka mwigo.
Wafanye wanawake wakufukuzie
Kufanya wanawake wakufukuzie inaweza kuwa rahisi sana. Kile ambacho unahitajika ni kutoka nje umakinike na kujifurahisha muda wote. Weka tabasamu katika uso wako na ujiinjoy wewe mwenyewe. Hii itamfanya mwanamke kukunotice na kutamani kuungana na wewe ili muinjoy pamoja.

Friday, June 28, 2019
Waziri Mkuu: Mpango Wa Blueprint Kuanza Julai Mosi Mwaka Huu
WAZIRI MKU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Julai Mosi mwaka huu Serikali itaanza kutekeleza Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini (Blueprint) kwa lengo la kurahisisha mazingira ya kufanya biashara.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 28) wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, jijini Dodoma. Amesema wakati kazi hiyo inaendelea Serikali itafanya ufutialiaji kuhusu utekelezaji wa mpango huo na kutathmini kama lengo limefikiwa.
"Utekelezaji wa mpango huo unakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kurahisisha mazingira ya kufanya biashara nchini, unaojidhihirisha kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo imefuta tozo kwamishi 54 zilizobainishwa kwenye mpango huo."
Waziri Mkuu ametaja tozo zilizoondolewa au kupunguzwa ni pamoja na zinazosimamiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Wizara ya Mifugo na Uvuvi hususan kwenye Sekta ya Mifugo, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Maji
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo unaleta tija, ameielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara ishirikiane na Ofisi ya Waziri Mkuu kusambaza blueprint pamoja na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa wizara zote kwa ajili ya kusimamia utekelezaji katika maeneo yao.
Amesema kupitia mpango wa bajeti ya 2019/2020, Serikali itaendelea kuweka mazingira rahisi ya ufanyaji biashara kwa kutoa unafuu katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na shughuli nyingine jumuishi.
Wakati huohuo,Waziri Mkuu amesema katika kukabiliana na kilimo tegemezi cha mvua hususani kwenye zama hizi za mabadiliko ya tabia nchi, Serikali kwa sasa inaboresha kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuwatoa wananchi katika kilimo hicho.
Amesema hatua zilizochukuliwa hadi sasa ni pamoja na kuunda upya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambayo inalenga kuiwezesha tume hiyo kusimamia ipasavyo shughuli za umwagiliaji. Pia Serikali imehamishia tume hiyo Wizara ya Kilimo ambayo ndiyo yenye dhamana ya kuendeleza kilimo nchini.
"Ili tuweze kufikia lengo la kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 475,056 za sasa hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2025, tayari nimeielekeza Wizara ya Kilimo isimamia kwa karibu na kutekeleza majukumu yake kwa weledi."
Waziri Mkuu amesema Wizara ya Kilimo inatakiwa ihakikishe inasimamia vema miradi 22 ya umwagiliaji inayoendelea sasa pamoja na miradi mipya minane itakayojengwa nchini katika pindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Ty Dolla Sign afutiwa mashtaka yake ya kukutwa na dawa za kulevya
Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa rapper Ty Dolla $ign amefutiwa mashtaka yote ya dawa za kulevya aliyowahi kufunguliwa mwaka 2018, hii ni baada ya kukamilisha darasa lake la mafunzo na elimu juu ya dawa za kulevya kama alivyokubaliana na Mahakama.
Inaelezwa kuwa baada ya Ty kuingia kwenye sakata hilo mwezi September 2018 na kukamatwa kwa makosa hayo ilibidi aingie kwenye makubaliano na waendesha mashtaka na kupanga kuwa endapo atafata masharti ya kukamilisha darasa hilo basi hana budi ya kufutiwa mashtaka yake yaliyokuwa yakimkabili.
Ty Dolla $ign alikamatwa September 2018 akiwa na wenzake sita katika mtaa wa Martin Luther King Jr. Dr Atlanta Marekani na kuelezwa kuwa Polisi walisikia harufu ya Marijuana pamoja na Cocaine Latina gari alilokuwa akiendesha Ty na ndipo hapo alipofunguliwa mashtaka hayo.

Kampuni Ya China Yawekeza $1 Bilioni Sekta Ya Kilimo Tanzania
Kampuni ya Super Agri Technology ya China imesaini makubaliano na kampuni ya Tanzania Agriculture Export Process Zone kuwekeza $1 bilioni katika sekta ya kilimo na usindikaji kwa kipindi cha miaka mitano.
Makubaliano hayo yamesainiwa katika mkutano wa China-Africa Economic& Trade Expo yanayofanyika mji wa Changsha.
Katika hafla hiyo kampuni ya Tanzania Agriculture Export Process Zone iliwakilishwa na Afisa wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, Lilian Ndosi.
Bado tupo kwenye mashindano' - Samatta
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amesema moja ya makosa ambayo yalipelekea timu ya taifa ya Tanzania kupoteza mchezo wake wa dhidi ya Kenya, ni wachezaji wa Tanzania kushindwa kulinda ushindi ambao waliupata kwenye kipindi cha kwanza.
Nahodha Samatta amefunguka hayo nchini Misri ikiwa ni saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo ambao Stars ilifungwa kwa taabu bao 3 -2 na kuifanya kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi C lenye timu za Algeria, Senegal na Kenya.
"Mimi nafikiri ni timu nzima tulishindwa kulinda ushindi wetu, bado tupo kwenye mashindano naamini siku zote kuanguka ni kujifunza, sisi tupo na tunaendelea kupambana, kama Mungu yupo na sisi tunaendelea kumwamini, nadhani Watanzania tumewaangusha sana na tungeweza kuwa na matokeo chanya leo." amesema Capt. Samatta
Katika mchezo jana mabao ya Taifa Stars yalifungwa na Simon Msuva kunako dakika ya 6 huku bao la pili la Stars likifungwa na Mbwana Samatta akifunga dakika ya 40.
Mabao ya Kenya yamefungwa na Michael Olunga dakika 39,82, na Omollo.
Mechi ya mwisho wa Taifa Stars inacheza na Algeria Julai 1, 2019 ambapo nafasi pekee iliyobaki ni Taifa Stars kushinda mchezo huo, na watakuwa nafasi kubwa ya kupita kwa nafasi ya upendeleo maarufu kama Best Looser endapo atafikisha alama 3, huku akitegemea mchezo wake dhidi ya Kenya na Senegal mmoja wapo ashinde na Taifa Stars ipate ipate ushindi za zaidi ya mabao 3

TARIME: Kaka Amuua MDOMO wake wa Darasa la Kwanza Kisa Kupendwa na baba
Mniko Chacha (20) Mkazi wa Tarime, amemuua mdogo wake Hassan Chacha(7) mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kitagutiti Kijiji cha Getenga Kata ya Mbogi Wilayani Tarime, kwa kumshambulia, kumning'iniza juu na kisha kumtupa chini
Chanzo cha kaka kufanya tukio hilo kimetajwa kuwa ni na mdogo wake kupendwa sana na baba yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime /Rorya, Henny Mwaibambe amethibitisha tukio hilo ambapo amesema tukio hilo linasikitisha sana.
Alisema, kaka wa marehemu alimwambia marehemu kuwa kwanini wewe unapendwa sana, marehemu huyo ni mapacha Kurwa na Dotto, aliyefariki ni Dotto.
Mwaibambe amesema, ukiangalia umri wa mtoto huyo ni mdogo hivyo ni lazima apendwe tu na wazazi na kaka yao ni mtu mzima hakupaswa kufanya huo ukatili.
"Alimshambulia kwa kumning'iniza juu na kumtupa chini mara mbili akidai kwanini anapendelewa na baba yao kwa kuitwa mara kwa mara jikoni, marehemu alipata maumivu ambapo alikimbizwa katika kituo cha afya cha Dk. Steven na alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu," ameongeza.
Aidha Kamanda Mwaibambe amesema kuwa mtuhumiwa alitoroka baada ya kutenda tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea.
Fahamu Chanzo Halisi cha Kupungukiwa Nguvu za Kiume
Wanaume wengi kwa sasa wanasumbuliwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile kuwa mafupi na wengi wao huamua kutafuta tiba ili waweze kujilejeshea nguvu zao za asili bila kujua ni nini chazo cha hilo tatizo
Tambua kuwa hakuna dawa ya kuongeza maumbile ya kiume kama ulikuwa mdogo tangu unazaliwa, labda kama tatizo limeazia ukubwani kwa kujichua ( kupiga punyeto) au kutokana na magonjwa
Pia hakuna dawa ya kuongeza nguvu za kiume kama tatizo umezaliwa nalo bali zipo tiba za kutibu na ukapona matatizo hayo kama yameanzia ukubwani kutokana na sababu zifatazo ;
1,Unene kupita kiasi
2.Kuvaa nguo za kubana
3.Magonjwa ya moyo,kisukar,presha,vidonda vya tumbo,ngiri,tumbo kuunguruma na kujaa gesi,kupiga punyeto,Msongo wa mawazo.
Haya ndo mambo makuu yanayosababisha tatizo hilo. kwa ushauri zaidi , piga simu 0683645920

Sikutaka kuolewa na staa na kuigiza kwenye mapenzi- Shilole
Msanii wa muziki, muigizaji, na mjasiriamali Zuwena Mohammed maarufu kama "Shilole" amefunguka kuwa, ukiwa na mahusiano na mtu star huwa hakuna mapenzi.
Shilole ambaye yupo katika ndoa na mume wake Uchebe, kwa mwaka wa pili sasa, amesema hayo leo kupitia mahojiano na EATV na EARadio Digital.
"Inategemea mtu anataka mtu wa aina gani , kama mimi nilitaka mtu ambaye sio staa, ili niweze kuishi kwa raha, maana ukiwa na mahusiano na staa mtavimbiana , itakuwa sio sawa, hakuna mapenzi inakuwa mnaleteana maigizo".
Aidha msanii huyo amesema huwa anashika sana simu ya mume wake, na kama siku akikuta meseji ya msanii yeyote wa kike katika DM ya Uchebe atamtaja live. Pia ameweka wazi kuwa yeye na mume wake wanatumia simu moja kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.

Benki ya Azania yazindua Kampeni Ya ‘AMSHA NDOTO’ kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa Watanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Itembe Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Amsha Ndoto 'Amsha Ndoto' yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.Kulia kwake ni Mkurungezi wa Biashara wa Benki ya Azania Rhimo Nyansaho na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo mapema leo Jijini Dar es salaam.
***
Benki ya Azania (ABL) imetangaza uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina, 'Amsha Ndoto' yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.
Kampeni itaendeshwa kwa miezi mitatu, kuanzia 27 Juni 2019 hadi 27 Septemba 2019 na itahusisha wateja wa zamani na wapya ikijikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti(kwa ajili ya kila mmoja) na Watoto Akaunti(kwa ajili ya watoto tu).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Charles Itembe, Ili kustahili kupokea zawadi, wateja wanapaswa kuwa na akiba yenye thamani ya TZS 1,000,000 kwenye akaunti zao na kuendelea ili kuwawezesha kustahili kuingia kwenye fainali ya droo na hatimaye kuweza kushinda. Washindi wa 3 watapatikana kila mwezi. Kupitia kampeni hii wateja wataweza kujishindia mpaka mara mbili ya kiwango walichoweka kwenye akaunti, ambapo kiwango hiki cha zawadi huweza kufikia mpaka Shilingi milioni Tatu
Akiongelea kuhusu vigezo vya washiriki, Itembe alisema kuwa wateja ni lazima waweke akiba ya kiasi cha TZS 500,000 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima, na wale watakaoweka akiba kiasi cha TZ 1,000,000 watapewa tokeni zitakazowawezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho itakayowapata washindi.
"Tunawahamasisha watanzania wote, wateja wetu wa sasa na wapya,wazazi na walezi kufungua akaunti hizi ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuongeza mitaji, kulipia kodi za pango na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye", alisema Itembe, akigusia pia kuwa akaunti hizi zitakuwa fursa ya kuwahimiza kuweka akiba kwa ajili ya .
Promosheni hii, yenye kaulimbiu: 'Weka Akiba Ushinde,tumuwezeshe ada ya shule', itawasilishwa kupitia radio na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, Google Display placement na tovuti za ndani. ABL pia imetengeneza tovuti ndogo kwa wateja wapya kujiunga na inaweza kupatikana kupitia linki hii: amshandoto.com.
Masharti na vigezo kuzingatiwa
Thursday, June 27, 2019
Waziri Mkuu afungua Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Dodoma
WAZIRI MKU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji na biashara.
Amesema mpaka sasa, hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Juni 27, 2019) jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la uwekezaji la mkoa wa Dodoma kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.
"Miongoni mwa hatua hizo ni uwepo wa usafiri wa uhakika na wa haraka wa abiria na mizigo kwa kujenga reli ya kiwango cha kimataifa (Standard GaugeRailway)."
Pia, Waziri Mkuu amesema uwanja wa ndege wa Dodoma umeboreshwa na kuruhusu ndege kubwa na ndogo kutua usiku na mchana.
"Mashirika ya ndege yanayotoa huduma yameongezeka na maandalizi ya awali ya ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa ndege katika eneo la Msalato yanaendelea."
Waziri Mkuu amesema mkoa wa Dodoma una barabara za kuaminika za kiwango cha lami zinazoiunganisha na mikoa mingine pamoja na nchi jirani.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuboresha huduma za afya na Dodoma kuna hospitali ya Benjamin Mkapa yenye uwezo kama wa Muhimbili na Mloganzila.
Amesema ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji 'Stiegler's Gorge'wenye uwezo wa kuzalisha MW 2,115, utaongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini.
"Mradi huo utaongeza upatikanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya viwanda na uwekezaji nchini ikiwemo na katika mkoa wa Dodoma.
Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea na utekelezaji wa mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (The Blue Print) utakaoanza Julai mosi mwaka huu.
Waziri Mkuu amesema anatarajia kuwa kongamano hilo litawezesha kupatikana kwa wawekezaji mahiri kwa maendeleo ya uchumi na wananchi wa Tanzania.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge alisema katika azma ya Selikali ya kujenga uchumi wa viwanda wameandaa kongamano hilo ili kutangaza fursa zilizopo.
Alisema kaulimbiu ya kongamano hilo ni 'Dodoma Fursa Mpya Kiuchumi Tanzania, Wekeza Dodoma Tukufanikishe', inatanabaisha nafasi ya mkoa huo kwa sasa na baadaye.
Dkt. Mahenge alitaja baadhi ya fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Dodoma kuwa ni pamoja na uwepo wa ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo, viwanda na taasisi (afya, elimu).

Siku Nikiamua Kuondoka CCM Nitaondoka Hadharani – Mbunge Bashe
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe ameonesha kutofurahishwa, baada ya yeye, Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye, kutajwa kuwa miongoni mwa watu ambao washajiunga na chama cha ACT – Wazalendo na wanasubiri kipindi cha Ubunge kiishe.
Hussein Bashe ameonesha hali hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya mtu anayedaiwa kudukua mawasiliamo ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuchapisha taarifa juu ya Wabunge hao kujiunga na ACT – Wazalendo muda wowote.
Mdukuzi ameandika kuwa "nawakaribisha pia Hussein Bashe na Nape Nnauye ambao tayari wameshachukua kadi za uanachama ACT – Wazalendo na wanachosubiri ni kuvunjwa tu kwa Bunge na bila kumsahau mdogo wangu Januari Makamba,"
Akijibu madai hayo Mbunge wa Nzega Hussein Bashe ameandika kuwa "wanaofahamu siasa za Tanzania na wanaonifahamu vizuri misimamo ama maamuzi yangu ya kisiasa, huwa sifanyi kwa njia za kificho ama za kichimvi, Siku nikiamua kuondoka CCM nitaondoka hadharani ,sitasubiri njia za kificho"
"Hili Genge la kihuni ambalo linaongozwa na wahuni wachache ipo siku nitawataja kwa majina, ila mpango wenu wakutaka kunifanya nione CCM si chama sahihi kwa mimi kuwatumikia wananchi wa Nzega na Tanzania hautafanikiwa,CCM bado nipo sana" amemaliza Bashe.
Bashe Ageuka Mbogo Baada ya Kutajwa kwenye Tweets za Zitto Kabwe....."
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe ameonesha kutofurahishwa, baada ya yeye, Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye, kutajwa kuwa miongoni mwa watu ambao washajiunga na chama cha ACT - Wazalendo na wanasubiri kipindi cha Ubunge kiishe.
Hussein Bashe ameonesha hali hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya mtu anayedaiwa kudukua mawasiliamo ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuchapisha taarifa juu ya Wabunge hao kujiunga na ACT - Wazalendo muda wowote.
Mdukuzi ameandika kuwa "nawakaribisha pia Hussein Bashe na Nape Nnauye ambao tayari wameshachukua kadi za uanachama ACT - Wazalendo na wanachosubiri ni kuvunjwa tu kwa Bunge na bila kumsahau mdogo wangu Januari Makamba,"
Akijibu madai hayo Mbunge wa Nzega Hussein Bashe ameandika kuwa "wanaofahamu siasa za Tanzania na wanaonifahamu vizuri misimamo ama maamuzi yangu ya kisiasa, huwa sifanyi kwa njia za kificho ama za kichimvi, Siku nikiamua kuondoka CCM nitaondoka hadharani ,sitasubiri njia za kificho"
"Hili Genge la kihuni ambalo linaongozwa na wahuni wachache ipo siku nitawataja kwa majina, ila mpango wenu wakutaka kunifanya nione CCM si chama sahihi kwa mimi kuwatumikia wananchi wa Nzega na Tanzania hautafanikiwa,CCM bado nipo sana" amemaliza Bashe.
Hussein Bashe ameonesha hali hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya mtu anayedaiwa kudukua mawasiliamo ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuchapisha taarifa juu ya Wabunge hao kujiunga na ACT - Wazalendo muda wowote.
Mdukuzi ameandika kuwa "nawakaribisha pia Hussein Bashe na Nape Nnauye ambao tayari wameshachukua kadi za uanachama ACT - Wazalendo na wanachosubiri ni kuvunjwa tu kwa Bunge na bila kumsahau mdogo wangu Januari Makamba,"
Akijibu madai hayo Mbunge wa Nzega Hussein Bashe ameandika kuwa "wanaofahamu siasa za Tanzania na wanaonifahamu vizuri misimamo ama maamuzi yangu ya kisiasa, huwa sifanyi kwa njia za kificho ama za kichimvi, Siku nikiamua kuondoka CCM nitaondoka hadharani ,sitasubiri njia za kificho"
"Hili Genge la kihuni ambalo linaongozwa na wahuni wachache ipo siku nitawataja kwa majina, ila mpango wenu wakutaka kunifanya nione CCM si chama sahihi kwa mimi kuwatumikia wananchi wa Nzega na Tanzania hautafanikiwa,CCM bado nipo sana" amemaliza Bashe.
Mwanamke Aliyemkatakata Mtoto Wake na Kumpika Supu kufikishwa Mahakamani
Mwanamke aliyefanya tukio la aina yake Mkoani Geita, anayejulikana kwa jina la Happines Shadrack (36), aliyemchinja mwanaye kisha kumkatakata vipande na kumpika supu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo, ambapo amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kubaini kama kosa hilo alitenda kwa kukusudia, na atafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji.
''Bado tunamshikilia ili kubaini mambo mbalimbali na uchunguzi utakapokamilika tutampeleka mahakamani, na kesi yake inahusu mauaji na unajua kesi hizi huwa hazipelekwi katika Mahakama za kawaida huwa zinapelekwa Mahakama kuu''. - Ameeleza.
Tukio hilo lilitokea Juni 23 mwaka huu, katika kijiji cha Bulige kata ya Senga Mkoani Geita, ambapo alimpika supu mwanaye wa kumzaa Martha Yakobo (1).

Kilimanjaro, Lindi tishio soka wasichana UMITASHUMTA
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Timu za mikoa ya Kilimanjaro, Lindi na Manyara zimekuwa tishio kwa timu nyingine zinazoshiriki michuano ya UMITASHUMTA inayoendelea katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara baada ya jana kutoa vipigo vikali kwa wapinzani wao.
Timu ya soka wasichana ya mkoa wa Kilimanjaro iliibugiza Katavi magoli 7-0, Lindi nayo ikiifunga Ruvuma 5-0 huku Mara nayo ikitoa kipigo kama hicho kwa kuichapa Rukwa 5-0.
Matokeo mengine katika mchezo huo yanaonyesha kuwa Manyara iliifunga Singida 2-1, Simiyu ilipata ushindi wa chee baada ya Arusha kutofika uwanjani, Kagera imeifunga Mbeya 2-0, huku Iringa ikifungwa na Geita 0-3.
Katika mchezo wa soka maalum Kagera iliifunga Katavi magoli 9-0, Shinyanga wakiibugiza Rukwa magoli 6-0, Njombe walifungwa na Kilimanjaro 0-1, Manyara ikitoka sare na Singida ya 0-0, Tanga ikifungwa na Mtwara magoli 1-4, Dodoma ikiichapa Geita 1-0, na Mara ilifungwa na Ruvuma 1-3.
Kwa upande wa soka wavulana matokeo yanaonyesha kuwa Dodoma walifungwa na Dar es salaam 2-3, Kilimanjaro iliifunga Tanga 1-0, Singida iliifunga Mara 2-0, Lindi ilitoka suluhu ya bila kufungana na Simiyu, na Mtwara ilifungwa na Pwani magoli 0-3.
Iringa ilifungwa na Mwanza magoli 1-5, Manyara ilichapwa na Shinyanga magoli 0-5, Ruvuma iifungwa na Geita 0-2, Kigoma iliichapa Njombe 1-0, huku Songwe nayo ikpata kipigo kutoka kwa Kagera kwa magoli 0-2, Tabora ilitoka suluhu Rukwa na Arusha ilifungwa na Morogoro magoli 1-3.
Michezo mingine iliyochezwa leo ni pamoja na mchezo wa mpira wa mikono ambapo matokeo yanaonyesha kuwa Kagera ilifungwa na Songwe magoli 3-11, Tabora wasichana walifungwa na Lindi magoli 5-9, Rukwa wavulana walifungwa na Dar es salaam magoli 12-31, Mbeya walitoka sare na Mara kwa kufungana magoli 10-10, Tabora waliifunga Iringa 19-14, na kagera walifungwa na Pwani 9-10.
Matokeo mengine Njombe wavulana walifungwa na Tanga magoli 4-27, Dodoma wasichana waliifunga Shinyanga magoli 15-7, Shinyanga wavulana walifungwa na Manyara 6-13, Lindi wasichana waliifunga Kagera 13-1, Kagera wavulana walifungwa na Dodoma 12-23, Manyara wasichana na Tabora walitoka sare 8-8, Pwani wavulana iliifunga Njombe 11-8, na Mbeya wavulana walifungwa na Morogoro 6-15.
Shinyanga wasichana iliifunga katavi 10-9, Mtwara wavulana ilifungwa na Arusha 5-9, Morogoro wasichana waliichapa Mtwara 17-7, Songwe wavulana waliibugiza katavi magoli 20-13, Tanga wavulana waliifunga Kigoma 11-9, Mara wasichana iliipa kipigo Songwe 19-01, Mara wavulana ilifungwa na Morogoro 17-19, Dar es salaam wavulana iliifunga Ruvuma 24-03, na Mwanza wasichana iliichapa Singida 08-03.
Katika mchezo wa riadha kuruka juu wavulana medali ya dhahabu imechukuliwa na Lomnyaki Yakobo wa Manyara ambaye aliruka urefu wa mita 1 na sentimita 62, medali ya fedha ilikwenda kwa mwanariadha Daniel Kileo wa Manyara abaye aliruka urefu wa mita 1 na sentimita 60, huku medali ya shaba ikichukuliwa na mwanariadha Nguruko Mashaka wa Pwani aliyeruka urefu wa mita 1 na sentimita 58.
Dalili zitakazokuonesha msichana anayekupenda ila anashindwa kukuambia
Kwa hivi sasa kumekuwapo na imani potofu kwa wanawake kwamba hawawezi kumwambia ukweli mwanaume anampenda kwanza mpaka mwanaume aanze lakini ukweli usiopingika ni kwamba wao pia hupendi na mara nyingi wao wakianza kupenda hupenda kweli kufikia hatua hata ya kuhisi kuumwa.
Hizi ni dalili za mwanamke anaekupenda ila anagoma kukwambia tu;
Huwa anapenda kukugusa sehemu yako ya mwili.
Haoni aibu kugusa sehemu ya mwili wako. Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomasa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahishishia kazi ya kuwa na wewe.
Kupenda kucheka tena muda mwingine kwa nguvu
Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli.
Wivu.
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi na hupenda yale afanyiwe yeye tu hata kama sio mpenzi wako.
Hukumbuka matukio mengi yanayokuhusu wewe.
Anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifauli mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza.
Hupenda kuangaliana na wewe muda mwingi.
Eye contact hupendelea sana kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utamuelewa ni kiasi gani anakupenda kupitia vile anavyokuangalia. Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda hivyo huweka jicho la wizi na kukuvizia.
Hupenda kukaa muda mwingi na wewe.
Hupenda kukaa muda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe na akikaa na wewe hupendelea sana mwanzoni kukujua wewe zaidi na hukujengea mazingira ya wewe uwemuwazi ili umwambie mengi kuhusu wewe na pia akiwa na wewe atakuwa muwazi zaidi hadi mavazi aliyovaa hupenda sana kujua yako na kukuambia yake na hupenda kujua ni mavazi gani yeye akivaa anakuvutia zaidi na atajitahidi kuwa anavaa ya style hiyo kukufurahisha.
Hupenda kutatua mikwaruzano yenu kwa amani
Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakwambia nakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikitokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose.
Hupenda kukununulia zawadi za mitego
Mwanamke anaekupenda hupenda kujua mengi sana kuhusu wewe na hapo inamsaiia kukununulia zawadi za mitego kama boxer , na mara nyingi hupenda rangi nyeupe, au kukununulia perfume , sabuni ya kuoge ya manukato,soksi, vest, bukta, saa,raba, t-shirt. Na kama mkitoka wote mkaenda shopping ataakutega kwa kukuonyesha vitu na wewe ukionekana umependa kitu hatonunua siku hiyo ila atanunua siku inayofuata na kukuletea kama suprise.
Kupenda mle wote
Mwanamke anaekupenda ili akujue zaidi hupendelea msosi mle sehemu mmoja na kama ikitokea mwanaume hawezi kuhama sehemu anayokula mwanamke yupo radhi kubadili na kumfuata mwanaume hatakama sehemu hiyo yeye haipendi na kama unakula kwako basi atakutega na kuja kupika kwako ili mle na atakuwa anapenda kununua vitu vya kupika ili tu akutekena uone upendo wake.
NB: Kuwa makini, sio kila mwanamke atakaye onesha dalili hizi anakupenda kwa dhati, wengine hutaka kukuweka mtu kati ili akugagadue mpunga wako.

Wednesday, June 26, 2019
VIDEO: James Kotei aondoka rasmi Simba, aacha ujumbe huu mzito
Kiungo wa Simba SC raia wa Ghana KJames Kotei "Jiwe" aetangaza rasmi kujiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu. Kotei kupitia mtandao wa Instagram amethibitishsa kuondoka Simba kwa kuwaaga mashabiki wa timu hiyo kwa ujumbe mzito ambao unaweza kuwatoa machozi.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE
Source
Misri yatema mchezaji kambini kwa utovu wa nidhamu
Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Hani Abu Reda ametangaza kumtema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Amr Medhat Warda.
Warda mwenye umri wa miaka 25, ametemwa ikiwa ni masaa machache kabla ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi katika michuano ya AFCON inayoendelea nchini humo, mchezo ambao utapigwa leo dhidi ya Congo DR majira ya saa 5:00 usiku.
Imetajwa kuwa nidhamu mbovu ndiyo sababu za kuachwa kwake, ambapo kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Misri, mchezaji huyo amehusika katika unyanyasaji dhidi ya mwanamitindo raia wa nchi hiyo, Merhan Keller.
"Hani Abu Reda amefikia uamuzi huo baada ya kuwasiliana na benchi la ufundi ili kulinda nidhamu katika kambi ya timu. Timu ya taifa itamaliza ratiba iliyobaki ya mashindano na idadi ya wachezaji 22", imesema taarifa kutoka katika tovuti ya chama cha soka nchini humo.
Warda ni kiungo mshambuliaji katika klabu ya PAOK ya nchini Ugiriki.

BASI LAGONGA LORI NA KUJERUHI KAHAMA
NA SALVATORY NTANDU
Abiria saba Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamenusurika kifo baada lori la mizigo aina ya Fuso lenye T 322 ACC walilokuwa wakisafiria kugongana na basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 245 AJS Kwela Classic Mali ya Laurent Ncheye mkazi wa Kahama linalofanya safari za Kahama kwenda mkoani Kigoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanya Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo leo asubuhi baada ya dereva wa basi hilo kuligonga lori hilo lilokuwa limebeba magunia 100 ya mahindi katika eneo hilo na kusababisha lori hilo kupinduka na kusababisha majeruhi wa ajali hiyo.
Amesema majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama na hali zao zinaendelea vizuri na kuwataka madereva wote wilayani humu kuheshimu alama za barabarani husasni wanapotaka kuingia katika makutano ya barabara ili kuzuia ajali zinazoweza kuzuilika.
Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajali hiyo ni Uzembe wa Dereva wa basi hilo kutochukua tahadhari pindi anapongia katika makutano ya barabara kwa kuingia katika barabara hiyo kwa mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo ambayo imeharibu miundo mbinu ya barabara na nyumba za watu zilizopo karibu na eneo hilo.
Amefafanua kuwa dereva wa basi hilo amejisalimisha katika kituo cha polisi kahama na baada ya kuhojiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinayomkabili.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama DK, George Masasi amesema amepokea majeruhi hao Saba na hali zao zinaendelea vizuri ambao ni pamoja na dereva wa lori hilo ambao wameumia katika sehemu mbalimbali za miili yao.
Mmoja wa shuhuda wa Tukio hilo Amosi Joseph amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 11 alfajiri baada ya dereva wa basi kupita katika eneo hilo kwa mwendo kasi kwa lengo la kuwahi abiria katika kituo kikuu cha mabasi kahama kwaajili ya kuanza safari na kusababisha abiria waliokuwepo katika lori hilo kujeruhiwa.
Mbali na Kamanda Abwao amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuchukua hatua kali kwa madereva wote wazembe ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani .
BREAKING: Jaguar akamatwa na Polisi nchini Kenya
Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles 'Jaguar' Njagua, amekamtwa nje ya majengo ya Bunge kufuatia kauli zake za 'kibaguzi' akiwataka wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wanaoendesha shughuli zao katika masoko mjini Nairobi na miji mingineyo kuondoka nchini humo ndani ya saa 24.
Kwa mujibu wa mtandao wa kituo cha Televisheni cha K24, Mbunge huyo amekamata leo, Jumatano baada ya kauli yake hiyo kuzua taharuki katika baadhi ya miji katika nchi zilizotajwa huku Serikali yake ya Kenya ikimkana na kusema hayo ni maoni yake na Tanzania ikiwataka Watanzania kuwa na utulivu wakati jambo hilo likishughulikiwa.
Kupitia msemaji wake, Kanali mstaafu Cyrus Oguna , Serikali ya Kenya imelaani vikali matamshi ya Jaguar na kuapa kuwalinda wafanyibiashara halali wa kigeni walioko nchi humo pamoja na mali zao.
Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Kauli Ya Serikali Bungeni Kuhusu Watanzania Kufukuzwa Kenya
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Kenya imesema kauli iliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Starehe nchini humo, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar si kauli ya Serikali, hivyo amewataka Watanzania wawe watulivu.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Juni 25, 2019) wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu kauli ya iliyotolewa na mbunge huyo ya kuwataka wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania waondoke nchini Kenya ndani ya saa 24.
Amesema baada ya mbunge huyo kutoa kauli hiyo, Serikali ilianza kulifanyiakazi jambo hilo ambapo ilimuita Balozi wa Kenya nchini Tanzania ili kujua kama huo ni msimamo wa Serikali yao ama la, ambapo balozi huyo alimesema ile si kauli ya Serikali ya Kenya wala wananchi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mbali na kuwasiliana na Balozi huyo, pia Serikali imewasiliana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya ili afuatilie kuhusu kauli ya Mbunge huyo, hivyo amewataka Watanzania waendelee kushirikiana na Wakenya.
"Si kauli nzuri na kauli hii iliyotolewa na mtu mmoja linajenga chuki baina ya mtu na mtu, nchi na nchi na tayari Serikali ya Kenya inalifanyia kazi suala hili na imetuomba Watanzania tuendelee kuwa wavumilivu."
Waziri Mkuu amesema tamko lile linaweza kuibua chuki na vurugu miongoni mwa nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika Mashariki na tayari Wabunge wa Bunge Afrika Mashariki wanaoendelea na kikao cha Bunge hilo jijini Arusha wamepinga na kulaani kauli hiyo.

Wamesema hawatoa nafasi kwa mtu yeyote kuvuruga nchi hizo.
Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania popote walipo waendelee kuishi vizuri na Wakenya kwa kuwa wao hawana chuki na Watanzania bali ni mtu binafsi. Pia amewatahadharisha wananchi wa Afrika Mashariki wawe makini na kauli zao ili kuepusha vurugu.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Source
Tuesday, June 25, 2019
Fahamu kuhusu saratani ya shingo ya kizazi
Ugonjwa huu husababishwa na virusi vinavyoitwa Human papilloma, ambapo mtu anaweza kupatwa na virusi hawa wakati wa kujamiana na mtu mwenye maambukizi. Human Papillomavirus aina ya 16 na 18 husababisha kansa ya aina hii kwa asilimia 75 duniani kote huku aina ya 31 na 35 zikisababisha maambukizi kwa asilimia 10.
Watu walio katika hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu ni kwa ujumla wanawake wote lakini zaidi wale wasiokwenda kufanyiwa uchunguzi wa kila mwaka kuhusiana na ugonjwa huu unaojulikana kitaalamu kama pap smear, wanawake walioathirika na virusi vya human papillomavirus HPV au genital warts, wanaovuta sigara, wenye ukimwi na wasiokula vyakula bora hasa wasiozingatia mboga na matunda katika lishe zao.
Kutokana na uchunguzi huo, timu ya wataalamu wa ugonjwa huo imeeleza sababu zinazochangia kupata saratani ya shingo ya kizazi na kubainisha dalili ambazo huonekana kwa mtu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo.
Kimsingi mabadiliko ya awali ya saratani hii hayatoi dalili yoyote ya moja kwa moja hadi mwanamke afanyiwe uchunguzi au vipimo vingine vya ugonjwa huo. Dalili zinazoonesha kuwepo kwa saratani ya shingo ya kizazi ni pamoja na kutokwa na damu ambayo si ya hedhi, kutokwa na uchafu, majimaji au usaha sehemu za siri.
Hata hivyo dalili nyingine ni pamoja na kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana na kusababisha kutokwa na damu baada ya tendo hilo ambapo pia ni pamoja na maumivu ya tumbo chini ya kitovu sambamba na maumivu ya kiuno.
Kufanyiwa uchunguzi wa pap smear ili kubaini ugonjwa huu kuna nafasi kubwa katika kuzuia watu kupatwa na saratani ya shingo ya kizazi. Uchunguzi wa awali wa saratani ya shingo ya kizazi unatakiwa kufanyiwa wanawake walio katika mahusiano ya ndoa na pia wanatakiwa kupima mara kwa mara hadi wanapofikia umri wa miaka 69.
Mwanzoni uchunguzi huu unatakiwa ufanyike mara kwa mara kwa muda wa miaka mitatu mfululizo. Ikitokea katika miaka mitatu mfululizo uchunguzi huo haujatoa dalili zozote za kuwepo saratani basi mwanamke anaweza kuendelea kufanyiwa uchunguzi mara moja kila baada ya miaka miwili na mitatu hadi pale atakapofikisha umri wa miaka 69.

Rosa Ree is Back With ‘Champion’ This Girl is Just Talented
Rosa Ree is back on Champion this time featuring Ruby. You mean a woman must get rich through a Niggah? Not my words but Rosa's. This girl is just talented. Champion seems like a diss to me, seems like she is responding to some beef somewhere.
Champion talks about women. It says that women have the power and for sure this an encouragement to women.
The rap goddess has a tone and it really sounds good. Rosa has the power and the energy. Her merger with Ruby for this jam shows that this women are champion. The voices, although Ruby does very little in this jam it is a women affair thing.
Ruby has been silent for sometime and now this collaboration shows her making a comeback to her world.
Audio Production of 'Champion'
There is that voice that when it hits your airwaves you definitely want to listen. Rosa Ree is that girl. The audio in this jam is well crafted and just flows. Also, the beats are great. You know that Rosa has her own tune, right? Well this is evident in this audio. Whoever works on her sound tracks is one to watch.
Champion is produced by Luffa. Well seems Tanzanians are going far and are quick in succeeding the music industry.
Lyrical Presentation
Ruby has done the chorus. It is just dope. She also plays the back up role. This is the best jam I have heard today. The words are just right. We are all used to Rosa using swahili while delivering her work, well this time she has done English and Swahili.
Her lines are not vulgar in this jam. Could she be changing to a new style? They are full of wisdom though.
There is a line that says that she has the right to do what she wants and love who she wants to. She is very right on this one. In short people should stop living a double standard life.
Click on the link below for the audio.
Mbunge Ashauri Tozo Ya Pombe ,sigara Ipande Maradufu
Na.Faustine Gimu Galafoni,
Ikiwa leo Juni 25,2019 Bunge la Tanzania likiwa lina piga kura ya ndio au hapana ya kuipitisha au kutoipitisha bajeti kuu ya serikali,wabunge wamekuwa wakitoa michango na maoni mbalimbali kuhusu bajeti hiyo ambapo mbunge wa Rujiji Mohamed Mchengelwa ameishauri serikali kuongeza tozo kwenye Pombe na sigara .

Mhe.Mchengelwa amesema kuongeza tozo kwenye pombe na sigara itasaidia kulinda afya za watu kwani watapungua kunywa pombe na sigara kutokana na gharama kubwa ya bidhaa hizo ambazo sio muhimu kwa maisha ya binadamu kwani husababisha madhara kiafya pamoja ,uchumi kudumaa, migogoro kutokana na walevi kuwa na fujo zisizo za msingi.
Hivyo Mbunge huyo amesema serikali hutumia gharama kubwa katika matibabu kwa watu walioathirika na utumiaji wa pombe na sigara Mfano,TB, ili kupunguza gharama hizo na kuepusha madhara kwa watanzania ni wakati sasa umefika tozo za pombe na Sigara zikawa kubwa maradufu.
Katika hatua nyingine mbunge huyo ameishauri serikali kufanya tathmini ya Madhara ya Ukoloni uliotokea na kubainisha hasara na madhara ya ukoloni ili Tanzania ifungue kesi ya kimataifa dhidi ya nchini zilizokuwa makoloni ya Tanzania ambazo ni Ujerumani na Uingereza ili ziweze kuipa fidia Tanzania kwani baadhi ya nchi za Afrika zilishawahi kufanya hivyo na kulipwa.
Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya miezi ya hivi karibuni kuona clip ya video ya Bunge la Ujerumani ikishinikiza Taifa la Tanzania kusitisha utekelezaji wa mradi wa umeme wa mto Rufiji wa Stieglers Gorge wakidai kuwa wao ni koloni la Tanzania.
Ikumbukwe kuwa mradi wa umeme wa Mto Rufiji Stieglers Gorge unagharimu dola za kimarekani Bilioni 2.9 na ukikamilika utazalisha Megawati 2,100 na hatua hiyo ya utekelezaji imekuja baada ya miaka 40 ya utafiti.
Offset na Cardi B kumfanyia mtoto wao Kulture birthday ya Milioni 900
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper kutokea kundi la Migos Offset pamoja na mke wake Cardi B wanampango wa kumfanyia mtoto wao Kulture sherehe ya kutimizia mwaka mmoja itakayogharimu kiasi cha dola za Kimarekani 400,000 sawa na zaidi ya Tsh Mil.900
Inaelezwa kuwa Kulture anatimiza mwaka mmoja Julai 10 mwaka huu 2019 na kutajwa kuwa zawadi itakayotolewa kutoka kwa Cardi B na Offset ni vito vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2o0 za Kitanzania ambapo sonara Eliantte ndio ametajwa kuandaa vito hivyo.
Kupitia Insta Live ya Cardi B aliwahi kufunguka na kusema kuwa hii ndio sherehe ya kuzaliwa ya kwanza ya mtoto wake hivyo anataka kuifanya kuwa ya kipekee. Inaelezwa kuwa Cardi B aliwahi kumnunulia mtoto wake bangili yenye thamani zaidi ya Mil.100 za kitanzania.

WAFANYAKAZI WA TARURA' WAFARIKI KWA AJALI YA GARI
Wafanyakazi wawili wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Songwe wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wamepanda kugongana na lori maeneo ya Izazi kata ya Izazi tarafa ya Ismani wilaya ya Iringa na mkoa wa Iringa katika barabara kuu ya Iringa-Dodoma.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire Makanya ajali hiyo imetokea Juni 25,2019 majira ya saa 11 na dakika 45 alfajiri ambapo gari lenye namba za usajili STL 3807 aina ya toyota Hilux mali ya TARURA ikiendeshwa na Lodrick Richard Ulio( 35) mkazi wa Dar es salaam likitokea Iringa kuelekea Dodoma liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T 146 BAZ aina ya Mitsubishi fuso mali ya Wilson Msenga wa Iringa likiendeshwa na Amos wa iringa likitokea Dodoma kuelekea Iringa.
Kamanda Makanya amewataja waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Lodrick Richard Ulio (dereva wa TARURA) na Joyce Enezar Mlay (45) ambaye ni mkazi wa Moshi na majeruhi kuwa ni Ernest Mgeni (49) mkazi wa Mbozi, Gervas Myovela (44) mkazi wa Mbozi na Jamadin Mikata( 32) mkazi wa Mbozi wote wakiwa ni wafanyakazi wa TARURA mkoa wa Songwe na wamehamishiwa hospitali ya rufaa Iringa kwa matibabu.
Amesema miili ya marehemu imekabidhiwa kwa meneja wa TARURA Manispaa ya Iringa na kupelekwa Dodoma tayari kwa utaratibu wa mazishi.
"Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa fuso kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhama upande mmoja na kugongana uso kwa uso ambaye amekimbia mara baada ya ajali hiyo na anatafutwa",ameeleza Kamanda.
Kamanda Makanya ametoa wito kwa madereva wawe makini wanapotumia barabara wasijione wako peke yao bali waheshimu sheria na watumiaji wengine wa barabara.
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog - Iringa
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog - Iringa
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...