Friday, December 13, 2024

Siri ya Saudi Arabia Kuteuliwa Kuandaa Kombe la Dunia Mwaka 2034

Siri ya Saudi Arabia Kuteuliwa Kuandaa Kombe la Dunia Mwaka 2034


Oktoba 2023 rasmi FIFA ilifungua dirisha la maombi ya kuandaa WORLD CUP 2030 na 2034

Ili kuhakikisha wanatenda haki kwa bara linalopewa kuandaa WORLD CUP. FIFA wana sheria yao inayoitwa PRINCIPLE OF CONFEDERATION ROTATION.

Hii ni sheria ambayo inahakikisha kunakua na mazingira bora kuelekea maandalizi au kuchaguliwa kwa bara kupewa nafasi ya kuandaa World Cup. Kila bara linaruhusiwa kuandaa World Cup kila baada ya miaka 

Chini ya PRINCIPLE OF CONFEDERATION ROTATION, Fifa ina mabara 6 ambayo ni UEFA, CONMEBOL (South America), Asia (AFC), Africa (CAF), Oceania (OFC) & CONCACAF (Amerika ya kati na kaskazini)

Kombe la dunia linalofuata 2026 litaandaliwa na bara la CONCACAF ( Mexico, Canada & USA). So katika yale mabara 6, kimsingi hapo yanakua yamebakia mabara 5 kuelekea maandalizi ya World Cup 2030 na 2034

Sasa imekuaje Saudi Arabia ambayo ipo bara la ASIA amepata hii nafasi ya kuandaa World Cup 2034, wakati 2022 tayari Qatar walishaandaa, na kwa utaratibu ASIA ilitakiwa nafasi yao waipate tena mwaka 2042?

Sasa nisikilize kwa makini nikuelekeze

Saudi Arabia ambayo ipo ASIA imepata nafasi ya kuandaa tena World Cup 2034 japo haikua nafasi yao kwa sababu zifuatazo;

Kombe la dunia la 2030 litafanyika kwa kuhusisha mabara matatu kwa pamoja ( CAF, UEFA na CONMEBOL) kwa sababu FIFA itakua inatimiza miaka 100 ya kuandaa kombe la dunia.

So maana yake ni kwamba kwa kuwa 2030 kombe la dunia limeandaliwa kwa mabara matatu kwa mpigo hvyo kwa mwaka 2034 nafasi ya kuandaa World Cup inabakia kwa mabara ya Oceania na Asia.

Bara la Oceania ambalo kimsingi linahusisha nchi kama New Zealand na Australia, ila Australia ilishajitoa Oceania na ikajiunga na bara la Asia tangu mwaka 2006

Fifa ikasema nchi kama New zealand na wenzake hawana uwezo kuandaa World Cup. So bara la Oceania likawa limechinjiwa baharini kinamna hiyo

So nafasi ikabaki tena kwa Asia ambayo sasa nchi kama Indonesia, Vietnam, Thailand na Australia wote hao wakaamua kwa pamoja kumuunga mkono Saudi Arabia.

Saudi Arabia akabakia yeye pekee yake ambae alipeleka bid Oktoba mwaka jana na hvyo alishinda nafasi ya kuandaa kombe la dunia kwa mwaka 2034

Shaffih Dauda

Thursday, December 12, 2024

EWURA YAHAMASISHA WADAU KUPELEKA HUDUMA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA VIJIJINI KAHAMA




MENEJA EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher, amewahamasisha wamiliki wa vituo vya mafuta kupeleka huduma ya nishati safi ya kupikia vijijini ili kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mhandisi Christopher ametoa wito huo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wadau wa mafuta Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga .

Mhandisi Christopher amesema kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kutumia Nishati Safi ya kupikia ili kulinda afya, kuokoa gharama na muda sambamba na kulinda Mazingira. 

"Nishati Safi ya kupikia ina manufaa makubwa kwetu binadamu na mazingira kwa ujumla hivyo nawaomba wamiliki wa vituo vya mafuta muunge mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kupeleka huduma hiyo kwa wananchi wa vijijini ili waweze kutumia nishati safi ya kupikia", amesema Mhandisi Christopher

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAPSOA Wilaya ya Kahama, Bw. Alley Abeid Salum ameishukuru EWURA kwa elimu na anaamini kuwa itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili wadau wa mafuta.

GDSS YALETA MAFANIKIO CHANYA DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI 2024


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WANAHARAKATI kupitia Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) wameweza kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii hasa katika kuhakikisha mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla wanapata haki zao za msingi pamoja na kupambana na unyanyasaji wa kijinsia.

Akizungumza jana Desemba 12, 2024 wakati wa Semina za Jinsia na Maendeleo ambazo hufanyika kila Jumatano katika viwanja vya TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam, Mwanaharakati kutoka Mabibo, Bw. Venance Peter amesema kupitia semina hizo wameweza kujengewa uwezo na kuwa sehemu ya kuelimisha jamii na kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikitokea kwenye jamii zao ikiwemo kumlinda mwanamke na mtoto dhidi ya ukatili.

Amesema wamekuwa ni sehemu ya mabadiliko katika jamii hasa katika kuelimisha makundi rika kupitia Gender Club za mashuleni na kuweza kupunguza vitendo vya ukatili mashuleni na kwenye jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwanaharakati kutoka Mbezi Beach, Bi. Flora Baltazary amesema kupitia semina hizo wananchi wameweza kupata hamasa zaidi kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na wanwake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi.

"Kwenye semina hizi hamasa zilitokea huku, wanawake kuwaambia wanaweza na wanaweza kweli kwani tumeona sehemu nyingi wameweza kugombea kitu ambacho ni matokeo wanaGDSS kwa mwaka huu 2024". Amesema

Aidha amesema wamekuwa wakipaza sauti dhidi ya ukatili ambao ulikuwa ukiendelea na kuweza kuleta matokeo chanya kwa wahusika kufikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua stahiki.

Mnada madini ya vito kuzinduliwa rasmi Desemba 14 Mirerani, Manyara

Na John Walter
▪️Lengo ni kuyaongezea thamani
▪️Kudhibiti utoroshaji
▪️Kuuzwa kwa bei ya ushidani

WAZIRI wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mnada wa  madini ya  vito  unaotarajiwa kufanyika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, ili kuyaongezea thamani madini hayo.

Mnada huo ambao ulisimama kwa muda, umepangwa kufanyika tena kwa mara ya kwanza Desemba 14, 2024.

Akizungumza leo Desemba 12, 2024, Mavunde amesema madini ya vito, yanafanyiwa mnada kama mkakati wa kuyatangaza na    kuyaongezea thamani kimataifa.

Mavunde amesema utaratibu wa kufanya mnada huo ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

Amesema, mnada huo utashirikisha wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi na atakayenunua madini hayo katika mnada ni atakayeshinda bei iliyowekwa.

"Mnada huu utaendeshwa kwa usalama mkubwa kwa kuwa madini hayo hususan Tanzanite yana thamani kubwa. Serikali imeimarisha ulinzi ili kujihadhari na watu wasio waaminifu,"amesema Waziri Mavunde.

Aidha, amesema mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki na kodi kwa uwazi ili kuchangia pato la Taifa na kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji, wanunuzi na mali zao.

Minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za Afrika zenye madini ya vito kama vile Zambia (emerald), Zimbabwe (almasi) na Afrika Kusini (almasi).

FADLU Afunguka: Kwa Kweli, Kucheza Nyumbani ni Faida kubwa kwetu, Lazima Tushinde

FADLU Afunguka: Kwa Kweli, Kucheza Nyumbani ni Faida kubwa kwetu, Lazima Tushinde


"Kwa kweli, kucheza nyumbani ni faida kubwa kwetu. Tutakuwa na programu za mazoezi kwa siku chache zilizopo mbele yetu ili kuwa tayari kwa mchezo huu. Nitahakikisha mpango wetu wa kimbinu ni tofauti na ule tulioutumia kule Algeria."

"Nidhamu ya kulinda itakuwa sehemu muhimu ya mchezo wetu, lakini tunahitaji kuwa na mashambulizi ya haraka na kuzuia makosa tuliyofanya kwenye mchezo wa awali, Lengo ni kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri na kuweka hesabu zetu sawa katika michuano hii ya CAF."

.

Je? Umesumbuka na Matatizo ya UTI Sugu, Nguvu za Kiume, Mapenzi, Presha na Ganzi Mwilini Bila Suluhisho? Muone Dr. Marium Atakusadia


Je? Umesumbuka na Matatizo ya UTI Sugu, Nguvu za Kiume, Mapenzi, Presha na Ganzi Mwilini Bila Suluhisho? Muone Dr. Marium Atakusadia



Je? Umeshawahi kusumbulia na habari za uchumba? Mahusiano ya kimapenzi? Ndoa? Magonjwa? Kazi? Hupati pesa Kwa mpenzi wako? Ngungu za kiume? Maumbile madogo? Uume uliosinyaa? Sukari? Presha? Ganzi? Miguu kuwaka moto? Acha kuumiza roho yako bure Dr. Marium atakusaidia Sasa.


Anatibu presha, sukari, nguvu za kiume, maumbile yaliyo sinyaa, kurefusha maumbile madogo.


Anatibu suala Zima la mahusiano mwanaume hakupendi, hakujali, hakupi ukitakacho , atakupa chochote ukitakacho, pia Dr. Marium anamrudisha mpenzi wako aliepotea ama ambae Hana mapenzi na wewe Kwa dawa zake za mvuto ndani ya masaa 24 tu, Dr. Marium anaouwezo Kwa kumvuta mpenzi wako hata Alie nje ya nchi na atakutimizia utakacho .


Dr. Marium anatibu magonjwa ya presha, sukari, tezi dume, ganzi, miguu kuwaka moto au kupasua, vidonda vya tumbo, mgoro, pumu, kukosa hamu ya kula vyote hivi Dr. Marium anatibu Kwa miti shamba asilia.

Dr. Marium anazo dawa za kupunguza unene kupunguza uzito ama kuongeza unene dawa hizi anazo pia.

Dr. Mariamu anatibu matatizo ya uzazi Kwa kina mama ambae hawajawahi kupata mtoto atapata ujauzito, machngo ya kina mama, anazo dawa za kina mama za kumfanya mwanaume ampende kipndi Cha tendo LA ndoa.

Anatoa Pete za Bahati pia Anatibu Matatizo ya UTI Sugu 


Dr. Marium anapatikana dar es salaam Kwa simu namba hii 0741799737 pia inapatikana watsup Dr. Anatibu hata Kwa aliembali pia 

Wednesday, December 11, 2024

Ahmedy Ally Awaita Yanga Maiti Baada ya Kufungwa Algeria

Ahmedy Ally Awaita Yanga Maiti Baada ya Kufungwa Algeria


 "Sisi hatufanani na wao na timu yetu ni bora kuliko timu yeyote kwa sasa na haiwezi kufanana na timu yeyote kwa ukanda huu wa Afrika mashariki".

.

"Sisi tumefungwa Algeria na wo wamefungwa Algeria wasiseme kama tunafanana na kama wote tupo mochwari sisi ni wahudumu na wao ni maiti".

.

Anasema; Ahmed Ally meneja habari.

Mchezaji Israel Mwenda Asajiliwa na Yanga Rasmi......

Mchezaji Israel Mwenda Asajiliwa na Yanga Rasmi......

Klabu ya Yanga imethibitisha kunasa saini ya Israel Mwenda kwa mkopo akitokea Singida Black Stars.

Mwenda pia aliwahi kuwatumikia Simba Sc kabla ya kutimkia Singida.

Wakati yupo Alliance alikuwa mshambuliaji halafu kingine watu wasichokifahamu kuhusu Israh ni mpiga free kicks mzuri tu.

"Kuna 'mahusiano mazuri kati ya Yanga na Singida Black Stars , Kevin Nashon, Israh, Guede, Mauya, Kibabage, hawa wote wametoka Yanga Sc kwenda Singida Black Stars na Singida kwenda Yanga Sc"

Tuesday, December 10, 2024

Polisi Wanawake Manyara waadhimisha kilele cha siku 16 za kupinga ukatili kwa matendo ya huruma


Na John Walter -Babati 

Wanawake Polisi Mkoa wa Manyara wameungana na dunia kuadhimisha kilele cha Siku 16 za Kupinga Ukatili kwa njia ya vitendo vya huruma na kuhamasisha jamii kupinga vitendo hivyo.

Katika maadhimisho haya, walitoa misaada kwa kituo cha kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kiitwacho Hossana kilichopo Managhat wilayani Babati, wakionesha mfano wa upendo na mshikamano kwa jamii.

Misaada hiyo ilihusisha chakula kama vile mahindi, maharage,mchele, mafuta ya kupikia na ya kujipaka, vinywaji pamoja na sabuni za kufulia, vyote vikilenga kuboresha watoto hao.

Wanawake hao walionyesha kuwa jukumu la kupambana na ukatili linaweza kuanza kwa matendo madogo yanayojenga matumaini kwa wale walioathirika zaidi.

Mbali na kutoa misaada, walifanya kampeni ya kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto, na aina nyingine za ukandamizaji. Walisisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana kuimarisha ulinzi na usalama wa makundi yaliyo hatarini.

Akizungumza wakati wa tukio hilo  Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Kamishna msaidizi wa polisi Lucas Mwakatundu amesema wanapoadhimisha siku 16 wanatuma ujumbe wa matumaini kwa wahanga wa ukatili na kuiasa jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha Manyara panakuwa salama bila matendo hayo.

Aidha Mwakatundu ametoa wito kwa viongozi wa kijamii, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wananchi kwa ujumla kushirikiana katika juhudi za kumaliza ukatili, huku wakihamasishwa kuripoti matukio ya ukatili na kusaidia wahanga kupata msaada unaostahili.

Akikabidhi misaada hiyo mkuu wa Polisi wilaya ya Babati na Mwenyekiti wa mtandao wa Polisi Wanawake wilayani humo SP Ernesta Mwambinga, amewasihi wananchi wenye mapenzi mema kujitolea kusaidia shughuli za ujenzi zinazoendelea na misaada mingine.

Maadhimisho haya ni sehemu ya juhudi za Wanawake Polisi Manyara kuhakikisha mabadiliko chanya katika jamii yanapatikana kupitia mshikamano, huruma, na vitendo vya kujenga.

Mkuu wa dawati la jinsia na watoto polisi mkoa wa Manyara Afande Wilnes Kimario naye aliongozana na jopo hilo kutoa Misaada hiyo.

Kaulimbiu ya Mwaka huu, Kuelekea miaka 30 ya Beijing, chagua kutokomeza Ukatili wa kijinsia.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...