Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amesema moja ya makosa ambayo yalipelekea timu ya taifa ya Tanzania kupoteza mchezo wake wa dhidi ya Kenya, ni wachezaji wa Tanzania kushindwa kulinda ushindi ambao waliupata kwenye kipindi cha kwanza.
Nahodha Samatta amefunguka hayo nchini Misri ikiwa ni saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo ambao Stars ilifungwa kwa taabu bao 3 -2 na kuifanya kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi C lenye timu za Algeria, Senegal na Kenya.
"Mimi nafikiri ni timu nzima tulishindwa kulinda ushindi wetu, bado tupo kwenye mashindano naamini siku zote kuanguka ni kujifunza, sisi tupo na tunaendelea kupambana, kama Mungu yupo na sisi tunaendelea kumwamini, nadhani Watanzania tumewaangusha sana na tungeweza kuwa na matokeo chanya leo." amesema Capt. Samatta
Katika mchezo jana mabao ya Taifa Stars yalifungwa na Simon Msuva kunako dakika ya 6 huku bao la pili la Stars likifungwa na Mbwana Samatta akifunga dakika ya 40.
Mabao ya Kenya yamefungwa na Michael Olunga dakika 39,82, na Omollo.
Mechi ya mwisho wa Taifa Stars inacheza na Algeria Julai 1, 2019 ambapo nafasi pekee iliyobaki ni Taifa Stars kushinda mchezo huo, na watakuwa nafasi kubwa ya kupita kwa nafasi ya upendeleo maarufu kama Best Looser endapo atafikisha alama 3, huku akitegemea mchezo wake dhidi ya Kenya na Senegal mmoja wapo ashinde na Taifa Stars ipate ipate ushindi za zaidi ya mabao 3
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...