Saturday, March 1, 2025

WAZIRI RIZIKI PEMBE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE NA WANAWAKE WENYE ULEMAVU... "WANAUME MSITUMIE SILAHA ZENU VIBAYA KUBAKA WATOTO"

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu yaliyofanyika Mkoani Shinyanga leo, Machi 1, 2025 - Picha na Malunde

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma, amewataka wanaume kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda wanawake na watoto badala ya kuwa chanzo cha vikwazo.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu yaliyofanyika Mkoani Shinyanga leo, Machi 1, 2025, Mhe. Riziki ameweka wazi kuwa jamii inapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kuimarisha haki, usawa, na uwekezaji, akisisitiza kuwa wanaume wanahitaji kuchukua jukumu kubwa la kuwalinda wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Shujaa Wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali yakiongozwa na kauli mbiu "Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwekezaji".
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma

"Tuendelee kupinga ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto. Wenye silaha za kufanyia ukatili ni wanaume, wenye silaha za ubakaji na ulawiti ni wanaume, naomba akina baba silaha zihifadhini vizuri, zitumike vizuri, pahala sahihi kwa watu sahihi, zisitumike kwa watoto wetu… zisionekane hovyo",amesema Mhe. Riziki.

Aidha, Mhe. Riziki ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi ujao wa 2025, akisema kwamba wanawake wanapaswa kujiandaa kushiriki kwa wingi ili kuungana na viongozi wanaume katika kuboresha maendeleo ya taifa.

Amewashauri wanaume kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono mgombea mwanamke ili kuongeza uwakilishi wa wanawake katika uongozi, akisema "Wanawake wanapokuwa katika uongozi, huongeza mchango wa uchumi wa familia na jamii nzima."

Mhe. Riziki pia amewapongeza wanawake wenye ulemavu kwa bidii na juhudi zao katika kuchangia maendeleo ya jamii, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali kuhakikisha kundi hilo linapata nafasi sawa katika sekta zote.

"Siku ya Wanawake Duniani ni fursa ya kutambua mchango wa wanawake wote, wakiwemo wenye ulemavu, katika maendeleo ya taifa. Ni jukumu letu kuhakikisha wanapata haki zao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi," amesema Mhe. Riziki.

Amesema wanawake wenye ulemavu wanastahili pongezi kwa mchango wao katika jamii licha ya changamoto wanazokutana nazo, na kusema, "Siku ya Wanawake Duniani ni alama muhimu ya kutambua mchango wa wanawake wote, bila kujali hali zao. Tunapaswa kuhakikisha kuwa wanawake wenye ulemavu wanapata nafasi sawa katika elimu, ajira, na uongozi, ili wawe sehemu ya maendeleo ya nchi."

Aidha, ameongeza kuwa serikali inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha huduma za jamii kwa wanawake wote, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa elimu, huduma za afya, na maji safi, ili kuhakikisha wanapata mazingira bora ya maisha.

Akisoma risala, Katibu wa Idara ya Wenye Ulemavu SMAUJATA Taifa, Imani Axwesso, amebainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake wenye ulemavu, ikiwemo ukosefu wa ajira, mitaji ya biashara, mikopo, na nafasi za uongozi.

"Jamii inapaswa kuhakikisha kuwa wanawake wenye ulemavu wanashirikishwa kikamilifu katika nafasi za kimaendeleo ili waweze kujitegemea na kushiriki katika maamuzi ya uongozi," amesema Axwesso.

Katibu wa Idara ya Wenye Ulemavu SMAUJATA Taifa, Imani Axwesso

Amesema changamoto zingine zinazowakabili wanawake wenye ulemavu, kama vile ukatili wa kijinsia, unyanyapaa, na ubaguzi katika jamii. 

Aidha, amehimiza serikali na wadau wa maendeleo kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha kiuchumi, na kuhakikisha wanapata huduma bora za elimu na afya.

Kwa upande mwingine, amehamasisha umuhimu wa malezi bora kwa watoto, hasa akijikita katika kutoa ushauri kwa wazazi na walezi kuwaepusha watoto na mazingira hatarishi, kama vile kuwalaza na wageni, ili kuepuka ukatili wa kijinsia.

"Kila kundi linapaswa kulindwa. Tuache ukatili wa kijinsia. Tunawapongeza SMAUJATA kwa jitihada zao za kupambana na ukatili wa kijinsia," ameongeza Mhe. Riziki.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu  amekiri juhudi za serikali katika kuboresha hali ya maisha kwa watu wenye ulemavu, hasa wanawake na watoto, kupitia mikopo na ajira.

Vilevile, amesema kuwa haki za watu wenye ulemavu zitazidi kuimarishwa na serikali itaendelea kutekeleza sheria na taratibu zinazolinda haki zao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amesema kuwa serikali na wadau wameendelea kushirikiana katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia, na ameelezea matumaini kuwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia itashinda, akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kupigania haki za wanawake na watoto.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Christina Mzava, ameelezea mfano bora wa Rais Samia Suluhu, ambaye anapigania haki za wanawake na wanawake wenye ulemavu.

"Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, wanawake na watu wenye ulemavu, tusikubali kubaki nyuma. Tuchukue fomu na tushiriki katika nafasi za uongozi ili kuwa na sauti katika ngazi za maamuzi",amesema.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Sospeter Mosewe Bulugu.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Sospeter Mosewe Bulugu, amewakumbusha wanaume kuacha kunyanyasa wanawake na kuhakikisha wanawake wanapata usalama, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikisha wanawake wenye ulemavu katika masuala ya uongozi.

Amesema kuwa SMAUJATA ni jumuiya ya kijamii inayolenga kuchochea mabadiliko chanya na kuleta maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi na ilianzishwa ili kuchochea shughuli za maendeleo na ustawi wa jamii, huku akieleza kuwa ilizinduliwa rasmi na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, mnamo Juni 16, 2022.

"Dira ya SMAUJATA ni kuwa na taifa lenye kizazi huru chenye haki na usawa, kitakachoweza kujitegemea na kuzitambua fursa, na kutumia ujuzi, maarifa, na vipaji katika kujenga jamii yenye maendeleo endelevu," amesema Bulugu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu yaliyofanyika Mkoani Shinyanga leo, Machi 1, 2025 - Picha na Malunde
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Sospeter Mosewe Bulugu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Sospeter Mosewe Bulugu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga , Nabila Kisendi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga , Nabila Kisendi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa, Daniel Kapaya akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha wakicheza muziki/wimbo na Kwaya ya AICT Shinyanga

Marekani Chini ya Utawala wa Trump Haita Ipa Tena Ukraine Msaada wa Kivita.....

Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump imetangaza kuwa haitoendelea tena kuisaidia Ukraine kifedha wala silaha za kivita kwasababu kipaumbele cha Marekani ni majadiliano ya amani na kumaliza vita ya Ukraine na Urusi.

Uamuzi huu wa Marekani umetangazwa usiku wa kuamkia leo March 01,2025 na Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Caroline Leavitt ikiwa imepita siku moja tangu Trump na Rais wa Ukraine Zelensky wazozane mbele ya camera za Waandishi wa Habari.

Caroline amesema "Hatutoendelea tena kuandika check kufadhili vita, hatutoendelea kuifadhili nchi ambayo haitaki amani ya kudumu, ilikuwa vizuri kwamba camera zimeonesha ule mzozo wa Trump na Rais wa Ukraine na Wamarekani na Dunia nzima imeona kile ambacho Trump na Timu yake wanashughulika nacho nyuma ya pazia wakati wa majadiliano ya kumaliza vita"

Wednesday, February 26, 2025

Amnesty yamtaka Rais Joe Biden kulifunga gereza la Guantanamo

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limemtaka Rais Joe Biden kuitimiza ahadi yake ya kulifunga gereza la Guantanamo wakati ambapo maadhimisho ya miaka 20 tangu kufunguliwa kwake yakiwa yanakaribia. Gereza hilo lilifunguliwa mahsusi kwa ajili ya kuwazuia washukiwa wa ugaidi waliokamatwa na Marekani katika vita vyake dhidi ya ugaidi. Ni gereza lililo kwenye …

The post Amnesty yamtaka Rais Joe Biden kulifunga gereza la Guantanamo appeared first on Bongo5.com.

Saturday, February 22, 2025

DAWASA WATANGAZA FURSA LUKUKI KWA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire ametangaza fursa lukuki kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Kigamboni zitakazotokana na ushirikiano bora uliitengenezwa baina yao na Mamlaka hiyo.

Mhandisi Bwire amebainisha fursa hizo katika kikao kazi na wenyeviti hao kilicholenga kuboresha mahusiano na kujenga ukaribu baina ya Serikali za Mitaa na DAWASA.

"Ukaribu huu unakuja na fursa nyingi ndugu wenyeviti ambazo zitanufaisha pande zote mbili , Serikali pamoja na wenyeviti kama mtu mmoja mmoja, kuanzia saa wwenyekiti atakaetusaidia kuhamasisha maunganisho na kutuletea wateja atapata kiasi cha Shilingi 10,000 kwa kila mteja mmoja anaemleta," amesema Mhandisi Bwire.

Bwire amesema sio hivyo tu lakini hata kwa wale ambao watasaidia kufichua wahujumu kwa Mamlaka mfano wezi wa maji hawataacha hivi hivi bali nao watanufaika kwa uzalendo watakaouonyesha.

"Ndugu zangu wenyeviti kwa kila mmoja wenu atakae saidia kubaini mwizi wa maji na tukamkamata na kumpiga faini basi Mwenyekiti uliesaidia kubaini hilo utapata asilimia 30 ya fedha zitakazolipwa kama faini," amesema Mhandisi Bwire

Bwire amesema motisha hii kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa itakua chachu ya wao kushirikiana na Mamlaka zaidi katika shughuli za kila siku kuwapatia huduma ya maji wananchi.

Mhandisi Bwire amesema hawataishia hapo tu bali watatoa motisha kwa kila Mwenyekiti atakaesaidia kushawishi mteja aliesitishiwa huduma Kulipa deni lake na kurudi kutumia huduma za DAWASA.

Hatua hii imepokelewa vyema na wenyeviti waliohudhuria kikao kazi hicho huku wakiahidi kufanya kazi bega kwa bega na DAWASA kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora ya Majisafi wakati wote.

Kamati ya kudumu ya Bunge yaridhishwa kasi ujenzi Soko la Kariakoo

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeridhishwa na ujenzi  unaoendelea wa Mradi wa Soko la Kariakoo jijini Dar es salaam.

Akizungumza hii leo tarehe 21 Februari, 2025 mara baada ya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Mradi wa Soko la Kariakoo pamoja na kujionea eneo lilipotokea tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Florent Kyombo ameipongeza Serikali  ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ilivyopambana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha inaokoa watu na mali wakati yalipotokea maafa  nchini.

Makamu Mwenyekiti huyo ameleza kuwa kuanza kwa ujenzi wa mradi wa soko la Kariakoo ni hatua nzuri ambayo itasaidia wafanyabiashara na wengine wanaopata huduma katika eneo hilo kufanya shughuli zao katika eneo rafiki na salama.

Akizungumza kuhusu jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo amesema Serikali imeendelea kuratibu vyema masuala ya menejimenti ya maafa nchini kwa kuchukua hatua za haraka katika kunusuru uhai na mali za watu wake pindi maafa yanapotokea.

"Tunaendelea kuishukuru na kuipongeza Serikali kupitia Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake mkubwa na moyo wa kujali aliouonesha wakati wote tulipopatwa na haya maafa hadi sasa Serikali inapoendelea kuimarisha miundombinu na kurejesha hali," Amesema Mhe. Kyombo.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu  anayeshughulikia  masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga ameipongeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa uamuzi wake wa kutembelea na kujionea athari zilizotokana na kuanguka kwa ghorofa hilo na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi wa Soko la Kariakoo.

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake tangu maafa haya yalipotokea hadi sasa katika hatua zote za uokoaji wa watu na mali zao. Pia niwapongeze vyombo vya ulinzi na Watanzania wote kwa ushirikiano wote waliouonesha wakati wote wa maafa yalipotokea hadi kufikia hapa Serikali inapoendelea kufanya kila jitihada za  kurejesha hali," Alipongeza Mhe. Nderiananga.

Ikumbukwe Ghorofa hilo liliporomoka mnamo tarehe 16 Novemba, 2024 muda wa saa tatu asubuhi katika Mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala, Kata ya Kariakoo, Mtaa wa Kariakoo Magharibi, Barabara ya Mchikichi Kiwanja Na. 12 Kitalu Na.7. Jengo hilo, lililokuwa likitumika kwa shughuli za kibiashara ikiwemo maduka na maghala ya kuhifadhi bidhaa za wafanyabiashara. Tukio hilo lilisababisha Vifo vya watu 31 na kujeruhi watu 71.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...