Sunday, June 30, 2019

Polepole Awapa Makavu Wanachama CCM....."Usitumie uongozi kama mali yako"


Katibu  wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Humphrey Polepole amesema ugonjwa mkubwa ndani ya CCM ni ubinafsi na kuwataka kuacha kupendekeza wagombea ambao wananchi hawawataki.

Aidha aliwataka viongozi wa chama wakiwemo mabalozi wa nyumba 10 kuacha kupanga safu za watu wanaowataka badala yake wahakikishe wanasimamia utaratibu.

Polepole alitoa maaelekezo hayo kwa makamisaa nchini kote kukisema Chama cha Mapinduzi kinachofanya kazi zake chini ya Rais John Magufuli ili wananchi waelewe .Aliyasema hayo jana Jijini Arusha katika kikao maalumu cha kupokea Ilani ya Uchaguzi wa CCM 2015/2020 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha Julai 2018 hadi Machi 2019.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema anayepanga safu, aliyepangwa katika safu, kanuni za chama zinatoa adhabu kwa wale wote waliosababisha ukiukwaji wa uchaguzi au uteuzi wa wagombea

"Chama hakiangalii mtu kwa sura, mtatandikwa adhabu kali, uongozi ni dhamana usitumie uongozi kama mali yako na wale wabaya nawaambia acheni kupanga safu na tunawakata wale wote wasioheshimu maadili ya chama…

"Acheni kupanga safu za uongozi na nitawasubiri kwenye sekretarieti nitahangaika na wewe ulalo ulalo hadi kieleweke kura hazipigwi na viongozi wa CCM zinapigwa na wanachama wa CCM hivyo achene mambo yenu," alisema.

Alisema kwenye serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wekeni watu wanaokubalika na kama mnaona hawakubaliki kata weka wengine na mwaka kesho kwenye udiwani, madiwani wa CCM wafanye mikutano katika kata zao na wasiofanya mikutano wote watajulikana.

Polepole alisema Tanzania imepata bahati ya kuwa na Rais wa kipekee kwani Rais Magufuli amevunja historia nchini katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi sita rais amejenga hospitali za wilaya 67 na vituo vya afya 353 nchi nzima.

Alisema yapo mengi mazuri Rais Magufuli amefanya ikiwa ni pamoja na kutoa ndege yake kwa ajili ya wananchi kuipanda na amenunua ndege kubwa mbili mpya, ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme wenye uwezo wa kuvuna megawati za umeme zaidi ya 2000.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...