Thursday, June 27, 2019

Kilimanjaro, Lindi tishio soka wasichana UMITASHUMTA


Na Mathew Kwembe, Mtwara

Timu za mikoa ya Kilimanjaro, Lindi na Manyara zimekuwa tishio kwa timu nyingine zinazoshiriki michuano ya UMITASHUMTA inayoendelea katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara baada ya jana kutoa vipigo vikali kwa wapinzani wao.

Timu ya soka wasichana ya mkoa wa Kilimanjaro iliibugiza Katavi magoli 7-0, Lindi nayo ikiifunga Ruvuma 5-0 huku Mara nayo ikitoa kipigo kama hicho kwa kuichapa Rukwa 5-0.

Matokeo mengine katika mchezo huo yanaonyesha kuwa Manyara iliifunga Singida 2-1, Simiyu ilipata ushindi wa chee baada ya Arusha kutofika uwanjani, Kagera imeifunga Mbeya 2-0, huku Iringa ikifungwa na Geita 0-3.

Katika mchezo wa soka maalum Kagera iliifunga Katavi magoli 9-0, Shinyanga wakiibugiza Rukwa magoli 6-0, Njombe walifungwa na Kilimanjaro 0-1, Manyara ikitoka sare na Singida ya 0-0, Tanga ikifungwa na Mtwara magoli 1-4, Dodoma ikiichapa Geita 1-0, na Mara ilifungwa na Ruvuma 1-3.

Kwa upande wa soka wavulana matokeo yanaonyesha kuwa Dodoma walifungwa na Dar es salaam 2-3, Kilimanjaro iliifunga Tanga 1-0, Singida iliifunga Mara 2-0, Lindi ilitoka suluhu ya bila kufungana na Simiyu, na Mtwara ilifungwa na Pwani magoli 0-3.

Iringa ilifungwa na Mwanza magoli 1-5, Manyara ilichapwa na Shinyanga magoli 0-5, Ruvuma iifungwa na Geita 0-2, Kigoma iliichapa Njombe 1-0, huku Songwe nayo ikpata kipigo kutoka kwa Kagera kwa magoli 0-2, Tabora ilitoka suluhu Rukwa na Arusha ilifungwa na Morogoro magoli 1-3.

Michezo mingine iliyochezwa leo ni pamoja na mchezo wa mpira wa mikono ambapo matokeo yanaonyesha kuwa Kagera ilifungwa na Songwe magoli 3-11, Tabora wasichana walifungwa na Lindi  magoli 5-9, Rukwa wavulana walifungwa na Dar es salaam magoli 12-31, Mbeya walitoka sare na Mara kwa kufungana magoli 10-10, Tabora waliifunga Iringa 19-14, na kagera walifungwa na Pwani 9-10.

Matokeo mengine Njombe wavulana walifungwa na Tanga magoli 4-27, Dodoma wasichana waliifunga Shinyanga magoli 15-7, Shinyanga wavulana walifungwa na Manyara 6-13, Lindi wasichana waliifunga Kagera 13-1, Kagera wavulana walifungwa na Dodoma 12-23, Manyara wasichana na Tabora walitoka sare 8-8, Pwani wavulana iliifunga Njombe 11-8, na Mbeya wavulana walifungwa na Morogoro 6-15.

Shinyanga wasichana iliifunga katavi 10-9, Mtwara wavulana ilifungwa na Arusha 5-9, Morogoro wasichana waliichapa Mtwara 17-7, Songwe wavulana waliibugiza katavi magoli 20-13, Tanga wavulana waliifunga Kigoma 11-9, Mara wasichana iliipa kipigo Songwe 19-01, Mara wavulana ilifungwa na Morogoro 17-19, Dar es salaam wavulana iliifunga Ruvuma 24-03, na Mwanza wasichana iliichapa Singida 08-03.

Katika mchezo wa riadha kuruka juu wavulana medali ya dhahabu imechukuliwa na Lomnyaki Yakobo wa Manyara ambaye aliruka urefu wa mita 1 na sentimita 62, medali ya fedha ilikwenda kwa mwanariadha Daniel Kileo wa Manyara abaye aliruka urefu wa mita 1 na sentimita 60, huku medali ya shaba ikichukuliwa na mwanariadha Nguruko Mashaka wa Pwani aliyeruka urefu wa mita 1 na sentimita 58.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...